Kuwa Kama Yeye
Ni kwa usaidizi wa kiungu wa Mwokozi pekee kwamba tunaweza sote kukua kuelekea kuwa kama Yeye.
Hata kwa mwanafunzi makini wa maisha na huduma ya Yesu Kristo, mawaidha ya Mwokozi ya kuwa “hata vile nilivyo” 1 ni ya kuogofya na yanayoonekana kutofikika. Pengine wewe ni kama mimi—unajua vyema mapungufu na kushindwa kwako, hivyo unaweza kuhisi vizuri kiakili kutembea njia isiyo na mpando na yenye ukuaji mdogo. “Kwa hakika, fundisho hili si halisi na ni mbalagha,” tunajipa moyo pale tunapochagua bila hofu njia yenye upinzani kidogo, hivyo kupunguza kalori chache za badiliko linalohitajika.
Lakini vipi ikiwa kuwa “hata vile [Yeye alivyo]” si kistiari, hata katika hali yetu ya maisha haya? Vipi ikiwa ni kweli, kwa kiasi fulani, inawezekana katika maisha haya na, hakika, ni la msingi kwenye kuwa pamoja Naye tena? Vipi ikiwa “hata vile nilivyo” ni sawasawa na dhahiri ya kile kilichomaanishwa na Mwokozi? Kisha nini? Ni kipimo gani cha juhudi tutakuwa radhi kutoa ili kualika nguvu Yake ya muujiza kwenye maisha yetu ili kwamba tuweze kubadili asili yetu hasa?
Mzee Neal A. Maxwell alifundisha: “Tunapotafakari amri tuliyopewa na Yesu ya kuwa kama Yeye, tunaona kuwa hali yetu ya sasa ni ile ambayo kwayo si lazima tuwe waovu, lakini, ni ile ambayo kwayo tunajitoa kidogo na hivyo kukosa ari kwenye kusudi Lake—ambalo ni kusudi letu, pia! Tunamtukuza lakini kwa nadra tunafuata mfano Wake.” 2 Mtumishi kijana, Charles M. Sheldon, alielezea maoni kama haya kwa njia hii: “Ukristo wetu unapenda sana urahisi na faraja yake kiasi cha kushindwa kuchukua chochote ambacho ni kigumu na kizito kama msalaba.” 3
Kwa kweli, sote tupo chini ya mwongozo wa kuwa kama Yeye, kama vile Yesu Kristo alivyokuwa kama Baba. 4 Tunapoendelea mbele, tunakuwa wazima zaidi, waliokamilika zaidi na waliositawi zaidi. 5 Fundisho kama hilo halijikiti tu kwenye mafundisho ya dhehebu moja bali huja moja kwa moja kutoka kwa Bwana Mwenyewe. Ni kupitia lenzi hii kwamba maisha yanapaswa kuwa, mawasiliano kuzingatiwa, na mahusiano kuendelezwa. Hakika, hakuna njia nyingine ya kuponya majeraha ya mahusiano yaliyovunjika au ya jamii iliyovunjika zaidi ya kila mmoja wetu kufuata kwa ukamilifu zaidi mfano wa Mfalme wa Amani. 6
Acha tuzingatie jinsi ya kuanza utafutaji wa kina, wa hadhari, na wa makusudi wa kuwa jinsi Yeye alivyo kwa kupata sifa hasa za Yesu Kristo.
Azimia na Tenda
Miaka michache iliyopita, mimi na mke wangu tulisimama chini ya mlima mrefu zaidi wa Japan, Mlima Fuji. Tulipoanza upandaji wetu tulitazama juu kileleni na kujiuliza ikiwa tungeweza kufika huko.
Tulipoendelea kusonga, uchovu, misuli kuvimba, na madhara ya mwinuko viliingia. Kimawazo, ilikuwa muhimu kwetu kufokasi tu kwenye hatua iliyofuata. Tungesema, “Ninaweza nisifike kileleni sasa, lakini ninaweza kupiga hatua hii inayofuata sasa hivi.” Baada ya muda jukumu la kuogofya hatimaye likatekelezeka—hatua kwa hatua.
Hatua ya kwanza katika njia hii ya kuwa kama Yesu Kristo ni kuwa na tamaa ya kufanya hivyo. Kuelewa mawaidha ya kuwa kama Yeye ni vizuri, lakini uelewa huo unahitaji kuunganishwa na tamaa ya kujibadilisha, hatua moja baada ya nyingine, kupita uanadamu wa tabia ya asili. 7 Ili kukuza tamaa, lazima tufahamu Yesu Kristo ni nani. Lazima tujue jambo fulani juu ya sifa Yake, 8 na lazima tutafute sifa Zake katika maandiko, huduma za kuabudu, na sehemu zingine takatifu. Tunapoanza kufahamu mengi kuhusu Yeye, tutaona sifa Zake zikiakisiwa na wengine. Hii itatutia moyo katika utafutaji wetu wenyewe, kwani ikiwa wengine wanaweza kupata kwa kiasi fulani sifa Zake, nasi tunaweza.
Ikiwa tu waaminifu na nafsi zetu, Nuru ya Kristo 9 ndani yetu inanong’ona kwamba kuna umbali kati ya sisi tulipo ikilinganishwa na sifa iliyokusudiwa ya Mwokozi. 10 Uaminifu kama huo ni muhimu ikiwa tunataka kuendelea katika kuwa kama Yeye. Hakika, uaminifu ni moja ya sifa Zake.
Sasa, wale kati yetu ambao ni majasiri wanaweza kufikiria kumwuliza mwanafamilia, mwenza, rafiki, au kiongozi wa kiroho mwenye kuaminika ni sifa ipi ya Yesu Kristo tunaihitaji—na tunaweza kuhitaji kujiimarisha kwa ajili ya jibu! Nyakati zingine tunajitazama kwa vioo vya kuharibu uhalisia ambavyo vinatuonyesha wingi zaidi au uchache zaidi ya vile tulivyo hasa.
Marafiki wa kuaminika na familia wanaweza kutusaidia kujiona wenyewe kwa usahihi zaidi, lakini hata wao, kadiri ambavyo wangetamani kupenda na kusaidia, wanaweza kuona mambo pasipo ukamilifu. Kama matokeo, ni muhimu kwamba sisi pia tumuulize Baba yetu ya Mbinguni mwenye upendo kile tunachohitaji na wapi tufokasi juhudi zetu. Yeye ana uoni mkamilifu juu yetu na kwa upendo atatuonyesha udhaifu wetu. 11 Pengine utajifunza kwamba unahitaji uvumilivu, unyenyekevu, hisani, upendo, tumaini, bidii, au utiifu mkubwa, nikitaja machache. 12
Muda mfupi uliopita, nilipata uzoefu wa kuinua nafsi wakati kiongozi wa Kanisa mwenye upendo alipotoa pendekezo la moja kwa moja kwamba ningeweza kutumia kwa kiasi kikubwa sifa fulani. Kwa upendo hakuharibu ukweli. Usiku ule, nilishiriki uzoefu wangu kwa mke wangu. Alikuwa mwenye rehema na hisani hata pale alipokubaliana na pendekezo la kiongozi. Roho Mtakatifu alinithibitishia kwamba ushauri wao ulitoka kwa Baba wa Mbinguni mwenye upendo.
Inaweza pia kusaidia kukamilisha kwa uaminifu shughuli ya sifa kama za Kristo katika sura ya 6 ya Preach My Gospel. 13
Mara unapokuwa umefanya tathmini ya uaminifu na kuazimia kuanza kupanda juu ya mlima, utahitaji kutubu. Rais Russell M. Nelson kwa upendo alifundisha: “Wakati tunapochagua kutubu, tunachagua kubadilika! Tunamruhusu Mwokozi kutubadilisha kuwa toleo zuri zaidi la sisi wenyewe. Tunachagua kukua kiroho na kupokea shangwe—shangwe ya ukombozi katika Yeye. Tunapochagua kutubu, tunachagua kuwa zaidi kama Yesu Kristo.” 14
Kuwa kama Yesu Kristo alivyo kutahitaji kubadili mioyo na mawazo yetu, hakika, tabia yetu hasa, na kufanya hivyo kunawezekana tu kupitia rehema ya kuokoa ya Yesu Kristo. 15
Tambua na Tenda
Wakati sasa umeazimia kubadilika na kutubu na umetafuta mwongozo kupitia sala, kutafakari kwa dhati, na pengine kushauriana na wengine, utahitaji kuchagua sifa ambayo kwa bidii itakuwa fokasi yako. Utahitaji kujitolea kwenye kutoa juhudi yenye maana. Sifa hizi hazitakuja kwa gharama rahisi na ghafla, bali kupitia neema Yake zitakuja kwa kuongezeka wakati ukifanya bidii.
Sifa kama za Kristo ni vipawa kutoka kwa Baba wa Mbinguni mwenye upendo ili kutubariki sisi na wale walio karibu yetu. Vivyo hivyo, juhudi zetu za kupata sifa hizi zitahitaji sala ya dhati kwa ajili ya usaidizi wake wa kiungu. Ikiwa tutatafuta vipawa hivi ili kuwatumikia wengine vizuri zaidi, Yeye atatubariki katika juhudi zetu. Kutafuta kipawa kutoka kwa Mungu kwa ubinafsi kutapelekea kwenye kukata tamaa na kuvunjika moyo.
Kwa kufokasi kwa kina kwenye sifa moja inayohitajika, wakati ukiendelea katika kupata sifa hiyo, sifa zingine zitaanza kuongezeka kwako. Je, haiwezekani mtu anayefokasi kwa kina kwenye hisani kuongezeka katika upendo na unyenyekevu? Je, haiwezekani mtu anayefokasi kwenye utiifu kupata unyenyekevu na tumaini kubwa? Juhudi zako muhimu za kupata sifa moja huwa maji ya kujaa na kupwa ambayo hunyanyua mashua zote katika bandari.
Weka kumbukumbu na Endelea
Ni muhimu kwangu pale ninapojitahidi kuwa kama Yeye kuweka kumbukumbu za uzoefu wangu pamoja na kile ninachojifunza. Ninapojifunza nikiwa na moja ya sifa Zake mawazoni, maandiko huwa mapya pale ninapoona mifano ya sifa hii katika mafundisho Yake, huduma Yake, na wafuasi Wake. Jicho langu pia huwa lililofokasi zaidi katika kutambua sifa hiyo kwa wengine. Nimewaona watu wema kote ndani na nje ya Kanisa ambao wana sifa zinazoakisi mfano Wake. Wao ni mifano yenye nguvu ya jinsi sifa hizo zinavyoweza kudhihirika kwa binadamu wa kawaida kupitia neema Yake ya upendo.
Ili kuona maendeleo halisi, utahitajika kuweka juhudi endelevu. Kama jinsi kupanda mlima kunavyohitaji matayarisho kabla na uvumilivu na ustahimilivu wakati wa kupanda, ndivyo pia safari hii itakavyohitaji juhudi na dhabihu halisi. Ukristo wa kweli, ambapo tunajitahidi kuwa kama Bwana wetu, daima umekuwa ukihitaji juhudi zetu bora zaidi. 16
Sasa neno fupi la tahadhari. Amri ya kuwa kama Yeye haikusudii kukufanya ujisikie mwenye hatia, usiye na thamani au usiyependwa. Uzoefu wetu wote wa maisha haya ni kuhusu kuendelea, kujaribu, kushindwa, na kufanikiwa. Kadiri ambavyo mimi na mke wangu tungetamani kwamba tungefumba macho yetu na kwa mazingaombwe tujisafirishe mpaka kileleni, hilo si kusudi la maisha.
Wewe ni mzuri vya kutosha, unapendwa, lakini hiyo haina maana kwamba umekamilika. Kuna kazi ya kufanya katika maisha haya na yajayo. Ni kwa usaidizi Wake wa kiungu pekee kwamba sote tunapiga hatua kuelekea kuwa kama Yeye.
Katika nyakati hizi, ambapo “mambo yote [yanaonekana] kuwa katika taharuki; na … hofu [inaonekana] juu ya watu wote,” 17 kiuasumu pekee, tiba pekee, ni kujitahidi kuwa kama Mwokozi, 18 Mkombozi 19 wa wanadamu wote, Nuru ya Ulimwengu, 20 na kumtafuta Yeye aliyetangaza, “Mimi ndimi njia.” 21
Ninajua kwamba kuwa kama Yeye kupitia usaidizi Wake na nguvu zake za kiungu kunawezekana hatua kwa hatua. Kama si hivyo, Yeye asingetupatia amri hii. 22 Ninalijua hili—kwa sehemu kwa sababu ninaziona sifa Zake kwa wengi wenu. Kwa mambo haya ninashuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.