2010–2019
Mtu wa Ukuhani
Aprili 2014


16:23

Mtu wa Ukuhani

Unaweza kuwa mfano bora, wa wastani, au mfano mbaya. Unaweza Kufikiria haijalishi kwako, lakini inajalisha kwa Bwana.

Kila mmoja wetu ana mashujaa, hasa tukiwa vijana. Nilizaliwa na kukulia Princeton, New Jersey, Marekani. Timu moja maarufu ya michezo karibu ya nilipoishi ilikuwa na makao makuu pale katika Mji wa New York. Ilikuwa ndio nyumbani kwa timu tatu za kulipwa za besiboli katika siku hizo za kitambo: timu ya Brooklyn Dodgers, timu ya New York Giants, na timu ya New York Yankees. Philadelphia ilikuwa ni karibu na nyumbani kwetu na ilikuwa ni nyumbani kwa Wanariadha na timu za besiboli za Phillies. Kulikuwa na mashujaa wengi wa besiboli kwangu mimi kwenye timu hizo.

Joe DiMaggio, aliyeichezea New York Yankees, alikuwa shujaa wangu wa besiboli. Wakati kaka na marafiki zangu walipocheza besiboli kwenye viwanja vya shule karibu na nyumbani kwetu, nilijaribu kupembeza beti kama Joe DiMaggio alivyofanya. Hii ilikuwa kabla ya siku zile za televisheni (hii ni historia ya kale), hivyo nilikuwa na picha kutoka kwenye magazeti za kutumia kunakili jinsi ya kupembeza.

Nilipokuwa nikikua, baba yangu alinipeleka kwenye Uwanja wa Yankee. Huu ulikuwa wakati pekee nilimuona Joe DiMaggio akicheza. Kama ambaye bado niko pale katika mawazo yangu ninaweza kumuona akipembeza beti na kuona mpira mweupe wa besiboli ukipaa moja kwa moja hadi kwenye sehemu ya kukaa katikati ya uwanda.

Sasa, ujuzi wangu wa besiboli haukuweza kuja karibu na ule wa shujaa wangu wa utotoni. Lakini mara chache ninaweza kuupiga mpira wa besiboli vyema, niliigiza kiwango cha kupembeza kwake jinsi vyema nilivyoweza.

Tunapowachagua mashujaa, tunaanza kuigiza, kwa kufahamu au pasipo kufahamu, kile tunachokipenda ndani mwao.

Kwa furaha, wazazi wangu wenye hekima waliwaweka mashujaa wakubwa katika njia yangu nikiwa kijana. Baba yangu alinipelekwa mpaka Uwanja wa Yankee mara moja kushuhudia shujaa wangu akicheza, lakini kila Jumapili aliniacha nimtazame mtu mwenye ukuhani aliyetokea kuwa shujaa. Shujaa Yule alibadilisha maisha yangu. Baba yangu alikuwa Rais wa Tawi katika tawi dogo ambalo lilikutana nyumbani kwetu. Hati hivyo, kama ungekuja kwenye gorofa ya kwanza Jumapili asubuhi, ungekuwa katika kanisa. Tawi letu halikuwa na watu zaidi ya 30 katika mahudhurio.

Kulikuwa na kijana ambaye alimwendesha mama yake kwenye nyumba yetu wakati wa mikutano, lakini hakuwahi kuingia ndani ya nyumba. Hakuwa mshiriki. Ilikuwa ni baba yangu aliyefanikiwa kwa kwenda nje kwake pale alipokuwa ameegesha gari na kumwalika nyumbani kwetu. Alibatizwa na kuwa mtu wa kwanza na kiongozi wangu wa pekee wa Ukuhani wa Haruni. Alitokea kuwa shujaa wangu wa ukuhani. Bado nakumbuka sanamu ya mbao aliyonipa kama zawadi baada ya kumaliza mradi wa kukata kuni kwa ajili ya mjane. Nimejaribu kuwa kama yeye pale ninapotoa sifa zenye kufaa kwa mtumishi wa Mungu.

Nilimchagua shujaa mwingine katika tawi lile dogo la Kanisa. Alikuwa na mwanamaji mwanajeshi wa Marekani aliyekuja kwenye mikutano akivalia sare zake za kijani za kijeshi. Ilikuwa ni wakati wa vita, hivyo hiyo pekee ilimfanya shujaa. Alikuwa ametumwa kwenda Chuo Kikuu cha Princeton na jeshi kwa ajili ya kuendeleza elimu yake. Lakini mbali na kuzihusudu sare zake za jeshi, nilimtazama akicheza kwenye Uwanja wa Palmer kama Kapteni wa timu ya mpira wa Chuo Kikuu cha Princeton. Nilimuona akicheza kwenye timu ya mpira wa Kikapu ya Chuo na vile vile nikamuona akicheza kama nyota mdakaji katika timu ya besiboli.

Lakini zaidi ya hapo, alikuja nyumbani kwetu katikati ya wiki kunionyesha jinsi ya kurusha mpira wa kikapu kwa mikono yangu yote, wa kulia na kushoto. Aliniambia kwamba ningehitaji ujuzi huo kwa sababu ningekuja baadaye kucheza kwenye timu nzuri. Sikutambua hilo wakati huo, lakini kwa miaka mingi alikuwa, kwangu, mfano mzuri wa mwanaume wa ukuhani.

Kila mmoja wenu atakuwa ni mfano mzuri wa mwanaume wa ukuhani kama anataka au la. Ulikuwa mshumaa uliowashwa ulipokubali ukuhani. Bwana alikuweka katika kibebea mshumaa kuwaangazia njia wengine walio karibu nawe. Hiyo ni kweli kwa wale walio katika jamii ya ukuhani. Unaweza kuwa mfano mzuri, wa wastani, au mfano mbaya. Unaweza kufikiria haijalishi kwako, lakini inajalisha kwa Bwana. Amesema hivi:

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.

“Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango, nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.

“Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”1

Nimebarikiwa na mifano ya wenye ukuhani wakuu katika jamii ambako nilikuwa na bahati ya kutumikia. Unaweza kufanya kile walichokifanya kwangu kwa kuwa mfano kwa wengine kufuata.

Nimegundua sifa tatu za kawaida za wenye ukuhani ambao ni mashujaa wangu. Moja ni mwenendo wa sala, pili ni tabia ya huduma, na tatu ni uamuzi mgumu kama jiwe wa kuwa waadilifu.

Sote tunasali, lakini mwenye ukuhani unayetaka kuwa husali mara nyingi na kwa madhumuni maalumu. Jioni utapita magoti na kumshukuru Mungu kwa ajili ya baraka za siku. Utamshukuru kwa ajili ya wazazi, walimu, na kwa mifano mizuri ya kufuata. Utaelezea katika maombi yako kimahususi wale waliobariki maisha yako na kwa jinsi gani, katika siku hiyo. Hiyo itachukua zaidi ya dakika chache na zaidi ya wazo dogo. Itakushangaza na kukubadilisha.

Unapoomba msamaha, utajikuta unasamehe wengine. Unapomshukuru Mungu kwa wema Wake, utawafikiria wengine, kwa majina, ambao wanahitaji wema wako. Tena, uzoefu huu utakushangaza kila siku, na baada ya muda utakubadilisha.

Moja ya njia ambayo itakubadilisha kwa sala hiyo madhubuti ni, Mimi nakuahidi, kwamba utahisi kikweli kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Unapojua kwamba wewe ni mtoto wa Mungu, utajua pia kwamba anategemea mengi kutoka kwako. Kwa sababu wewe ni mtoto Wake, atakutarajia ufuate mafundisho Yake na mafundisho ya Mwanawe, Yesu Kristo. Atakutarajia kuwa mkarimu na mpole kwa wengine. Atakatishwa tamaa kama wewe una majivuno na ni mwenye kujipenda. Atakubariki kuwa na hamu ya kuweka maslahi ya wengine mbele ya yale ya kwako mwenyewe.

Baadhi yenu tayari ni mifano mizuri ya huduma ya ukuhani isiyo na choyo. Katika mahekalu duniani kote, wenye ukuhani hufika kabla ya jua kuchomoza. Na wengine hutumikia muda mrefu baada ya jua kutua. Hakuna kutambulika au kupongenzwa hadharani katika dunia hii kwa ajili ya dhabihu ya muda na juhudi zao. Nimeenda na vijana wanavyowatumikia wale walio katika dunia ya kiroho, ambao hawawezi kujipatia baraka za hekaluni wao wenyewe.

Ninavyoona furaha badala ya uchovu katika nyuso za wale wanaotumika pale mapema na jioni sana, najua kuna zawadi kubwa katika maisha haya kwa kazi hiyo ya huduma ya ukuhani isiyo na choyo, lakini ni ishara tu ya furaha ambayo watashiriki na wale ambao wanawatumikia katika dunia ya kiroho.

Nimeona furaha hiyo hiyo katika nyuso za wale wanaoongea na wengine kuhusu baraka ambazo zinatokana na kuwa katika ufalme wa Mungu. Ninamjua rais wa tawi ambaye karibu kila siku huleta watu kwa wamisionari kwa ajili ya kufundishwa. Kama miezi michache iliyopita hakuwa mshiriki wa kanisa. Sasa hivi kuna wamisionari wanaofundisha na tawi linakua katika idadi na nguvu kwa sababu yake. Lakini zaidi ya hayo, yeye ni mwanga kwa wengine ambao watafungua midomo yao na hivyo kuharakisha mkusanyiko wa Bwana wa watoto wa Baba wa Mbinguni.

Unavyosali na kuwatumikia wengine, elimu yako kwamba wewe ni mtoto wa Mungu na hisia zako kumhusu Yeye itakua. Utatambua zaidi kwamba anasikitika kama utakuwa mwaminifu katika kila njia. Utatambua zaidi kulitii neno letu kwa Mungu na wengine. Utatambua zaidi kutochukua chochote ambacho si cha kwako. Utakuwa mwaminifu kwa mwajiri wako. Utatambua zaidi kuwa katika muda na kumaliza kazi zako ambazo umepewa na Bwana ambazo umezikubali kuzifanya.

Mbali na kushangaa kama walimu wa nyumbani wao watakuja, watoto katika familia mlizoitwa kufundisha watatazamia kwa matumaini matembezi yako. Watoto wangu wamepokea baraka hiyo. Walipokuwa wanakua, walikuwa na mashujaa waliowasaidia kuweka mtazamo katika kumtumikia Bwana. Mfano huo uliobarikiwa sasa unapitia kwa kizazi cha tatu.

Ujumbe wangu pia ni mmoja wa shukrani.

Nawashukuru kwa maombi yenu. Ninawashukuru kwa kupiga magoti katika kutambua ukweli kwamba hamna majibu ya maswali yote. Mnasali kwa Mungu wa Mbinguni kuelezea shukrani zenu na kuita baraka zake katika maisha yenu na ya familia zenu. Ninawashukuru kwa huduma yenu kwa wengine na kwa nyakati mlizohisi hakuna haja ya kutambuliwa kwa ajili ya huduma yenu.

Tumekubali onyo la Bwana kwamba kama tutatafuta kusifiwa katika dunia hii kwa ajili ya huduma yetu, basi na tunaweza kukosa baraka kuu. Mtakumbuka maneno haya:

“Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

“Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.

“Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume:

“Sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.”2

Wale ambao wamekuwa mifano mizuri ya wenye ukuhani mkuu hawatambui kirahisi kwamba wana ubora wa kishujaa. Kwa kweli, wanaonekana kuwa na ugumu kufahamu vitu vile ambavyo navitamani katika wao. Nilisema kwamba baba yangu alikuwa rais mwaminifu wa tawi dogo Kanisa pale New Jersey. Baadaye alikuwa mshiriki wa Bodi kuu ya Shule ya Jumapili kwa Kanisa. Hata hivyo ninakuwa makini kuongea kwa unyenyekevu kuhusu huduma ya ukuhani, kwa sababu alikuwa na maadili.

Vivyo hivyo ni kweli kwa yule mwanamaji mwanajeshi aliyekuwa shujaa wangu utotoni. Hakuwahi kuongea nami kuhusu huduma ya ukuhani au yale aliyoyatimiza. Alinipa huduma tu. Nilijua kuhusu uaminifu wake kutoka kwa wengine. Hata kama angeona tabia alilonazo ambazo nilitamani, nisingemwambia.

Hivyo ushauri wangu kwenu ambao mnataka kuwabariki wengine kwa ukuhani wenu inabidi mtende kwa maisha yenu lile lililo la kisiri kwa wote ila kwa Mungu.

Sali Kwake. Mshukuru kwa yale yote mazuri katika maisha yako. Muombe kujua ni watu gani amewaweka kwenye njia yako ili uwasaidie. Muombe kwamba atakusaidia kutoa huduma hii. Sihi hivyo ili uweze kusamehe na ili uweze kusamehewa. Halafu watumikie, wapende, na kuwasamehe.

Juu ya yote, kumbuka kwamba huduma zote unazozitoa, hakuna iliyo kubwa zaidi ya kusaidia watu kuchagua kustahiki uzima wa milele. Mungu ametoa maelekezo hayo ya kiungu kwetu jinsi ya kutumia ukuhani wetu. Yeye ni mfano mzuri wa hilo. Huu ni mfano tunaouona katika sehemu ndogo katika uzuri wa watumishi wake hapa duniani:

“Na Bwana Mungu akasema kwa Musa, akisema: Mbingu hizi, ziko nyingi, nazo haziwezi kuhesabika kwa mwanadamu; lakini zinahesabika kwangu, kwa kuwa ni zangu.

“Na kama vile dunia moja itakavyopita, na mbingu zake na hivyo nyingine zitakuja; na hakuna mwisho wa kazi zangu, wala wa maneno yangu.

“Kwa maana tazama, hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”3

Tunatakiwa kusaidia katika kazi hiyo. Kila mmoja wetu anaweza kuleta tofauti. Tumeandaliwa kwa wakati na sehemu zetu katika siku za kazi hio tukufu. Kila mmoja wetu amebarikiwa na mifano ya wale ambao wameifanya kazi ile kupita madhumuni ya muda wao duniani.

Ninaomba kwamba tusaidiane kuinuka katika fursa hiyo.

Mungu Baba yu hai na atajibu maombi yako kwa msaada unaouhitaji kumtumikia vyema. Yesu Kristo amefufuka. Hili ni Kanisa Lake. Ukuhani unaoshikilia una nguvu ya kutenda katika jina Lake katika kazi Yake ya kuwahudumia watoto wa Mungu. Unapoojitolea kwa moyo wako wote katika kazi hii, atakukuza. Ninaahidi hayo katika Jina la Yesu Kristo, Mwokozi wetu, amina.