Mpaka Tutapokutana Tena
Na Roho tuliyohisi katika hizi siku mbili iwe na iendelee kuwa nasi tunapoendelea na vile vitu vinavyotushughulisha sisi kila siku.
Ndugu na dada zangu, jinsi gani mkutano huu umekuwa wa ajabu. Tumelishwa kiroho tuliposikia maneno yenye maongozo ya wanaume na wanawake waliotuhutubia. Muziki umekuwa wa wajabu, jumbe zimeandaliwa na kutolewa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, na maombi yametuleta karibu na mbinguni. Tumeinuliwa katika kila njia tunavyoshiriki pamoja.
Natumaini kwamba tutachukua muda wa kusoma jumbe za mkutano mkuu wakati zitakapokuwa zinapatikana katika LDS.org katika siku chache zifuatayo na zitakapochapishwa katika toleo zijazo za magazeti ya Ensign na Liahona kwa kuwa zinastahili ukaguzi wetu wa makini na utafiti.
Najua unajiunga pamoja nami katika kuonyesha shukrani zetu za dhati kwa wale ndugu na kina dada walioachiliwa wakati wa mkutano huu. Wamehudumu vyema na wametoa mchango mkubwa katika kazi ya Bwana. Kujitolea kwao kumekuwa kamili.
Pia tumeidhinisha, kwa mikono iliyoinuliwa, kina ndugu walioitwa kwa nafasi mpya za wajibu. Tunawakaribisha na tunawataka wajue kwamba tunatarajia kuhudumu pamoja nao katika kazi ya Bwana.
Tunapotafakari jumbe tulizosikia, na tuweze kuamua kufanya vizuri kidogo kuliko tulivyofanya katika siku za nyuma. Tuweze kuwa wakarimu na wenye upendo kwa wale ambao hawashiriki imani yetu na viwango vyetu. Mwokozi alileta katika dunia hii ujumbe wa upendo na ukarimu kwa wanaume na wanawake wote. Na tuweze kufuata mfano Wake milele.
Tunakabiliwa na changamoto nyingi kali katika dunia ya leo, lakini nawahakikishia kuwa Baba yetu wa Mbinguni anatukumbuka sisi. Atatuongoza na kutubariki tunapoweka imani na matumaini yetu Kwake na atatuongoza kushinda kila matatizo yatakayokuja njiani mwetu.
Baraka za mbinguni ziweze kuwa na kila mmoja wetu. Nyumba zetu ziweze kujazwa na upendo na heshima na kwa Roho wa Bwana. Na daima tuweze kuboresha shuhuda zetu za injili, ili kwamba ziweze kuwa ulinzi kwetu sisi dhidi ya karamu ya adui. Acha Roho tuliohisi katika siku hizi mbili zilizopita iwe na ikae nasi tunapofanya mambo yale ambayo yanayotushughulisha kila siku, na tuweze kupatikana milele tukifanya kazi ya Bwana.
Mimi natoa ushuhuda kwamba kazi hii ni ya kweli, kwamba Mwokozi wetu yu hai, na kwamba analinda na kuongoza Kanisa Lake hapa duniani. Nawaachieni ushahidi wangu na ushuhuda wangu kwamba Mungu Baba yetu wa milele yu hai na anatupenda. Hakika Yeye ni Baba yetu, na Yeye ni binafsi na halisi. Na tuweze kutambua ni kwa kiasi gani anaweza kutukaribia sisi, ni umbali gani Yeye anaweza kwenda ili kutusaidia, na kwa kiasi gani Yeye anatupenda.
Ndugu na dada zangu, Mungu awabariki. Amani Yake alioahidi iwe pamoja nanyi sasa na siku zote.
Ninawaageni mpaka tutakapokutana tena katika muda wa miezi sita, na ninafanya hivyo katika jina la Yesu Kristo, Bwana wetu na Mwokozi, amina.