Nguvu ya Uchajimungu
Kila hekalu la Mungu ni nyumba ya tukufu na takatifu ya Mungu, na ndani yake kila mmoja wetu anaweza kujifunza na kujua nguvu za ucha Mungu.
Miezi michache tu kabla ya kifo cha Nabii Joseph Smith, alikutana na wale Kumi na Wawili kuzungumza kuhusu mahitaji makubwa ambayo Kanisa lilikuwa linakabiliwa nayo katika wakati ule mgumu. Aliwaambia, “Tunahitaji hekalu zaidi ya kitu kingine chochote.”1 Kwa hakika, hivi leo katika nyakati hizi za majaribu, kila mmoja wetu na familia zetu tunahitaji hekalu zaidi ya kitu kingine chochote.
Wakati wa kuweka wakfu hekalu hivi majuzi, nilisisimshwa na tukio lote zima. Nilipenda ufunguzi wa hekalu, kuwaamkia wageni wengi waliokuja kuona hekalu; sherehe za kitamaduni pamoja na uchangamfu na msisimko wa vijana, ikifuatiwa na vikao vya ajabu vya uwekaji wakfu. Roho mzuri alitanda. Watu wengi walibarikiwa. Na kisha asubuhi iliyofuata, mke wangu nami tuliingia katika birika ya ubatizo kushiriki katika ubatizo kwa niaba ya baadhi ya mababu zetu. Nilipoinua mkono wangu kuanza ibada, nilikuwa karibu nizidiwe na nguvu za Roho. Nikatambua tena kwamba nguvu halisi za hekalu ziko katika ibada.
Kama Bwana alivyofunua, ukamilifu wa ukuhani wa Melkizediki unapatikana katika hekalu na ibada zake, “kwani ndani yake funguo za ukuhani mtakatifu zimewekwa, ili mpate kupokea heshima na utukufu.”2 “Kwa hiyo, katika ibada hizo, nguvu za uchajimungu hudhihirika.”3 Ahadi hii ni kwa ajili yako na kwa ajili ya familia yako.
Jukumu letu ni “kupokea” kile ambacho Baba yetu anatoa4 “Kwani yule apokeaye atazidishiwa tele, hata uwezo.”5 uwezo wa kupokea yote ambayo Yeye anaweza na atatupatia—sasa na milele;6 uwezo wa kuwa wana na mabinti wa Mungu,7 kujua “nguvu za mbinguni,”8 kunena katika jina Lake,9 na kupokea “nguvu za Roho Yake.”10 Hizi nguvu zinapatikana kibinafsi kwa kila mmoja wetu kupitia ibada na maagano ya hekalu.
Nefi aliona siku yetu katika ono lake kuu: Mimi Nefi, niliona nguvu za mwana kondoo wa Mungu, kwamba ziliwashukia watakatifu wa kanisa la mwanakondoo, na kwa watu wa agano wa Bwana, ambao walitawanyika kote usoni mwa dunia; na walikuwa wamejikinga kwa utakatifu na kwa nguvu za Mungu katika utukufu mkuu..”11
Nilipata fursa hivi majuzi ya kuwa kwenye ufunguzi wa hekalu pamoja na Rais Russell M. Nelson na familia yake alipokuwa anawakusanya kuzunguka madhabahu ya kuunganisha na akawaeleza kwamba kila kitu tunachofanya ndani ya Kanisa—kila mkutano, shughuli, somo, na huduma—ni kumtayarisha kila mmoja wetu kuja hekaluni na kupiga magoti kwenye madhabahu kupokea baraka zote Baba alizotuahidi milele na milele.12
Tunapohisi baraka za hekaluni katika maisha yetu, mioyo yetu hugeukia familia zetu, wote walio hai na wafu.
Hivi majuzi, nilishuhudia familia ya uzao wa tatu wakishiriki katika ubatizo pamoja kwa niaba ya mababu zao. Hata bibi alishiriki—ingawa alikuwa na hofu kiasi kuhusu kwenda chini ya maji mwenyewe. Wakati alipoibuka kutoka kwenye maji na kumkumbatia mumewe, alikuwa na machozi ya furaha. Babu na Baba kisha walibatizana wao kwa wao na wengi wa wajukuu. Ni furaha kubwa jinsi gani familia inaweza kupata uzoefu pamoja? Kila hekalu lina kipaumbele cha muda maalumu kwa familia kuwaruhusu ninyi kama familia kupanga muda kwenye sehemu ya kubatizia.
Muda mfupi kabla ya kifo chake, Rais Joseph F. Smith alipokea maono ya ukombozi wa wafu. Alifundisha kwamba wale walio kwenye ulimwengu wa kiroho wanategemea kikamilifu juu ya ibada ambazo tunapokea kwa niaba yao. Maandiko yanasema, “Wafu wanaotubu watakombolewa, kwa njia ya utii kwa ibada za nyumba ya Mungu.”13 Tunapokea ibada kwa niaba yao, lakini wanafanya na wanawajibika kwa kila agano lililohusika na kila ibada. Kwa hakika, pazia ni nyembamba kwetu sisi na sehemu kamilifu kwao katika hekalu.
Nini basi ni majukumu yetu binafsi kushiriki katika kazi hii, kama wateja na kama wafanyakazi? Nabii Joseph Smith aliwafundisha watakatifu katika mwaka 1840 kwamba “Juhudi kubwa lazima ifanywe, na dhamira itahitajika—na hivyo kazi [ya kujenga hekalu] lazima iharakishwe katika uadilifu, hamna budi watakatifu kuwekea uzito umuhimu wa vitu hivi, katika akili zao, … na kisha kuchukua hatua hizo kama za lazima kuwapeleka kwenye kufanya kazi; na kujiandaa wenyewe kwa ujasiri, kuamua kufanya yote wanayoweza, na kujisikia wenyewe hivyo kupendezewa kama vile kazi yote iliwategemea wao peke yao.14
Katika kitabu cha Ufunuo tunasoma:
“Je watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Nao wanakwenda wapi?
“… Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwanakondoo.
“Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake: na yeye aketie katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.”15
Hamwezi kuona tu katika macho ya akili zenu wale wanaohudumu hekaluni leo?
Ni zaidi ya wafanya kazi wa ibada 120,000 katika mahekalu 150 yanayofanya kazi ulimwenguni kote. Bado kuna nafasi kwa hata wengi kuwa na uzoefu huu mzuri. Wakati Rais Gordon B. Hinckley alipotangaza wazo la mahekalu madogo mengi ulimwenguni kote, alifundisha kwamba “wafanya kazi wote wa ibada watakuwa watu wa pale pale ambao watahudumu katika nafasi zao katika kata zao na vigingi vyao.”16 Kwa kawaida, wafanya kazi huitwa kuhudumu kwa miaka miwili hadi mitatu, kukiwa na uwezekano wa kuongeza muda. Haikusudiwi kwamba mara unapoitwa, utakaa ilimradi una uwezo. Wengi wa wafanya kazi waliohudumu kwa muda mrefu wanaondoka na upendo wao kwa hekalu pamoja nao wakati wanapopumzishwa ili kuwapa nafasi wengine, wafanyakazi wapya wahudumu.
Ni karibu miaka 100 iliyopita, Mtume John A. Widtsoe alifundisha: “Tunahitaji wafanyakazi zaidi kukamilisha [hii] kazi ya ajabu. …Tunahitaji waumini wengi kwenye kazi ya hekalu, wakichukuliwa kutoka rika zote. … Muda umefika, … katika huu mwendo mpya wa hekalu kuwaleta kwenye huduma hai watu wote, wa rika zote. … Kazi ya hekaluni ni … ya kunufaisha sana kwa vijana na watendaji, kama ilivyo kwa wazee, walioacha nyuma yao mizigo mingi ya maisha. Kijana anahitaji sehemu yake katika hekalu hata zaidi ya baba yake na babu yake, walioimarika na uzoefu wa maisha; na msichana ambaye ndio kwanza anaanza maisha, anahitaji roho, ushawishi na mwelekeo ambao unakuja kutoka ushiriki katika ibada za hekaluni.”17
Katika mahekalu mengi, marais wa mahekalu wanawakaribisha wamisionari wapya na wale ambao wameshapata endaumenti, vijana, kuhudumia kwa muda mfupi tu kama wafanyakazi wa ibada kabla ya kwenda MTC. Vijana hawa hawabarikiwi tu kuhudumu, lakini “wanaongeza uzuri na roho kwa wote wanaohudumia katika hekalu.”18
Niliwauliza baadhi ya vijana ambao wamehudumu kabla na baada ya misheni zao kushiriki hisia zao Walitumia vishazi kama ifuatayo kuelezea uzoefu wao hekaluni:
Ninapohudumia hekaluni
-
Ninaguswa na “hisia ya kuwa karibu sana na Baba yangu na Mwokozi”;
-
Nilijihisi “amani kamili na furaha”;
-
Ninahisia ya “kuwa nyumbani”;
-
Ninapokea “utakatifu, nguvu, na uwezo”;
-
Ninahisi “umuhimu wa maagano yangu matakatifu”;
-
“Hekalu limekuwa sehemu yangu”;
-
“Wale ambao tunawahudumia wanakuwa karibu wakati wa ibada”;
-
“Inanipa mimi uwezo wa kushinda vishawishi”; na
-
“Hekalu limebadilisha maisha yangu milele.”19
Kuhudumu katika hekalu ni fahari na uzoefu wenye nguvu kwa watu wa rika zote. Hata baadhi ya wanandoa wapya wanahudumu pamoja. Rais Nelson amefundisha, “Huduma katika hekalu … ni shughuli tukufu ya familia.”20 Kama wafanyakazi wa ibada, zaidi ya kupokea ibada kwa mababu zenu, mnaweza pia kuongoza ibada kwa ajili yao.
Kama Wilford Woodruff alivyosema:
“Ni wito gani mkuu mwanaume yoyote [au mwanamke] anaweza kuwa nao usoni mwa dunia kama kushika mikononi mwake uwezo na mamlaka kwenda mbele na kusimamia katika ibada za wokovu? …
“… Unakuwa chombo katika mikono ya Mungu katika wokovu wa roho ile. Hakuna kitu walichopewa binadamu ambacho ni sawa na hicho.”21
Pia Alisema:
“Minong’ono mitamu ya Roho Mtakatifu utapawa na tunu za mbinguni, ushirika wa malaika, utaongekeza mara kwa mara.”22
“Hii inastahili kwenu nyote ama ninaweza kujitolea katika [kipindi] cha miaka michache tunayohitajika kutumia hapa duniani.”23
Rais Thomas S. Monson hivi majuzi alitukumbusha kwamba “baraka za hekaluni ni za gharama kubwa sana.”24 “Hakuna dhabihu iliyo kubwa sana.”25
Njooni hekaluni. Njooni kila mara. Njooni pamoja na kwa ajili ya familia yako. Njooni na muwasaidie wengine waje pia.
“Hawa ni nani waliovikwa mavazi meupe?” Ndugu na dada zangu, ninyi ndiyo wale—ninyi ambao mmepokea ibada za hekaluni, ambao mmeweka maagano yenu hata kwa dhabihu; ninyi mnaosaidia familia zenu kupata baraka za huduma ya hekaluni na mliowasaidia wengine wakati wote. Asanteni kwa huduma zenu. Ninashuhudia kwamba kila hekalu ni nyumba takatifu ya Mungu, na kwamba ndani yake kila mmoja wetu tunaweza kujifunza na kujua nguvu ya uchaji mungu, katika jina la Yesu Kristo, amina.