Agano la Kale 2022
Mei 22. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Shukrani Zangu kwa Mungu? Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34


“Mei 22. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Shukrani Zangu kwa Mungu? Kumbukumbu ya Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Mei 22. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Shukrani Zangu kwa Mungu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
mvulana akitembea ufukoni

Mei 22

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Shukrani Zangu kwa Mungu?

Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30;34

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua zaidi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Utunzaji wa wale wenye shida. Tunaweza kufanya nini au kusema ili kuwafikia wale wanaoweza kuhisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Mungu anatutunza daima na kutubariki. Lakini kwa vurugu zote na majaribu tunayokabiliana nayo, ni rahisi kusahau kumhusu Yeye. Hili lilitokea kwa Waisraeli mara nyingi, ikijumuisha wakati wa nyakati ngumu walipokuwa wakizunguka-zunguka jangwani. Lakini Bwana kwa rehema aliwaongoza hadi nchi ya ahadi—mahali pa faraja kuu na majaribu mengi, ambapo wangejaribiwa kumsahau Yeye baadaye tena. Maelekezo ya Bwana katika Kumbukumbu la Torati 6 yalikusudiwa kuwasaidia Waisraeli kumkumbuka Yeye daima na maneno Yake (ona mstari wa 6– 9).

Ni kwa jinsi gani tunaweza kumweka Bwana na maneno Yake mioyoni mwetu—“ili msimsahau Bwana”? Kumbukumbu la Torati 6:12. Ni kwa jinsi gani kumkumbuka Bwana hutusaidia kuhisi shukrani katika hali zote za maisha yetu? Unapojiandaa kufundisha, fikiria kupitia tena Kumbukumbu la Torati 12:6–9, 12 na Luka 17:11–19. Unaweza pia kupitia tena ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Shukrani katika Hali Zote” (Liahona, Mei 2014, 70–77).

Picha
msichana akijifunza

Kumkumbuka Bwana kunaweza kutusaidia kuhisi shukrani katika hali zote za maisha.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanzisha mjadala kuhusu kumkumbuka Bwana, unaweza kuwaalika vijana kushiriki uzoefu wakati walisahau kitu muhimu. Matokeo yalikuwa nini? Ni nini hutokea tunaposahau mambo makuu Bwana aliyoyafanya kwa ajili yetu? Alika darasa lako au akidi yako kupitia tena Kumbukumbu la Torati 6–9, 20–25. Mistari hii inafundisha nini kuhusu kukumbuka wema wa Mungu katika maisha yetu? Chagua shughuli moja au zaidi hapa chini ili kuwasaidia wale unaowafundisha kujifunza jinsi ya kuhisi shukrani zaidi kwa ajili ya wema wa Mungu na kuonyesha shukrani zao Kwake.

  • Kusoma Luka 17:11–19 pamoja kunaweza kuwasaidia vijana kufikiria kuhusu kwa nini ni muhimu kwetu kuonyesha shukrani zetu kwa Mungu. Fikiria kuuliza maswali ambayo yatawasaidia kuhusisha hadithi hii na maisha yao. Kwa mfano, ni baadhi ya sababu gani kwa nini wakoma tisa hawakutoa shukrani kwa Mwokozi? Kwa nini wakati mwingine tunashindwa kuonyesha shukrani kwa Mungu? Waombe wale unaowafundisha kufikiria kuhusu nyakati ambapo walihisi shukrani, hata wakati ilikuwa vigumu. Ni athari gani kuonyesha shukrani huwa juu yetu? Kwa nini ni muhimu kuonyesha shukrani zetu kwa Mungu? (Ona marejeo ya maandiko katika “Nyenzo Saidizi” kwa ajili ya baadhi ya majibu.) Tunaweza kufanya kuonyesha shukrani zetu kwa Mungu?

  • Kuna nyimbo nyingi za sifa na kutoa shukrani, kama vile “How Great Thou Art” na “Count Your Blessings” (Hymns, na. 86, 241). Ungeweza kuwaomba vijana wapekue maneno ya nyimbo hizi kwa ajili ya vitu wanayohisi shukrani kwa ajili yake. Waalike washiriki vitu walivyopata na waelezee kwa nini wana shukrani kwa ajili yake. Mngeweza kuimba nyimbo chache kati ya hizi pamoja.

  • Ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf’ “Mwenye Shukrani katika Hali Zote” hutusaidia kuelewa jinsi ya kuwa na shukrani zaidi. Njia moja ya kuwasaidia vijana kujifunza kutoka kwa ujumbe huu ni kuwagawa katika vikundi vidogo na kukipa kila kikundi sehemu moja ya ujumbe huu. Waombe washiriki virai au sentensi ambayo wanahisi ni muhtasari wa kile Rais Uchtdorf alichofundisha. Waalike kushiriki kitu fulani walichojifunza kuhusu shukrani. Ungeweza pia kutazama video “Rais Russell M. Nelson kuhusu Nguvu za Uponyaji wa Shukrani” (ChurchofJesusChrist.org). Tunaweza kufanya nini kuwa wenye “shukrani katika hali yo yote,” bila kujali ni nini? Ni mifano gani tuliyoiona ya watu walio na shukrani licha ya hali zao ngumu”?

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi anawajua wafuasi Wake, na nani wangeweza kuwa. Elimu hii ilishawishi njia aliyowafundishia. Ni kwa jinsi gani unaweza kujifunza kuhusu upendeleo, uhitaji, na changamoto za wale unaowafundisha ili uweze kuwafundisha kwa ufanisi zaidi?

Chapisha