Njoo, Unifuate
Oktoba 21–27. 1 na 2 Wathesalonike: ‘Msifadhaishwe Upesi hata Kuiacha Nia Yenu, wala Msisitushwe’


“Oktoba 21–27. 1 na 2 Wathesalonike: ‘Msifadhaishwe Upesi hata Kuiacha Nia Yenu, wala Msisitushwe’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Octoba 21–27. 1 na 2 Wathesalonike,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Dada wamisionari wakizungumza na kijana

Oktoba 21–27

1 na 2 Wathesalonike

“Msifadhaishwe Upesi hata Kuiacha Nia Yenu, wala Msisitushwe”

Unaposoma kwa sala 1 na 2 Wathesalonike watoto wakiwa akilini mwako, utapata kanuni ambazo wao wanahitaji kuelewa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Katika somo la wiki iliyopita, uliwaalika watoto kutumia kile walichojifunza kwa namna fulani? Waache watoto watumie dakika chache za mwanzo za darasa la wiki hii kushiriki uzoefu wao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

1 Wathesalonike 5:1–6

Ninapotii amri za Mungu, nitakuwa tayari kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

Ushauri wa Paulo unaweza kutusaidia kuwa tayari na kuitazamia siku ile kuu wakati Mwokozi anapokuja duniani tena.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mama mmoja kuzungumza kuhusu ilikuwaje kwake yeye kusubiri kuzaliwa kwa mtoto wake bila kujua kwa uhakika lini kuzaliwa huko kungetokea. Soma 1 Wathesalonike 5:2–3, na waeleze watoto kwamba Yesu Kristo atakuja duniani tena, lakini hakuna ajuaye kwa uhakika lini—kama vile mama asivyojua kwa uhakika lini mtoto atazaliwa.

  • Waombe watoto kuzungumza kuhusu muda walipojitayarisha kwa ajili ya matembezi au tukio. Walifanya nini ili kujiatayarisha? Lete saduku au begi na waache watoto wajifanye wanalipakia katika matayarisho ya safari au tukio. Eleza kwamba tunajitayarisha kwa ajili ya Yesu Kristo kuja tena kwa kusali, kusoma maandiko, kumfuata nabii, na kuishi kwa uaminifu kila siku. Waombe watoto kuchora picha za jinsi wanavyoweza kufanya hivi na kuziweka katika sanduku.

  • Wasomee watoto 1 Wathesalonike 5:6 na ueleza kwamba kama hatujajitayarisha kwa ajili ya Yesu kuja tena, ni kama tumelala usingizi na hatutakuwa tayari kwa ajili yake. Waalike watoto kujifanya wamelala. Eleza kwamba kama tunajitayarisha, ni kama tumeamka na tunamsubiri Yeye. Waalike kuamka. Imbeni pamoja “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82—83).

2 Wathesalonike 2:1–3

Paulo alifundisha kwamba Ukengeufu ungetokea kabla ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

Kanisa ambalo Yesu Kristo alilianzisha hatimaye lilianguka kwenye ukengeufu, inamaanisha kwamba mamlaka ya ukuhani na ukweli wa injili viliondolewa kutoka duniani. Paulo alitabiri kwamba ukengeufu huu, au “kupotoka”, kungetokea kabla ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Baada ya kusoma 2 Wathesalonike 2:3 pamoja na watoto, jenga mnara kutokana na vikombe vya plastiki au matofali. Waambie watoto kwamba vikombe au matofali vinawakilisha sehemu muhimu za Kanisa la kweli, kama vile ukweli wa injili, ukuhani, kuunganishwa hekaluni, na manabii. Baada ya Paulo na Mitume wengine kufariki, mambo haya yalipotea, na Kanisa la kweli halikuwepo duniani kwa miaka mingi. Mwalike mtoto kugonga na kuangusha mnara, na eleza kwamba hii iliitwa Ukengeufu au “kupotoka.” Wakati Yesu Kristo aliporudisha Kanisa lake, kuliitwa Urejesho. (Ona ”Ukengeufu,” Kweli kwa Imani, 13–14.)

  • Onyesha Kitabu cha Mormoni na picha za nabii na hekalu. Waombe watoto waseme “ukengeufu” wakati unaficha vitu hivyo katika mfuko na “ Urejesho” wakati unapovitoa vitu hivyo nje.

  • Imbeni nyimbo ambazo zinafundisha ukweli ambao uliondolewa wakati wa Ukengeufu na kurejeshwa katika siku yetu, kama vile “Mimi ni Mtoto wa Mungu,” “ The Church of Jesus Christ,” na “I Love to See the Temple” na (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3, 77, 95).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

1 Wathesalonike 5:1–6

Ninapotii amri za Mungu, nitakuwa tayari kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

Ushauri wa Paulo unaweza kutusaidia kuwa tayari na kuitazamia siku ile kuu wakati Mwokozi anapokuja duniani tena.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtoto asome 1 Wathesalonike 5:1–6 wakati watoto wengine wakifuatilia . Baada ya kila aya, muombe mtoto kufanya muhtasari wa kile yeye anafikiri aya hiyo inasema. Unaweza kutaka kueleza kwamba “siku ya Bwana” maana yake ni Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Je, ni kwa nini watoto wanafikiri Ujio wa Pili unafananishwa na mwizi wa usiku au mwanamke karibu ya kujifungua?

  • Waambie watoto wafikirie kwamba Mwokozi atatembelea darasa lenu wakati fulani leo. Tunawezaje kutayarisha madarasa yetu kwa ajili ya ziara yake? Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo tunayoweza kufanya ili kujitayarisha kwa ajili ya siku ambayo Yesu Kristo atakaporudi. Kwa mfano, tunaweza kutubu, kusamehe, kuendeleza uhusiano wetu na familia zetu, kumfuata nabii, na kushika maagano yetu. Watie moyo watoto kuchagua kitu kimoja watakachofanya ili kujitayarisha wenyewe kumpokea Mwokozi wakati wa Ujio Wake.

2 Wathesalonike 2:1–3

Paulo alifundisha kwamba Ukengeufu ungetokea kabla ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

Kama watoto wanaelewa kwamba Kanisa la Yesu Kristo na injili Yake viliondolewa kutoka duniani wakati wa Ukengeufu Mkuu, umuhimu wa Urejesho utakuwa wazi zaidi kwao.

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mmoja wa watoto asome 2 Wathesalonike 2:1–3. Kulingana na aya hizi, nini kingetokea kabla ya “siku ya Kristo” ambayo ina maana ya Ujio wa Pili Je, kuna mtoto yoyote anayejua “kuanguka” maana yake nini? Hakikisha kwamba watoto wanaelewa inamaanisha Ukengeufu Mkuu, ambao ulitokea baada ya vifo vya Mitume wa Mwokozi. Unaweza kutaka kushiriki taarifa kutoka ”Ukengeufu,” Kweli kwa Imani, 13–14.

  • Wasaidie watoto kuorodhesha ubaoni baadhi za kweli na baraka tunazofaidi kwa sababu ya injili. (Baadhi ya mifano ni pamoja na mahekalu, manabii, ukuhani, na karama za Roho Mtakatifu.) Futa vitu hivi kimoja kimoja, na waulize watoto jinsi gani maisha yao yangekuwa tofauti bila vitu hivi. Elezea kwamba kweli hizi zilipotea wakati wa Ukengeufu Mkuu. Kwa nini ilikuwa muhimu kwamba Kanisa la Yesu Kristo lirejeshwe duniani katika siku za mwisho? Waalike watoto “kurejesha” au kuandika upya ukweli na baraka ubaoni.

2 Wathesalonike 3:7–13

Baba wa Mbinguni ananitaka nifanye kazi.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuona kazi kama baraka, sio kitu cha kukwepa?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma aya kutoka 2 Wathesalonike 3:7–13 na kutafuta matatizo ambayo Watakatifu walikuwa wanakabiliana nayo. Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anataka tufanye kazi? Je, kingetokea nini kama katu hatungejifunza kufanya kazi kwa bidii? Waache watoto wachukue zamu kuigiza kazi za kawaida za kila siku wakati watoto wengine wanakisia nini wanachokifanya.

  • Waalike watoto wazungumze kuhusu wakati ambapo walifanya kazi kwa bidii kwenye kazi, mradi au lengo. Walijisikiaje wenyewe walipomaliza? Inamaanisha nini kuwa “msichoke katika kufanya mema”? (2 Wathesalonike 3:13).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumwambia mwana familia au rafiki sababu moja ya kushukuru kuwa tuna injili duniani leo (ukurasa wa shughuli wa wiki hii unaweza kuwasaidia kukumbuka).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie wazazi wa watoto. “Wazazi ni walimu muhimu sana wa injili kwa watoto wao—wana vyote jukumu kuu na nguvu kubwa zaidi ya kuwashawishi watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–7). Unapofundisha watoto Kanisani, kwa maombi tafuta njia za kuwasaidia wazazi wao katika jukumu lao muhimu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha