Agano la Kale 2022
Juni 26. Kwa Nini Usafi wa Kimwili ni Muhimu katika Mpango wa Mungu ? 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11


“Juni 26. Kwa Nini Usafi wa Kimwili ni Muhimu katika Mpango wa Mungu ? 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11,”” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Juni 26. Kwa Nini Usafi wa Kimwili ni Muhimu katika Mpango wa Mungu ? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
vijana wamekaa darajani

Juni 26

Kwa Nini Usafi wa Kimwili ni Muhimu katika Mpango wa Mungu ?

2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8;11

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua zaidi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumekaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaida watu binafsi?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tunaweza kujibu maswali ya marafiki zetu kuhusu Kanisa katika njia ambayo inaimarisha imani yao katika Mwokozi?

  • Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na binamu zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Baba Yetu wa Mbinguni, anatutaka tuwe na furaha, alitupatia sheria ya usafi wa kimwili. Na Shetani, ambaye anatutaka sisi tuwe na huzuni, anatufunza kwamba sheria hii si muhimu. Anafanya kila kitu anachoweza kutujaribu kutenda dhambi ya ngono. Vijana wanaweza kushawishiwa na picha na jumbe ambazo zinakinzana na kile Mungu anachofundisha kuhusu ujinsia. Kila mmoja wetu anahitaji kujihadhari na majaribu kama hayo na kujitahidi kuyaweka mawazo, maneno, na matendo safi kote katika maisha yetu yote. Tunajifunza somo hili kutoka kwa uzoefu wa kuhuzunisha wa Mfalme Daudi. Alikuwa mfano mkuu wa uaminifu. Lakini alikubali kushindwa katika majaribu na kuvunja sheria ya usafi wa kimwili (ona 2 Samweli 11:1–5).

Unaweza kujiandaa kufundisha kwa kusoma 2 Samweli 11, Ujumbe wa Mzee David A. Bednar “Tunaamini Katika Kuwa Wasafi Kimwili” (Liahona, Mei 2013, 41–44), na nyenzo zingine kuhusu usafi wa kimwili. Ni nini kinaweza kuvutia washiriki wa darasa au akidi kuona usafi wa kimwili kwa njia Mungu anavyouona. Ni nini kinaweza kuwasaida kukataa njia Shetani anavyouona?

Picha
darasa la wavulana

Ili kubakia waaminifu kwa sheria ya Mungu ya usafi wa kimwili, tunapaswa kujitahidi kila siku kuweka mawazo yetu, maneno yao, na matendo kuwa safi.

Jifunzeni Pamoja

Hapa kuna njia moja ya kutambulisha mada ya usafi wa kimwili wakati tukiwasaidia wale unaowafundisha kupitia tena kile walichokisoma katika maandiko. Andika maneno Daudi na Yusufu ubaoni. Kisha kupitia tena pamoja 2 Samweli 11:1–5 na Mwanzo 39: 7– 12. Ni kwa jinsi gani Daudi na Yusufu kila mmoja alijibu majaribu ya kutenda dhambi ya ngono? Tunajifunza nini kutoka kwenye mifano yao? Tumia shughuli zifuatazo au baadhi ya za kwako mwenyewe kuhimiza mjadala zaidi kuhusu kwa nini usafi wa kimwili ni muhimu katika mpango wa Mungu.

  • Vijana unaowafundisha wanaweza kufaidi kwa kuwafafanulia viwango vya Bwana vya usafi wa kujamiiana. Waalike kupitia tena “Usafi wa Kujamiiana” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ([kijitabu, 2011], 35–37) au ibara ya nne ya “The Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Bwana kuhusu ujinsia ni tofauti na kile Shetani anataka sisi tuamini? Vijana wanaweza kupitia tena “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” wakitafuta kauli ambazo zinaelezea kwa nini usafi wa kujamiiana ni muhimu katika mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Tunajifunza nini kutoka kwa kauli hizi ambacho kinatusaidia kuishi kwa haki katika ulimwengu wa leo?

  • Wakati mwingine watu wengine hawaelewi viwango vya maadili, hususani kwa sababu viwango hivi ni tofauti sana na vile watu wengi wanaamini. Ni kwa jinsi gani tunaweza kujibu maswali haya? Tunajifunza nini kutoka kwa Mzee na Dada Renlund katika video “Why Is Marriage Sacred to Heavenly Father?” kutoka katika “Face to Face with Elder and Sister Renlund” (ChurchofJesusChrist.org). Vijana pia wageweza kupekua maandiko katika “Nyenzo Saidizi” kwa ajili ya kauli ambazo zinaelezea baraka za usafi wa kimwili. Unaweza kuwaomba kushiriki mawazo yao kuhusu kwa nini wanachagua kutii viwango vya Bwana vya maadili ya kujamiiana.

  • Tamaduni pendwa kila mara zinafundisha kwamba hakuna haja ya kuwa wasafi kimaadili ya kujamiiana. Bado tamaduni hizi zinapuuza kweli kuhusu baraka za usafi wa kimwili na hatari za ukosefu wa maadili. Kujifunza zaidi kuhusu kweli hizi, vijana wangeweza kujifunza ujumbe wa Mzee David A. Bednar “Tunaamini katika Kuwa Wasafi Kimwili.” Wengine wangeweza kujifunza sehemu ya “Nia ya Adui,” na wengine wangeweza kujifunza “Baraka za Kuwa Wasafi Kimwili.” Kisha wangeweza kushiriki mmoja na mwingine kile walichojifunza. Wahimize waandike kirai kutoka katika ujumbe huu ambacho wanataka kukumbuka wakati mwingine wanapokabiliana na ujumbe wa uongo kuhusu kujamiiana. Unaweza pia kuwaelekeza kwenye sehemu yenye kichwa “Kanuni za Toba.” Jadilini jinsi Mwokozi anavyoweza kuwaponya wale wote ambao wanataka kutubu dhambi ya kujamiiana. Wakumbushe wale unaowafundisha kwamba wanaweza kuongea na wazazi wao au askofu kama wana maswali au haja ya kutubu.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Katika hali zote, Mwokozi alikuwa mfano na mnasihi. Aliwafundisha wafuasi Wake kusali kwa kusali pamoja nao. Aliwafundisha kupenda na kutumikia kwa mfano alivyowapenda na kuwatumikia. Aliwafunza jinsi ya kufundisha injili Yake kwa njia alivyoifundisha.

Chapisha