Mimi ni Mtoto wa Mungu
Ufahamu sahihi wa urithi wetu wa mbinguni ni muhimu kwa kuinuliwa.
Mafundisho yetu ya kimsingi kabisa hujumuisha ufahamu kwamba sisi ni watoto wa Mungu aliye hai. Hiyo ndio sababu moja ya majina Yake matakatifu zaidi ni Baba—Baba wa Mbinguni. Fundisho hili limefundishwa wazi na manabii kwa miaka:
-
Wakati alipojaribiwa na Shetani, Musa alimkemea, akisema: “Wewe ni nani? Kwa maana, tazama, mimi ni mwana wa Mungu.”1
-
Akizungumza na Israeli, Mtunga Zaburi alitangaza, “Wote nyinyi ni wana wa Aliye juu.”2
-
Paulo aliwafundisha Waathene juu ya mlima Mar kwamba walikuwa “wazao wa Mungu.”3
-
Joseph Smith na Sidney Rigdon walipata maono ambayo waliona Baba na Mwana, na sauti ya mbinguni ikatangaza kwamba waliomo duniani “ni wana na mabinti wa Mungu.”4
-
Mwaka 1995, Mitume 15 na manabii wanaoishi walithibitisha: “Wanadamu wote … wameumbwa kwa mfano wa Mungu. Kila moja ni mwana au binti mpendwa wa wazazi wa mbinguni.”5
-
Rais Thomas S. Monson alishuhudia: “Sisi ni wana na mabinti wa Mungu aliye hai. … Hatuwezi kwa dhati kushikilia imani hii bila kupata uzoefu wa nguvu na uwezo mpya wenye maana sana.”6
Fundisho hili ni la kimsingi sana, linalotamkwa kila mara, rahisi kiasi kwamba linaweza kuonekana kuwa la kawaida, wakati katika hali halisi ni miongoni mwa maarifa ya ajabu zaidi tunazoweza kupata. Ufahamu sahihi wa urithi wetu wa mbinguni ni muhimu kwa kuinuliwa. Ni kitu cha kimsingi kufahamu mpango mtukufu wa wokovu na kwa kukuza imani katika Mzaliwa wa kwanza wa Baba, Yesu Kristo, na katika Upatanisho Wake wa huruma.7 Zaidi ya hayo, hutoa motisha daima kwetu sisi kufanya na kuweka maagano yetu muhimu ya milele.
Isipokuwa kwa wachache, kila mtu anayeshiriki katika mkutano huu anaweza sasa hivi, bila kuona mistari iliyoandikwa au muziki, kuimba, “I Am a Child of God.”8 Wimbo huu wa kupendeza ni mojawapo wa zile huimbwa mara nyingi katika Kanisa hili. Lakini swali muhimu ni “Je, kwa kweli tunajua?” Je, tunajua katika akili, katika mioyo yetu na nafsi zetu? Je, uzazi wetu wa mbinguni ni utambulisho wetu wa kwanza na wa maana zaidi?
Hapa duniani, tunajitambulisha kwa njia nyingi tofauti, ikiwemo mahali pa kuzaliwa kwetu, uraia wetu, na lugha yetu. Baadhi hata hujitambulisha kwa kazi zao au kitu wapendacho. Vitambulisho hivi vya kidunia si makosa isipokuwa vikizidi au kuhujumu utambulisho wetu wa milele—ule wa kuwa mwana au binti wa Mungu.
Wakati mtoto wetu mdogo alipokuwa na umri wa miaka sita na katika daraja la kwanza shuleni, mwalimu wake aliwapa watoto kazi ya kuandika darasani. Ilikuwa mwezi wa Oktoba, mwezi wa Halloween, likizo ambayo huzingatiwa katika baadhi ya maeneo ya dunia. Ingawa si likizo nipendayo, nadhani kunaweza kuwa na baadhi ya vipengele bora vya Halloween.
Mwalimu alitoa kipande cha karatasi kwa wanafunzi vijana. Upande wa juu kulikuwa ni picha iliyochorwa ya mchawi kisasili (niliwaambia hii haikuwa likizo yangu niipendayo) akisimama juu sufuria kubwa lililokuwa linachemka. Swali liliandikwa juu ya kurasa, ili kuhamasisha mawazo ya watoto na kutathmini ujuzi wao wa kuandika, ilikuwa “Sasa hivi umekunywa kikombe cha mvinyo wa mchawi. Ni nini kilichokutokea?” “Tafadhali jua kwamba kwamba hadithi hii haitolewi kama mapendekezo kwa walimu.
“Wewe tayari umekunywa kikombe cha mvinyo wa mchawi. Ni nini kilichokutokea? “Kwa maandishi yake bora ya mwanafunzi, kitoto chetu kiliandika, Nitapendezwa na huko. Ningekupenda kwa sababu ni mahali bora pa kuwa kwa sababu uko pamoja na Baba yako wa Mbinguni” Jibu hili pengine lilishangaza mwalimu wake; hata hivyo, wakati binti yetu alipoleta zoezi lililokamilika nyumbani, tulitambua kwamba alipewa nyota, daraja ya juu.
Katika maisha haya, tunakumbana na shida halisi, si za kufikirika. Kuna maumivu—ya kimwili, kihisia, na kiroho. Kuna kuvunjika moyo wakati hali ni tofauti sana na kile tulichotarajia. Kuna udhalimu wakati hatuonekani kustahili hali yetu. Kuna kukatishwa tamaa wakati yule tuliyemwamini anapotuangusha. Kuna vikwazo vya kiafya na vya kifedha ambavyo vinaweza kutukanganya. Kunaweza kuwa na nyakati ya wasiwasi wakati suala la mafundisho au la historia ni zaidi ya ufahamu wetu wa sasa.
Wakati mambo magumu yanapotokea katika maisha yetu, mjibizo wetu wa haraka ni upi? Je, ni kuchanganyikiwa au shaka au kuudhika kiroho? Je, ni pigo kwa imani yetu? Je, tunamlaumu Mungu au wengine kwa hali zetu? Au mjibizo wetu wa kwanza ni kukumbuka sisi ni kina nani—kwamba sisi ni watoto wa Mungu mwenye upendo? Je, hiyo ikijumuishwa pamoja na uaminifu kamili kwamba Yeye anaruhusu baadhi ya mateso ya kidunia kwa sababu Anajua yatatubariki, kama moto wa msafishaji, ili kuwa kama Yeye na kupata urithi wetu wa milele?9
Juzi nilikuwa katika mkutano na Mzee Jeffrey R. Holland. Katika kufundisha kanuni kwamba maisha ya duniani yanaweza kuwa machungu lakini matatizo yetu yana madhumuni ya milele—hata kama hatuielewi kwa wakati huo—Mzee Holland alisema, “Unaweza kupata unachotaka, au unaweza kupata kitu kizuri zaidi.”
Miezi mitano iliyopita, mke wangu, Diane, nami tulikwenda Afrika na Mzee na Dada David A. Bednar. Nchi ya sita na ya mwisho tuliotembelea ilikuwa ni Liberia. Liberia ni nchi bora yenye watu wazuri, yenye historia tele, lakini mambo hayajakuwa rahisi huko. Miongo kadhaa ya machafuko ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimezidifisha baa la umaskini. Juu ya hayo, ugonjwa wa kutisha wa Ebola umeuwa karibu watu 5,000 huko wakati wa mlipuko wa majuzi. Tulikuwa kundi la kwanza la Viongozi wa Kanisa kutoka nje ya eneo kutembelea Monrovia, mji mkuu, tangu Shirika la Afya Duniani kuitangaza kuwa ni salama kufanya hivyo baada ya janga la Ebola.
Katika Jumapili moja asubuhi yenye joto sana na unyevunyevu, tulisafiri hata kwenye kituo cha mkutano kilichokodiwa katikati mwa jiji. Kila kiti kilichopatikana kiliwekwa, jumla ya viti 3,500. Hesabu ya mwisho ya waliohudhuria ilikuwa 4100. Karibu wote waliokuja iliwabidi kusafiri kwa miguu au aina fulani ya usafiri duni wa umma; haikuwa rahisi kwa Watakatifu kukusanyika. Lakini walifika. Wengi walifika masaa kadhaa kabla ya wakati uliowekwa wa mkutano. Tulipokuwa tukiingia ukumbini, hali ya kiroho ilikuwa ajabu! Watakatifu walikuwa tayari kufundishwa.
Wakati mnenaji aliponukuu andiko, waumini wangeisema aya hiyo kwa sauti. Haikujalisha—ni andiko fupi au refu, mkutano mzima ulijibu kwa pamoja. Sasa, si lazima tupendekeza haya, lakini hakika ilikuwa ya kuvutia kwamba wangeweza kufanya hivyo. Na kwaya—ilikuwa ya nguvu. Na mkurugenzi wa kwaya mwenye shauku na kijana mwenye umri wa 14 kwenye kinanda, waumini waliimba kwa uhodari na nguvu.
Kisha Mzee Bednar akanena. Hii, bila shaka, ilikuwa ndio kilele cha kilichotarajiwa cha mkutano—kusikia Mtume akifundisha na kushuhudia. Hakika pamoja na mwelekeo wa kiroho, katikati mwa hotuba yake, Mzee Bednar alitua, na kusema, “Je, mnajua ‘How Firm a Foundation’?”
Ilionekana kuwa sauti 4100 zilinguruma kwa kujibu, “NDIO!”
Kisha akauliza, “Je, mnajua mstari wa 7?”
Tena kundi zima likajibu, “NDIO!”
Mpangilio wa wimbo wenye nguvu “How Firm a Foundation” unaoimbwa na Kwaya ya Mormon Tabernacle kwa miaka 10 iliyopita imejumuisha mstari wa 7, ambao haukuwa ukiimbwa sana hapo awali. Mzee Bednar alielekeza, “Hebu tuimbe mstari wa 1, 2, 3, na 7.”
Bila kusita, mkurugenzi wa kwaya aliruka juu na mwenye Ukuhani wa Haruni wa kucheza kinanda akaanza mara moja kucheza kwa nguvu mistari za utangulizi. Na kwa kiwango cha imani kuu ambayo sijawahi kuona mbeleni katika wimbo wa umati, tuliimba mstari wa 1, 2, na 3. Kisha nguvu ya sauti na uwezo wa kiroho uliinuliwa wakati sauti 4100 walipoimba mstari wa saba na kutangaza:
Nafsi iliyo kwa Yesu imeelekea kwa mapumziko
Sitaki, siwezi, kuasi kuenda kwa maadui zake;
Nafsi hiyo, hata kama kuzimu yote itajaribu kuitikisa,
Sitaweza, siwezi, Sitaweza, siwezi,
Sitaweza, siwezi, kutoroka kamwe!10
Katika mojawapo ya matukio ya ajabu zaidi ya kiroho ya maisha yangu, nilifundishwa somo la kushangaza siku hiyo. Tunaishi katika dunia ambayo inaweza kutufanya kusahau uhalisi wetu. Kadri tunavyozingirwa na mahangaiko mengi ndivyo ilivyo rahisi kudunisha, kisha kupuuza, na kisha kusahahu uhusiano wetu na Mungu. Watakatifu wa Liberia wana mali kidogo, na bado wanaonekana kuwa na kila kitu kiroho. Kile tulichoshuhudia siku hiyo Monrovia ilikuwa ni kundi la wana na mabinti wa Mungu—ambao walijua hilo!
Katika dunia ya leo, haijalishi tuliko na haijalishi hali zetu zilivyo, ni muhimu kwamba utambulisho wetu wa maana ni kuwa mtoto wa Mungu. Kujua hayo kutaruhusu imani yetu kushamiri, kutahamasisha toba yetu ya daima, na kutatoa nguvu ya kuwa “imara na kutokutingisika” katika safari yetu ya dunia.11 Katika jina la Yesu Kristo, amina.