Agano la Kale 2022
Julai 24. Ni Baraka Gani Zinazokuja Kutokana na Kupokea Ibada za Hekaluni? Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8


“Julai 24. Ni Baraka Gani Zinazokuja Kutokana na Kupokea Ibada za Hekaluni? Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Julai 24. Ni Baraka Gani Zinazokuja Kutokana na Kupokea Ibada za Hekaluni? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
hekalu

Julai 24

Ni Baraka Gani Zinazokuja Kutokana na Kupokea Ibada za Hekaluni?

Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayopitia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia tekinolojia kama chombo cha kushiriki injili?

  • Unganisha familia milele. Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja kwa Kristo?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Wakati Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni katika Babeli, walikuta Yerusalemu na hekalu lake likiwa magofu (ona 2 Wafalme 25:1–10; 2 Mambo ya Nyakati 36:17–19). Watu walitamani sana kujenga upya hekalu. Kwa hiyo, katika muda mchache, walianza mchakato wa kujenga upya na kufuahia wakati hekalu lilipomalizika (ona Ezra 3:8–13; 6:16–22). Leo, kama watu wa agano wa Mungu, sisi pia tunajenga mahekalu na kufurahia wakati hekalu jipya linapojengwa. Kwa nini? Kwa sababu ibada za hekaluni huongoza kwa baraka kuu za Baba wa Mbinguni. Zinaleta uwezo wa kiroho. Zinatupa mwelekeo Na zinatusaidia kuwa kama Mungu na kupokea yale yote Yeye aliyonayo. Ona Mafundisho na Maagano 84:19–22; 109:22–26.

Ni kwa jinsi gani utawasaidia vijana kutamani hekalu kama Waisraeli walivyofanya? Ni kwa jinsi gani utawasaidia wao kutamani kwa mioyo yao yote kufanya maagano na Mungu katika nyumba Yake takatifu. Unapojiandaa kufundisha, fikiria kupitia tena ujumbe wa Thomas S. Monson “Baraka za Hekalu” (Liahona, Mei 2015, 91–93) na katika makala “Kwa Nini Ibada na Maagano ya Maana” katika temples.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
vijana nje ya hekalu

Ibada za hekaluni zinatusaidia kuwa kama Mungu na kupokea yale yote Yeye aliyonayo.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kutazamia baraka wanazoweza kupokea kutokana na ibada za hekaluni, ungeweza kuwaalika wapitie tena Ezra 3:10–13; 6:16, 21–22. Waombe washiriki maneno au virai vinavyoonyesha jinsi Wayahudi wa kale walihisi kuhusu kulijenga upya hekalu lao. Kwa nini ujenzi wa hekalu ni kitu cha kusherehekea? Ni kwa jinsi gani mahekalu yetu leo na kazi tunazofanya huko hutusaidia kuwa karibu na Mwokozi? Hapa kuna baadhi ya mawazo ya kuwasaidia vijana kuelewa baraka wanazoweza kupokea hekaluni.

  • Wakati Joseph Smith alipoweka wakfu Hekalu la Kirtland, alitoa maombi ya kuweka wakfu yanayopatikana katika Mafundisho na Maagano 109. Maombi haya yanaelezea baraka nyingi tunazoweza kupokea kupitia ibada za hekaluni? Washiriki wa darasa au akidi wanaweza kupekua sehemu za maombi haya, hasa mstari wa 12–26, wakitafuta baraka ambazo Joseph Smith aliziombea. Wanaweza kuorodhesha baraka hizi ubaoni. Unaweza kuwaomba vijana kujadili jinsi kila moja ya hizi baraka inaweza kuwaimarisha wao sasa na siku za usoni. Shiriki ushuhuda wako juu ya baraka ambazo umezipokea kupitia ibada za hekaluni.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kushiriki hisia zao kuhusu hekalu, waombe kukamilisha sentensi hii: “Ninapofikiria kuhusu hekalu, ninahisi …” Unaweza kuwaalika wao kusoma aya tano za kwanza za ujumbe wa Mzee Kent F. Richards “Nguvu za Uungu” (Liahona, Mei 2016, 118–20). Kwa nini tunahitaji hekalu zaidi ya kitu chochote kingine? Tunajifunza nini kuhusu nguvu za Mwokozi anazotupatia kupitia ibada za hekaluni? Vijana wanaweza kisha kupekua ujumbe wa Mzee Richards, wakitafuta baraka ambazo zinakuja kwetu tunaposhiriki katika ibada za hekaluni. Au wanaweza kutafuta baraka hizi katika ujumbe wa Rais Thomas S. Monson “Baraka za Hekalu.”

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kutafakari juu ya dhabihu ambazo wengi wako radhi kufanya ili kupokea baraka za hekaluni, unaweza kuonyesha video “Temples Are a Beacon” (ChurchofJesusChrist.org). Kwa nini familia ya Mou Tham walikuwa radhi kufanya dhabihu kubwa kiasi hicho ili kwenda hekaluni? (Ona pia Rais Thomas S. Monson, “Hakelu Takatifu—Mnara kwa Ulimwengu,” Liahona, Mei 2011, 90–94.) Ni dhabihu gani tunahitaji kufanya ili kupokea baraka za hekaluni? Labda mtu ambaye aliyekuwa hekaluni hivi karibuni anaweza kujiunga na mkutano na kushiriki uzoefu wake. Unaweza kuwaalika vijana kupekua ujumbe wa Mzee Ronald A. Rasband “Kujikabithi kwa Bwana” (Liahona, Nov. 2020, 22–25) na kushiriki baraka za kuwa na kibali cha hekaluni. Mnaweza pia kupitia tena maswali ya kibali cha hekaluni pamoja (ona Russell M. Nelson, “Maneno ya Kufunga,” Liahona, Nov. 2019, 120–22).

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Unapofundisha, badala ya kupashana taarifa tu, wasaidie vijana kugundua kweli za injili wao wenyewe katika maandiko na maneno ya manabii” (Kufundisha katika Nija ya Mwokozi, 28).

Chapisha