Yeye Anatuomba Tuwe Mikono Yake
Huduma ya kweli ya kama Kristo haina choyo na imewalenga wengine.
“Pendaneni; kama nilivyowapenda.”1 Maneno haya, yaliimbwa na kwaya ya ajabu, yalizungumzwa na Yesu masaa kadhaa kabla ya dhabihu yake kuu ya upatanisho—dhabihu Mzee Jeffrey R. Holland aliyoelezea kama “Dhihirisho la hali ya juu ya upendo wa dhati ambao haujawahi kudhihirishwa katika historia ya dunia hii.2
Yesu hakutufundisha tu kupenda, bali pia aliishi kile alichokifundisha. Katika huduma Yake yote, Yesu akizunguka huku na huko akitenda kazi njema”3na “aliwaelekeza wote kufuata Mfano Wake.”4Alifundisha,“ Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”5
Rais Thomas S. Monson, ambaye ameelewa na kuishi onyo la upendo, alisema: “Ninaamini Mwokozi anatuambia kwamba tusipojipoteza wenyewe katika huduma, kuna maana ndogo katika maisha yetu wenyewe. Wale wanaoishi tu kwa ajili yao mwishowe hunyauka na … kupoteza maisha yao, huku wale wanaopoteza maisha yao katika huduma kwa wengine hukua na kunawiri—na kwa hakika kuokoa maisha yao.”6
Huduma ya kweli ya kama Kristo haina choyo na imewalenga wengine. Mwanamke mmoja ambaye alikuwa anamhudumia mume wake asiyejiweza alielezea, “Usiifikirie kazi yako kama mzigo, ifikirie kama fursa katika kujifunza kwamba upendo ni nini hasa.”7
Akinena katika Ibada BYU, Dada Sondra D. Heaston aliuliza: “Ingekuwaje kama tungeweza kuona yaliyomo kwenye kila mmoja wetu? Je tungeweza kuwaelewana vyema? Kwa kuhisi kile wanachokihisi, kuona kile wanachokiona, na kusikia kile wanachokisikia, je tungefanya, na kuchukua, muda kuwatumikia wengine, na je tungewatendea wengine tofauti? Je tungewatendea wengine kwa upendo zaidi, ukarimu zaidi, na kwa uvumilivu zaidi?”
Dada Heaston alituelezea uzoefu wake kutokana na kutumikia katika Kambi ya Wasichana. Alisema:
“Mmoja wa … wanenaji katika ibada … alitufundisha kuhusu ‘kuwa.’ Moja kati ya sentensi yake ilikuwa ni ‘Kuwa mmoja kati ya wale ambao hujitolea kujua na kuwatumikia wengine—tupilia mbali vioo na tazama kupitia dirishani.’
Kudhihirisha hili, alimuita mmoja katika ya wasichana na kumuomba msichana huyo kusimama akimuangalia. Baadaye akavuta kioo na kukiweka kati ya yule msichana na yeye mwenyewe ili kwamba yeye, [mnenaji], alikuwa anaangalia kwenye kioo wakati alipojaribu kuongea na msichana huyo. Haishangazi, haikuanza hata kuwa mazungumzo yenye kugusa au ya moyoni. Hili lilikuwa ni somo la nguvu ambalo lilidhihirisha jinsi ilivyo vigumu kuwasiliana na kuwatumikia wengine kama tunajishughulikia na kuona tu mahitaji yetu. Baadaye akakiweka pembeni kioo, akatoa fremu ya dirisha, na akakiweka kati yake na yule msichana …Tuliweza kuona kwamba yule msichana amekuwa ndio kiini na kwamba huduma ya kweli huhitaji kwamba tuangalie kwa karibu mahitaji na fikra za wengine. Wakati mwingine tunajihofia na kushughulikia maisha yetu ya kila siku—tunapojiangalia kwenye kioo wakati tunajaribu kutafuta fursa za kuhudumu—kwamba tusione bayana kupitia kwenye dirisha la huduma,”8
Mara kadhaa Rais Monson ametukumbusha kwamba “tumezungukwa na wale wanaohitaji usikivu wetu, hamasa yetu, msaada wetu, ukarimu wetu—iwe ni wanafamilia, marafiki, watu wa karibu, au wageni.” Alisema, “Sisi ni mikono ya Bwana hapa duniani, tukiwa na jukumu la kutumikia na kuwainua watoto Wake. Anatutegemea kila mmoja wetu.”9
Mwaka jana mnamo Januari, magazeti ya Friend na Liahona yaliwaalika watoto duniani kote kufuata ushauri wa Rais Monson—kuwa mikono ya Bwana. Watoto waliombwa kufanya matendo ya huduma—makubwa kwa madogo. Walitiwa moyo vile vile kuchora kufuatilia mikono yao kwenye karatasi, kuikata, na kuandika kwenye hiyo karatasi huduma waliyoifanya, na kuituma kwenye magazeti. Wengi wenu mnaonisikiliza usiku huu mnaweza kuwa kati ya maelfu ya watoto waliofanya huduma hii ya upendo na kuituma.10
Watoto wanapotambua jinsi ya kupenda na kutumikia wengine wangali wadogo, wanaweka mpangilio wa huduma katika maisha yao yote. Mara nyingi watoto hutufundisha kwamba kuonyesha upendo na huduma haitakiwi kuwa kwa njia kubwa ili iwe na maana na kufanya utofauti.
Mwalimu wa Msingi alifundisha mfano ufuatao. “Leo,” alisema, ‘darasa letu la watoto wa miaka mitano na sita wametengeza mikufu ya upendo. Kila mtoto alichora picha katika kipande cha karatasi: moja yao wenyewe, ya Yesu, na baadhi ya wanafamilia na wale wanaowapenda. Tumegundisha vipande hivyo katika mzunguko ambao unajirudia kuwapitia wote na kutengeneza mnyororo ambao tumeugeuza kuwa mkufu wa upendo. Walipokuwa wanachora, watoto walizungumzia kuhusu familia zao.
“Heather alisema, ‘Sifikirii kama dada yangu ananipenda. Kila mara tunagombana. … mpaka najichukia. Nina maisha mabaya.’ Na anakiweka kichwa chake mikononi mwake.
“Nilifikiria kuhusu mazingira ya familia yake na kuhisi kwamba labda alikuwa na ugumu wa maisha. Lakini baada ya Heather kusema hivi, Anna, aliyekuwa upande mwingine wa meza, alijibu, ‘Heather, ninakuweka kwenye mkufu wangu kati yangu mimi na Yesu kwa sababu anakupenda na mimi nakupenda.’
“Anna aliposema hivyo, Heather alitambaa chini ya meza kumwelekea Anna na kumkumbatia.
“Mwishoni mwa darasa, bibi yake alipokuja kumchukua, Heather alisema, ‘Wajua, Bibi? Yesu ananipenda.”
Tunapojitolea katika upendo na huduma hata katika njia ndogo, mioyo inabadilishwa na kulainishwa wakati wengine wakihisi upendo wa Bwana.
Wakati mwingine, hata hivyo, kwa sababu ya idadi ya watu isiyohesabika ambao wanahitaji msaada na nafuu kutokana na mizigo yao, inaweza kuwa vigumu kuyafikia mahitaji mengi ya muhimu.
Akina dada, baadhi yenu mnaosikiliza mnaweza kufikiria kuwa mmesukumwa kushinda kiasi katika kusaidia katika mahitaji ya wanafamilia. Kumbuka, katika shughuli hizo za kila siku ambazo mara nyingi ni za kuchosha, mko “katika huduma ya Mungu.”11
Wengine wenu mnaweza kuhisi utupu ambao unaweza kujazwa unapoangalia ujirani wako au jamii kwa ajili ya fursa kusaidia kupunguza mizigo ya wengine.
Sote tunaweza kujumuisha baadhi ya huduma katika maisha yetu. Tunaishi katika dunia yenye ugomvi Tunatoa huduma bila kukosoa, tunapokataa kusengenya, tunakataa kuhukumu, tunapotabasamu, tunaposema asante, tunapokuwa na subira na wenye upole.
Aina nyingine za huduma huchukua muda, mipangilio yenye dhumuni, na nguvu za ziada. Lakini zinastahili kila juhudi yetu. Labda tuanze kwa kujiuliza maswali haya:
-
Nani yupo kwenye mzunguko wa ushawishi ambaye ninaweza kumsaidia leo?
-
Je nina muda na nyenzo gani?
-
Ni kwa njia gani ninaweza kutumia talanta zangu na uzoefu katika kuwabariki wengine?
-
Tunaweza kufanya nini kama wanafamilia?
Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:
“Lazima ufanye … kile wafuasi wa Kristo wamefanya katika wakati wote: shaurianeni pamoja, tumieni kila zana inayopatikana, tafuteni mwongozo wa Roho Mtakatifu, mwombe Mungu uthibitisho Wake, na kunjeni mashati yenu na enendeni mkafanye kazi.
“Ninawaahidi,” alisema, “Kama utafuata mpangilio huu, utapokea mwongozo maalumu kama vile nani, nini, lini, na wapi pa kutoa kwa njia ya Bwana.”12
Kila nikistajaabu itakavyokuwa wakati Mwokozi atakaporudi tena, nafikiria matembezi Yake kwa Wanefi aliposema:
“Mnao wowote ambao ni wagonjwa miongoni mwenu? Waleteni hapa. Mnao wowote ambao ni viwete, au vipofu, au wa kupooza, au vilema, au ukoma, au walionyauka au ni viziwi, au ambao wameteseka kwa njia yoyote? Waleteni hapa na nitawaponya, kwani ninayo huruma juu yenu; matumbo yangu yamejaa huruma. …
“… [Mwokozi] aliwaponya wote.”13
Kwa sasa, Anatuomba tuwe mikono Yake.
Nimekuja kugundua kwamba ni upendo wa Mungu na jirani ambao hutupa maana ya maisha. Na tufuate mfano wa Mwokozi na maonyo Yake na kuwafikia wengine kwa upendo.
Nashuhudia katika ukweli wa ahadi ya Rais Henry B. Eyring “kwamba kama tutatumia karama zetu kuwatumikia wengine, [tutahisi] upendo wa Bwana kwa ajili ya mtu yule. Vile vile tutahisi upendo Wake kwetu.14Katika Jina la Yesu Kristo, amina.
Maelezo: Mnamo Aprili 2, 2016, Dada Esplin alipumzishwa kama mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Msingi.