“Nimewapa Kielelezo”
Mwelekezi mkuu aliyewahi kuishi duniani ni Mwokozi wetu. …Yesu Kristo. Anatualika tufuate kielelezo chake kamilifu.
Nilivyotafakari wajibu wangu kushiriki injili, nimefikiria juu ya watu ninaowapenda ambao ushawishi wao umenisaidia kupata njia ya kiungu iliyosaidia kuendelea kwangu kiroho. Katika wakati muhimu maishani mwangu, Baba aliye Mbinguni alinibariki na mtu aliyenijali zaidi ya kusaidia kushawishi chaguo zangu katika njia ifaayo. Walifuata ushauri huu kutoka kwa Mwokozi: “Kwa kuwa nimewapa kielelezo, ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.”1
Nilipokuwa mtoto mdogo, babangu hakuwa mshiriki wa Kanisa na mamangu alikuwa hashiriki kikamilifu. Tuliishi Washington D.C, na wazazi wa mamangu waliishi maili 2,500 (4,000 km) mbali katika jimbo la Washington. Miezi kadhaa baada ya siku yangu ya kuzaliwa ya nane, Bibi Whittle alikuja kutoka upande moja wa nchi hadi upande mwingine kuja kututembelea. Bibi alikuwa na sikitiko kwamba sikuwa nimebatizwa wala kakangu mkubwa. Sijui aliwaambia nini wazazi wangu kuhusu haya, lakini ninajua kwamba asubuhi moja alichukua kakangu pamoja nami kwa bustani na kushiriki nasi hisia zake juu ya umuhimu wa kubatizwa na kuhudhuria mikutano ya Kanisa kila wakati. Siwezi kumbuka yale hasa aliyosema, lakini maneno yake yalinivutia na punde kakangu pamoja nami tulibatizwa.
Bibi aliendelea kutusaidia. Ninakumbuka kwamba kila wakati kakangu ama mimi tulipewa jukumu la kutoa hotuba kanisani, tungempigia simu ili atupe mapendekezo kuhusu yale tungesema. Kwa siku chache hotuba iliyoandikwa kwa mkono ungekuja kwa posta. Baada ya muda mapendekezo yake yalibadilika na kuwa mwongozo uliohitaji jitihada zaidi kutoka kwetu.
Bibi alitumia tu kiasi cha kutosha cha ujasiri na heshima ili kumsaidia baba yetu kutambua umuhimu wa kutubeba katika gari lake kwenda kanisani kwa mikutano yetu. Katika kila njia iliyofaa, alitusaidia kuhisi haja ya injili katika maisha yetu.
Muhimu zaidi, tulijua Bibi alitupenda na kwamba aliipenda injili. Alikuwa kielelezo kizuri! Ninashukuru sana kwa ushuhuda alioshiriki nami nilipokuwa mdogo sana. Ushawishi wake ulibadili mwelekeo wa maisha yangu milele.
Baadaye, nilipokuwa karibu kuhitimu kutoka chuo kikuu, nilimpenda msichana mrembo aliyeitwa Jeanene Watkins. Nilidhani alikuwa anaanza kunipenda pia. Usiku moja tulipokuwa tunazungumza kuhusu siku za usoni, aliongeza katika majadiliano kauli ambayo ili badili maisha yangu milele. Alisema, “Nitakapoolewa, itakuwa katika hekalu kwa mmisionari mwaminifu aliyerejea nyumbani kutoka misheni.
Sikuwa nimefikiria sana kuhusu kuhudumu misheni kabla ya siku hiyo. Usiku huo motisha yangu ya kuzingatia huduma ya umisionari ilibadilika kabisa. Nilienda nyumbani na singefikiria juu ya chochote kingine. Nilikuwa macho usiku mzima. Nilikuwa nimeondoshwa kutoka masomo yangu siku iliyofuata. Baada ya maombi mengi niliamua kukutana na askofu wangu na kuanza kujaza makaratasi ya kuhudumu misheni
Jeanene kamwe hakuniuliza nihudumu misheni kwa ajili yake. Alinipenda ya kutosha kushiriki imani yake na kisha alinipa fursa ya kujiamulia mwelekeo wa maisha yangu mwenyewe. Sote tulihudumu misheni na baadaye tuliunganishwa milele katika hekalu. Ujasiri wa Jeanene na msimamo wake katika imani yake umeleta mabadiliko yote muhimu katika maisha yetu pamoja. Nina uhakika hatungepata furaha tunaofurahia bila imani yake dhabiti katika kanuni ya kumtumikia Bwana kwanza. Yeye ni kielelezo chema, cha haki!
Wote Bibi Whittle na Jeanene walinipenda ya kutocha kushiriki imani yao kwamba maagizo ya injili na kutumikia Baba wa Mbinguni kungebariki maisha yangu. Hakuna aliyenilazimisha ama aliyenifanya nihisi vibaya juu ya mtu niliyekuwa. Walinipenda tu na kumpenda Baba aliye Mbinguni. Wote walijua Yeye angefanya zaidi na maisha yangu kushinda niwezavyo pekee yangu. Kila mmoja kwa ujasiri alinisaidia kwa njia ya upendo kuishi kwa njia ambayo ingeniletea furaha kuu.
Kila mmoja wetu anawezaje kuwa kielelezo muhimu? Lazima tuhakikishe tunawapenda kwa dhati wale tunaotaka kusaidia kwa haki ili waweze kuanza kukuza imani katika upendo wa Mungu. Kwa watu wengi duniani, changamoto ya kwanza katika kukubali injili ni kukuza imani katika Baba aliye Mbinguni, anayewapenda kikamilifu. Ni rahisi kukuza imani hiyo wakati wako na marafiki ama wana familia ambao wanaowapenda kwa njia hiyo hiyo.
Kuwapa uhakikisho katika upendo wako kunaweza kuwasaidia kukuza imani katika upendo wa Mungu. Kisha kupitia kwa mawasiliano yako yenye upendo na makini, maisha yao yatabarikiwa kwa kushiriki masomo uliyojifunza, uzoefu ulizopata, na kanuni ulizofuata ili kupata suluhu kwa matatizo yako mwenyewe. Onyesha kujali kwako kwa dhati kwa maisha yao; kisha shiriki maarifa yako ya injili ya Yesu Kristo.
Unaweza kusaidia kwa njia ambazo zinahushisha kanuni na mafundisho ya injili. Himiza wale unaowapenda watafute kuelewa kile Bwana angewataka wafanye. Njia moja ya kufanya hivi ni kuwauliza maswali yanayowafanya wafikirie na kisha kuwakubalisha muda wa kutosha- iwe masaa, siku, miezi, ama zaidi-kutafakari na kutaka kupata majibu yao wenyewe. Huenda ukahitaji kuwasaidia kujua jinsi ya kuomba na jinsi ya kutambua majibu ya maombi yao. Wasaidie kujua kwamba maandiko ni nyenzo muhimu ya kupokea na kutambua majibu. Kwa njia hiyoutawasaidia kujitayarisha kwa fursa na changamoto za siku za usoni.
Lengo la Mungu ni “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”2 Hiyo ndiyo kanuni ya msingi inayohamasisha yote tunayofanya. Wakati mwingine sisi hushughulika na vitu tunavyopata kuwa vya kuvutia sana ama hujishughulisha kabisa na majukumu ya kidunia hadi tunasahau malengo ya Mungu. Unapolenga maisha yako mara kwa mara kwenye kanuni za msingi, utapata ufahamu ya yale unayopaswa ufanye, na utafanya zaidi kutimiza malengo ya Bwanana furaha nyingi kwako mwenyewe.
Unapolenga maisha yako kwenye kanuni za msingi za mpango wa wokovu, utajihusisha vyema zaidi katika kushiriki kile unachojua kwa sababu unaelewa umuhimu wa milele wa maagizo ya injili. Utashiriki kile unchojua kwa njia inahimiza marafiki zako kutaka kuimarishwa kiroho. Utawasaidia wapendwa wako watake kujitolea kutii amri Zake zote na kujichukulia juu yao wenyewe jina la Yesu Kristo.
Kumbuka kwamba uongofu wa watu binafsi ni sehemu tu ya kazi ya wokovu. Daima taka kuimarisha familia. Fundisha ukiwa na muono wa umuhimu wa familia kuunganishwa milele katika hekalu. Na familia zingine huenda zikachukua miaka. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na wazazi wangu. Miaka mingi baada ya mimi kuzaliwa, baba yangu alibatizwa, na baadaye familia yangu ilifunganishwa hekaluni. Baba yangu alihudumu kama mfunguji hekaluni, na mama yangu akahudumu pale pamoja naye. Unapokuwa na ono la maagizo ya kufunga ya hekalu, utasaidia kujenga ufalme wa Mungu.
Kumbuka kuwapenda ndio msingi wa nguvu wa kushawishi wale unaotaka kuwasaidia. Ushawishi wa Bibi yangu Whittle na mke wangu, Jeanene, ungekuwa bila thamani kama singejua mwanzoni kwamba walinipenda na walitaka niwe na maisha bora zaidi.
Kama mwenza kwa upendo huo, waamini. Katika baadhi ya matukio huenda ikaonekana vigumu kuamini, lakini tafuta njia ya kuwaamini. Watoto wa Baba aliye Mbinguni wanaweza kufanya vitu vya ajabu wanapohisi kuaminiwa. Kila mtoto wa Mungu duniani alichagua mpango wa Mwokozi. Amini kwamba wakiwa na fursa watachagua vivyo hivyo tena.
Shiriki kanuni ambazo zitawasaidia wale unaowapenda kusukuma mbele kwa njia ya uzima wa milele. Kumb uka sote tunakuwa mstari juu ya mstari. Umefuata mpangilio huo huo katika ufahamu wako wa injili. Shiriki injili kwa njia rahisi.
Ushuhuda wako wa kibinafsi wa Upatanisho wa Yesu Kristo una ushawishi mzito. Nyenzo zingine ni maombi, Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine, na kujitolea kwako kwa maagizo ya ukuhani. Hizi zote zitasaidia kupokea mwongozo wa Roho, ambao ni muhimu sana kwako kutegemea.
Ili kuwa bora na kufanya kama vile Kristo amefanya,3 tia maanani kanuni hii ya msingi ya injili: Upatanisho wa Yesu Kristo unatuwezesha kuwa zaidi kama Baba wetu aliye Mbinguni, ili kwamba tuweze kuishi pamoja milele katika vitengo vyetu vya familia.
Hakuna mafundisho ya kimsingi zaidi kwa kazi yetu kushinda Upatanisho wa Yesu Kristo. Katika kila fursa ya kufaa shuhudia juu ya Mwokozi na uwezo wa dhabihu Yake ya Upatanisho. Tumia maandiko yanayofundisha kumhusu Yeye na kwa nini Yeye ndiye mfano kamilifu kwa kila mtu duniani.4 Utahitaji kujifunza kwa bidii. Usijishughulishe sana na vitu visivyo na umuhimu ili kwamba ukose kujifunza maafundisho na mafunzo ya Bwana. Kwa msingi dhabiti wa mafundisho, wa kibinafsi, utakuwa chanzo kuu cha kushiriki kweli muhimu na wengine wanaozihitaji kwa dhati.
Tunawatumikia vyema zaidi Baba wetu aliye Mbinguni kwa kuwashawishi na kuwatumikia wengine kwa haki.5 Mwelekezi mkuu aliyewahi kuishi duniani ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Huduma yake duniani ilijaa kufundisha, kutumikia, na kupenda wengine. Aliketi chini na watu waliohukumiwa kuwa wasiostahiki urafiki Wake. Alipenda kila mmoja wao. Alibainisha mahitaji yao na kuwafundisha injili Yake. Anatualika tufuate kielelezo Chake kamilifu.
Ninajua kwamba kuishi kulingana na injili Yake ndiyo njia ya kupata amani na furaha katika maisha haya. Natumaini kwamba tutakumbuka kufanya kama alivyofanya. Kwa kushiriki upendo wetu, tumanini, na ufahamu wa ukweli na wengine ambao bado hawajakubali kikamilifu injili tukufu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.