Mkutano Mkuu
Mungu Atafanya Kitu Kisichofikirika
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2020


15:17

Mungu Atafanya Kitu Kisichofikirika

Mungu amewaandaa watoto Wake na Kanisa Lake kwa ajili ya muda huu.

Si muda mrefu baada ya kufika katika bonde la Salt Lake, Watakatifu wa Siku za Mwisho walianza kujenga hekalu takatifu. Walihisi walikuwa hatimaye wamepata sehemu ambapo wangeweza kumwabudu Mungu kwa amani na kuwa huru toka mateso

Hata hivyo, wakati msingi wa hekalu ulikuwa karibu kumalizika jeshi la wanajeshi wa kimarekani lilikuja kwa ulazima kumuweka gavana mpya.

Kwa kuwa viongozi wa Kanisa hawakujua ni kwa namna gani jeshi lingekuwa na upinzani Brigham Young aliwamuru Watakatifu kuondoka na kufukia msingi wa hekalu.

Ninauhakika baadhi ya waumini wa Kanisa walishangazwa kwa nini juhudi zao za kujenga ufalme wa Mungu zilikuwa kila mara zikiingiliwa.

Hatimaye, hatari ilipita, na misingi ya hekalu ilifukuliwa na kukaguliwa. Ilikuwa ndipo waasisi wajenzi waligundua kwamba mengi ya mawe ya asili yalikuwa na nyufa, zikiyafanya yasifae kwa ajili ya msingi.

Kwa hiyo, Brigham aliwaambia warekebishe msingi ili kwamba uweze kwa uhakika kuhimili kuta za mawe aina ya matale1 za hekalu tukufu la Salt Lake2 Hatimaye, Watakatifu wangeweza kuimba wimbo wa dini “How Firm a Foundation”3 na kujua hekalu lao takatifu lilikuwa limejengwa kwenye msingi imara ambao ungedumu kwa vizazi vingi.

Msingi wa Hekalu la Salt Lake

Simulizi hii inaweza kutufundisha jinsi Mungu anavyatumia taabu ili kukamilisha kusudi Lake.

Maradhi yaliyoenea ulimwenguni kote

Kama hili inaonekana ya kwaida kwa hali zilizopo ambapo sisi hujikuta leo hii , ni kwa sababu ndivo ilivyo.

Nina shaka kama kuna mtu ambaye anaisikia sauti yangu au kusoma maneno yangu ambaye hajaathiriwa na maradhi yaliyoenea ulimwenguni kote.

Kwa wale ambao wanaomboleza kupotea kwa familia au marafiki, tunaomboleza pamoja nanyi. Tunaomba kwa Baba wa Mbinguni kuwafariji na kuwatuliza.

Matokeo ya muda mrefu ya kirusi hiki huenda mbali zaidi ya afya ya kimwili pekee. Familia nyingi zimepoteza vipato na wanatishwa na njaa, kutokuwa na uhakika wa yajayo, na woga. Tunafurahia juhudi zisizo za kibinafsi za wengi za kuzuia ueneaji wa ugonjwa huu. Tunanyenyekezwa kwa dhabihu tulivu na juhudi za dhati za wale ambao wameweka hatarini usalama wao wenyewe ili kusaidia kuponya, na kusaidia watu wenye uhitaji. Mioyo yetu imejaa shukrani kwa sababu ya uzuri wenu na huruma.

Tunasali kwa dhati kwamba Mungu atafungua madirisha ya mbinguni na kujaza maisha yenu baraka za Kiungu za milele.

Sisi Ni Mbegu

Bado kuna mengi yasiyojulikana kuhusu kirusi hiki Lakini kama kuna kitu kimoja ninachokijua kirusi hiki hakikumpata Baba wa Mbinguni kwa kushitukiza. Hakuwa na haja ya kupanga jeshi la ziada la malaika , kuwa na mikutano ya dharura au kugawanya rasilimali za uumbaji wa dunia ili kukabiliana na hitaji ambalo halikutarajiwa.

Ujumbe wangu leo ni kwamba hata kama janga hili si kile ambacho tulikitaka , au kutarajia, Mungu amewaandaa watoto Wake na Kanisa Lake kwa muda huu.

Tutavumilia hili, ndio. Lakini tutafanya zaidi ya kusaga meno yetu tu, kubaki palepale na kusubiri vitu kurudia katika hali yake ya kawaida ya awali. Tutasonga mbele, na tutakuwa bora zaidi kama matokeo ya hilo.

Kwa njia fulani sisi ni mbegu. Na ikwa mbegu kufikia ukamilifu wake, lazima zizikwe kabla ya kuweza kuchipua. Ni ushuhuda wangu kwamba japo wakati mwingine tuna hisi kufunikwa na majaribu ya kimaisha au kuzungukwa na hisia za kiza, upendo wa Mungu na baraka za injili ya urejesho ya Yesu Kristo vitaleta kitu kisichotarajiwa kuchipuka

Baraka huja Kutokana na Magumu

Kila kipindi kimekumbana na nyakati za majaribu na magumu.

Enoko na watu wake waliishi katika wakati wa uovu, vita na umwagaji wa damu. “Lakini Bwana alikuja na kukaa pamoja na watu wake.” Mawazoni Mwake alikuwa na kitu kisichotarajiwa kwa ajili yao. Aliwasidia kuanzisha Sayuni—watu wa moyo mmoja na wazo moja” ambao “waliishi katika haki.”4

Kijana Yusufu, mwana wa Yakobo, alitupwa katika shimo, kuuzwa utumwani, kusalitiwa, na kukataliwa.5 Yusufu lazima alishangazwa kama Mungu alikuwa amemshahau. Mungu alikuwa na kitu kisichotarajiwa kwa ajili ya Yusufu. Alitumia muda huu wa majaribu kuimarisha tabia ya Yusufu na kumuweka katika nafasi ya kuitumukia familia yake.6

Joseph katika Jela ya Liberty

Fikiria kuhusu Joseph smith nabii alipokuwa ndani ya gereza la Liberty, jinsi alivyosihi ili kupata nafuu kwa ajili ya Watakatifu waliokuwa wakiteseka. Lazima alikuwa ameshangazwa jinsi gani Sayuni ingeweza kujengwa katika hali kama zile. Lakini Bwana alizungumza amani kwake, na ufunuo wa kitukufu ambao ulifuata ulileta amani kwa Watakatifu—na unaendelea kuleta amani kwako na kwangu.7

Ni mara ngapi katika miaka ya mwanzoni ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za Mwisho Watakatifu walikata tamaa na kujiuliza kama Mungu alikuwa amewasahau? Lakini kupitia mateso, majanga, na vitisho vya kuuwawa, Bwana Mungu wa Israeli alikuwa na kitu kingine akilini kwa ajili ya kundi lake dogo. Kitu kisichofikirika.

Je tunajifunza nini kutoka katika mifano hii—na mamia mingine katika maandiko?

Kwanza: Watakatifu hawapewi pasi ya bure ambayo huwaruhusu wao kuepuka mabonde ya kiza. Sote lazima tutembee kupitia nyakati ngumu, kwani ni katika nyakati hizi za shida ambazo tunajifunza kanuni za kuimarisha tabia zetu na kutusababisha kusonga karibu na Mungu.

Pili: Baba yetu wa Mbinguni anajua kwamba tunateseka na kwasababu sisi tu watoto Wake, Yeye hatatuacha.8

Fikiria kuhusu mwenye huruma, Mwokozi ambaye alitumia maisha yake kwa wingi katika kuhudumia wagonjwa, wapweke, wenye shaka na wenye kukata tamaa.9 Je unafikiria Yeye hafikirii sana kuhusu wewe leo hii?

Rafiki zangu wapendwa, kaka na dada zangu wapendwa, Mungu anawaangalia na kuwachunga nyakati hizi za mashaka na woga. Anawajua. Anasikia maombi yenu Ni mwaminifu na wa kutegemewa. Atatimiza ahadi zake.

Mungu mawazoni Mwake ana kitu kisichofikirika kwa ajili yako binafsi na Kanisa kwa ujumla—kazi ya kushangaza na maajabu .

Tunakushukuru, Ewe Mungu, kwa Ajili ya Nabii

Siku zetu nzuri siko mbele yetu. Ni kwa sababu hii Mungu hutupatia ufunuo wa kisasa! Bila huo, maisha yanaweza kuonekana kama yanapaa katika mpangilio wa kushikilia, kusubiri ukungu utoweke ili tuweze kutua salama. Malengo ya Bwana kwetu sisi ni makubwa zaidi ya hilo. Kwa sababu hili ni Kanisa la Kristo aliye hai, na kwa sababu Yeye huwaongoza manabii Wake, tunasonga mbele na juu kwenye sehemu ambayo hatukuwahi kuwepo katika vina ambavyo hatuwezi kuvifikiria.

Sasa, hii haimaanishi hatutapata dhoruba katika ndege yetu kupitia maisha ya hapa duniani. Haimaanishi hakutakuwa na kuharibika kwa kifaa kusikotegemewa, kushindikana kwa utendaji wa kimakenika, na changamoto hatarishi za hali ya hewa. Na kwa kweli, vitu vinaweza kuwa vibaya zaidi kabla ya kuwa vizuri.

Kama rubani mpiganaji na mwongoza ndege, nilijifunza kwamba wakati ambapo sikuweza kuchagua shida ambayo nigekutana nayo wakati nikiwa kwenye ndege, ningeweza kuchagua jinsi ambavyo nilijiandaa na jinsi ningetenda. Kinachohitajika wakati wa nyakati za majanga ni utulivu na uaminifu wa kweli

Tunafanyaje hili?

Tunakabiliana na ukweli na tunarudi kwenye yaliyo ya msingi, kwenye kanuni za msingi za injili, kwenye kile chenye umuhimu zaidi. Unaimarisha tabia yako binafsi juu ya dini—kama vile sala na kujifunza maandiko na kushika amri za Mungu. Unafanya maamuzi kulingana na tamaduni nzuri zilizothibitika.

Fokasi kwenye vitu unavyoweza kufanya na si kwenye vile ambavyo huwezi.

Unathubutu na imani yako. Na uanasikiliza kwa ajili ya neno ongozi la Bwana na nabii Wake kukuongoza kwenye usalama.

Kumbuka, hili ni Kanisa la Kristo—Yeye yu katika usukani.

Fikiria kuhusu maboresho mengi ambayo yaliyotokea kwenyekatika kipindi cha mwongo mmoja pekee uliopita. Kuyataja machache tu:

  • Sakramenti ilisisitizwa kama kiini cha kuabudu siku ya Sabato.

  • Njoo, Unifuate ilitolewa kama zana inayelenga nyumbani na kusaidiwa na Kanisa ili kuimarisha watu binafsi na familia.

  • Tulianza njia ya juu na takatifu ya kuhudumia kwa wote.

  • Kutumia teknolojia kushiriki injili na kufanya kazi ya Bwana vimesambaa kote Kanisani.

Hata vipindi hivi vya mkutano mkuu visingewezekana bila vifaa vya ajabu vya teknolojia.

Akina kaka na dada, Kristo akiwa katika usukani, vitu vyote si tu vitakuwa sawa, vitakuwa visivyofikirika .

Kazi ya kuikusanya Israeli Inasonga Mbele

Kwa mara ya kwanza iliweza kuonekana kwamba janga la ulimwenguni kote lingeweza kuwa kikwazo kwenye kazi ya Bwana. Kwa mfano, tamaduni za kawaida za kushiriki injili zimekuwa haziwezekaniki. Hata hivyo, janga linafunua njia mpya na za kibunifu zaidi za kuwafikia wale walio wa kweli wa moyo. Kazi ya kuikusanya Israeli inaongezea kwa nguvu na ari. Mamia na maelfu ya hadithi zinashuhudia hili.

Rafiki mzuri aishiye huko Norway alituandikia kuhusu ongezeko la ubatizo la hivi karibuni. “Katika maeneo ambayo Kanisa ni changa,” aliandika, “vikundi vidogo vitakuwa matawi, na matawi yatakuwa kata!”

Huko Latvia, mwanamke ambaye aligundua Kanisa kwa kubofya kwenye tangazo la mtandaoi alikuwa na shauku ya kujifunza kuhusu injili ya Yesu Kristo kwamba alikuwepo kwenye mkutano saa moja kabla, na kabla ya wamisionari hawajamaliza somo la kwanza aliuliza tarehe ya kubatizwa kwake.

Katika Ulaya ya Mashariki mwanamke mmoja ambaye alipokea simu kutoka kwa wamisionari alijibu kwa mshangao, “akina Dada, kwanini hamkunipigia mapema? Nimekuwa nikisubiri!”

Wengi wa wamisionari wetu wana kazi nyingi kuliko hapo awali. Wengi wanafundisha watu zaidi kuliko awali. Kuna ongezeko la ushirikiano kati ya waumini na wamisionari.

Hapo awali tungekuwa tumefungwa na tamaduni ambapo ililazimu janga kufungua macho yetu. Pengine tutaendelea kujenga na mawe ya mchanga wakati tayari mawe imara yanapatikana. Cha muhimu, sasa tunajifunza jinsi ya kutumia njia mbalimbali, ikijumuisha teknolojia, kuwaalika watu—katika njia ya kawaida na ya asili—kuja na kuona, kuja na kusaidia, na kuja na kuwa sehemu ya.

Kazi Yake, Njia Zake

Hili ni kazi ya Bwana. Anatualika kutafuta njia zake za kuifanya, na zinaweza kutofautiana kutoka na uzoefu wetu uliopita.

Hii ilitokea kwa Simoni Petro na wanafunzi wengine ambao walikwenda kuvua samaki kwenye bahari ya Tiberia.

“Usiku huo hawakupata chochote.

“Bali asubuhi … [kulipokucha], Yesu alisimama ufuoni. …

“Akawaambia, litupeni jarife upande [mwingine] wa chombo, ninyi mtapata.”

Wakatupa nyavu upande wa pili “ hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.”10

Mungu amefunua na ataendelea kufunua Mkono wake mkuu. Siku itafika ambapo wakati tutaangalia nyuma na kujua kwamba wakati huu wa shida, Mungu alikuwa akitusaidia kupata njia nzuri zaidi—njia yake— kujenga ufalme Wake kwenye msingi imara

Ninatoa ushuhuda wangu kwamba hii ni kazi ya Mungu na Yeye ataendelea kufanya vitu vingi visivyotarajiwa kati ya watoto Wake, watu Wake. Mungu ametuweka kwenye kiganja chake chenye kujali na mikono yenye huruma.

Ninashuhudia kwamba Rais Russell M. Nelson ni nabii kwa wakati wetu.

Kama mtume wa Bwana, ninawaalika na kuwabariki ili “kwa furaha mfanye vitu vyote vilivyo katika uwezo [wenu] na ndipo muweze [kusimama] wima, kwa uhakika mkubwa , kuuona wokovu wa Mungu, na kwa mkono wake kufunuliwa.”11 Na nina ahidi kwamba Bwana atasababisha vitu visivyotarajiwa kuja kutoka katika kazi zenu za haki Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Madini ya Quartz ambayo yanaonekana kama marumaru kutoka kwenye machimbo kwenye bonde la Cottonwood, maili 20 kusini mashariki mwa jiji.

  2. Kwa uchunguzi zaidi wa kina wa kina wa historia ya kipindi hiki, ona Watakatifu: Hadithi ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, vol. 2, No Unhallowed Hand, 1846–1893 (2020), ukurasa wa 17, 19, na 21.

  3. Ona “How Firm a Foundation,” Nyimbo, no.85

    Beti za wimbo huu zinaweza kutumika kama mada kwa ajili ya nyakati zetu na, wakati tunaposikiliza mashairi kwa masikio yetu mapya, hutoa umaizi kwenye chanagamoto tunazokumbana nazo:

    In every condition—in sickness, in health,

    In poverty’s vale or abounding in wealth.

    At home or abroad, on the land or the sea—

    As thy days may demand … so thy succor shall be.

    Fear not, I am with thee; oh, be not dismayed,

    For I am thy God and will still give thee aid.

    I’ll strengthen thee, help thee, and cause thee to stand,

    Upheld by my righteous … omnipotent hand.

    When through the deep waters I call thee to go,

    The rivers of sorrow shall not thee o’erflow,

    For I will be with thee, thy troubles to bless,

    And sanctify to thee … thy deepest distress.

    When through fiery trials thy pathway shall lie,

    My grace, all sufficient, shall be thy supply.

    The flame shall not hurt thee; I only design

    Thy dross to consume … and thy gold to refine.

    The soul that on Jesus hath leaned for repose

    I will not, I cannot, desert to his foes;

    That soul, though all hell should endeavor to shake,

    I’ll never, no never … no never forsake!

  4. Ona Musa 7:13–18.

  5. Yusufu pengine alikuwa na miaka 17 wakati kaka zake walipomuuza kwenye utumwa (ona Mwanzo 37:2) Alikuwa na miaka 30 wakati alipoingia kwenye huduma ya Farao (ona Mwanzo41:46) Je unaweza kufikiria jinsi ilivyokuwa vigumu kwa kijana katika umri wake kusalitiwa, kuuzwa utumwani, kimakosa kushutumiwa, na kisha kufungwa gerezani? Yusufu kwa hakika ni mfano si tu kwa vijana wa Kanisa lakini kwa kila mwanaume na mwanamke, na mtoto ambaye anatamani kujichukulia msalaba na kumfuata Mwokozi.

  6. Ona Mwanzo 45:4-11; Musa 50:20-21. Katika Zaburi 105:17–18, tunasoma ‘Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani: walimwumiza miguu yake kwa pingu, akatiwa katika minyororo ya chuma.” Katika tafsiri nyingine, mstari wa 18 unasomeka, “Walimwumiza kwa pingu miguuni mwake, mnyororo wa chuma ukapenya nafsini mwake” (Young’s Literal Translation). Kwangu mimi hii inapendekeza kwamba magumu ya Yusufu yalimpa nafsi iliyo imara na kakamavu kama chuma—sifa ambayo angeihitaji kwa ajili ya siku za mbeleni kuu na zisizotarajiwa ambazo Bwana alikuwa amemuandalia.

  7. Ona Mafundisho na Maagano 121–23.

  8. Kama mungu amewaamuru watoto wake kuwa na ufahamu wa na kuwa na huruma kwa wale wenye njaa, wenye uhitaji, walio uchi, wanaoumwa na kuteseka, hakika Yeye anajua na ni mwenye huruma kwetu sisi watoto Wake (ona Mormoni 8:39)

  9. Ona Luka 7:11–17.

  10. Ona Yohana 21:1-6.

  11. Mafundisho na Maagano 123:17.