“Yoyote Atakayewapokea, Ananipokea Mimi”
Tunahitaji kuwafikia vijana wale waohisi kuwa wapweke, walioachwa nyuma, au wako nje ya ua.
Mungu anawapenda watoto. Anawapenda watoto wote. Mwokozi alisema, Ruhusu watoto wadogo …Waje kwangu: kwani hao ni ufalme wa mbinguni.”1
Watoto leo wanajikuta katika familia nyingi tofauti na zenye mipangilio changamani.
Kwa mfano, leo, kuna watoto maradufu katika Marekani wanaoishi na mzazi mmoja kuliko ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.2 Na kuna familia nyingi ambazo hazijaungana katika upendo wa Mungu na zilizotayari kushika amri Zake.
Katika hii vurugu inayoongezeka kiroho, injili ya urejesho itaendelea kubeba kiwango, kilicho bora, mpangilio wa Bwana.
“Watoto wamepewa haki ya kuzaliwa ndani ya mapatano ya ndoa, na kulewa na baba na mama wanaoheshimu kiapo cha ndoa kwa uadilifu kamili. …
“Mume na mke wana jukumu la dhati kupenda na kujaliana na kwa watoto wao. … Wazazi wana kazi takatifu ya kulea watoto wao katika upendo na haki, kuwapa mahitaji yao ya kimwili na kiroho, na kuwafundisha kupendana na kuhudumiana wao kwa wao [na] kutii amri za Mungu.”3
Tunawatambua wazazi wengi wazuri wa imani zote ulimwenguni kote ambao kwa upendo wanawajali watoto wao. Na kwa shukrani tunatambua familia katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho zilizokumbatiwa katika uangalizi wa baba na mama walioongolewa kwa Mwokozi, ambao wameunganishwa na mamlaka ya ukuhani, na wanaojifunza katika upendo wa kifamilia na kumwamini Baba yao wa Mbinguni na Mwanawe,Yesu Kristo.
Lakini ombi langu leo ni kwa mamia na maelfu ya watoto, vijana wadogo, na vijana wakubwa ambao hawatoki kwenye familia kama hizo, kwa kukosa neno lifaalo,” mfano kamili wa familia.” Sizungumzii tu kuhusu vijana waliopata tukio la kifo, talaka, au kufifia kwa imani ya wazazi wao, lakini pia na makumi ya maelfu ya wavulana na wasichana ulimwenguni kote wanaokumbatia injili bila mama au baba wa kuja Kanisani pamoja nao.4
Hawa vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaingia Kanisani kwa imani kubwa. Wanatumaini kuanzisha familia kamili katika maisha yao wenyewe siku za usoni.5 Katika muda ufaao, wanakuwa sehemu muhimu ya kikosi chetu cha umisionari, vijana wetu wazima wenye haki, na hao wanaopiga magoti kwenye madhabahu kuanza familia zao wenyewe.
Tutaendelea kufundisha mpangilio wa Bwana kwa familia, lakini sasa kwa waumini mamilioni, na hali kuwa anuwai tuliyonayo katika watoto wa Kanisa, tunahitaji kuwa makini zaidi na wepesi wa kuhisi. Utamaduni wetu wa Kanisa na lugha wakati mwingine ni wa kipekee kabisa. Watoto wa Msingi hawataacha kuimba “Families Can be Togather Forever,”6 lakini wakati wanapoimba, “Ninafurahi sana wakati baba anapokuja nyumbani.”7 au “pamoja na baba na mama wakiongoza njia,”8 sio watoto wote watakuwa wanaimba kuhusu familia zao.
Rafiki yetu Bette alishiriki uzoefu kanisani wakati alipokuwa na umri wa miaka 10: Alisema: “Mwalimu wetu alikuwa anashiriki somo kuhusu ndoa ya hekaluni. Aliniuliza hasa, ‘Bette, wazazi wako hawakuoana katika hekalu, ama sivyo?’ [Mwalimu wangu na darasa zima] walijua jibu.” Somo la mwalimu likafuata, na Bette alifikiria mabaya zaidi. Bette alisema, “Nilikuwa na jioni nyingi za machozi. Wakati nilipopatwa na matatizo ya moyo miaka miwili baadaye na nikafikiri nilikuwa naenda kufa, nilipata hofu, nikifikiri ningekuwa peke yangu milele.”
Rafiki yangu Leif alihudhuria kanisani peke yake.” Wakati fulani akiwa katika Msingi, aliombwa kutoa mahubiri mafupi. Alikuwa hana mama au baba kanisani kusimama kando yake na kumsaidia kama amesahau nini cha kusema. Leif aliogopa. Kuliko kujiaibisha mwenyewe, alikaa mbali na kanisa kwa miezi kadha.
“Yesu akaita mtoto mdogo, akamweka katikati yao …
“Na [akasema] ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi.”9
Watoto na vijana hawa wamebarikiwa na mioyo ya kuamini na karama kubwa za kiroho. Leif aliniambia,”Nilijua kwenye kina katika maficho ya akili zangu kwamba Mungu alikuwa Baba yangu na kwamba alinijua na kunipenda.”
Rafiki yetu Veronique alisema, “Nilipojifunza kanuni za injili na kujifunza Kitabu cha Mormoni, ilikuwa kama nilikuwa nakumbuka vitu ambavyo nilikuwa tayari nimeshajua lakini nilikuwa nimesahau.”
Rafiki yetu Zuleika anatoka Alegrete, Brazil. Ingawa familia yake haikuwa ya kidini, katika umri wa miaka12, Zuleika alianza kusoma Biblia na kutembelea makanisa ya palepale, akitafuta kujua zaidi kuhusu Mungu. Na kwa kutotaka kutoa ruhusa kwa wazazi wake, alijifunza na wamisonari, akapata ushuhuda, na alibatizwa. Zuleika aliniambia: “Wakati wa mazungumzo, nilionyeshwa picha ya Hekalu la Salt Lake na kuambiwa kuhusu ibada ya kufunganisha. Kutoka wakati huo, nilitamani siku moja niingie katika nyumba ya Bwana na kuwa na familia ya milele.”
Huku hali ya kidunia ya mtoto inaweza isiwe kamili, DNA ya kiroho ni kamili, kwa sababu utambulisho wa kweli wa mtu ni sawa na mwana au binti wa Mungu.
Rais Thomas S. Monson alifundisha: “Wasaidie watoto wa Mungu kuelewa ni kipi cha kweli na muhimu katika maisha haya. Wasaidie kujenga uwezo wa kuchagua njia ambazo zitawaweka salama kwenye njia ya maisha ya milele,”10 Na tuifungue mikono na mioyo yetu kwa upana zaidi. Vijana hawa wanahitaji muda wetu na shuhuda zetu.
Brandon, aliyejiunga na Kanisa Colorado akiwa katika shule ya upili, alizungumza nami kuhusu wale waliomfikia kabla na baada ya ubatizo wake. Alisema: “Nilikuwa majumbani mwa familia ambazo ziliishi injili. Ilinionyesha kiwango ambacho nilihisi ningeweza kuwa nacho katika familia yangu.”
Veronique, aliyezaliwa Netherlands, alisomea katika shule moja na binti yetu Kristen wakati tulipoishi Ujerumani. Veronique alisema: “Wanafunzi ambao walikuwa waumini wa Kanisa walikuwa na nuru iliyowazunguka. Nilikuja kugundua kwamba nuru ilikuja kutoka kwenye imani yao katika Yesu Kristo na kuishi mafundisho Yake.”
Rafiki yangu Max alibatizwa akiwa na umri wa miaka 8. Baba yake hakuwa muumini wa kanisa lolote, na Max angeweza kwenda kanisani au kutokwenda.
Kama kijana, baada ya kutohudhuria kwa miezi kadha, Max akawa na hisia kwamba alihitaji kurudi Kanisani na akaamua Jumapili moja atarudi. Lakini uamuzi wake ukafifia alipokuwa anakaribia mlango wa mbele wa Kanisa, na akawa na hofu.
Pale, akisimama mlangoni, alikuwa askofu mpya. Max hakumjua, na alihisi kwa hakika askofu hakumjua Max. Wakati Max aliposonga mbele, uso wa askofu ulichangamka, na alinyoosha mkono wake na kusema, “Max, ni vizuri sana kukuona!”
“Wakati aliposema maneno hayo,” Max alisema, “ hisia ya kusisimua ilikuja juu yangu na nikajua nimefanya jambo sahihi.”11
Kujua jina la mtu kunaweza kuleta tofauti.
“Na [Yesu] aliamuru kwamba watoto wao wadogo wapelekwe [kwake]. …
“Na … Aliwachukua [wao] mmoja mmoja, na kuwabariki, na kuomba kwa Baba juu yao.
“Na wakati alipofanya hivi alilia.”12
Kwa maombi ya wazazi, vijana wengi wanaopenda injili wanasubiri kwa miaka kubatizwa.
Wazazi wa Emily walitalikiana wakati akiwa mtoto, na hakupata ruhusa kubatizwa mpaka alipokuwa na umri wa miaka 15. Rafiki yetu Emily anamzungumzia kwa shauku kiongozi wa Wasichana ambaye “daima alimfikia na kumsaidia kuimarisha ushuhuda [wake].”13
Colten na Preston ni vijana wanaoishi Utah. Wazazi wao wametalikiana, na hawajapata ruhusa kubatizwa. Hata kama hawawezi kupitisha sakramenti, wanaleta mkate kila wiki. Na hata kama hawawezi kuingia hekaluni kufanya ubatizo pamoja na vijana wakati kata yao inakwenda hekaluni, ndugu hawa wawili wanatafuta majina ya familia kwenye kituo cha historia ya familia karibu nao. Kivutio kikubwa kwenye kuwasaidia vijana wetu wahisi wanajumuisha ni vijana wengine wenye haki.
Ninahitimisha na mfano wa rafiki mpya, mtu fulani tuliyekutana wiki chache zilizopita wakati tukitembelea Misheni ya Zambia Lusaka.
Mzee Joseph Sengooba anatoka Uganda. Baba yake alikufa alipokuwa na umri wa miaka saba. Akiwa na umri wa miaka tisa, baada ya mama yake na jamaa kushindwa kumtunza, alikuwa peke yake. Akiwa na umri wa miaka12, alikutana na wamisionari na akabatizwa.
Joseph aliniambia kuhusu siku yake ya kwanza kanisani: “Baada ya mkutano wa sakramenti, nilifikiri ulikuwa muda wa kwenda nyumbani, lakini wamisionari walinitambulisha kwa Joshua Walusimbi. Joshua aliniambia kwamba angekuwa rafiki yangu, na alinipa Kitabu cha Nyimbo za Watoto ili nisiende darasa la Msingi mikono mitupu. Katika Msingi, Joshua aliweka kiti cha ziada karibu kabisa na yeye. Rais wa Msingi alinikaribisha mbele na akaomba darasa zima la msingi kuniimbia ‘Mimi mtoto wa Mungu.’ Nikajihisi mtu maalumu sana.
Rais wa tawi alimchukua Joseph kwa familia ya Pierre Mungoza, na huko kukawa nyumbani kwake kwa miaka minne iliyofuata.
Miaka minane baadaye wakati Mzee Joseph Sengooba alipoanza umisionari wake, kwa mshangao wake mkufunzi wake alikuwa Mzee Joshua Walusimbi, mvulana aliyemfanya kujihisi kukaribishwa vizuri kwenye siku yake ya kwanza kwenye Msingi. Na Rais wake wa misheni? Ni Rais Leif Erickson, mvulana mdogo aliyejitenga mbali na Msingi kwa sababu aliogopa kuhusu kutoa mahubiri. Mungu huwapenda watoto Wake.
Wakati Kathy nami tulipokuwa Afrika wiki chache zilizopita, tulitembelea Mubji-Mayi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa sababu jengo la kanisa halikuwa kubwa kutosha waumini 2,000, tulikutana nje chini ya turubai kubwa la plastiki lililoshikiliwa na nguzo za mianzi Wakati mkutano ulipoanza tuliweza kuona madazeni ya watoto wakituangalia, wakining’inia kwenye nguzo nje ya ua wa fito za chuma ambao ulizunguka uwanja. Kathy alinong’ona kimya kimya, “Neil, unafikiri kwamba ungependa kuwaalika watoto waingie?” Nilimsogelea Rais wa Wilaya Kalonji kwenye jukwaa na kumuuliza kama angewakaribisha watoto walio nje ya ua waje wajumuike nasi.
Kwa mshangao wangu, kwa mwaliko wa Rais Kalonji, watoto hawakuja tu bali walikuja wakikimbia—zaidi ya 50, labda 100—baadhi na nguo zilizochanika na miguu pekupeku lakini wote wenye tabasamu nzuri na nyuso za furaha.
Nilisisimka sana na tukio hili na nikaliona kama ishara ya mahitaji yetu kuwafikia vijana wanaojihisi wako peke yao, wameachwa nyuma, au nje ya ua. Na tufikirie kuhusu hao, tuwakaribishe, tuwakumbatie, na kufanya kila kitu tunachoweza kufanya ili kuimarisha upendo wao kwa Mwokozi. Yesu alisema, “Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja … kama huyu kwa jina langu anipokea mimi.”14 Katika jina la Yesu Kristo, amina.