Gharama---na Baraka---za Ufuasi
Kuweni wenye nguvu. Muishi injili kwa uaminifu hata kama wengine wanaowazunguka hawafanyi hivyo kamwe.
Rais Monson, tunakupenda. Umetoa Moyo wako na Afya yako kwa kila wito Bwana aliowahi kukupa, hususani ofisi takatifu unayoshikilia sasa. Kanisa hili zima linakushukuru kwa uthabiti wa huduma yako na kwa kujitolea kwa kazi kusikoshindwa.
Kwa upendo na kwa kutia moyo kwa yeyote atakayetaka kubaki kuwa thabiti katika siku hizi za mwisho, nawaambia nyote na hususani vijana wa Kanisa kwamba kama hamjajikuta tayari, mtajikuta siku moja mnaitwa kulinda imani yenu au pengine hata kuvumilia baadhi ya manyanyaso ya binafsi kwa sababu wewe ni mshiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Wakati kama huo utahitaji ujasiri na heshima kwa upande wako.
Kwa mfano, Dada mmisionari hivi karibuni aliniandikia: “Mwenzi wangu na Mimi tulimwona mwanaume amekaa kwenye benchi katika bustani ya mji akila chakula chake cha mchana. Tulipokuwa tuna mkaribia, aliangalia juu na akaona vishikizo vyetu vya umishinari. Kwa mwangalio wa kuogofya jichoni mwake aliruka juu na kuinua mkono wake ili anipige. Nilikwepa kwa wakati mzuri, na ikamfanya yeye anitemee chakula chake mwili mzima na akaanza kuapa mambo mabaya dhidi yetu. Tuliondoka na hatukusema lolote. Nilijaribu kufuta chakula toka kwenye uso wangu, mara nilisikia bonge la viazi vilivyosagwa likinipiga kisogoni.Wakati mwingine ni vigumu kuwa mmisionari kwa sababu palepale nilitaka kurudi, nimnyakuwe mwanaume yule mdogo, na kusema, “TAFADHALI!” Lakini sikuweza.”
Kwa mmisionari huyu mwenye kujitolea nasema, mtoto mpendwa, katika njia yako mwenyewe ya unyenyekevu umepiga hatua katika duara ya wanawake na wanaume mashuhuri sana ambao kama Nabii Yakobo wa Kitabu cha Mormoni alivyosema, “[ali] ona kifo cha Kristo], na [ali] teseka msalaba wake na [alichukua] aibu ya ulimwengu.” 1
Hakika, kumhusu Yesu Mwenyewe, Ndugu wa Yakobo Nefi aliandika: “Na ulimwengu, kwa sababu ya uovu wao, utamhukumu kuwa kitu cha kubeza; kwa sababu hio, watampiga kwa mijeledi, na atateseka; na watamgonga, na atateseka. Ndiyo, watamtemea mate, na atateseka, kwa sababu ya upendo wake wa huruma na ustahimilivu wake kwa ajili ya watoto wa watu.” 2
Kwa kuwa katika uwiano na uzoefu wa Mwokozi mwenyewe, kumekuwa na historia ndefu ya kukataliwa na gharama kubwa sana kulipwa na manabii na mitume, wamisionari na washiriki katika kila uzao---wale wote waliojaribu kuheshimu wito wa Mungu, kuinua familia ya binadamu kwenye “njia iliyo bora zaidi.” 3
“Na niseme nini zaidi [ya wao]?” mwandishi wa kitabu cha Waebrania anauliza.
“[Wao] ambao … walizuia midomo ya simba,
“Walizima nguvu za moto, wakatoroka ncha ya upanga, … wakawa jasiri katika mapambano, wakageuza …[majeshi]…kukimbia …
“[Waliona] wafu wao wakifufuka…[wakati] wengine waliteswa, …
“Na… walipata majaribu ya mizaha ya kikatili na kupigwa mijeledi,..ya utumwa na kifungo;
“Walipigwa mawe, … walichanwa kwa msumeno vipande vipande, walijaribiwa,waliuwawa kwa upanga: …walizurura huko na huko wakiwa katika ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; wakiwa fukara, kuteseka, [na]walipata maumivu makali;
“([Wao] ambao ulimwengu haukustaili:) … walizurura katika majangwa, na katika milima, na katika mashimo ya wanyama na mapango ya dunia.”4
Kwa hakika malaika wa mbinguni walilia waliporekodi gharama hii ya ufuasi katika ulimwengu ambao mara kwa mara una uhasama kwa amri za Mungu. Mwokozi mwenyewe alitoa machozi Yake mwenyewe juu ya wale ambao kwa mamia ya miaka walikuwa wamekataliwa na kuuawa katika huduma Yake. Na sasa alikuwa anakataliwa na karibu kuuliwa.
“O Yerusalemu,Yerusalemu,” Yesu alilia, “wewe ambaye unauwa manabii, na kuwapiga mawe wale wanaotumwa kwako, mara ngapi ningewakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku anavyowakusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, na huku taka!
“Tazama, nyumba yako imeachwa kwako hame.”5
Na humo mna ujumbe kwa kila kijana na msichana katika Kanisa hili.Unaweza kushangaa kama inastahili kuchukuwa msimamo wa kijasiri wa kimaadili katika shule ya upili au kwenda kwenye umisionari tu kupata kuwa imani yako uliyothamini kwa upendo mkubwa imeshutumiwa au kupambana dhidi ya mengi katika jamii ambayo wakati mwingine yana dhihaki maisha ya upendo wa dini. Ndiyo, inastahili, kwa sababu uchaguzi mbadala ni kuwa na “nyumba” zetu tulizoachiwa “mahame”—watu binafsi waliotelekezwa, familia zilizotelekezwa, majirani waliotelekezwa, na mataifa yaliyotelekezwa.
Kwa hiyo hapa tuna mzigo wa wale walioitwa kubeba ujumbe wa kimasiya. Zaidi ya kufundisha, kushawishi, na kufurahisha watu juu ya (hiyo ni sehemu ya kufurahisha ya ufuasi), mara kwa mara wajumbe hawa hawa huagizwa kuhofisha, kuonya, na wakati mwingine kulia tu (hiyo ndio sehemu ya kuumiza ya ufuasi).Wanajua vizuri sana kwamba njia inayoongoza kwenda nchi ya ahadi “inayo tiririka kwa maziwa na asali”6 kwa vyovyote vile inapita njia ya Mlima Sinai unaotiririka kwa “itakubidi” na “haita kubidi.”7
Kwa bahati mbaya wajumbe wa amri zilizoidhinishwa za kitakatifu mara nyingi huwa hawapendwi kamwe siku hizi kuliko walivyokuwa hapo zamani, kama vile misionari aliyetemewa viazi atakavyoshuhudia sasa. Chuki ni neno baya, hata hivyo wapo wale leo ambao watasema pamoja na mfisadi Ahabu, “Namchukia [nabii Mika]; kwani hakutabiri mazuri kwangu, lakini siku zote [alitabiri] maovu.”8 Aina ile ya chuki kwa uaminifu wa nabii ilimgarimu Abinadi maisha yake. Kama alivyosema kwa mfalme Nuhu: “Kwa sababu nimewaambia ukweli mnanikasirikia. … Kwa sababu nimezungumza neno la Mungu mmenihukumu kuwa mini nina kichaa.” 9 au, tunaweza kuongeza, mshamba, ya baba mkuu, mlokole, asiye na huruma, nyembamba, mwenye mtindo wa kizamani, na wa kizee.
Ni Bwana mwenyewe aliomboleza kwa nabii Isaya:
“[Hawa] watoto….wasiotaka kusikia sheria ya Bwana:
“[Wao] wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo:
“Tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu.”10
La kuhuzunisha sana, marafiki zangu vijana, ni tabia ya umri wetu kwamba kama watu wanataka miungu wowote, wanawataka wawe miungu wasio dai mengi, miungu wa kustarehe, wale ambao sio tu hawayumbishi mashua lakini hata makasia hawa pigi, miungu wanaotupongeza kwa kutuhimiza, wanatufanya tuchekecheke, kisha wanatuambia tukimbie na tukachune maua ya marigold.11
Tazama mwanadamu akimuumba Mungu kwa mfano wake! Wakati mwingine—na hii inaonekana kejeli kubwa ya zote—watu hawa wanaomba kwa jina la Yesu kama mmoja ambaye alikuwa aina hii ya “miungu wa kustarehe”. Kweli? Yeye ambaye alisema sio tu tusivunje sheria, lakini hata tusifikiri kuhusu kuzivunja. Na kama tutafikiri kuhusu kuzivunja, tayari tumeshazivunja katika mioyo yetu. Je, hiyo inasikika kama kanuni ya “kustarehe”, rahisi masikioni na inayopendwa na wote?
Na vipi wale ambao wanataka tu kuangalia dhambi au kuigusa toka mbali? Yesu alisema kwa upesi, jicho lako likikukosesha, ling’oe. Mkono wako ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe.12 “Sikuja [kuleta] amani, bali upanga,”13 Aliwaonya wale ambao walifikiri alizungumza tu maneno ya kawaida ya kubembeleza. Siyo ajabu kwamba, mahubiri baada ya mahubiri, jamii za eneo hilo, “ [zilimsihi] aondoke mipakani mwao.”14 Siyo ajabu, muujiza baada ya muujiza, uwezo Wake haukufikiriwa unatoka kwa Mungu bali kwa shetani.15 Ni wazi kwamba swali kwenye kibandikio cha dafrau “Yesu angefanya nini?” mara nyingi halitaleta jibu linalopendwa.
Katika kilele cha huduma yake katika maisha duniani, Yesu alisema “Mpendane kama nilivyowapenda.”16 Ili kuhakikisha kuwa walielewa maana ya upendo aliyomaanisha, Alisema “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu”17 na “Basi … mtu yeyote …atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa … mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni.”18 Upendo ulio kama wa Kristo ni haja kuu zaidi tulio nao duniani kwa sababu wema daima ilipaswa kuufuata. Kwa hivyo ikiwa upendo ni mwito wetu, kama unavyofaa kuwa, basi kwa neno lake ambaye ni mfano wa upendo ni sharti tuache dhambi na ishara yoyote ya kuitetea kwa wengine. Yesu bila shaka alielewa kile wengi katika utamaduni wa kisasa wanaonekana kusahau: kuwa kuna tofauti muhimu kati ya amri ya kusamehe dhambi (ambayo alikuwa na uwezo usio na kifani kufanya) na onyo dhidi ya kuikubali (jambo ambalo kamwe hakuwahi kilifanya hata mara moja).
Marafiki, hususani marafiki zangu vijana, muwe na moyo. Upendo halisi wa Kristo unaotiririka kutoka kwenye uadilifu wa kweli unaweza kubadili ulimwengu. Nina shuhudia kwamba Injili ya kweli na inayoishi ya Yesu Kristo iko duniani na ninyi ni washiriki wa Kanisa lake la kweli na linaloishi, mkijaribu kulishiriki. Ninatoa ushuhuda wa injili hiyo na Kanisa hilo, lililo na ushuhuda mahsusi wa urejesho wa funguo za ukuhani zinazofungua nguvu na uwezo wa ibada za wokovo. Nina hakika zaidi kwamba funguo hizo zimerejeshwa na kwamba ibada hizo zinapatikana tena kupitia Kanisa la Yesu kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho zaidi ya vile nina hakika nina simama mbele yenu kwenye mimbari hii na mmekaa mbele yangu katika mkutano huu mkuu.
Kuweni wenye nguvu. Ishini injili kwa uaminifu hata kama wengine wanaowazunguka hawa fanyi hivyo kamwe. Teteeni imani yenu kwa heshima na huruma, lakini iteteeni. Historia ndefu ya sauti zilizoongozwa, pamoja na zile mtakazosikia katika mkutano huu mkuu na sauti mliyosikia hivi punde ya Rais Thomas S. Monson, zinawaelekezeni kwenye njia ya ufuasi wa Kikristo. Ni njia nyembamba, na iliyosonga bila uhuru mkubwa nyakati fulani, lakini inaweza kusafiriwa kwa kusisimua na kwa mafanikio, “na imani imara katika Kristo... mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote.”19 Kwa kufuatilia kwa ujasiri njia kama hii, utaendelea kuwa na imani isiyoyumba, utapata usalama dhidi ya pepo mbaya zinazo piga, hata shimo katika kimbunga, na mtahisi nguvu kama ya mwamba ya Mkombozi wetu, ambapo juu yake kama mtajenga ufuasi wa kumcha Mungu, hamwezi anguka.20 Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.