Njoo, Unifuate 2024
Kiambatisho D: Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano.


“Kiambatisho D: Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Kiambatisho D,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024

Kiambatisho D

Kwa ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana—Ajenda ya Mkutano.

Tarehe ya mkutano:

Mwendeshaji (mshiriki wa darasa au urais wa akidi):

Ufunguzi

Wimbo (si lazima):

Sala:

Rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni.

Shaurianeni pamoja

Wakiongozwa na mtu anayeendesha mkutano, darasa au akidi hutumia dakika kama 5 hadi 10 kushauriana pamoja kuhusu wajibu wao katika kazi ya wokovu na kuinuliwa. Hii ni fursa kwa ajili ya urais wa darasa au akidi kufuatilia mambo yaliyojadiliwa katika mkutano wa urais au mkutano wa kata wa baraza la vijana.

Mtu mwenye kuendesha angeweza pia kutumia moja au zaidi ya maswali haya.

Kuishi injili

  • Ni tukio lipi la hivi karibuni limeimarisha ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo na injili Yake?

  • Ni kipi tunaweza kufanya ili tusogee karibu zaidi na Mwokozi? Ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Ni kwa jinsi gani tumehisi mwongozo wa Bwana katika maisha yetu?

Kuwajali wale wenye mahitaji

  • Ni nani tumehisi kuongozwa kumsaidia au kumhudumia? Ni majukumu yapi umeyapokea kutoka kwa uaskofu ili kumsaidia mtu aliye na shida?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayopitia?

  • Je, Kuna mtu amehamia karibuni kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wahisi kukaribishwa?

Kuwaalika watu wote waipokee injili

  • Ni kitu gani tunaweza kufanya ili kuwasaidia wengine wahisi upendo wa Mungu?

  • Je, kuna shughuli zipi zinazotarajiwa ambazo tunaweza kuwaalika marafiki zetu wahudhurie?

  • Ni mipango ipi ya kushiriki injili imejadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana la kata? Ni kwa jinsi gani darasa letu au akidi yetu inaweza kushiriki?

Kuunganisha familia milele

  • Ni kwa njia zipi tunaweza kuunganika vyema na wanafamilia ikijumuisha mababu na binamu zetu?

  • Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili tuwasaidie wengine wapate majina ya mababu zao?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki zaidi katika kazi ya hekalu—binafsi, na kama darasa au akidi?

Jifunzeni Pamoja

Kiongozi mtu mzima au mshiriki wa akidi au darasa huongoza maelekezo kuhusu kusoma Njoo, Unifuate kwa wiki hii. Yeye hutumia mawazo ya kujifunza katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani. Wazo la kujifunza lenye ikoni hii linaenda sambamba na seminari na linafaa hasa kwa vijana. Hata hivyo, wazo lolote la kujifunza linaweza kutumika. Sehemu hii ya mkutano kwa kawaida huchukua dakika 35 hadi 40.

Kufunga

Mtu anayeendesha mkutano huu.

  • Anatoa ushuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Anajadili jinsi darasa au akidi watakavyotenda juu ya kile ambacho wamejifunza—kama kundi au mtu binafsi.

Sala:

Chapisha