Agano la Kale 2022
Julai 10 Kwa Nini ni Muhimu Kuwafuata Manabii Hai wa Mungu? 2 Wafalme 2–7


“Julai 10. Kwa Nini ni Muhimu Kuwafuata Manabii Hai wa Mungu? 2 Wafalme 2–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Julai 10. Kwa Nini ni Muhimu Kuwafuata Manabii Hai wa Mungu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

kijana akiangalia mkutano mkuu katika simu

Julai 10

Kwa Nini ni Muhimu Kuwafuata Manabii Hai wa Mungu?

2 Wafalme 2–7

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Ni hatua gani tunaweza kuchukua kulingana na mjadala huo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho hutuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki shangwe hiyo na wengine?

  • Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na binamu zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kunaweza kuwa sehemu ndogo ya Naamani mkoma ndani yetu wote (ona 2 Wafalme 5:1–15). Kama vile Naamani, ambaye alikasirika wakati nabii Elisha alipomwambia kujiosha tu katika mto ili aponywe, tunaweza daima tusilewe sababu za ushauri wa manabii wetu. Tunaweza kufikiria kwamba baadhi ya ushauri hauleti maana kwetu na kwa hiyo haufai kwetu. Lakini Mungu anaahidi baraka kuu kama tu wanyenyekevu vya kutosha kumfuata nabii (ona Mafundisho na Maagano 21:4–7). Ni kwa jinsi gani kumfuata nabii kulikusaidia kusogea karibu na Bwana? Ni mifano gani ingine kutoka 2 Wafalme 4– 6 inaonyesha jinsi tunavyobarikiwa tunapomfuata nabii hai?

Unapojiandaa kufundisha kuhusu baraka ambayo huja kutokana na kumfuata nabii hai, fikiria kuhusu changamoto ambazo vijana wanakabiliana nazo. Ni kwa jinsi gani kumfuata nabii huwasaidia na changamoto hizi? Unaweza pia kusoma ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Nabii wa Mungu” (Liahona, Mei 2018, 24–27) au ujumbe wa Mzee L. Whitney Clayton “Lolote Atakalowaambia, Fanyeni” (Liahona, Mei 2017, 97–99).

darasa la wavulana

Kumfuata nabii kunaweza kuwasaidia vijana na changamoto wanazokabiliana nazo.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanzisha mjadala, ungeweza kuomba kila mmoja wa washiriki wa darasa au akidi (au vikundi vidogo) kupitia tena mojawapo ya matukio yafuatayo: 2 Wafalme 4:1–7; 5:6–14; 6:8, 13–17. Waombe kutafuta kitu fulani ambacho kinawavutia kusoma na kufuata mafundisho ya manabii na mitume wa leo. Baada ya kila kikundi kushiriki kitu fulani walichopata, unaweza kuwaomba vijana wachache kukamilisha sentensi hii: “Ninapowafuata manabii na mitume hai, mimi …” Ili kuendeleza kujadiliana kuhusu kuwafuata manabii, chagua wazo moja au zaidi kati ya yafuatayo.

  • Kwa sababu manabii hai wanapatikana tu katika Kanisa la Bwana la urejesho, washiriki wa darasa lako au akidi wanaweza kupata fursa za kujibu maswali kuhusu manabii hai. Unaweza kuandika ubaoni maswali yafuatayo ambayo watu wanaweza kuwa nayo kuhusu nabii hai: Kwa nini mna nabii? Nabii huchaguliwa vipi? Unajuaje kwamba nabii kwa kweli huzungumza kwa naiba ya Mungu? Vijana wanaweza kutafuta majibu ya maswali haya katika nyenzo chini ya “Nyenzo Saidizi.” Wanaweza kufanya mazoezi ya kujibu maswali haya na mengine waliyonayo wakitumia kweli wanazozipata na mawazo na uzoefu wao wenyewe.

  • Ni kwa jinsi gani maneno ya nabii wetu hai yanaweza kutusaidia tunapokabiliana na changamoto binafsi? Ili kuwasaidia vijana kujibu swali hili, ungeweza kuwaalika kuorodhesha ubaoni baadhi ya ushauri na mialiko nabii aliyoitoa katika mkutano mkuu wa hivi karibuni. Tumefanya nini kutenda juu ya ushauri na mialiko yake? Ni mabadiliko gani tumeyaona katika maisha yetu kwa sababu ya juhudi hizi? Unaweza kumwalika mtu kushiriki uzoefu binafsi ambao kwao ushauri wa nabii ulimsaidia katika changamoto binafsi.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba kumfuata nabii kutawasaidia kusogea karibu na Mwokozi? Njia moja ingekuwa ni kumpa kila mmoja kadi ndogo na kuwaalika kusoma sehemu ya ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Nabii wa Mungu.” Wanaweza kuandika upande mmoja wa kadi kitu walichojifunza kuhusu jinsi nabii anavyoweza kuwasaidia kusogea karibu na Kristo. Upande mwingine wa kadi, wangeweza kuandika kitu kinachowavutia kufanya kumfuata nabii. Waalike kushiriki kile walichoandika.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

  • Gary E. Stevenson, “Moyo wa Nabii,” Liahona, Mei 2018, 17–20 (Nabii huchaguliwa vipi)

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Uongofu wa kweli unahusisha zaidi ya kuhisi Roho tu akithibitisha ukweli katika nafsi zetu; ni lazima pia tuzifanyie kazi kweli hizo. Zaidi ya kuwasaidia wanaojifunza kuhisi na kumtambua Roho, wasaidie kutenda juu ya ushawishi wanaoupokea” (Kufundisha katika njia ya mwokozi 10).