Agano la Kale 2022
Agosti 28. Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Wakati wa Majaribu Yangu? Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150


Agosti 28 Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Wakati wa Majaribu Yangu? Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

Agosti 28 Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Wakati wa Majaribu Yangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
msichana akitabasamu

Agosti 28

Ni kwa Jinsi Gani Mwokozi Anaweza Kunisaidia Wakati wa Majaribu Yangu?

Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni uzoefu gani wa karibuni uliotuleta karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Je, Kuna mtu amehamia kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa karibuni? Tunawezaje kuwasaidia wajisikie kukaribishwa?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, kuna shughuli zozote zinazokuja ambazo tunaweza kuwaalika marafiki zetu kuhudhuria?

  • Unganisha familia milele. Je, Ni juhudi gani tunaweza kufanya za kuandika historia yetu binafsi?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Changamoto tunazokabiliana nazo zinaweza kutufanya tuhisi kuchoka, kukata tamaa, kushindwa na wapweke. Waandishi wa Zaburi walielewa hisia hizo vyema na kuzionyesha kwa nguvu sana: “Moyo wangu ulipigwa, na kunyauka kama majani ; … Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro aliye peke yake juu ya nyumba” (Zaburi 102:4, 7). Lakini kwa nguvu tu kama, walivyoshuhudia kwamba kumgeukia Mwokozi kungeleta nafuu: “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote: akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhili na rehema” (Zaburi 103:2–4).

Fikiria kuhusu baraka ambazo zitawajia washiriki wa darasa lako au akidi wanapoelewa vyema kabisa jinsi Mwokozi anaweza kuwasaidia katika majaribu yao. Ni kwa jinsi gani Mwokozi amekusaidia? Unapojiandaa kufundisha, anaweza kupitia tena ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Kujaribiwa, Kuthibitishwa, na Kunga’arishwa” (Liahona, Nov. 2020, 96–99) na “Dhiki” katika Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org).

Picha
mkutano mkuu wa vijana

Mwokozi atatusaidia na kutufarijii sisi katika majaribu yetu.

Jifunzeni Pamoja

Unaweza kuanzisha kwa kuwaomba washiriki wa darasa au akidi kupitia tena Zaburi 102, 103, na116, wakitafuta jinsi Mwokozi hutusaidia katika juhudi zetu za kushinda majaribu. Wanaweza kufanya kazi kibinafsi au katika kikundi kuandika sentensi chache kuhusu kile walichopata na kisha kushiriki kile walichoandika. Chagua moja au zaidi ya shughuli zifuatazo kuwasaidia kuelewa mada hii kwa kina zaidi.

  • Nyimbo zinaweza kumwalika Roho na hufundisha fundisho katika njia ya nguvu. Fikiria kupitia tena wimbo kuhusu jinsi Mwokozi hutusaidia wakati wa majaribu yetu, kama vile “How Firm a Foundation” (Nyimbo, na. 85). Ni nini wimbo unafundisha kuhusu msaada Mwokozi anaweza kutupa sisi? Vijana wanaweza kisha kupitia tena vifungu vya maandiko katika “Nyenzo Saidizi.” Wao wanaweza kufaidi kutokana na kuandika kirai kutoka kwenye wimbo au maandiko ambacho kinawakumbusha kumtafuta Mwokozi wakati wa dhiki zao

  • Ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Kujaribiwa, Kuthibitishwa, na Kunga’arishwa” unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema maswali kama yafuatayo: Ni nini baadhi ya madhumuni ya majaribu yetu ya duniani? Ni kwa jinsi gani Mwokozi anatusaidia katika changamoto zetu? Tunaweza kufanya nini ili tupate msaada na nguvu za Mwokozi? Fikiria kuandika maswali haya ubaoni. Washiriki wa darasa au akidi wanaweza kutafuta majibu katika ujumbe wa Rais Eyring. Kwa mfano, tunajifunza nini kutokana na hadithi kuhusu mama yake Rais Eyring hapo mwanzoni na mwishoni mwa ujumbe? Unaweza kumuomba kila mtu atafakari jinsi wanavyoweza kutumia kile walichojifunza katika majaribu yao. Baadhi ya vijana wanaweza kuwa radhi kushiriki mawazo yao.

  • Dada Lisa L. Harkness alisimulia tukio la Mwokozi akituliza dhoruba ili kufundisha kwamba Yeye anaweza kutuliza dhoruba katika maisha yetu (ona Marko 4:35–41; “Nyamaza Utulie,” Liahona, Nov. 2020, 80–82). Ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa au akidi kuja akiwa amejiandaa kushiriki kile anachojifunza kumhusu Mwokozi kutokana na tukio la kimaandiko. Mtu huyu anaweza pia kuonyesha picha (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na.40). Vijana wanaweza kisha kupitia tena kile Dada Harkness alifundisha kuhusu jinsi Mwokozi “yuko katika chombo chetu” tunapokabiliana na changamoto. Unaweza kuwaalika watu kushiriki jinsi Mwokozi alivyowasaidia katika majaribu yao, ikijumuisha jinsi Yeye alivyowasaidia kupitia watu wengine. Wahimize vijana kushiriki uzoefu wao na mtu fulani wanayemjua ambaye anahitaji amani ya Mwokozi.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Kuuliza maswali ambayo yanahimiza wanafunzi kushiriki ushuhuda kuhusu kanuni ambazo zinafundishwa inaweza kuwa njia yenye nguvu ya kumwalika Roho. … Ushuhuda wao—na shuhuda za wengine darasani—zitakua wakati Roho anapotoa ushuhuda wa ukweli” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,32).

Chapisha