“Aprili 10. Ni kwa Jinsi Ninaweza Kuimarisha Imani Yangu katika Yesu Kristo kila Siku? Kutokai 14–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Aprili 10. Ni kwa Jinsi Ninaweza Kuimarisha Imani Yangu katika Yesu Kristo kila Siku? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Aprili 10
Ni kwa Jinsi Ninaweza Kuimarisha Imani Yangu katika Yesu Kristo kila Siku?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha, kama nyongeza kwa kushauriana kwa pamoja kuhusu mahitaji mahususi ya darasa au akidi, mnaweza kutaka kujadili misukumo na dhamira kutoka mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.
-
Ni dhamira zipi au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu? Ni nini kuliimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?
-
Ni nini kiliimarisha shuhuda zetu juu ya manabii walio hai? Ni nini tulihisi kushawishika kufanya kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?
-
Ni nini tunahitajika kufanya kama darasa au akidi ili kukumbuka na kutendea kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Iliongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Ili kunusurika jangwani, watoto wa Israeli walihitaji kujifunza jinsi ya kumtegemea Bwana. Walimtegemea Yeye kwa miujiza ya kuokoa maisha, kama vile kutawanywa kwa Bahari ya Shamu, na pia miujiza ya kukidhi maisha, kama mana kutoka Mbinguni. Hiyo pia ni kweli kwa wale unaowafundisha. Kama watanusurika safari yao ya kiroho katika nyika ya kiroho duniani, lazima wafanye imani katika Yesu Kristo. Na ni sharti wafanye hiyo imani kila siku, sio tu mara kwa mara. Baadhi ya wale unaowafundisha wanaweza wasihisi kwamba imani yao ni kwa kipekee imara. Unaweza kuwasaidia wao kuona kwamba imani hukua kidogo kidogo, siku baada ya siku. Inarutubishwa kupitia mambo madogo na rahisi ambayo tunafanya daima. Tafakari mambo haya unapojifunza Kutoka 14–17 wiki hii. Unaweza pia kujifunza ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Vitu Vidogo na Rahisi” (Liahona, Mei 2018, 89–92).
Jifunzeni Pamoja
Ili kuanza mjadala, ungeweza kuwaomba vijana washiriki baadhi ya tabia zao za kila siku ambazo zinawasaidia kufanya mambo mazuri. Vitu hivi vinaweza kujumuisha kudumisha afya njema au kuimarisha shuhuda zao. Ni nini kingetokea kwetu kama hatukudumisha tabia hizi? Ni kwa jinsi gani juhudi zetu za kila siku za kufanya mambo mazuri zinalinganishwa na maelekezo ambao Bwana aliwapa Waisraeli ya kukusanya mana? (ona Kutoka 16:16–21). Ungeweza kusaidia darasa au akidi kulinganisha uzoefu wa Waisraeli na juhudi zetu za kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo kila siku. Kwa mfano, ni nini Bwana anatupatia sisi ambacho ni kama mana ya kila siku ambayo Yeye aliwapa Waisraeli? Tunaweza kufanya nini ambacho ni kama kukusanya mana? Ili kuendelea na mjadala wako, tumia moja au zaidi ya shughuli zilizopo chini au moja yako mwenyewe.
-
Someni pamoja Alma 37:6–7. Kama darasa au akidi, orodhesha ubaoni baadhi ya “vitu vidogo na rahisi” ambavyo Bwana ametualika tuvifanye kila siku ili kuja Kwake. Wale unaowafundisha wanaweza kisha kupitia tena ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Vitu Vidogo na Rahisi” ili kupata vitu vidogo vya ziada ambavyo vinaweza kuwa na ushawishi mkubwa katika maisha yetu. Ni athari gani vitu hivi vinaweza kuwa nayo? Tumetiwa moyo kufanya nini ili kufanya vitu hivi kuwa sehemu thabiti ya maisha yetu ya kila siku?
-
Kwa nini imani katika Yesu Kristo inahitaji kurutubishwa kila siku? Ili kuwasaidia washiriki kuelewa vyema hili, ungeweza kuonyesha moja au zaidi ya video zilizoorodheshwa katika “Nyenzo Saidizi.” Katika video hizi, Mzee D. Todd Christoferson alifundisha kuhusu haja ya juhudi za kila siku za kuhimili imani yetu. Waalike wale unaowafundisha kushiriki vitu walivyojifunza ambayo vinawashawishi kuongeza imani katika Yesu Kristo kila siku.
-
Juhudi thabiti za kila siku ni njia bora ya kuimarisha imani yetu katika Kristo. Ili kujadili wazo hili, someni pamoja pendekezo la tatu la Mzee David A. Bednar katika ujumbe wake “Uwe na Bidii Sana na Ujishughulishe Nyumbani” (Liahona, Nov. 2009, 17–20). Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa maelezo yake ya mchoro katika ofisi yake? Ni kwa jinsi gani masomo haya yanatumika katika juhudi zetu za kujenga imani yetu katika Yesu Kristo? Kusoma pamoja Alma 32: 21, 26–43 kunaweza kuwa nyongeza katika mjadala wenu. Ni umaizi gani tunaoupata kuhusu jinsi ya kuweza kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?
-
Tunaweza kuongeza imani yetu kwa kuchagua kujifunza kutokana na uzoefu ambao unaijaribu. Unaweza kuonyesha video ”Spiritual Whirlwinds (ChurchofJesusChrist.org). Jadilianeni pamoja kile tunachoweza kufanya wakati wa jaribu kuimarisha imani yetu. (Ona pia Neil L. Andersen, “Vimbunga vya Kiroho,” Liahona, Mei 2014, 18–21.) Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa au akidi kushiriki juu ya nyakati walihisi kwamba imani yao katika Kristo alijaribiwa na nini walifanya kuimarisha imani yao wakati huo. Taja wazi kwamba Kutoka 14–17 huelezea manung’uniko wa kila mara, au malalamika, ya Waisraeli walipokuwa wanapata majaribu. Ni kwa jinsi gani kunung’unika wakati wa majaribu kunadhoofika imani yetu? Kuna tofauti gani kati ya kunung’unika na kuonyesha wasiwasi wetu kwa Baba wa Mbinguni katika nyakati ngumu?
2:24
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
“Daily Bread: Pattern,” “Daily Bread: Change,” “Daily Bread: Experience” (videos), ChurchofJesusChrist.org