Agano la Kale 2022
Mei 8. Ni kwa Jinsi Gani Nitajua Kwamba Mungu Amenisaheme? Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19


“Mei 8. Ni kwa Jinsi Gani Nitajua Kwamba Mungu Amenisaheme? Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Mei 8. Ni kwa Jinsi Gani Nitajua Kwamba Mungu Amenisaheme? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
wasichana wakicheka

Mei 8

Ni kwa Jinsi Gani Nitajua Kwamba Mungu Amenisaheme?

Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16;19

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani kumgeukia Bwana kunatusaidia kukabiliana changamoto zetu na majaribu ?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Nani tunayemjua ambaye anahitaji maombi yetu na urafiki wetu?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni mipango gani ya kushiriki injili imejadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana la kata? Ni kwa jinsi gani darasa letu au akidi yetu inaweza kuhusika?

  • Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi kufanya kazi ya historia ya familia kunaweza kuimarisha mahusiano yetu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Watu wakati mwingine hushangaa kama “wamefanya vya kutosha” kusamehewa dhambi. Ingawa inachukuwa juhudi kutubu, hatimaye hatusamehewi kwa sababu tumemaliza orodha ya kukagulia au tumefanya kazi fulani. Tunasamehewa tunapokubali rehema inayotolewa na Yesu Kristo. Ni kwa njia hii kwamba asili yetu inaweza kubadilishwa.

Nyakati za kale, matambiko na dhabihu za sheria ya Musa ziliwaelekeza Waisraeli kwenye Upatanisho wa Mwokozi. Kama Bwana alivyoelezea katika Mambo ya Walawi 16:30: “Katika siku hiyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yenu, kuwatakasa, ili muweze kuwa wasafi kutoka kwenye dhambi zenu zote mbele ya Bwana.” Bila shaka, tambiko peke yake haliwezi kutupatia msamaha wa dhambi. Msamaha huja kutoka kwa Yesu Kristo. Katika siku yetu, ibada kama ubatizo na sakramenti zinaelekeza akili zetu na mioyo yetu kwa Mwokozi. Zinatusaidia kuelewa kwamba Yeye daima atatusamehe tunapotubu.

Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni amekusaidia kujua umesamehewa? Unaweza kujifunza Mosia 4:1–3 na ujumbe wa Rais Tad R. Callister “Upatanisho wa Yesu Kristo” (Liahona, Mei 2019, 85–87). Ujumbe huu unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni hutusamehe tunapotubu?

Picha
kijana akiomba

Tumesamehewa tunapokubali rehema iliyotolewa na Yesu Kristo.

Jifunzeni Pamoja

Unaweza kuanza kwa kuonyesha picha za Mwokozi akiwa Gethsemane na msalabani (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56–57). Waalike vijana kupekua Mambo ya Walawi 1:1–9; 16:15–16, 30. Waombe washiriki virai ambavyo vinawakumbusha juu ya Upatanisho wa Mwokozi. Ni kwa jinsi gani dhabihu zilizoelezwa katika mistari hii ziliwasaidia Waisraeli kutazamia Upatanisho wa Mwokozi? Ni nini kinatusaidia kukumbuka Upatanisho wa Mwokozi? Ni nini kinatusaidia kuhisi upendo na msamaha wa Mwokozi? Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia vijana kuelewa vizuri kwamba Mungu atatusamehe.

  • Watu kadhaa katika maandiko walielezea hisia walizokuwa nazo wakati Baba wa Mbinguni alipowasamehe. Washiriki wa darasa lako au akidi wangeweza kusoma baadhi ya mifano (ona “Nyenzo Saidizi”). Waalike wao kutengeneza orodha ya virai kutoka katika hii mistari ambayo inayoelezea vile inahisi kusamehewa. Unaweza kuwaomba waeleze kwa maneno yao wenyewe msamaha unavyokuwa kwao. Tunaweza kujifunza nini kuhusu Mungu kutokana na hisia hizi? Labda unaweza kushiriki hisia zako mwenyewe kuhusu msamaha.

  • Wakati mwingine watu hawana uhakika wamesamehewa kwa sababu hawana uhakika wametubu kikweli. Ujumbe wa Mzee Dale G. Renlund “Toba: Chaguo lenye Furaha” huelezea jinsi ya kutubu kikweli na kupokea msamaha wa Mungu (Liahona, Nov. 2016, 121–24). Ungeweza kuandika ubaoni vichwa Toba Halisi na Mambo Ambayo Yanatatiza katika Toba. Waombe wale unaowafundisha kupata mafundisho katika ujumbe ambao unahusiana na vichwa. Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi na msamaha Wake kutoka kwenye vifungu vitatu vya mwisho za ujumbe huu?

  • Baadhi ya watu wanaweza kuwa wametubu lakini hawahisi wamesamehewa. Hii inaweza kuwa sababu wao hawajaweza kujisamehe wenyewe. Ushauri katika ujumbe wa Rais Tad R. Callister “Upatanisho wa Yesu Kristo” ungeweza kuwasaidia. Darasa lako au akidi ingeweza kusoma sehemu ambayo huanza na “2. Dhambi.” Waombe watafute ushauri wanaoweza kushiriki na rafiki au mwanafamilia ambaye bado anahisi ana hatia hata baada ya kutubu. Toa muda kwa ajili ya vijana kushiriki hisia zao kuhusu Mwokozi, aliyefanya iwezekane kwetu kutubu na kusamehewa.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi ametufundisha kutumia maandiko kutafuta majibu ya maswali yetu wenyewe. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kutamani kugeukia maandiko na maneno ya manabii wanapotafuta majibu?

Chapisha