Daima Kuhifadhi Msamaha wa Dhambi
Na kwa nguvu ya utakaso ya Roho Mtakatifu kama mwenza wetu wakati wote, tunaweza daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu.
Kishazi chenye maana sana kilichotumiwa na Mfalme Benjamini katika mafundisho yake kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake kimekuwa mada inayojirudia ya mafunzo yangu na tafakari kwa miaka mingi.
Katika mahubiri yake ya kusisimua kiroho ya kuagana na watu aliowahudumia na kuwapenda, Mfalme Benjamini alielezea umuhimu wa kujua utukufu wa Mungu na kuonja upendo Wake, wa kupokea msamaha wa dhambi, siku zote kukumbuka ukuu wa Mungu, na kusali kila siku na kusimama thabiti katika imani.1 Aliahidi pia kwamba kwa kufanya vitu hivi, “mtapokea furaha daima, na kujazwa na upendo wa Mungu, na daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zenu.”2
Ujumbe wangu unalenga kwenye kanuni ya daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu. Ukweli unaoelezwa katika kishazi hiki unaweza kuimarisha imani yetu katika Bwana Yesu Kristo na kuongeza ufuasi wetu. Ninaomba Roho Mtakatifu atatupa maongozi na kutuadilisha tunapofikiria pamoja kweli muhimu za kiroho
Kuzaliwa Upya Kiroho
Katika maisha ya duniani tunapata uzoefu wa uzazi wa kimaumbile na nafasi kwa kuzaliwa upya kiroho.3 Tunaonywa na manabii na mitume “[kuamka] katika Mungu,4 “tuzaliwe upya”5 na kuwa “viumbe vipya … katika Kristo6 kwa kupokea katika maisha yetu baraka zilizofanywa ziwezekane kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. “Stahiki, … rehema, na neema za Masiya Mtakatifu”7 inaweza kutusaidia kushinda juu ya kujifikiria wenyewe na tabia za ubinfasi za mtu wa kawaida na kuwa bila choyo, mkarimu, na mtakatifu. Tumesihiwa kuishi hivyo ili kwamba tuweze “kusimama bila mawaa mbele [ za Bwana] katika siku ya mwisho.”8
Roho Mtakatifu na Ibada za Ukuhani.
Nabii Joseph Smith alifanya muhtasari wazi wa wajibu muhimu wa ibada za ukuhani katika injili ya Yesu Kristo: “Kuzaliwa tena huja kwa Roho wa Mungu kupitia ibada.”9 Maombi haya yanayopenya moyoni yanasisitiza wajibu wa vyote Roho Mtakatifu na ibada takatifu katika mchakato wa kuzaliwa upya kiroho.
Roho Mtakatifu ni mshiriki wa tatu wa Uungu. Yeye ni mtu wa kiroho na anashuhudia ukweli wote. Katika maandiko Roho Mtakatifu hutajwa kama mfariji,10 mwalimu,11 na Mfunuaji.12 Kwa nyongeza, Roho Mtakatifu ni mtakasaji,13 anaesafisha na kuchoma takataka na uovu kutoka roho za binadamu kama vile kwa moto.
Ibada takatifu ni muhimu katika injili ya Mwokozi na katika mchakato wa kuja Kwake na kutafuta kuzaliwa upya kiroho. Ibada ni matendo matakatifu ambayo yana kusudi la kiroho, umuhimu wa milele, na yana uhusiano na sheria na amri za Mungu.14 Ibada zote za wokovu na ibada ya sakramenti lazima ziidhinishwe na anayeshikilia funguo za ukuhani zinazohitajika.
Ibada za wokovu na kuinuliwa zinazoendeshwa katika Kanisa la urejesho la Bwana ni zaidi ya kaida za kidini au utendaji wa kiishara. Bali, zina mikondo iliyoidhinishwa ambayo kwayo baraka na nguvu za mbinguni zinaweza kutiririka kwenye maisha yetu binafsi.
“Na ukuhani huu mkuu huhudumia injili na hushikilia ufunguo wa siri za ufalme, hata ufunguo wa ufahamu wa Mungu.
“Kwa hiyo, katika ibada hizo, nguvu ya uchamungu hujidhihirisha.
“Na pasipo ibada hizo, na mamlaka ya ukuhani, nguvu za uchamungu haziwezi kujidhihirisha kwa mwanadamu katika mwili.“15
Ibada zilizopokelewa na kuheshimiwa kwa uadilifu ni muhimu kwa kupata nguvu ya ucha mungu na baraka zote zilizopatikana kupitia Upatanisho wa Mwokozi.
Kupata na Kuhifadhi Msamaha wa Dhambi kupitia Ibada
Kuelewa kikamilifu zaidi mchakato ambao kwake tunaweza kupata na daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu, tunahitaji kwanza kuelewa uhusiano usiotenganika miongoni mwa ibada tatu takatifu ambazo zinatoa fursa kwa nguvu za mbinguni: Ubatizo kwa kuzamishwa, kuwekewa mikono kwa karama ya Roho Mtakatifu, na sakramenti.
Ubatizo kwa kuzamishwa kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu “ni ibada ya mwanzo ya injili”16 ya Yesu Kristo na lazima itanguliwe na imani katika Mwokozi na kwa toba ya kweli. Ibada hii “ni ishara na amri ambayo Mungu ameweka kwa ajili ya [watoto Wake] kuingia katika ufalme Wake.”17 Ubatizo unaendeshwa kwa mamlaka ya Ukuhani wa Haruni. Katika mchakato wa kuja kwa Kristo na kuzaliwa upya kiroho ubatizo unatoa mahitaji ya usafishaji wa kwanza wa roho zetu kutokana na dhambi.
Maagano ya ubatizo yanajumuisha masharti matatu ya msingi: (1)Kuwa radhi kujichukulia juu yetu jina la Yesu kristo, (2) na daima kumkumbuka, na (3) kushika amri Zake. Baraka zilizoahidiwa kwa kuheshimu agano hili ni “kwamba [sisi] tuweze daima kuwa na Roho Wake pamoja [nasi].”18 Hivyo, ubatizo ni matayarisho muhimu kupokea nafasi iliyoidhinishwa kwa wenza wa daima wa mshiriki wa tatu wa Uungu.
“Ubatizo [kwa] maji … sharti ufuatwe na ubatizo wa Roho ili uweze kuwa kamili.”19 Kama Mwokozi alivyomfundisha Nikodemu, “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”20
Kauli tatu za Nabii Joseph Smith zinasisitiza unganisho la lazima kati ya ibada za ubatizo kwa kuzamishwa kwa msamaha wa dhambi na kuwekewa mikono kwa karama za Roho Mtakatifu.
Kauli ya 1 “Ubatizo ni ibada takatifu matayarisho ya mapokezi ya Roho Mtakatifu, ni njia na ufunguo ambao kwake Roho Mtakatifu atatolewa.”21
Kauli ya 2 “Unaweza vile vile kubatiza mfuko wa mchanga kama mtu, kama haukufanywa kwa kuzingatia msamaha wa dhambi na kumpata Roho Mtakatifu. Ubatizo kwa maji ni bali nusu ya ubatizo, na hauna faida yoyote bila ya nusu ya upande mwingine—ambayo ni, ubatizo kwa Roho Mtakatifu.”22
Kauli ya 3 “Ubatizo wa maji, bila ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu anayesimamia, ni bure. Ni muhimu na umeunganika na hauwezi kutengana.”23
Muunganiko thabiti miongoni mwa kanuni ya toba, ibada ya ubatizo na kupokea karama ya Roho Mtakatifu, na baraka tukufu za msamaha wa dhambi umesisitizwa mara kwa mara katika maandiko
Nefi alitangaza,”Kwani mlango ambao mtaingilia ni toba na ubatizo kwa maji, na kisha unakuja msamaha wa dhambi zenu kwa moto na kwa Roho Mtakatifu.”24
Mwokozi Wenyewe alitangaza, ”Sasa hii ndiyo amri: Tubuni nyinyi nyote katika sehemu zote za dunia, na mje kwangu na mbatizwe katika jina langu, kwamba muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili msimame mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho.”25
Kuwekewa mikono kwa karama za Roho Mtakatifu ni ibada ambayo inaendeshwa katika mamlaka ya Ukuhani wa Melkizediki. Katika mchakato wa kuja kwa Mwokozi na kuzaliwa upya kiroho, kupokea nguvu ya kutakasa ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu hutengeneza uwezekano wa utakaso unaoendelea wa nafsi zetu kutokana na dhambi. Baraka hizi za furaha ni muhimu kwani “na hakuna kitu kichafu chaweza kuishi na Mungu.”26
Kama waumini wa Kanisa la urejesho la Bwana, tumebarikiwa kwa vyote kwa utakaso wetu wa mwanzo kutoka dhambini unaohusiana na ubatizo na kwa uwezo wa utakaso unaoendelea kutoka dhambini uliowezeshwa kupitia wenza na nguvu ya Roho Mtakatifu—hata mshiriki wa tatu wa Uungu.
Fikiria jinsi mkulima anavyotegemea mpangilio usiobadilika wa kupanda na kuvuna. Kuelewa uhusiano kati ya kupanda na kuvuna ni chanzo cha siku zote cha kusudi na hushawishi maamuzi yote na vitendo mkulima anavyovifanya katika majira yote ya mwaka. Kwa njia hiyo hiyo, muungano usiotenganika kati ya ibada za ubatizo wa kuzamishwa kwa msamaha wa dhambi na kuwekewa mikono kwa karama za Roho Mtakatifu unapaswa kuathiri kila kipengele cha ufuasi wetu katika majira ya maisha yetu yote.
Sakramenti ni ibada ya tatu muhimu katika kupata njia ya kufikia nguvu ya ucha mungu. Ili tuweze kwa ukamilifu zaidi kujiweka bila mawaa kutokana na ulimwengu, tumeamriwa kwenda kwenye nyumba ya sala na kutoa sakramenti zetu katika siku takatifu ya Bwana.27 Tafadhali fikiria kwamba ishara za mwili na damu ya Bwana, mkate na maji, vyote vimebarikiwa na kutakaswa. “Ee Mungu, Baba wa milele, tunakuomba kwa jina la Mwanao Yesu Kristo, ubariki na utakase mkate huu [au maji haya] kwa roho za wale wote watakaoula [au kunywa].”28 Kutakasa ni kufanya safi na takatifu. Ishara za sakramenti hutakaswa kwa ukumbusho wa usafi wa Kristo, na utegemezi wetu juu ya Upatanisho Wake, na wajibu wetu kuheshimu ibada zetu na maagano kwamba tuweze “kusimama bila mawaa mbele [Yake] siku ya mwisho.”29
Ibada ya sakramenti ni mwaliko mtakatifu wa kurudiwa rudiwa kutubu kikweli na kufanywa wapya kiroho. Kitendo cha kushiriki sakramenti, ndani yake na chenyewe, hakitoi msamaha wa dhambi. Lakini tunapojitayarisha kwa dhamira na kushiriki katika ibada hii takatifu kwa moyo uliovunjika na roho iliyopondeka, basi ahadi ni kwamba tunaweza daima kuwa na Roho wa Bwana pamoja nasi. Na kwa nguvu ya utakaso ya Roho Mtakatifu kama mwenza wetu wakati wote, tunaweza daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu.
Kikweli tunabarikiwa kila wiki kwa nafasi ya kutathimini maisha yetu kupitia ibada ya sakramenti, tunaporudia tena maagano yetu, na kupokea ahadi hii ya maagano.30
Kubatizwa Tena
Wakati mwingine watakatifu wa siku za mwisho wanaonyesha matakwa yao kwamba wangebatizwa tena—na kwa kufanya hivyo wawe wasafi na kustahili kama siku ambayo walipokea ibada yao ya kwanza ya injili ya wokovu. Kwa heshima naomba kupendekeza kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae Mpendwa hawakusudii sisi tupate hisia kama hizo za kufanywa upya kiroho, kuchangamshwa, na urejesho mara moja tu katika maisha yetu. Baraka za kupata na daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu kupitia ibada za injili zinatusaidia kuelewa kwamba ubatizo ni sehemu ya kuondokea katika safari yetu ya kiroho duniani, sio kikomo cha safari tunafaa kutamani sana kupitia upya tena na tena.
Ibada za ubatizo wa kuzamishwa, kuwekewa mikono kwa karama ya Roho Mtakatifu, na sakramenti sio matukio yaliyotengana na yasioungana; bali, ni misingi katika mahusiano na nyongeza ya mpangilio wa mwendeleo wa ukombozi. Kila ibada inayofuata inaongeza na kukuza azma, matamanio, na utendaji wetu kiroho. Mpango wa Baba, Upatanisho wa Mwokozi, na ibada za injili hutoa neema tunayohitaji kusonga mbele na kuendelea mstari kwa mstari na kanuni juu ya kanuni kuelekea majaliwa yetu ya milele.
Ahadi na Ushuhuda
Sisi ni binadamu tusio kamili tunaojitahidi kuishi duniani kulingana na mpango kamili wa Baba wa Mbinguni kwa maendeleo ya milele. Mahitaji ya mpango Wake ni adhimu, yenye huruma, na yenye msimamo. Tunaweza wakati mwingine kujazwa na uamuzi na wakati mwingine kuhisi kutotosheleza kabisa. Tunaweza kushangaa kama kiroho tunaweza kutimiza amri ya kusimama bila mawaa mbele Zake siku ya mwisho.
Pamoja na msaada wa Bwana na kupitia nguvu za Roho Wake “kutufundisha [sisi] vitu vyote,31 kwa kweli tunaweza kubarikiwa kuelewa uwezekano wetu wa kiroho. Ibada hualika azma ya kiroho na nguvu katika maisha yetu tunapojitahidi kuzaliwa upya na kuwa wanaume na wanawake wa Kristo.32 Udhaifu wetu unaweza kuondolewa, na ufinyu wetu unaweza kushindwa.
Ingawa hakuna kati yetu anayeweza kupata ukamilifu katika maisha haya, tunaweza kuongezeka kustahili na kuwa bila mawaa tunapokuwa “tumeoshwa na damu ya mwanakondoo.”33 Ninaahidi na kushuhudia tutabarikiwa na imani iliyoongezeka katika Mwokozi na uhakika mkubwa wa kiroho tunapotafuta daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zetu na, mwishowe, kusimama bila mawaa mbele ya Bwana siku ya mwisho. Ninashuhudia haya katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina