“Pale Hazina Yenu Ilipo …”
Kama sisi hatutakuwa makini, tutaanza kufukuzana na mambo ya muda badala ya, ya kiroho.
Muda mfupi baada ya kuhutubia kwenye mkutano mkuu mnamo Octoba 2007, mmoja kati ya ndugu zangu aliniambia kuwa ingekuwa miaka saba kabla ya kupata uzoefu huu mgumu tena. Nilifarijika na kumwambia kwamba ningelitilia maanani “miaka yangu saba ya shibe.” Vyema, nipo hapa sasa; miaka yangu saba ya shibe imefikia mwisho.
Januari iliyopita mke wangu mpenzi, Grace, na mimi tulipokea kazi ya kutembelea washiriki katika Ufilipino ambao walikuwa katika wakati mgumu wa kiuchumi kutokana na matetemeko na kimbunga kikubwa. Tulifurahia kwa sababu kazi hiyo ilikuwa ni jibu la maombi yetu na shuhuda kwa rehema na upendo wa Baba yetu aliye Mbinguni anayetupenda. Ilitupa utumilifu kiasi katika jinsi tulivyojielezea kwao upendo wetu na hofu yetu.
Washiriki wengi tuliokutana nao walikuwa bado wanaishi katika mahema ya muda, vituo vya jamii, na majumba ya mikutano ya Kanisa. Nyumba tulizozitembelea labda zilikuwa na paa nusu au hakuna paa kabisa. Watu wenyewe hawakuwa na kitu chochote kabisa, na hicho kidogo walichokuwanancho kilipotea. Kulikwa na matope na taka kila sehemu. Ingawaje, walikuwa wamejawa na furaha kwa msaada mdogo walioupokea na walikuwa na furaha na katika roho nzuri licha ya wao kuwa katika wakati mgumu sana. Tulipowauliza jinsi gani walikuwa wanaendelea vipi, kila mmoja wao alijibu kwa sauti dhabiti, “Tuko Sawa.” Kwa kawaida, imani yao katika Yesu Kristo iliwapa tumaini kwamba kila kitu kingekuwa na matokeo mazuri mwishowe. Nyumba baada ya nyumba, hema baada ya hema, Dada Teh nami tulikuwa tunafundishwa na watakatifu hawa.
Nyakati za machafuko au majanga, Bwana ana njia ya kutuongoza na katika vipaumbele vyetu. Mara tu, vitu vyote vya kidunia ambavyo tumevifanyia kazi kubwa kuvipata havijalishi. Kinachojalisha ni familia zetu na mahusiano yetu na wengine. Dada mmoja mzuri alisema hivi: “Baada ya maji kupwa na ilikuwa ni wakati wa kusafisha, niliangalia nyumbani mwangu na kufikiria, ‘Eeh, nimekusanya takataka nyingi sana kwa miaka yote hii.”’
Ninadhania kwamba dada huyu alipata uelewa mzuri na hivyo atakuwa makini sana katika kuamua ni vitu gani vya muhimu na ni vitu gani anaweza kuishi bila kuwa navyo.
Katika kufanya kazi na washiriki wengi kwa miaka mingi, tumefurahishwa kugundua wingi wa nguvu za kiroho. Pia tumeona yote wingi na upungufu wa mali miongoni mwa hawa washiriki waaminifu.
Kutokana haja, wengi wetu tumejihusisha katika kupata hela na kupata baadhi ya vitu vya duniani ili tuweze kuzitunza familia zetu. Inahitaji sehemu kubwa ya muda wetu na umakini. Hakuna mwisho wa kile dunia inaweza kutoa, kwa hiyo ni muhimu sana kwamba tujifunze kutambua wakati “tunapokuwa na vya kutosha.” Kama sisi si makini, tutaanza kuwa na tamaa ya kutafuta zaidi vitu vya kidunia zaidi ya vitu vya kiroho. Tamanio letu ya vitu vya kiroho na vya milele litachukua kiti cha nyuma badala ya vinginevyo. Cha kusikitisha, inaonekana kuna mwelekeo mkubwa wa kupata zaidi na zaidi na kupata bidhaa mpya na kistaraabu.
Je, tunawezaje kuhakikisha kwamba hatushawishiwi kwenye njia hii? Yakobo anatoa ushauri huu: “Kwa hivyo, msitumuie pesa zenu kwa yale yasiyo na thamani, wala nguvu zenu kwa yale yasiyotosheleza. Mnisikilizeni kwa makini, na mkumbuke yale maneno ambayo nimezungumza; na mje kwa Yule Mtakatifu wa Israeli, na mle yale yasiyoangamia, wala kuharibiwa, na mruhusu nafsi zenu zifurahie unono.”1
Natumaini hakuna mmoja wetu anayetumia hela kwa kile ambacho hakina dhamani au kufanyia kazi kile ambacho hatoshelezwi nacho.
Mwokozi alifundisha yafuatayo kwa wote Wayaudi na Wanefi:
“Msijiwekee hazina duniani, ambapo nondo na kutu huozesha, na pale wezi wanavunja na kuiba;
“Lakini mjiwekee hazina zenu mbinguni, ambapo nondo wala kutu haziozeshi, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuingia wala kuiba.
“Kwani mahali ambapo hazina yako ipo, pale pia moyo wako utakuwa.”2
Katika mazingira mengine tofauti, Mwokozi alitoa mithali hii:
“Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana;
“Akaanza kuwanza moyoni mwake, akisema, nifanyeje, maana sina pa kuweka akiba ya mavuno yangu?
“Akasema, Nitafanya hivi: nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
“Kisha nitajiambia Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, na ufurahi.
“Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako; na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
“Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.”3
Rais Dieter F. Uchtdorf alitoa ushauri ufuatao sio muda mrefu sana:
“Baba Yetu wa Mbinguni anaona umuhimu wetu halisi. Anajua vitu vinavyotuhusu ambavyo hatuvijui. Anatupa ushawishi wakati wa maisha yetu yote ili kutimiza mgawo wa uumbaji wetu, kuishi maisha mazuri, na kurudi katika uwepo Wake.
“Kwa nini, tena, tunatumia muda wetu mwingi sana na nguvu kwenye vitu ambavyo ni vya muda tu, ambavyo si vya umuhimu, na kwa muonekano wa nje si halisi? Tunakataa kuona ujinga wa kujitahidi kutimiza mambo yasiyo ya muhimu na ya muda?”4
Sote tunajua kwamba orodha ya hazina za kidunia inajumuisha kiburi, utajiri, vitu vya vifaa, nguvu, na heshima kwa wanadamu. Havidhamanishi muda mwingine na kujali, hivyo, badala yake, nitalenga kwenye vitu vinavyojumuisha hazina yetu mbinguni.
Je, ni hazina gani mbinguni ambazo tunaweza kujiwekea? Kwa kuanzia, itakuwa vyema kwetu kupata tabia za Kristo za imani, tumaini, unyenyekevu, na hisani. Tumeshauriwa mara kwa mara [kuuweka] mbali ubinadamu wa kawaida na... [kuwa] kama mtoto.”5 Onyo la Mwokozi ni kwetu sisi kuwa wakamilifu kama Yeye na Baba Yetu wa Mbinguni.6
Pili, tunahitaji kutoa muda wetu mzuri zaidi na nguvu katika kuimarisha uhusiano wa familia zetu. Hata hivyo, “familia imetawazwa na Mungu. Na ndio kitengo muhimu katika maisha haya na maisha ya milele.”7
Tatu, kuwatumikia wengine ni hali ya ufuasi wa kweli wa Kristo. Alisema, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.”8
Nne, kuelewa mafundisho ya Kristo na kuimarisha ushuhuda wetu ni kazi ambayo itatuletea furaha ya kweli na ya kutosheleza. Tunahitaji kujifunza maneno ya Kristo kila mara kama yanavyopatikana katika maandiko na maneno ya mitume walio hai. “Kwani tazama, maneno ya Kristo yatawaelezea vitu vyote mnavyostahili kutenda.”9
Ningependa kumalizia na hadithi ya bibi mmoja mjane mwenye miaka 73 ambaye tulikutana naye wakati wa safari yetu kule Ufilipino.
Wakati tetemeko lilipopiga kisiwa cha Bohol, nyumba ambayo yeye na marehemu mumewe walikuwa wamefanya juhudi nyingi kuijenga ilibomoka hata ardhini, ikamuua binti yake na mjukuu wa kiume. Sasa peke yake, anahitaji kufanya kazi kujitunza. Anafanya udobi (kwa kutumia mikono yake mwenyewe) na inabidi apande vilima kubwa mara kadhaa kwenda kutafuta maji. Tulipomtembelea alikuwa bado anakaa kwenye hema.
Haya ni maneno yake: “Mzee, Ninakubali kila kitu ambacho Bwana ameniomba kukipitia. Sina fikra zenye hasira. Ninathamini sifu yangu ya hekalu na ninaiweka chini ya mto wangu. Tafadhali jua kwamba ninalipa zaka kamili katika kipato changu kidogo kutoka kwa kufanya udobi. Haijalishi nini kinatokea, nitalipa zaka daima.”
Natoa ushuhuda wangu kwamba vipaumbele, tabia, mahitaji, matakwa, hamu, na matamanio yatakuwa na matokeo ya moja kwa moja katika hali yetu ijayo. Na tukumbuke daima maneno ya Mwokozi: “Kwani mahali ambapo hazina yako ipo, pale pia moyo wako utakuwa” Natumaini kuwa mioyo yetu itakuwa kwenye sehemu sahihi ni maombi yangu, katika jina la Yesu Kristo, amina.