2010–2019
Kizazi Kiteule.
Aprili 2014


11:23

Kizazi Kiteule.

Ninyi mliteuliwa kushiriki katika kazi Yake katika wakati huu kwa sababu Yeye anawaamini mtafanya chaguo sahihi.

Wavulana, huenda mmesikia hapo awali kwamba nyinyi ni “kizazi kiteule ” ikimaanisha kwamba Mungu aliwachagua na kuwatayarisheni kuja duniani wakati huu kwa kusudi kubwa. Najua hii kuwa kweli. Hata hivyo jioni hii ningependa kuwahutubia kama “kizazi kiteule” kwa sababu kamwe haijapata katika historia watu binafsi kubarikiwa na chaguo nyingi. Chaguo nyingi zinaleta fursa nyingi, na fursa nyingi zinaleta kuwa na uwezo wa kufanya mazuri na, kwa bahati mbaya, uovu. Ninaamini Mungu aliwaleta hapa wakati huu kwa sababu anawaamini mtafanikiwa kubainisha chaguo zilizopo zenye kuchanganya akili.

Mnamo mwaka wa 1974, Rais Spencer W. Kimball alisema, “Ninaamini kwamba Bwana ana hamu ya kuweka mikononi mwetu uvumbuzi ambao sisi watu wa kawaida hatukuweza kuona hata mara moja.”(When the world Will Be Converted,” Ensign, Oct. 1974, 10).

Na amefanya hivyo! Mnakua mkiwa na mojawapo wa vifaa vikubwa sana vya kutenda mema katika historia ya binadamu: Intaneti. Pamoja nayo unakuja mchanganuo wa chaguo kadhaa. Wingi huu wa chaguo, hata hivyo, unakuja nao sehemu sawa ya uwajibikaji. Hurahisisha uwezo wenu wa kupata vyote vizuri sana na vibaya sana ulimwengu unavyotoa. Kwayo unaweza kukamilisha vitu vikubwa kwa muda mfupi sana, au unaweza kushikwa katika vitanzi visivyo na mwisho vya kipuuzi ambavyo vinapoteza muda wako na kushusha uwezo wako. Kwa kubonyeza kibonyezo, unaweza kupata chochote moyo wako unatamani. Hiyo ndiyo funguo---moyo wako unatamani nini? Je, unavutiwa na nini? Matamanio yako yatakuelekeza wapi?

Kumbuka kwamba Mungu “hutoa kwa watu kulingana na kutaka kwao” (Alma 29:4) na kwamba Yeye “atawahukumu watu wote kulingana na matendo yao, kulingana na tamaa za mioyo yao” (M&M 137:9; ona pia Alma 41:3).

Mzee Bruce R.McConke alisema: Kwa dhana ya kweli ingawa ya kitamadhali, kitabu cha maisha ni kumbukumbu ya matendo ya watu kwa hivyo yameandikwa kwenye miili yao … Yaani kila wazo, neno, na kitendo kina [adhari]katika mwili wa binadamu; vyote hivi huacha alama zake, alama zinazoweza kusomwa na Yeye ambaye ni wa Milele kwa urahisi kama maneno katika kitabu yanavyosomeka” (Mormon Doctrine,,2nd ed.[1966],97.

Intaneti pia inaweka kumbukumbu za tamaa zako, zilizodhihirishwa katika aina ya mapekuzi na mibofyo. Kuna vikosi vikubwa vinavyosubiri kutimiza tamaa hizo. Unapotambaa katika intaneti, unaacha mburuzo---kile unachowasiliana, mahali umekuwa, muda gani umekuwa hapo, na aina ya vitu ambavyo vinakuvutia. Kwa njia hii, Intaneti hukutengenezea umbo la saiba---kwa aina fulani, “kitabu cha maisha ya saiba” yako. Kama katika maisha, Intaneti itakuletea zaidi na zaidi ya kile ambacho unatafuta—. Kama tamaa zako ni safi, intaneti inaweza kuzikuza, na kufanya rahisi zaidi kushiriki katika kufuatilia vinavyostahili. Lakini, kinyume cha hayo ni kweli pia.

Mzee Neal A. Maxwell aliielezea kwa njia hii:

“Kile tunachosisitiza kutaka, kwa muda, ndicho hatimaye tutachokuwa na ndicho tutachopokea katika maisha ya milele. …

“… Ni kwa kuelimisha pekee na kufundisha tamaa zetu ndivyo zinaweza kuwa marafiki zetu badala ya kuwa maadui!” (“According to the Desire of [our] Hearts,” Ensign,,Nov. 1996, 21–22)

Ndugu zangu wadogo, kama hamhamasiki katika kuelimisha tamaa zenu, ulimwengu utawafanyia hivyo. Kila siku, ulimwengu hutafuta kushawishi tamaa zenu, ukiwashawishi kununua kitu fulani, kubonyeza kitu fulani, kucheza kitu fulani, usome au utazame kitu fulani. Hatimaye, uchaguzi ni wako. Una wakala. Ni uwezo sio tu wa kutendea juu ya tamaa zako lakini pia kutakasa, kusafisha, na kuinua tamaa zako. Wakala ni uwezo wako wa kuwa. Kila uchaguzi unakupeleka karibu na au mbali kutoka kwa kile unachotakiwa kuwa; kila mbofyo una maana. Wakati wote jiulize mwenyewe, “uchaguzi huu utakuelekeza wapi?” Kuza uwezo wa kuona mbali na muda wa sasa.

Shetani anataka kuongoza wakala wako ili aweze kudhibiti kile utakachokuwa. Anajua kwamba mojawapo wa njia nzuri ya kufanya hivi ni kwa kukutega na tabia inayokutawala. Chaguo zako zinaamua kama teknolojia itakupa uwezo au itakufanya mtumwa.

Naomba nitoe kanuni nne za kuwasaidieni, kizazi kiteule, kuelimisha tamaa zenu na kulinda matumizi yenu ya teknolojia.

Kwanza: Kujua Wewe Ni Nani Kihalisi Kunafanya Maamuzi Yawe Rahisi Zaidi

Nina rafiki aliyejifunza ukweli huu kwa njia ya kibinafsi. Mwanawe alilelewa katika injili, lakini alionekana kuyumbayumba kiroho. Mara kwa mara alikataa kuchukua nafasi za kutumia ukuhani. Wazazi wake walisikitishwa alipotangaza kwamba alikuwa ameamua kutokwenda kuhudumu misheni. Rafiki yangu aliomba kwa bidii kwa ajili ya mwanawe, akiwa na tumaini kwamba atabadilika moyoni mwake. Matumaini hayo yalivunjika wakati mwanawe alipotangaza kwamba alikuwa amechumbia kuoa. Baba alimsihi mwanawe apate baraka za baba mkuu kwanza. Kijana mwishowe alikubali lakini alisisitiza amtembelee baba mkuu peke yake.

Aliporudi baada ya baraka, alikuwa mwenye hisia kubwa. Alimtoa mpenziwe nje ambako angeweza kuongea naye kwa faragha. Baba alichungulia kupitia dirishani kuwaona wenzi wale vijana wakifutana machozi.

Baadaye alishiriki pamoja na baba nini kilichotokea. Kwa hisia kubwa, alielezea kwamba wakati wa kupatiwa baraka, alipata kuona kiasi kidogo tu cha alivyokuwa katika maisha kabla kuja duniani. Aliona jinsi alivyokuwa jasiri na mashuhuri katika kuwashawishi wengine kumfuata Kristo. Kwa kujua alikuwa nani kihalisia, ni vipi hasingeweza kuhudumu misheni?

Vijana, kumbukeni ninyi hasa ni nani. Kumbukeni kwamba mnao ukuhani mtakatifu. Hii itawatia moyo kufanya chaguo sahihi mnapotumia Intaneti na katika maisha yenu yote.

Pili: Tia Plagi Katika Nyenzo ya Nguvu

Hapo katika kiganja cha mkono wako una hekima ya miaka mingi---cha muhimu sana, maneno ya manabii, kutoka siku za Agano la Kale hadi Rais Thomas S. Monson. Lakini kama usipotia umeme kila mara kwenye simu yako, inakuwa kitu bure, na unajisikia kupotea na kuwachwa na ulimwengu. Haungefikiria kuwa na siku moja bile kutia umeme betiri yako.

Kama ilivyo muhimu kuondoka nyumbani kila siku na simu yako kama betri imejaa, ni muhimu zaidi kabisa kutiwa nguvu kiroho. Kila wakati ingiza simu katika plagi ya umeme, tumia hivyo kama kumbusho la kujiuliza mwenyewe kama imetia plagi katika nyenzo muhimu ya nguvu za kiroho---maombi na kujifunza maandiko, ambayo yanakusukuma kwa maongozi kupitia Roho Mtakatifu (ona M&M 11:12–14). Itakusaidia wewe kujua nia na mapenzi ya Bwana na kufanya chaguo ndogo lakini muhimu ambayo inaamua mwelekeo wako. Wengi wetu mara moja husitisha kile wanafanya ili kusoma ujumbe mfupi---hatupaswi kuweka hata umuhimu zaidi katika jumbe kutoka kwa Bwana? Kupuuza kuunganika na nguvu hizi kunafaa kutofikiriwa nasi (ona 2 Nefi 32:3).

Tatu: Kuwa na Smartphone Hakukufanyi uwe Stadi, lakini matumizi Yake ya Hekima Yanaweza kukufanya uwe.

Wavulana, msifanye mambo ya kipumbavu na smartphone zenu. Nyote mnajua namaanisha nini (ona Mosia 4:29). Kuna njia zisizohesabika teknolojia inaweza kukuvuta kimawazo kutoka kile kilicho cha muhimu zaidi. Fuata msemo “Kuwa pale ulipo, unapo kuwa hapo.” Unapo endesha gari, endesha gari. Unapokuwa darasani, zingatia masomo. Unapokuwa na marafiki, wape zawadi ya usikivu wako. Ubongo wako hauwezi kuunganisha vitu viwili mara moja. Kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja kunafikia kwa haraka kuhamisha lengo lako kutoka kitu kimoja kwenda kingine. Methali ya zamani inasema, “Kama unafukuza sungura wawili, hautaweza kumkamata yeyote kati yao.”

Nne: Bwana Anatoa Teknolojia Kutimiza Makusudi Yake.

Sababu takatifu ya teknolojia ni kuharakisha kazi ya wokovu. Kama washiriki wa kizazi kiteule, mnaelewa teknolojia kuliko yeyote yule. Itumieni kutia kazi maendeleo yenu kuelekea ukamilifu. Kwa sababu mmepewa mengi, nyie pia hamna budi kutoa pia (ona “BecauseI Have Been Given Much,” Hymns,, no. 219). Bwana anawategemea nyie kutumia vifaa hivi vyenye uwezo mkubwa kuchukua kazi yake kwenye usawa unaofuata, kushiriki injili kwa njia ambazo zimepita dhana zozote za kizazi changu. Ambapo vizazi vilivyopita vilishawishi majirani zao na miji yao, mna uwezo kupitia kwa intaneti na vyombo vya mawasiliano kufikia mbali zaidi ya mipaka na kushawishi ulimwengu mzima.

Ninashuhudia kwamba hili ni Kanisa la Bwana. Mliteuliwa kushiriki katika kazi Yake wakati huu kwa sababu anawaamini ninyi kufanya chaguo sahihi. Ninyi ni kizazi kiteule. Katika jina la Yesu Kristo, amina.