2010–2019
Watu wa aina gani?
Aprili 2014


11:57

Watu wa aina gani?

Ni mabadiliko gani yanayohitajika kutoka kwetu ili kuwa aina ya wanaume tunaofaa kuwa?

Tunapoona taswira ya mkutano huu mkuu wa ulimwenguni kote, tunakumbushwa kwamba hakuna chochote kinachoweza kufananishwa na mkusanyiko huu---popote. Kusudi la kikao cha ukuhani cha mkutano mkuu ni kufundisha wanaoshikilia ukuhani kwamba ni watu wa aina gani tunapaswa kuwa (ona 3 Nefi 27:27) na kutuvutia sisi kufikia ukamilifu ule.

Katika miaka yangu ya ukuhani wa Haruni katika Hawaii nusu karne iliyopita na kama mmisionari huko Uingereza, tulikusanyika katika nyumba za mikutano na (kwa juhudi nyingi) kusikiliza kikao cha ukuhani tukitumia muunganisho wa simu. Katika miaka ya baadaye, matangazo ya satelaiti yaliyoruhusiwa kwa mahali maalumu penye sahani kubwa za mapokezi ili tuweze sote kusikia na kuona mikutano.Tulikuwa na woga wa teknolojia! Wachache wangeweza kufikiria ulimwengu wa leo ambao yeyote mwenye njia ya kufikia Intaneti kwa smartphone, tarakilishi mpakato, au kompyuta anaweza kupokea mkutano huu.

Hata hivyo, ongezeko hili kubwa la upatikanaji wa sauti za watumishi wa Bwana, ambazo ni sawa kama sauti ya Bwana mwenyewe (ona M&M 1:38), ina thamani ndogo isipokuwa kama tupo tayari kupokea neno (onaM&M 11:21) na kisha kulifuata. Ikisemwa kwa urahisi, kusudi la mkutano mkuu na kikao hiki cha ukuhani litakamilishwa tu ikiwa tuko tayari kufanya kazi,---kama tuko tayari kubadilika.

Miongo kadha iliyopita nilikuwa nahudumu kama askofu. Kwa kipindi kirefu nilikutana na mtu katika kata yetu ambaye kwa miaka mingi alikuwa mkubwa kwangu. Ndugu huyu alikuwa na mahusiano ya usumbufu na mkewe na alikuwa amefarakana na watoto wao. Alikuwa na wakati mgumu sana kutunza ajira, hakuwa na rafiki wa karibu na aliona kuingiliana na washiriki wa kata ni vigumu sana mwishowe alikuwa hayuko tayari kuhudumu katika Kanisa. Wakati mmoja wa majadiliano ya kina sana kuhusu changamoto katika maisha yake, aliegemea kwangu –kama hitimisho kwa mazungumzo yetu mengi---na alisema, “ Askofu, nina hasira za karibu, na hivyo ndivyo nilivyo!”

Kauli hio ilinishtua usiku ule na imenisumbua tangu wakati huo. Mara tu mtu huyu alipoamua---mara tu yeyote kati yetu anapohitimisha---“Hivyo ndivyo nilivyo” tunasalimu amri kwa uwezo wetu wa kubadilika. Tunaweza basi vile vile kuinua bendera nyeupe, kuweka chini silaha zetu, kukubali kushindwa vita na kujisalimisha tu—matazamio yoyote ya kushinda yamepotea. Huku baadhi yetu tunaweza kufikiri kwamba hicho hakituelezei sisi, pengine kila mmoja wetu anadhihirisha kwa angalau tabia moja mbaya au mbili, “Hivyo ndivyo nilivyo”

Basi, tunakutana katika mkutano huu wa ukuhani kwa sababu kile tulicho sio kile tunaweza kuwa. Tunakutana hapa usiku huu katika jina la YesuKristo. Tunakutana pamoja kwa matumaini kwamba upatanisho Wake unampa kila mmoja wetu---haidhuru udhaifu wetu, kasoro zetu, mazoea yetu ya tabia mbaya---uwezo wa kubadilika.Tunakutana kwa matumaini kwamba wakati wetu ujao, haidhuru historia yetu, unaweza kuwa mzuri.

Wakati tunaposhiriki katika mkutano huu kwa “dhamira halisi” ya kubadilika (Moroni 10:4), Roho ina njia halisi ya kufikia mioyo na akili zetu. Kama Bwana alivyofunua kwa Nabii Joseph Smith: “Na itakuwa kwamba kadiri watakavyokuwa … kutenda imani kwangu”---kumbuka, imani ni kanuni ya nguvu na uwezo---“Nitaimwaga Roho yangu juu yao katika siku ile watakayokutana pamoja” (M&M 44:2). Hiyo ina maana, ni usiku huu!

Kama unafikiri changamoto zako hazishindiki, wacha mimi nikuelezee ya mtu mmoja niliyekutana naye katika kijiji kidogo nje ya Hyderabad, India, mwaka wa 2006. Mtu huyu alionyesha mfano wa kuwa tayari kubadilika. Appa Rao Nulu alizaliwa huko India vijijini. Alipokuwa na umri wa miaka mitatu, alishikwa na polio na aliachwa kimwili hajiwezi. Jamii yake ilimfundisha kwamba uwezo wake ulikuwa umepunguzwa vikali. Hata hivyo akiwa kijana, alikutana na Wamisionari wetu. Walimfundisha uwezo mkubwa, wa aina mbili katika maisha haya na katika maisha ya milele yajayo. Alibatizwa na kuthibitishwa mshiriki wa Kanisa. Pamoja na kuinuliwa kwa maana ya kuona mbali, aliweka lengo kupokea ukuhani wa Melkizedeki na kuhudumu umisionari. Mnamo mwaka wa1986 alitawazwa mzee na alipata wito wa kuhudumu nchini India. Kutembea kulikuwa sio rahisi; alijitahidi kwa uwezo wake mkubwa kutumia fimbo katika kila mkono na alianguka mara kwa mara; lakini kuacha haikuwa kamwe uchaguzi wake. Alifanya ahadi kwa heshima na kwa bidii kuhudumu misheni, na alitimiza.

Tulipokutana na Kaka Nulu, yapata miaka 20 baada ya umisionari wake, alituamkua kwa furaha pale barabara ilipoishia na kutuongoza kwenye njia ya matope ya miguu isiyo imara mpaka kwenye nyumba yenye vyumba viwili aliyoshirikiana pamoja na mkewe na watoto watatu. Ilikuwa siku ya joto kali na isiyo ya starehe. Tuliendelea kutembea kwa shida kubwa, lakini hapakuwa na kujionea huruma. Kwa kupitia jitihada za binafsi amekuwa mwalimu, akitoa mafunzo ya shule kwa watoto wa kijiji. Tulipoingia kwa nyumba yake ya wastani, mara moja alinipeleka kwenye kona na alichomoa boksi lililokuwa na mali yake ya muhimu sana. Alinitaka nione kipande cha karatasi. Kilisoma, “Pamoja na mapenzi mazuri na baraka nyingi kwa Mzee Nulu, Mmisionari shujaa na mwenye furaha; [tarehe] June 25, 1987;[iliyosainiwa] Boyd K. Packer.” Katika siku ile, wakati aliyekuwa wakati huo---Mzee Packer alipotembelea India na kuzungumza na kundi la wamisionari, alithibitisha kwa Mzee Nulu uwezo wake wa kuwa. Kimsingi, kile Mzee Nulu alikuwa ananiambia siku ile mwaka 2006 ilikuwa kwamba injili ilimembadilisha---kwa njia ya kudumu!

Kwa matembezi haya nyumbani kwa Nulu, tuliambatana na rais wa misheni. Alikuwa pale kumsaili Kaka Nulu, mkewe,na watoto wake---kwa wazazi kupata endaumenti zao na kufungishwa na watoto kufungishwa kwa wazazi wao. Pia tulikabidhi familia matayarisho kwao ya kusafiri kwenda hekaluni Hong Kong China kwa ibada hizi. Walilia kwa furaha kwani ndoto yao ya muda mrefu waliyoingoja ilikuwa ifanikishwe.

Nini kinategemewa kwa mwenye ukuhani wa Mungu? Ni mabadiliko gani yanatakiwa kwetu kuwa namna ya watu tunapaswa tuwe? Nilitoa mapendekezo matatu:

  1. Tunahitaji kuwa wanaume wa ukuhani! Kama sisi ni vijana wenye ukuhani wa Haruni au wanaume tunaoshikilia ukuhani wa Melkizedeki, tunahitaji kuwa wanaume wenye ukuhani tukionyesha, roho ya kupevuka kwa sababu tumefanya maagano. Kama Paulo alivyosema, “Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.” (1 Wakorintho 13:11). Tunatakiwa tuwe tofauti kwa sababu tunashikilia ukuhani---sio wenye kujisifu au wenye kiburi au wenye kudhalilisha---lakini wanyenyekevu na tunaofundishika na wapole. Kupokea ukuhani na ofisi zake mbalimbali kungemaanisha kitu fulani kwetu. Kusiwe ni aina ya mpito wa kidesturi katika kiwango fulani cha umri bali tendo takatifu la agano lililofanywa kwa kutafakari sana. Tunapaswa kuhisi kupendwa na kuhisi shukrani hata kila moja ya matendo yetu yadhihirishe. Ikiwa tunafikiria ukuhani kwa nadra sana, tunapaswa kubadilika

  2. Tunahitaji kuhudumu ! Msingi wa kushikilia ukuhani ni “Kutukuza mwito wetu” (ona M&M 84:33) kwa kuwahudumia wengine. Tukiepuka wajibu wetu muhimu wa kuwahudumia wake zetu na watoto wetu, kutokubali au kukosa shauku ya kutimiza wito katika Kanisa, au kutokujali kuhusu wengine isipokuwa kama inafaa sio tunavyo takiwa tuwe. Mwokozi alitangaza, “Unatakiwa umpende Bwana Mungu wako kwa Moyo wako wote,na kwa Roho yako yote,na kwa akili zako zote” (Mathayo 22:37)na baadaye akaongeza,”Kama wananipenda utanihudumia” (M&M 42:29). Uchoyo ni kinyume cha madaraka ya ukuhani, na kama ni tabia ya mioyo yetu,tunatakiwa tubadilike.

  3. Tunatakiwa tuwe tunaostahili! Yawezekana nisiwe na uwezo wa Mzee Jeffrey R.Holland, alipozungumza katika kikao cha ukuhani miaka michache iliyopita “kutazama karibu sana usoni mwako … , pua kwa pua, na moto wa kutosha hivi … kuchoma nyusi zako” (“We Are All Enlisted,”Ensign orLiahona, Nov. 2011, 45); lakini ndugu wapendwa tunatakiwa tuamke kuona jinsi mazoea ya kawaida yanayokubalika katika ulimwengu yanavyokaba uwezo wetu katika ukuhani. Kama tunafikiri tunaweza hata kuchezea picha za ngono au uvunjaji wa usafi wa mwili au kudanganya kwa namna yoyote ile na isitatuathiri vibaya sisi na familia zetu, basi tumedanganyika. Moroni alisema “Ona kwamba mnafanya vitu vyote katika ustahilifu ” (Mormoni 9:29). Bwana kwa nguvu alielekeza, “Na sana mimi natoa kwenu nyinyi amri ya kuwa waangalifu juu yenu wenyewe ili kufanya bidii ya usikivu kwa maneno ya uzima wa milele(M&M 84:43). Kama kuna dhambi zozote ambazo hazitatuliwa zinazozuia ustahiki wetu tunahitaji kubadilika.

Majibu yaliyo kamili tu kwa maswali yaliyoulizwa na Yesu Kristo, “Mnapaswa kuwa watu wa aina gani? ” ni mojawapo ya maneno mafupi na dhahirina yakiundani aliyoyatoa: “Hata vile nilivyo. (3 Nefi 27:27). Mwaliko wa “Mje kwa Kristo na mkamilishwe ndani yake” (Moroni 10:32) yote yanahitaji na yanategemea mabadiliko. Kwa huruma, hajatuacha sisi peke yetu. “Na ikiwa watu watakuja kwangu nitawaonyesha udhaifu wao. … Ndipo nitafanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu kwao” (Etheri 12:27). Kutegemea upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kubadilika. Katika haya nina uhakika. Katika jina la Yesu Kristo, amina.