“Kukidhi Mahitaji ya Watoto wenye Ulemavu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Kukidhi Mahitaji ya Watoto wenye Ulemavu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020
Kukidhi Mahitaji ya Watoto wenye Ulemavu
Viongozi wa msingi wanawajibika kufundisha injili ya Yesu Kristo kwa watoto wote, ikijumuisha wale wenye ulemavu. Katika msingi, kila mtoto anapaswa kukaribishwa, kupendwa, kutunzwa, na kujumuishwa. Katika mazingira haya ni rahisi kwa watoto wote kuelewa upendo wa Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuhisi na kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu. Mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu.
-
Jifunze kuhusu mahitaji maalumu ya mtoto. Njia nzuri ya kufanya hivi ni kuzungumza na wazazi wa mtoto au watoa huduma. Tafuta ni kwa jinsi gani mtoto anajifunza vizuri zaidi na mbinu zipi zina msaada zaidi. Ungeweza pia kushauriana na viongozi wengine na walimu wa Msingi ambao wana uzoefu na utambuzi wa kushiriki.
-
Tengeneza mazingira chanya ambapo kila mtoto anahisi salama na kupendwa. Jifunze majina ya watoto wote katika darasa lako, na wasaidie kuhisi kukubaliwa, kupendwa, na kujumuishwa. Watoto wenye ulemavu mara nyingi wanakosolewa, hivyo tafuta fursa za kuwasifu kwa tabia chanya.
-
Fanya urekebishaji ili kwamba kila mmoja aweze kushiriki. Mabadiliko madogo madogo yanaweza kufanywa kwenye shughuli ili kuhakikisha kwamba watoto wote wanaweza kujifunza, ikijumuisha wale wenye mapungufu ya kimaumbile au wenye shida ya kujifunza. Kwa mfano, kama shughuli inapendekeza kuonyesha picha, mnaweza kuimba wimbo unaohusiana kama mbadala ili kujumuisha watoto wenye mapungufu ya kuona.
-
Imarisha utaratibu na muundo endelevu wa darasa. Njia moja ya kufanya hivi ni kutengeneza bango lenye ratiba ya darasa likionyesha jinsi darasa litakavyoenda. Ratiba yako ingeweza kujumuisha sala, muda wa kufundisha, na muda wa shughuli. Hii inaweza kusaidia kupunguza hisia za mashaka ambazo zinaweza kuongeza wasiwasi kwa baadhi ya watoto.
-
Tumia ishara za kuonekana kwa macho. Watoto wenye ulemavu wa kuona au changamoto za tabia wanaweza kunufaika kutokana na ishara za kuonekana kwa macho, kama vile picha zinazoonyesha mtindo wa tabia zinazofaa kama kuinua mkono juu kabla ya kujibu swali.
-
Elewa kwa nini tabia zenye kuleta changamoto hutokea. Jifunze kuhusu ulemavu au hali ambazo zinaweza kushawishi mtoto kutenda isivyofaa. Kuwa makini sana kwenye kile kinachofanyika wakati tabia zenye kuleta changamoto zinapojitokeza. Kwa sala fikiria jinsi ya kurekebisha hali ili kumsaidia mtoto vizuri zaidi.