Njoo, Unifuate 2024
Kiambatisho C: Kwa ajili ya Msingi—Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti


“Kiambatisho C: Kwa ajili ya Msingi—Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Kiambatisho C,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024

Picha
watoto na mwalimu wakiimba

Kiambatisho C

Kwa ajili ya Msingi—Maelekezo kwa Ajili ya Muda wa Kuimba na Mawasilisho ya Watoto Kwenye Mkutano wa Sakramenti.

Nyimbo za Msingi ni zana yenye nguvu sana katika kuwasaidia watoto wajifunze kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni na kweli za msingi za injili ya Yesu Kristo. Wakati watoto wanapoimba kuhusu kanuni za injili, Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa kanuni hizo. Maneno na muziki vitakaa katika akili na mioyo ya watoto maisha yao yote.

Tafuta msaada wa Roho unapojiandaa kufundisha injili kupitia muziki. Toa ushuhuda wako juu ya kweli mnazoziimba. Wasaidie watoto waone jinsi muziki unavyohusiana na kile wanachopitia na kujifunza nyumbani na katika madarasa ya Msingi.

Miongozo kwa ajili ya Mawasilisho Kwenye Mkutano wa Sakramenti

Kwa maelekezo ya askofu, mawasilisho ya watoto kwenye mkutano wa sakramenti kwa kawaida hufanyika katika robo ya nne ya mwaka. Kama urais wa Msingi na kiongozi wa muziki, fanyeni kazi pamoja na mshauri katika uaskofu mwenye kusimamia Msingi ili kuanza kujadili mipango ya mawasilisho.

Mawasilisho yanapaswa kuwaruhusu watoto waoneshe kile ambacho wao na familia zao wamejifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni nyumbani na katika Msingi, ikijumuisha nyimbo za Msingi walizoziimba katika mwaka. Wakati ukipanga mawasilisho, fikiria njia ambazo mawasilisho hayo yanaweza kusaidia mkusanyiko kufokasi kwa Mwokozi na mafundisho Yake.

Matawi yenye idadi ndogo ya watoto yanaweza kufikiria njia ambazo wanafamilia wanaweza kushiriki pamoja na watoto wao. Mshiriki wa uaskofu anaweza kuhitimisha mkutano kwa hotuba fupi.

Wakati ukiandaa mawasilisho, kumbuka miongozo ifuatayo:

  • Mazoezi yasichukue muda usio wa lazima kutoka kwenye madarasa ya Msingi au familia.

  • Vitu vya kutazama, mavazi maalumu na mawasilisho ya kimtandao havifai kwa ajili ya mkutano wa sakramenti.

Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho12.2.1.2.

Maelekezo kwa ajili ya Muda wa Kuimba

Dakika 5 (Urais wa Msingi): Sala ya kufungua, andiko au makala ya imani, na hotuba moja

Dakika 20 (kiongozi wa muziki): Muda wa kuimba

Urais wa Msingi na kiongozi wa muziki huchagua nyimbo kwa ajili ya kila mwezi ili kuimarisha kanuni watoto wanazojifunza katika madarasa yao na nyumbani. Orodha ya nyimbo ambazo zinaimarisha kanuni hizi imejumuishwa katika mwongozo huu.

Unapofundisha nyimbo kwa watoto, waalike waeleze kile ambacho tayari wamejifunza kuhusu hadithi na kanuni za mafundisho zilizoko kwenye nyimbo. Waalike watoto watoe mawazo na hisia zao kuhusu kweli zinazopatikana katika nyimbo.

Kitabu cha Nyimbo za Watoto ni nyenzo ya muhimu kwa ajili ya muziki katika Msingi. Nyimbo kutoka kitabu cha nyimbo za dini na nyimbo kutoka kwenye gazeti la Rafiki pia zinafaa. Matumizi ya muziki wowote tofauti kwenye Msingi lazima yaidhinishwe na uaskofu (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla,12.3.4).

Picha
watoto wakiimba

Muziki kwa ajili ya Wakati wa Kuimba

Januari

  • Book of Mormon Stories,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 118–19

  • Keep the Commandments,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47

  • Fimbo ya Chuma,” Nyimbo za Dini, na. 158

Februari

  • Nephi’s Courage,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 120–21

  • I Feel My Savior’s Love,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75

  • Chagua Jema,” Nyimbo za Dini, na. 135

Machi

  • I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95

  • When I Am Baptized,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 103

  • Easter Hosanna,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 68–69

Aprili

Mei

  • Love One Another,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37

  • I Will Be Valiant,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162

  • Help Me, Dear Father,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 99

Juni

  • Ushuhuda,” Nyimbo za Dini, na. 69

  • We’ll Bring the World His Truth,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 172–73

  • Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11

Julai

  • I Want to Be a Missionary Now,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168

  • My Heavenly Father Loves Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29

  • Faith,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97

Agosti

Septemba

  • The Still Small Voice,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106–7

  • Samuel Tells of the Baby Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 36

  • I’m Trying to Be like Jesus,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79

Oktoba

  • Families Can Be Together Forever,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188

  • The Church of Jesus Christ,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77

Novemba

  • Dare to Do Right,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 158

  • Kristo Mwokozi,” Nyimbo za Dini, na. 66

Desemba

  • Search, Ponder, and Pray,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109

  • Away in a Manger,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 42–43

  • He Sent His Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35

Kutumia Muziki Kufundisha Mafundisho

Muda wa kuimba umekusudiwa kuwasaidia watoto wajifunze kweli za injili. Mawazo yafuatayo yanaweza kukuvutia wakati ukipanga njia za kufundisha kanuni za injili zinazopatikana katika nyimbo za dini na nyimbo za Msingi.

Soma maandiko yanayohusiana. Kwa nyimbo nyingi katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto na kitabu cha nyimbo za dini, marejeleo kwenye maandiko yanayohusiana yameorodheshwa. Wasaidie watoto wasome baadhi ya sehemu hizi, na zungumza kuhusu jinsi maandiko yanavyohusiana na wimbo. Ungeweza pia kuorodhesha marejeleo machache ya maandiko ubaoni na waalike watoto walinganishe kila rejeleo na wimbo au mstari kutoka kwenye wimbo.

Jaza nafasi zilizo wazi. Andika ubeti wa wimbo ubaoni kwa kuacha baadhi ya maneno muhimu. Kisha waombe watoto waimbe wimbo huo, na kusikiliza maneno ambayo yatajaza nafasi zilizoachwa wazi. Wakati wakijaza kila nafasi iliyo wazi, jadili kanuni zipi za injili mnajifunza kutokana na maneno yanayokosekana.

Picha
kiongozi wa muda wa kuimba

Toa ushuhuda. Toa ushuhuda mfupi kwa watoto kuhusu kweli za injili zinazopatikana kwenye wimbo wa Msingi. Wasaidie watoto waelewe kwamba kuimba ni njia mojawapo wanayoweza kutoa ushuhuda na kumhisi Roho.

Simama kama shahidi. Waalike watoto wafanye zamu kusimama na kueleza kile wanachojifunza kutoka kwenye wimbo wanaoimba au jinsi wanavyohisi kuhusu kweli zilizofundishwa katika wimbo. Waulize wanajisikiaje wakati wanapoimba wimbo na wasaidie watambue ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Tumia picha. Waombe watoto wakusaidie kupata au kutengeneza picha ambazo zinaendana na maneno muhimu au virai katika wimbo. Waalike waeleze ni jinsi gani picha zinahusiana na wimbo na kile ambacho wimbo unafundisha. Kwa mfano, kama unafundisha wimbo “Fimbo ya Chuma” (Nyimbo za Dini, na. 158), ungeweza kuweka picha kuzunguka chumba au chini ya viti zikionesha maneno muhimu kutoka kwenye wimbo (kama vile fimbo ya chuma, neno la Mungu, mwongozo, majaribu, na mbingu). Waombe watoto wakusanye picha na wazinyanyue juu katika utaratibu sahihi wakati mkiimba wimbo kwa pamoja.

Shiriki somo la vitendo. Unaweza kutumia vitendo ili kuhamasisha mjadala kuhusu wimbo. Kwa mfano, wimbo “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97 unaongelea kuhusu mbegu ndogo. Ungeweza kuwaonesha watoto mbegu na kuzungumza kuhusu jinsi tunavyoonesha imani pale tunapopanda mbegu; hii inaweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu njia tunazoonesha imani katika Yesu Kristo, kama ilivyoelezwa kwenye wimbo.

Alika ushiriki wa uzoefu binafsi. Wasaidie watoto waunganishe kanuni zilizofundishwa kwenye wimbo na uzoefu ambao wamekuwa nao wa kanuni hizo. Kwa mfano, kabla ya kuimba “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95), ungeweza kuwaomba watoto wainue mikono yao kama wamewahi kuona hekalu. Waalike, wanapoimba, wafikirie kuhusu jinsi wanavyoweza kuhisi wakati wanapoliona hekalu.

Uliza maswali. Kuna maswali mengi ambayo unaweza kuuliza wakati mnaimba nyimbo. Kwa mfano, unaweza kuwauliza watoto wanajifunza nini kutoka kwenye kila ubeti wa wimbo. Pia unaweza kuwaomba wafikirie maswali ambayo yanajibiwa na wimbo. Hii inaweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu kweli zinazofundishwa katika wimbo.

Tumia matendo rahisi ya mikono. Waalike watoto wafikirie kuhusu matendo rahisi ya mikono ili yawasaidie wakumbuke maneno na ujumbe wa wimbo. Kwa mfano, wakati mnapoimba ubeti wa pili wa “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29), ungeweza kuwaalika watoto waoneshe macho yao, waigize kama vipepeo, na waweke mikono yao katika umbo la mwimuko nyuma ya masikio yao. Waombe waweke mikono yao kwenye mioyo yao wakati wakiimba “Yes, I know Heavenly Father loves me.”

Chapisha