“Ili Niweze Kuwaleta Watu Wote Kwangu”
Tunapojongea karibu na Mungu, nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo zitakuja katika maisha yetu.
Ndugu na dada zangu wapendwa, nilipokuwa nakiishi Eneo la Afrika Kusini Mashariki, nilitaka ushauri toka kwa Mzee Wilford W. Andersen wa Sabini juu ya kuwasaidia Watakatifu wanaoishi katika umaskini. Miongoni mwa mambo mazuri aliyoshiriki nami ilikuwa ni: “Umbali mkubwa kati ya mtoaji na mpokeaji, ndivyo mpokeaji anavyoendeleza hisia ya haki.”
Kanuni hii ndiyo msingi wa mfumo wa Kanisa wa ustawi. Wakati waumini wanaposhindwa kukidhi mahitaji yao, kwanza wanazigeukia familia zao. Baada ya hapo, kama kuna inahitajika, pia wanaweza kuwageukia viongozi wao wa Kanisa ili kupata msaada wa mahitaji yao ya kimwili.1 Wana familia na viongozi wa Kanisa wapo karibu na wale wenye shida, mara nyingi wanakabiliwa na hali kama hiyo, na kuelewa namna bora ya kusaidia. Kwa sababu ya ukaribu wao na watoaji, wapokeaji ambao hupokea msaada kulingana na mpango huu wanashukuru na huenda wasijisikie kuwa na haki.
Dhana—“umbali mkubwa kati ya mtoaji na mpokeaji, ndivyo mpokeaji anavyoendeleza hisia ya haki”—pia ina matumizi makubwa ya kiroho. Baba yetu wa Mbinguni na Mwana Wake, Yesu Kristo, wao ni Watoaji wa mwisho. Kadiri tunavyojitenga kutoka Kwao, ndivyo tutakavyohisi kuwa na haki. Tunaanza kufikiri kwamba tunastahili neema na kudai baraka. Tunapendelea sana kuangalia karibu nasi, kutambua kukosekana kwa usawa, na kuhisi uchungu—hata kukosewa—kwa kukosekana kwa usawa tunaofikiria. Wakati kukosa usawa kunaweza kuanzia vitu vidogo hata kuchomwa sana tumboni, tunapokuwa mbali na Mungu, hata ukosefu mdogo unakuwa jambo kubwa sana. Tunahisi kwamba Mungu ana wajibu wa kurekebisha mambo—mara moja!
Tofauti inayoletwa na ukaribu wetu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo imeelezewa katika Kitabu cha Mormoni kwa uwazi kati ya Nefi na ndugu zake wakubwa, Lamani na Lemueli.
-
Nefi alikuwa na “nia kubwa ya kujua siri za Mungu, hivyo, alimwomba Bwana” na moyo wake ulilainishwa.2 Kwa upande mwingine, Lamani na Lemueli walikuwa mbali na Mungu—hawakumjua Yeye.
-
Nefi alikubali wajibu wenye changamoto bila ya kulalamika, lakini Lamani na Lemueli “walinung’unika katika mambo mengi.” Manung’uniko ni sawa na kimaandiko kulia kitoto. Maandiko yanasema kwamba “walinung’unika kwa sababu hawakujua mipango ya Mungu aliyewaumba.”3
-
Ukaribu wa Nefi kwa Mungu ulimwezesha kujua na kushukuru “huruma ororo” za Mungu.4 Kinyume chake, wakati Lamani na Lemueli walipomwona Nefi akipata baraka, walikuwa “na chuki naye kwa sababu hawakujua mipango ya Bwana.”5 Lamani na Lemueli waliona baraka walizopata kama haki yao na walifikiri walistahili kupata zaidi. Walionekana kuziona baraka za Nefi kama makosa yaliyofanywa dhidi yao. Hii ni sawa na kimaandiko haki ya kinyongo.
-
Nefi alionyesha imani kwa Mungu katika kutimiza yale aliyoambiwa kuyafanya.6 Upande mwingine, Lamani na Lemueli, “wakiwa wagumu katika mioyo yao, … Hawakumtegemea Bwana kama walivyopaswa.”7 Walionekana kuhisi kwamba Bwana aliwajibika kutoa majibu ya maswali ambayo hawakuyauliza. “Bwana hakufanya kitu kama hicho kijulikane kwetu,” walisema, lakini hawakufanya juhudi za kuuliza.8 Hii ni sawa kimaandiko na nadharia ya kushuku kwa kejeli.
Kwa sababu walikuwa mbali na Mwokozi, Lamani na Lemueli walinung’unika, wakawa wabishi, na hawakuwa na imani. Walihisi kwamba maisha hayakuwa na usawa na kwamba walistahili neema ya Mungu. Kinyume chake, kwa sababu yeye alimkaribia Mungu, Nefi lazima aligundua kwamba maisha yangekuwa si sawa kwa Yesu Kristo. Japokuwa alikuwa hana hatia, Mwokozi angeteseka sana.
Kadiri tunavyokuwa karibu na Yesu Kristo katika fikra na dhamira ya mioyo yetu, ndivyo tunavyothamini kuteseka Kwake bila hatia, ndivyo tunavyokuwa na shukrani kwa neema na msamaha, na ndivyo tunavyotaka kutubu na kuwa kama Yeye. Ukaribu wetu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni muhimu, lakini mwelekeo tunaokwenda ndio muhimu zaidi. Mungu anafurahishwa na watenda dhambi wanaotubu wanaojaribu kuja karibu Naye kuliko wenye haki, watu wanaotafuta kosa ambao, kama Wafarisayo na waandishi wa kale, hawatambui jinsi wanavyohitaji kutubu.9
Nikiwa mtoto, niliimba wimbo wa Krismasi wa Kiswideni ambao unafundisha somo rahisi lakini lenye nguvu—kuja karibu na Mwokozi hutusababisha kubadilika. Shairi linakwenda kama hivi:
Wakati asubuhi ya Krismasi ikiwa dhahiri
Nataka kwenda sehemu tulivu,
Ambayo Mungu hukaa nyakati za usiku
Tayari anakaa juu ya majani makavu.
Vizuri kiasi gani hata kutamani
Kuja chini duniani!
Sasa, sitaki kupoteza
Siku za utoto wangu katika dhambi tena!
Yesu, tunakuhitaji Wewe,
Wewe ni rafiki wa watoto wapendwa.
Sitamani kukuhuzunisha Wewe
Kwa dhambi zangu tena.10
Wakati kwa mfano tunapojisafirisha wenyewe hadi zizi la Bethlehemu “ambapo Mungu katika masaa ya usiku tayari alikaa juu ya majani makavu” tunaweza kumtambua vizuri Mwokozi kama zawadi kutoka kwa Baba wa Mbinguni mkarimu, mwenye upendo. Badala ya kuhisi kustahili baraka Zake na neema, tunaendeleza tamanio la kuacha kumsababishia Mungu huzuni zaidi.
Bila kujali mwelekeo wa sasa au umbali kwenda kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, tunaweza kuchagua kuwageukia Wao na kuwa karibu Nao. Watatusaidia. Kama vile Mwokozi alivyowaambia Wanefi baada ya Ufufuko Wake:
“Na Baba yangu alinituma ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba; na baada ya kuinulia juu kwenye msalaba, kwamba ningeleta watu wote kwangu.
“Na kwa sababu hii nimeinuliwa juu; kwa hivyo, kulingana na uwezo wa Baba nitawaleta watu wote kwangu.”11
Kuwa karibu na Mwokozi, lazima tuongeze imani yetu Kwake, kuweka na kutii maagano, na kuwa na Roho Mtakatifu kuwa pamoja nasi. Lazima tutende katika imani, tukijibu mwongozo wa kiroho tunaoupata. Haya yote yanakuja katika sakramenti. Hakika, njia nzuri ninayoijua ya kuwa karibu na Mungu ni kujiandaa kwa makusudi na kupokea sakramenti kwa ustahiki kila wiki.
Rafiki yetu huko Afrika ya Kusini alishiriki jinsi alivyokuja kwenye utambuzi huu. Wakati Diane akiwa mwongofu mpya, alihudhuria tawi nje ya Johannesburg. Jumapili moja, alipokaa kwenye umati, jinsi kanisa lilivyopangwa shemasi hakumwona wakati sakramenti ikiwa inapitishwa. Diane alikatishwa tamaa lakini hakusema kitu. Muumini mwingine aliona mapungufu na akamwambia rais wa tawi baada ya kipindi. Wakati kipindi cha Shule ya Jumapili kilipoanza, Diane alipelekwa kwenye darasa lisilokuwa na mtu.
Mwenye ukuhani akaja. Alipiga magoti, akabariki mkate na kumpa kipande. Akala. Alipiga tena magoti na kubariki maji na kumpa kikombe kidogo. Akanywa. Baada ya hapo, Diane alikuwa na mawazo mawili ya haraka: Kwanza,“Ee, yeye [mwenye ukuhani] amefanya hivi kwa ajili yangu.” Na kisha, “Yeye [Mwokozi] amefanya hivi kwa ajili yangu.” Diane ihisi upendo wa Baba wa Mbinguni.
Kutambua kwake kwamba dhabihu ya Mwokozi ilikuwa kwa ajili yake kulimsaidia kuhisi kuwa karibu na Yeye na kutamani kutunza hisia zile kwenye moyo wake, siyo Jumapili pekee, bali kila siku. Aligundua kwamba japokuwa alikaa katika umati kupokea sakramenti, maagano aliyoyafanya upya kila Jumapili yalikuwa yake binafsi. Sakramenti ilimsaidia—na inaendelea kumsaidia—Diane kuhisi uwezo wa upendo wa kiungu, kuhisi mkono wa Bwana katika maisha yake, na kuwa karibu na Mwokozi.
Mwokozi alianzisha sakramenti kama sharti la msingi wa kiroho. Alisema:
“Na ninawapatia amri kwamba mtafanya hivi vitu [kupokea sakramenti]. Na ikiwa mtafanya hivi vitu daima mna baraka, kwani mmejengwa juu ya mwamba wangu.
“Lakini yeyote miongoni mwenu ambaye atafanya ndogo kuliko haya hajajengwa juu ya mwamba wangu, lakini wamejengwa kwenye msingi wa mchanga; na wakati mvua itateremka, na mafuriko kuja, na upepo kuvuma, na kujipigisha juu yao, wataanguka.”12
Yesu hakusema “kama mvua itanyesha, kama mafuriko yatakuja, kama na upepo utavuma, lakini“wakati.” Hakuna mwenye kinga ya changamoto za maisha; wote tunahitaji usalama ambao unatokana na kupokea sakramenti.
Siku ya Ufufuko wa Mwokozi, wafuasi wawili walisafiri kwenda kijiji cha Emausi. Bila kutambulika, Bwana mfufuka aliungana nao katika safari. Wakiwa wanasafiri, Aliwafundisha toka kwenye maandiko. Walipofika mwisho wa safari, walimkaribisha ale nao chakula.
“Na ikatokea kwamba, alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.
“Mara macho yao yakafumbuliwa, na wakamtambua ni yeye; naye akatoweka kati yao.
“Basi wakaambiana, je mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu, wakati alipokuwa anatufafanulia maandiko matakatifu kule njiani?
“Na wakaondoka saa ile ile, na wakarudi Yerusalemu, na wakawakuta wale [Mitume] wamekusanyika.”
Na kisha wakawashuhudia Mitume kwamba “hakika Bwana amefufuka. …
“Na wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.”13
Hakika sakramenti inatusaidia kumjua Mwokozi. Pia inatukumbusha mateso Yake bila hatia. Kama maisha yalikuwa sawa, kamwe wewe na mimi hatungefufuka, wewe na mimi hatungeweza kuwa wasafi mbele za Mungu. Katika hili, ninafurahi kwamba maisha hayako sawa.
Wakati huo huo, ninaweza kusema kwamba, kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, hatimaye, katika mpango wa milele wa mambo, hakutakuwa na kukosekana kwa usawa. “Yote ambayo si haki juu ya maisha yanaweza kufanywa haki.”14 Hali yetu ya sasa inaweza isibadilike, lakini kwa njia ya huruma ya Mungu, wema, na upendo, sisi wote tutapokea zaidi ya tunachostahili, zaidi ya tunavyoweza kupata, na zaidi ya tunavyoweza tarajia. Tumeahidiwa kwamba “Mungu atayafuta machozi yao yote, maana kifo hakitakuwepo tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita.”15
Bila kujali unasimama wapi katika uhusiano wako na Mungu, ninawaalika kuwa karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambaye ni Mfadhili na Mtoaji Kamili wa yote ambayo ni mema. Ninawaalika mhudhurie kipindi cha sakramenti kila wiki na kupokea ishara takatifu ya damu na mwili wa Mwokozi. Ninawaalika kuhisi ukaribu wa Mungu kama anavyojidhihirisha kwetu, kama ilivyokuwa kwa wafuasi wa kale, wakati wa “kumega mkate.”
Mnapofanya hivyo, ninawaahidi kwamba mtahisi kuwa karibu na Mungu. Maelekeo ya asili yenye kunung’unika kitoto, kinyongo, na wasiwasi wa kejeli utatawanywa. Maneno hayo yatabadilishwa na hisia za upendo mkuu na shukrani kwa ajili ya zawadi ya Baba wa Mbinguni ya Mwana Wake. Tunapojongea karibu na Mungu, nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo zitakuja katika maisha yetu. Na, pamoja na wafuasi wakielekea Emausi, tutaona kwamba Mwokozi amekuwa karibu muda mwingi. Ninatoa ushahidi na kushuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.