Njoo, Unifuate
Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto


“Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto

Nyenzo hizi zote zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kubadilisha shughuli kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika darasa lako la Msingi. Usiwe na hofu kama watoto tayari wamekwishafanya shughuli hizi pamoja na familia zao nyumbani; marudio husaidia watoto kujifunza. Watoto wanaweza kuhitaji kukuambia jinsi walivyofanya shughuli pamoja na familia zao na kile walichojifunza.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kwa kuongezea kwenye matoleo ya machapisho ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za picha na video ya nyimbo nyingi za Kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika LDS Music na LDS Media Library apps.

Tazama Watoto Wako

Mada nyingi zinazofundishwa katika kitabu cha Kiada cha chekechea Tazama Watoto Wako: Kitabu cha Kiada cha Chekechea zinafanana na zile utakazofundisha katika Msingi. Hususani kama unafundisha watoto wadogo, fikiria kuangalia katika kitabu cha kiada cha chekechea kwa ajili ya nyimbo za ziada, hadithi, shughuli, na ufundi.

Magazeti ya Friend na Liahona

Magazeti ya Friend na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuongezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Hadithi za Kitabu cha Mormoni

Hadithi za Kitabu cha Mormoni zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika medialibrary.ChurchofJesusChrist.org.

Maktaba ya Vyombo vya Habari

Sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia watoto kutazama mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Tembelea medialibrary.ChurchofJesusChrist.org kupitiapitia mkusanyiko wa Kanisa wa nyenzo za vyombo vya habari, ikijumuisha mkusanyiko wa Video za Kitabu cha Mormoni, ambazo zinaonyesha kwa michoro matukio katika Kitabu cha Mormoni. Nyenzo za vyombo vya habari pia zinapatikana kwenye LDS Media Library app.

Sanaa ya Injili

Sanaa inaweza kuwasaidia watoto kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Kitabu cha Mormoni. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili, katika medialibrary.ChurchofJesusChrist.org, na kwenye LDS Music na LDS Media Library apps.

Kweli katika Imani

Ikiwa unahitaji msaada wa ziada kuelewa kanuni za msingi utakazowafundisha watoto, fikiria kuangalia katika Kweli katika Imani. Rejeleo hili linatoa maelezo rahisi ya mada za injili, zilizoorodheshwa kwa utaratibu wa alfabeti.

watoto wakiimba

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu na kutumia kanuni za mafundisho ya Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kutumiwa katika mikutano ya baraza la walimu.