Agano la Kale 2022
Aprili 24. Je, Kwa Nini Mungu Hutupatia Amri? Kutoka 18–20


“Aprili 24. Je, Kwa Nini Mungu Hutupatia Amri? Kutoka 18–20,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Aprili 24. Je, Kwa Nini Mungu Hutupatia Amri? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
Amri Kumi

Aprili 24

Je, Kwa Nini Mungu Hutupatia Amri?

Kutoka 18–20

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni uzoefu gani wa karibuni uliotuleta karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Je, Kuna mtu amehamia kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa? Tunawezaje kuwasaidia wao wajisikie kukaribishwa?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, kuna shughuli zozote zinazokuja ambazo tunaweza kuwaalika marafiki kuhudhuria?

  • Unganisha familia milele. Je, Ni juhudi gani tunaweza kufanya kuandika historia yetu binafsi?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kusoma Kutoka 20 kunaweza kukuchochea kufikiria kuhusu kwa nini tuna amri. Baadhi ya watu wanaona amri kama kizuizi au jaribu la kutudhibiti. Kwa sababu tunajua kwamba Mungu ni Baba mwenye upendo, tunaweza kutumaini kwamba sheria Zake ni kwa ajili ya faida yetu, hata kama daima hatujui sababu zake. Yeye ametuahidi kwamba tunaweza kujua amri Zake ni za kweli wakati tunapoziishi (ona Yohana 7:17).

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Kwa sababu Baba na Mwana wanatupenda kwa upendo usio na mwisho, na kamili na kwa sababu Wao wanajua hatuwezi kuona kila kitu Wao wanachoona, wametupatia sheria ambazo zitatuongoza na kutulinda. Kuna muunganiko thabiti kati ya upendo wa Mungu na sheria Zake” (“Upendo na Sheria za Mungu” [Brigham Young University devotional, Sept. 17, 2019], 2, speeches.byu.edu).

Kwa nini una shukrani kwa sababu ya amri? Ni kitu gani ungependa washiriki wa darasa au akidi waelewe kuhusu kwa nini Mungu ametupatia amri? Unaweza kujiandaa kufundisha kwa kupitia tena Kutoka 20 na ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Kuwapenda Wengine na Kuishi na Tofauti” (Liahona, Nov. 2014, 25–28).

Picha
mvulana akijifunza maandiko

Tunaweza kujua ya kwamba amri za Mungu ni za kweli wakati tunapoziishi.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasiadia washiriki wa darasa au akidi kupitia tena Amri Kumi, ungeweza kuwaomba waorodheshe amri nyingi wanavyoweza kukumbuka. Kama wangehitaji msaada, wangeweza kuangalia katika Kutoka 20:3–17. Kwa nini Mungu hutupatia amri? Ili kusaidia kujibu swali hili, wanaweza kujadili chache kati ya Amri Kumi katika vikundi vidogo. Ni kwa jinsi gani kuishi amri hizi kunatusaidia kupata furaha na kusogea karibu na Mungu? Mawazo yafuatayo yanaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kujifunza zaidi kuhusu kwa nini Mungu hutupatia amri.

  • Maandiko yana majibu ya swali “Kwa nini Mungu hutupatia amri? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa au akidi kutafuta majibu katika mojawapo au zaidi ya maandiko yanayopatikana katika “Nyenzo Saidizi.” Kisha waombe washiriki kitu fulani walichopata. Wanaweza pia kutazama video zifuatazo wakitafuta umaizi: “Instructions Included,” “Why Does God Give Us Commandments?” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kuelewa kwa nini Mungu hutupatia amri, unaweza kulinganisha kuwa na amri kutoka kwa Mungu na uzoefu wanaoweza kuhusisha nazo. Kwa mfano, unaweza kuwaomba wafikirie kwamba unasafiri kando kando ya barabara ya mlimani karibu na mteremko wa ghafula mkali na kuna ua kwenye upande wa barabara. Waombe wao wajadili na mtu mwingine maswali kama yafuatayo: “Je, ni kwa jinsi gani amri za Mungu ni kama ua? Ni kwa jinsi gani kutii amri kulitubariki? Ni milinganisho gani mingine inaweza kutusaidia kuelewa kwa nini Mungu hutupatia amri na kwa nini tunapaswa kuzitii? Kwa baadhi ya mifano, unaweza kuwaalika wapitie mojawapo ya jumbe au video zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi.” Waombe washiriki milinganisho wanayopata na kujadili kile walichojifunza.

  • Mjadala wako unaweza kuongoza washiriki wa darasa au akidi kujadili jinsi tunapaswa kuwatendea wale ambao hawaamini au wanaishi baadhi ya amri fulani. Unaweza kuwaalika kutafuta ushauri katika ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Kuwapenda Wengine na Kuishi na Tofauti.” Unaweza kuuliza maswali kama haya: Je, ni kwa jinsi gani tunapaswa kuwatendea wale ambao wanachagua kuishi kwa njia tofauti nasi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuona uzuri ndani ya wengine wakati wanafanya chaguzi tofauti kuliko tunazozifanya?

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeza kushiriki mawazo yao. Waalike wao wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Katika juhudi zako za kuishi na kufundisha zaidi kama Mwokozi, wakati mwingine ni vigumu kuepuka kukosea. Usikate tamaa; bali, acha makosa na udhaifu wako ukuelekeze kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,14).

Chapisha