2010–2019
Wala Mauti Haitakuwapo Tena
Aprili 2016


10:14

Wala Mauti Haitakuwapo Tena

Kwa wale wote ambao wameshaomboleza kwa ajili ya mtu wanayempenda, Ufufuko ni chanzo cha matuamini makubwa.

Wiki moja iliyopita ilikuwa Pasaka, na fikira zetu zilikuwa zimelenga tena dhabihu ya upatanisho na Ufufuo wa Bwana Yesu Kristo. Huu mwaka uliopita nimekuwa nikifikiri na kutafakari kuhusu Ufufuo kushinda kawaida.

Karibu mwaka mmoja uliopita, binti yetu Alisa aliaga. Alikabiliana na saratani kwa karibu miaka minane, na upasuaji mara kadhaa, matibabu mengi tofauti, miujiza ya kusisimua, na masikitiko makubwa. Tulitazama hali ya mwili wake ikidhoofika wakati alikuwa akikaribia mwisho wa maisha yake. Ilikuwa ni uchungu mkali kutazama haya yakimfanyikia binti yetu mpendwa—yule mtoto mdogo mwenye macho yenye kung’aa ambaye alikuwa amekua na kuwa na vipaji, mwanamke wa ajabu, mke, na mama. Nilidhani moyo wangu ungevunjika.

Alisa Johnson Linton

Mwaka jana wakati wa Pasaka, zaidi tu ya mwezi mmoja kabla ya yeye kuaga, Alisa aliandika: “Pasaka ni kumbusho la yale yote ninayotumainia kwangu mimi. Kwamba siku moja nitaponywa na siku moja nitakuwa mzima. Siku moja sitakuwa na chuma yoyote au plastiki ndani yangu. Siku moja moyo wangu utakuwa huru na hofu na akili yangu huru na wasiwasi. Siombi haya yafanyike hivi karibuni lakini, lakini nina furaha kwa kweli ninaamini katika maisha mazuri ya baadaye.”1

Ufufuo wa Yesu Kristo unahakikisha vitu ambavyo Alisa alitumainia na kuweka ndani ya kila mmoja wetu “sababu [ya] matumaini yaliyo ndani [yetu].”2 Rais Gordon B. Hinckley alizungumzia Ufufuo kama “tukio kuu zaidi ya yote katika historia ya binadamu.”3

Ufufuko uliletwa na Upatanisho wa Yesu Kristo na ndiyo kitovu cha mpango mkuu wa wokovu.4 Sisi ni watoto wa kiroho wa wazazi wa mbinguni.5 Tunapokuja katika haya maisha ya duniani, roho yetu uungana na mwili wetu. Sisi hupitia furaha yote na changamoto zote zinazohusika na maisha ya duniani. Wakati mtu anapoaga, roho yake inatenganishwa na mwili wake. Ufufuo unafanya kuwe na uwezo wa roho ya mtu na mwili kuunganishwa tena, lakini safari hii mwili huo utakuwa wa kutokufa na mkamilifu—usiohisi uchungu, magonjwa, au shida zingine.6

Baada ya ufufuo, roho haitawahi tena kutenganishwa na mwili kwa sababu Ufufuo wa Mwokozi ulileta ushindi kamili dhidi ya kifo. Ili tuweze kufikia hatima yetu ya milele, tunahitaji kuwa na nafsi hii ya kutokufa—roho na mwili—iliyounganishwa milele. Pamoja na roho na mwili wa kutokufa ikiwa imeunganishwa isitenganishwe tena, tunaweza kupokea ukamilifu wa furaha.7 Kwa kweli, bila Ufufuo hatungeweza kupokea ukamilifu wa furaha lakini tungalikuwa na huzuni milele.8 Hata watu wenye haki, waaminifu hutazama kutenganishwa kwa miili yao na roho zao kama utumwa. Tunaachiliwa kutoka kwenye utumwa huu kupitia Ufufuo, ambao ni ukombozi kutoka kamba na nyororo za kifo.9 Hakuna wokovu bila roho zetu na miili yetu.

Kila mmoja wetu ana upungufu na udhaifu wa kimwili, kiakili, na kihisia. Changamoto hizi, baadhi yazo zinaonekana kama kwamba haziwezi kusuluhishwa hivi sasa, hatimaye zitakuja kusuluhishwa. Hakuna shida yoyote ambayo itatukumba wakati tutakuwa tumefufuliwa. Alisa alifanya utafiti wa kiwango cha maisha ya watu walio na aina ya saratani ambayo alikuwa nayo, na idadi haikuwa ya kutia moyo. Aliandika: “Lakini kuna tiba, kwa hivyo sina hofu. Yesu tayari ametibu saratani yangu, na yako. … Mimi nitapata nafuu. Mimi nashukuru najua hivi.”10

Tunaweza kubadilisha neno saratani na magonjwa mengine yoyote ya kimwili, kiakili, au kihisia ambayo tunaweza kukumbana nayo. Kwa sababu ya Ufufuo yametibiwa tayari pia, Muujiza wa ufufuo, tiba ya mwisho, imeshinda nguvu za madawa ya kisasa. Lakini haijashinda nguvu za Mungu. Tunajua kwamba inaweza kufanyika kwa sababu Mwokozi amefufuka na anaweza kufufua kila mmoja wetu pia.11

Ufufuo wa Mwokozi unadhihirisha kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu na kwamba yale aliyofundisha ni ya kweli. “Amefufuka, kama alivyosema.”12 Hakuwezi kuwepo na ushahidi mkubwa wa utakatifu Wake kuliko Yeye akitoka kaburini akiwa na mwili wa kutokufa.

Tunajua kuhusu mashahidi wa Ufufuo katika Agano Jipya. Kuongezea kwa wale wanawake na wanaume tunaosoma kuhusu katika Injili, Agano Jipya linatuhakikishia ya kwamba mamia walimwona Bwana aliyefufuliwa.13 Na Kitabu cha Mormoni kinazungumzia kuhusu mamia ya wengine wengi: “Umati ulienda mbele, na kusukuma mikono yao ubavuni mwake, … na [wao] waliona na macho yao na kupapasa kwa mikono yao, na walijua ukweli na walishuhudia wenyewe kwamba ni Yeye, ambaye manabii waliandika kwamba atakuja.”14

Kwa hao mashahidi wa kale kumeongezeka mashahidi katika siku za mwisho. Kwa kweli katika mandhari ya kufungaka kwa kipindi hiki, Joseph Smith alimwona Mwokozi aliyefufuka pamoja na Baba.15 Manabii walio hai na Mitume wametoa ushuhuda kuhusu ukweli wa Kristo aliye hai, aliyefufuliwa.16 Kwa hivyo tunaweza kusema, “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi.”17 Na kila mmoja wetu anaweza kuwa sehemu ya wingu kubwa la mashahidi ambao wanajua kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu kwamba kile tunachosherehekea wakati wa Pasaka kwa kweli kilifanyika—kwamba Ufufuo ni wa kweli.

Ukweli wa Ufufuo wa Mwokozi huzidi kuvunjika moyo kwetu kwa matumaini kwa sababu kwayo huja uhakika kwamba ahadi zingine zote za injili ni halisi—ahadi ambazo sio chache kimiujiza kuliko Ufufuo. Tunajua kwamba Yeye anayo nguvu ya kutusafisha kutokana na dhambi zetu zote. Tunajua ya kwamba Yeye amejichukulia unyonge wetu wote, uchungu, na udhalimu tuliopitia.18 Tunajua kwamba Yeye “atafufuka [amefufuka] kutoka kwa wafu, na uponyaji katika mabawa yake.”19 Tunajua kwamba Yeye anaweza kutufanya wakamilifu bila kujali kile kilicho kasoro ndani yetu. Tunajua kwamba Yeye “atafuta kila chozi katika macho [yetu]; wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena.”20 Tunajua kwamba tunaweza “kukamilishwa kwa njia ya Yesu …, aliyekamilisha upatanisho huu mkamilifu”21 ikiwa tu tutakuwa na imani na tumfuate.

Kuelekea mwisho wa wimbo wa ufasaha yenye kutia msukumo Masiya, Handel alifanya muziki maridadi kutoka kwa maneno ya Mtume Paulo ambayo yanafurahia Ufufuo.

“Angalieni, [ninawaambia] ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

“Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho: … parapanda italia, na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

“Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, na huu wa kufa uvae kutokufa.

“… Hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.

“U wapi, Ewe mauti, Uchungu wako? “Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? …

“Lakini Mungu na ashukuriwe, atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.”22

Ninayo shukrani kwa ajili ya baraka ambazo ni zetu kwa sababu ya Upatanisho na Ufufuo wa Bwana Yesu Kristo. Kwa wale wote ambao wamemlaza mtoto kaburini au kulia juu ya jeneza la mume au mke ua omboleza kifo cha mzazi au mtu waliyempenda, Ufufuo ni chanzo cha matumaini makubwa. Itakuwa tukio la nguvu kiasi gani kuwaona tena—sio tu kama roho lakini wakiwa na miili iliyofufuliwa.

Ninayo hamu ya kumwona mamangu tena na kuhisi akinigusa kwa upole na kutazama katika macho yake ya upendo. Ninataka kuiona tabasamu ya baba yangu na kusikia kicheko chake na kumwona kama mtu aliyefufuka, mkamilifu. Kwa jicho la imani, ninamwona Alisa kikamilifu mbali na shida za dunia au ushindi wa kifo—Alisa aliyekamilika mshindi na mwenye furaha tele, aliyefufuka.

Pasaka chache zilizopita, aliandika tu: “Maisha kupitia jina Lake. Matumaini mengi. Daima. Kupitia kila kitu. Naipenda Pasaka kunikumbusha.”23

Ninashuhudia kuhusu ukweli wa Ufufuo. Yesu Kristo yu hai, na kwa sababu Yake, tutaishi tena. Katika jina la Yesu Kristo, amina.