“Machi 14–20. Mwanzo 42–50: ‘Mungu Aliyakusudia kuwa Mema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)
“Machi 14-20. Mwanzo 42–50,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022
Machi 14-20
Mwanzo 42–50
“Mungu Aliyakusudia kuwa Mema”
Kusoma maandiko kunamualika Roho. Sikiliza ushawishi Wake wakati unaposoma, hata kama hauhusiani moja kwa moja na kile unachosoma.
Andika Misukumo Yako
Imekuwa zaidi ya miaka 22 tangu Yusufu auzwe Misri na kaka zake. Aliteseka kwa majaribu mengi, ikijumuisha na kushtakiwa kwa makosa ya uongo na kufungwa gerezani. Wakati alipowaona kaka zake tena, Yusufu alikuwa gavana wa Misri yote, wa pili kutoka kwa Farao. Angeweza kwa urahisi kabisa kulipa kisasi kwao, na ukizingatia kile wao walichomtendea Yusufu, hilo lingeeleweka. Na bado Yusufu aliwasamehe kaka zake. Siyo hilo tu, lakini yeye aliwasaidia kuona kusudi takatifu katika mateso yake. “Mungu aliyakusudia kuwa Mema” (Mwanzo 50:20), yeye aliwaambia, kwa sababu hilo lilimweka yeye katika nafasi ya kuokoa “kaya yote ya baba yake” (Mwanzo 47:12) kutokana na njaa.
Katika njia nyingi, maisha ya Yusufu yanarandana na yale ya Yesu Kristo. Ingawa dhambi zetu zilimsababishia Yeye mateso makuu, Mwokozi anatupatia msamaha, akitukomboa sisi sote kutokana na maangamizi makubwa kuliko njaa. Iwe sisi tunahitaji kupokea msamaha au kutoa—mahali fulani sisi sote tunahitaji kufanya vyote—mfano wa Yusufu unatuelekeza sisi kwa Mwokozi, aliye chanzo cha kweli cha uponyaji na usuluhishi.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko
“Mungu alinipeleka mbele yenu ili niwaokoe ninyi.”
Uliposoma kuhusu Yusufu, je, umegundua mifanano yo yote kati ya historia yake na misheni ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi? Unaweza kutafakari jinsi gani nafasi ya Yusufu katika familia yake inavyofanana na nafasi ya Mwokozi katika familia ya Mungu. Ni usawa gani unaouona kati ya matukio ya Yusufu na misheni ya Mwokozi, ambaye alitumwa “ili kutuokoa [sisi] kwa ukombozi mkuu”? (Mwanzo 45:7).
Msamaha huleta uponyaji.
Kusoma kuhusu Yusufu kuwasamehe kaka zake kwa mambo ya kutisha waliyomfanyia inaweza kukushawishi wewe kufikiria kuhusu mtu unayehangaika kumsamehe. Au pengine jaribio gumu la msamaha katika maisha yako ya baadae. Kwa lolote, inaweza kusaidia kutafakari kwa nini Yusufu aliweza kusamehe Vidokezo gani kuhusu tabia na mitazamo ya Yusufu unapata katika Mwanzo 45; 50:15–21? Je, ni kwa jinsi gani uzoefu wake umemshawishi yeye kuwa mwenye kusamehe zaidi? Je, mfano wa Yusufu unashauri nini kuhusu jinsi ya kuweza kuwa mwenye kusamehe zaidi kwa msaada wa Mwokozi?
Fahamu pia baraka ambazo zilikuja katika familia ya Yusufu kwa sababu ya msamaha wake. Je, ni baraka gani umeziona kutokana na msamaha? Je, unajisikia kushawishika kumfikia mtu ambaye amekukosea?
Ona pia Mwanzo 33:1–4; Mafundisho naa Maagano 64:9–11; Larry J. Echo Hawk, “Hata kama Kristo Anavyokusameheni Ninyi, Vivyo Hivyo Nanyi Fanyeni,” Liahona, Mei 2018, 15–16.
Je, uashiriaji katika baraka za Yakobo unamaanisha nini?
Baraka za Yakobo kwa wazao wake zina picha zilizo wazi, lakini baadhi ya wasomajji wanaweza pia kuziona ngumu kueleweka. Tunashukuru, injili ya urejesho inatupa uelewa wa ziada. Unaposoma baraka za Yusufu katika Mwanzo 49:22–26, soma mistari ifuatayo pia, na uone ni utambuzi gani inatoa: 1 Nefi 15:12; 2 Nefi 3:4–5; Yakobo 2:25; Mafundisho na Maagano 50:44.
Unaposoma kuhusu baraka za Yuda katika Mwanzo 49:8–12, kumbuka kwamba mfalme Daudi na Yesu Kristo ni wa ukoo wa Yuda. Je, ni maneno na kifungu gani cha maneno katika mistari hii kinakukumbusha juu ya Mwokozi? Unapojifunza baraka za Yuda, inaweza kusaidia pia kusoma Ufunuo 5:5–6, 9; 1 Nefii 15:14–15; Mafundisho na Maagano 45:59; 133:46–50.
Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu wana wa Yakobo na makabila ya Israeli ambayo yalitokana na wao, kuna ingizo kwa ajili ya kila mmoja katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).
Mwanzo 50:24–25; Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24–38 (katika kiambatisho cha Biblia)
“Mwonaji Bwana Mungu wangu atamwinua.”
Kupitia ndoto za Yusufu (ona Mwanzo 37:5–11) na tafsiri yake ya ndoto za wengine (ona Mwanzo 40–41), Bwana alifunua mambo haya ambayo yangetokea siku au miaka ya baadae. Lakini Bwana pia alifunua kwa Yusufu kile ambacho kingetokea katika karne zijazo. Mahususi, alijifunza kuhusu misheni za kinabii za Musa na Joseph Smith? Unaposoma maneno ya Yusufu katika Mwanzo 50:24–25 na katika Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24–38 (katika kiambatisho cha Biblia), jiulize mwenyewe jinsi kujua mambo haya kulivyoweza kumbariki Yusufu na wana wa Israeli. Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Bwana kurejesha unabii huu kupitia kwa Joseph Smith? (Ona pia 2 Nefi 3).
Je, ni kwa jinsi gani Joseph Smith ametimiza unabii katika Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50: 27–28, 30–33? (ona Mafundisho na Maagano 1:17–23; 20:7–12; 39:11; 135:3).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani
-
Mwanzo 42–46.Familia yako pengine ingefurahia kuigiza hadithi ya Yusufu kuungana tena na kaka zake. (“Yusufu na Njaa,”katika Hadithi za Agano la Kale pengine itasaidia.) Ifurahieni—tumieni mavazi na vitu vingine mkitaka. Wahimize washiriki wa familia kujaribu kuelewa hisia na mitazamo ya wahusika. Mnaweza mkafokasi hususani juu ya hisia za Yusufu kwa kaka zake na juu ya jinsi ambavyo wao yawezekana walijisikia wakati yeye alipowasamehe. Hii inaweza kuwaongoza kwenye mjadala kuhusu jinsi msamaha unavyoweza kubariki familia yenu.
Wakati Yusufu alipokutana na kaka zake tena baada ya miaka mingi, je, ni jinsi gani wao walionyesha kwamba wamebadilika tangu yeye alipowaona mara ya mwisho? Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu toba kutokana na tukio lao hili?
-
Mwanzo 45:3–11; 50:19–21.Yusufu alitambua kwamba ingawa tukio lake katika Misri limekuwa gumu, “Mungu aliyakusudia kuwa mema” (Mwanzo 50:20). Je, familia yako imewahi kupata majaribu yo yote ambayo Mungu aliyageuza kuwa baraka?
Wimbo kuhusu wema wa Mungu wakati wa majaribu (kama vile “How Firm a Foundation” [Nyimbo za Kanisa, na. 85]) ungeweza kuboresha mjadala huu. Je, ni maelezo gani kutoka kwenye matukio ya Yusufu ni mfano wa kile wimbo unachofundisha?
-
Mwanzo 49:9–11, 24–25.Je, tunapata nini katika mistari hii ambacho kinatufundisha kuhusu nafasi na misheni ya Yesu Kristo? (Kwa ajili ya msaada wa kuelewa vifungu vya maneno katika mistari hii, ona maelezo kuhusu Mwanzo 49 katika “Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko.”)
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “How Firm a Foundation,” Nyombo za Kanisa, na. 85.