Agano la Kale 2022
Machi 27. Mimi ni Nani, na Mungu Anataka Mimi Niwe Nani Kutoka1–6


“Machi 27. Mimi ni Nani, na Mungu Anataka Mimi Niwe Nani Kutoka 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Machi 27. Mimi ni Nani, na Mungu Anataka Mimi Niwe Nani Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
mvulana akipiga gita

Machi 27

Mimi ni Nani, na Mungu Anataka Mimi Niwe Nani

Kutoka1–6

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tunawezaje kupata shangwe katika kumfuata Yesu Kristo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Nani katika kata yetu au jamii yetu anahitaji msaada wetu? Tunaweza kusaidia vipi?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana kujiandaa kwa ajili ya huduma ya ummisionari?

  • Unganisha familia milele. Je! Tunaweza kuchangia vipi kwa juhudi za kata zetu za kazi ya historia ya familia na kazi ya hekaluni?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kichaka kinachoteketea ambacho hakikuchomeka kingekuwa mandhari ya kuvutia, na kiliteka usikivu wa Musa. Lakini cha kuvutia sana ni kile kilichotokea baada ya hapo. Mungu alizungumza na Musa, na Musa alijifunza kujiona mwenyewe kama jinsi Mungu alivyomuona. Kwa mtazamo huo, Musa alitimiza kitu kwa msaada wa Bwana ambacho alikuwa amefikiria hakiwezekani: alimkabili Farao na kuwakomboa watu wa Mungu.

Sisi sote tunahitaji uzoefu ambao unatusaidia kubadili shaka zetu binafsi na uelewa wa Mungu wa sisi ni kina nani na tunaweza kuwa kina nani. Vijana, hasa, wanakabiliwa na jumbe za uongo kuhusu thamani yao binafsi. Na kama vile Musa, Mungu “ana kazi kwa ajili [wao] kufanya” (Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni). Wao wana mafarao wao wenyewe wa kukabiliana na watu wao wenyewe wa kukomboa. Utawasaidia vipi kukumbuka kwamba wao ni mabinti na wana wapendwa wa wazazi wa mbinguni “mwenye asili takatifu na takdiri ya milele”? (Dhamira ya Wasichana). Tafakari kuhusu hili unaposoma Kutoka 1–6. Fikiria pia kujifunza Mafundisho na Maagano 18:10–15 na ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Una Maana Kwake” (Liahona, Nov. 2011, 19–22).

Picha
kundi la wasichana likiwa nje

Maisha yetu yanaweza kubadilishwa wakati tunapoelewa utambulisho wetu wa kweli kama watoto wa Mungu.

Jifunzeni Pamoja

Washiriki wa darasa lako au akidi wanaweza kuwa wamesoma Kutoka 1–6 wiki hii. Ili kuwachochea kushiriki kile walichojifunza, ungeweza kuwauliza jinsi Musa alivyohisi kuhusu wito wake wa kuwaokoa watoto wa Israeli (ona Kutoka 3:11). Ni kweli gani ambazo Bwana alimfundisha Musa ili kubadili mtazamo wake? (ona Kutoka 3:4–15; 4:10–17; ona pia Musa 1:3–11). Ni kwa jinsi gani kweli hizi zilimsaidia Musa? Zinaweza kutusaidiaje sisi? Tumia shughuli kama mojawapo ya zifuatazo kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kugundiua kile Mungu amekifunua kuhusu utambulisho wao wa kweli, thamani yao, na uwezekano wao.

  • Rais Dieter F. Uchtdorf alisema, “Bwana hutumia mizani tofauti kabisa na ile ya ulimwengu kupima thamani ya nafsi” (“Una Maana Kwake,” 22). Ili kujadili wazo hili, ungeweza kuandika ubaoni Ni kwa jinsi gani ulimwengu unamwonyesha mtu kwamba yeye anathamaniwa? Waalike wale unaowafundisha kupendekeza majibu. Kama tungeamua thamani yetu katika njia hii, ni kwa jinsi gani hisia hizi zitaathiri chaguzi zetu? Kisha ungeweza kuandika ubaoni Ni kwa jinsi gani Mungu anamwonyesha mtu kwamba yeye anathaminiwa? Vijana wanaposhiriki majibu, wahimize wao wasome Yohana 3:16; Mafundisho na Maagano 18:10–15; Luka 15:3–6, 11–32. Wangeweza pia kusoma sehemu ya mwisho ya ujumbe wa Rais Uchtdorf. Kama tutaamua thamani yetu katika njia hii, ni kwa jinsi gani hisia hizi zitaathiri chaguzi zetu?

  • Sifa za kupachika huathiri jinsi tuvyohisi kuhusu kujitendea wenyewe na kuwatendea wengine. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi fikiria jinsi wao wanajipachika sifa wao wenyewe, unaweza kumpa kila mmoja wao vibandiko kadhaa vya majina visivyoandikwa. Kila kibandiko kinaweza kuwa na “Haloo, Mimi …” kimeandikwa hapo juu. Waalike kufikiria juu ya maneno au virai tofauti kadhaa wanavyoweza kuandika kwenye vibandiko vyao vya majina. Kama Baba wa Mbinguni alikuwa akijaza vibandiko vya majina kwa ajili yetu, Yeye angeandika nini? Ni nini Yeye angeandika kama kibandiko kingesema “Haloo, Mimi nataka kuwa …”? Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kutafakari maswali haya wakati wakisoma maandiko yafuatayo: 1 Yohana 3:1–3; Moroni 10:32–33; Mafundisho na Maagano 76:69–70; 84:37–38.

  • Jumbe za mkutano mkuu katika “Nyenzo Saidizi” zina mifano ya watu ambao maisha yao yalibadilishwa kwa sababu walijifunza utambulisho wao wa kweli kama watoto wa Mungu. Fikiria kumpa kila mshiriki wa darasa au akidi mojawapo ya mifano hii kutafakari na kushiriki pamoja na kundi. Unaweza pia kuzungumza kuhusu jinsi kujua kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu kumeathiri maisha yako. Waalike washiriki wa darasa au akidi kufanya vivyo hivyo.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Ikiwa vijana watahisi unawaamini, imani yao katika uwezo wao mtakatifu itakua, na watakushangaza na yale wanayoweza kutimiza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 28).

Chapisha