Agano la Kale 2022
Agosti 14. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Furaha kwa Kumfuata Mwokozi? Zaburi 1–2; 8; 19–33; 40; 46


Agosti 14. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Furaha kwa Kumfuata Mwokozi? Zaburi 1–2; 8; 19–33; 40; 46,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

Agosti 14. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Furaha kwa Kumfuata Mwokozi? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
vijana wakicheza nje

Agosti 14

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Furaha kwa Kumfuata Mwokozi?

Zaburi 1–2; 8; 19–33; 4046

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani ninaweza kupata furaha kwa kumfuata Yesu Kristo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Nani katika kata yetu au jamii yetu anahitaji msaada wetu? Tunawezaje kuwasaidia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana kujiandaa kwa ajili ya huduma ya ummisionari?

  • Unganisha familia milele. Je! Tunaweza kuchangia vipi katika juhudi za kata za kazi ya historia ya familia na kazi ya hekaluni?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Nini hukupatia shangwe? Watu wanaweza kusema wanapata shangwe wakiwa na marafiki na familia, uraibu pendwa au hata siku isiokuwa na majaribu. Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Furaha tuliyonayo haichangiwi na hali ya maisha yetu na kitu chochote kinachuhusiana na malengo ya maisha yetu. Wakati fokasi ya maisha yetu ipo katika mpango wa Mungu wa wokovu … na Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi furaha bila kujali nini kinatokea—au hakitokei—katika maisha yetu. Furaha huja kutoka kwa na kwa sababu Yake” (“Furaha na Kuendelea Kusalia Kiroho,” Liahona Nov. 2016,82). Nyingi za Zaburi zinapiga mwangwi ujumbe huo huo: “Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ni furaha tele” (Zaburi 16:11).

Fikiria baadhi ya changamoto ambazo washiriki wa darasa lako au akidi wanaweza kuwa wanakabiliana nazo. Ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia wao kuelewa kwamba furaha ya kweli huja kutokana na kufanya imani katika Mwokozi—hata katika wakati mgumu? Tafakari swali hili unapojiandaa kufundisha. Tafuta vifungu husika unavyoweza kushiriki na darasa lako au akidi katika Zaburi au ujumbe wa Rais Nelson “Furaha na Kuendelea Kusalia Kiroho.”

Picha
darasa la wavulana

Furaha ya kweli huja kutokana na kufanya imani katika Mwokozi, hata katika wakati mgumu.

Jifunzeni Pamoja

Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa lako au akidi kupitia tena chache ya zifuatazo Zaburi 1; 8; 19; 2327. Je, tunajifunza nini kutoka katika Zaburii hizi kuhusu kile kinachotuletea shangwe? Kisha ungeweza kutumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema kwamba furaha ya kweli huja kutokana na kumfuata Mwokozi.

  • Sisi sote tunataka kupata furaha, lakini tunahitaji kuelewa kile kinacholeta furaha ya kweli na kile hasa kinachoongoza kwenye huzuni. Waombe vijana kushiriki baadhi ya vitu ambavyo vinawaletea furaha na kwa nini vitu hivi hufanya hivyo. Andika ubaoni: “Wanadamu wapo, ili wapate shangwe” (2 Nefi 2:25). Kisha waalike vijana, kama watu binafsi au vikundi vidogo, kupitia tena moja au zaidi kati ya maandiko katika “Nyenzo Saidizi” na waorodheshe kile wanachopata ambacho huongoza kwenye furaha. Ungeweza pia kuonesha video “We Can Find Happiness” (ChurchofJesusChrist.org). Ni zipi baadhi ya njia watu wanajaribu kupata furaha ambazo hasa huongoza kwenye huzuni. Ni kwa jinsi gani Mwokozi ametuletea furaha?

  • Sote tunajua watu ambao wanakabiliana na changamoto hata ingawa wanajaribu kwa uwezo wao wote kuishi injili. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba tunaweza kupata furaha hata wakati maisha yetu yana changamoto? Ungeweza kuwaomba wapitie tena ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Furaha na Kuendelea Kusalia Kiroho” au ujumbe wa Rais Steven J. Lund “Kupata Furaha katika Kristo” (Liahona, Nov. 2020, 35–37). Ni mifano gani tuliyoiona ya watu waliopata furaha katika Kristo licha ya changamoto zao? Tunajifunza nini kutoka na uzoefu huu? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki?

  • Sisi sote ni wepesi kuhisi wasiwasi na mfadhaiko tunapokabiliana na changamoto za maisha. Kwa wengine, hisia hizi ni vita vya maisha yote. Darasa lako au akidi inaweza kufaidika kutokana na mjadala kuhusu changamoto hizi na kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kuwasaidia wake wanaotaabika na wasiwasi na mfadhaiko. Ili kuanzisha mjadala huu, unaweza kuwaomba vijana kupitia tena ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Kama Chombo Kilichovunjika,” hasa ibara nne za mwisho (Liahona, Nov. 2013, 40–42), au Ujumbe wa Dada Reyna I. Aburto “Iwe Mawingu au Jua, Bwana, Kaa pamoja Nami!” (Liahona, Nov. 2019, 57–59). Waalike washiriki wa darasa au akidi kutafuta kweli ambazo zina maana kwao na kushiriki kile watakachokipata. Wahimize vijana kuzungumza na mzazi au kiongozi wanayemuamini au watembelee mentalhealth.ChurchofJesusChrist.org kama wanahisi wanahitaji msaada.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi binafsi aliwajua wale Yeye aliowafundisha—na wangekuwa watu gani. Walipotaabika sana, Yeye aliendelea kuwapenda. Ni kwa jinsi gani unaweza kuonyesha kwamba unawapenda na kuwasaidia wale unaowafundisha?

Chapisha