“Juni 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusikia Sauti ya Bwana? Ruthu; 1 Samweli 1–3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Juni 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusikia Sauti ya Bwana? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Juni 12
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusikia Sauti ya Bwana?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua zaidi ya yale yaliyopo hapo chini au maswali yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Je, ni uzoefu gani ya hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Je, ni akina nani wanahitaji msaada wetu na sala zetu? Je, ni nini tunahisi kuvutiwa kukifanya ili kuwasaidia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa wanafamilia au marafiki ambao hawashiriki imani yetu?
-
Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo zaidi na ufadhili kwa familia zetu na kuleta tofauti chanya katika nyumba zetu.
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Washiriki wengi wa darasa lako au akidi wanaweza jihusisha na mvulana Samweli. Wakati Bwana aliongea naye, Samweli hakuwa na uzoefu wa kutosha wa ufunuo kutambua sauti ya Bwana. Eli, mnasihi wa Samweli, aliweza kumsaidia Samweli kujifunza kutambua sauti hii. Kama Eli, una fursa ya kushuhudia kwa wale unaowafundisha kwamba Bwana anataka kuzungumza na wao. Unaweza kuwasaidia kujifunza kutambua sauti ya Bwana, hata vile unavyojifunza kumsikiliza Yeye. Pamoja, unaweza kujifunza kile manabii Wake wamefundisha kuhusu ufunuo binafsi. Na unaweza kujifunza kusema na Bwana, kama Samweli alivyofanya, “Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.” (1 Samweli 3:10).
Kama nyongeza ya kusoma 1 Samweli 3:10 wiki hii, unaweza kujiandaa kwa kusoma ujumbe wa Rais Russel M. Nelson “Msikilize Yeye” (Liahona, Mei 2020, 88–92).
Jifunzeni Pamoja
Ili kuwaandaa wale unaowafundisha kwa ajili ya mjadala wa leo, fikiria kuwaomba wapitie tena 1 Samweli 3:1–14. Waalike kushiriki kile wanachojifunza kutoka maelezo haya kuhusu kuisikia sauti ya Bwana. Ni baadhi ya njia gani za ziada Bwana huwasiliana nasi? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia vijana kuzidisha uelewa wao wa ufunuo binafsi.
-
Hapa kuna njia moja ya kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa zaidi jinsi ya kupokea ufunuo. Ungeweza kuandika ubaoni marejeo ya maandiko yaliyopendekezwa katika “Nyenzo Saidizii” (au mengine unayoyajua). Waalike vijana kusoma kila maandiko. Wanaweza kisha kuandika ubaoni karibu ya kila rejeo kile maandiko hayo yanafundisha kuhusu kupokea ufunuo binafsi. Waalike kushiriki uzoefu walioupata wa kutafuta na kupokea ufunuo. Kama inavyofaa, shiriki uzoefu wako mwenyewe.
-
Tunapokea baraka kuu wakati tunapojifunza kusikiliza sauti ya Bwana. Ungeweza kuanzisha majadiliano kuhusu hili kwa kuwaomba vijana kushiriki sababu ambazo wangehitaji ufunuo. Kisha waombe wapekue ujumbe wa Rais Russel M. Nelson “Msikilize Yeye” (Liahona, Mei 2020, 88–92). Waalike kutafuta ushauri ambao unawasaidia kuelewa jinsi ya kusikiliza sauti ya Bwana. Ungeweza pia kuonesha moja au zaidi ya video kutoka mkusanyiko wa “Hear Him” (ChurchofJesusChrist.org/media). Kwa nini ni muhimu sana kwetu kujifunza kusikiliza sauti ya Bwana? Wahimize vijana kuandika kile walichojifunza katika shajara zao au kwenye vipande vya karatasi ili kuonyesha nyumbani kwao.
-
Vijana unaowafundisha wanaweza kushangaa juu jinsi ya kujua wakati Roho Mtakatifu anapozungumza nao. Fikiria kuonyesha video “How Can I Tell the Difference between the Holy Ghost and My Emotions?” na “How Can I Feel the Holy Ghost More Often?” kutoka katika “Face to Face with President Eyring and Elder Holland” (ChurchofJesusChrist.org). Tunajifunza nini kutokana na video hizi kuhusu kutambua kati ya mnong’ono wa Roho na mawazo yetu? Washiriki wa darasa au akidi wanaweza kushiriki jinsi watavyoweza kumjibu rafiki ambaye ana maswali sawa na yale yaliyojadiliwa katika video hizi.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
1 Wafalme 19:9–12; Helamani 5:29–31; Mafundisho na Maagano 6:14–16, 21–23; 8:2–3; 11:12–14 (Njia za Bwana anazozungumza nasi)
-
Mafundisho na Maagano 9:7–9 (Ufunuo huhitaji mawazo yako mwenyewe na kujifunza)
-
Ronald A. Rasband, “Acha Roho Mtakatifu Akuongoze,” Liahona, Mei 2017, 93–96
-
Rais Russell M. Nelson amefundisha, “Katika siku zijazo, haitawezekana kuendelea kuishi kiroho bila mwongozo, maelekezo, faraja na ushawishi wa mara kwa mara wa Roho Mtakatifu. Wapendwa akina kaka na dada zangu, ninawasihi muongeze uwezo wenu wa kiroho wa kupokea ufunuo” (“Ufunuo kwa Ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa Ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 96).