Njoo, Unifuate
Oktoba 12–18. 3 Nefi 20–26: “Ninyi ni Watoto wa Agano”


“Oktoba 12-18. 3 Nefi 20–26: Ninyi ni Watoto wa Agano,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Oktoba 12–18. 3 Nefi 20–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Kristo akiwatokea Wanefi

Mchoro wa Kristo akiwatokea Wanefi na Andrew Bosley

Oktoba 12–18.

3 Nefi 20–26

“Ninyi ni Watoto wa Agano”

Acha roho aongoze kujifunza kwako 3 Nefi 20–26. Atakusadia kutambua kanuni ambazo zitakuwa na maana maalum kwa watu unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Baada ya kusoma kwa pamoja maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 23:1, ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa nini walichokitafuta katika wiki hii wakati wakisoma maandiko. Je, walipata nini?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

3 Nefi 20:25–41; 21:9–11, 22–29

Katika siku za mwisho, Mungu atafanya kazi kubwa na ya kushangaza.

  • Mwokozi alizungumza kuhusu “kazi kubwa na ya kushangaza” (3 Nefi 21:9) ambayo Baba Yake angeifanya katika siku za mwisho. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu kazi hiyo wakati wakisoma sura hizi nyumbani. Maswali kama haya yangeweza kutia msukumo majadiliano: Je, Mwokozi alisema nini kingetokea katika siku zijazo? (Ona hasa 3 Nefi 20:30–32, 39–41; 21:22–29). Je, kwa nini aliviita vitu hivi “vikubwa” na “vya kushangaza”? Je, ni ushuhuda gani tunao kwamba kazi hii inatendeka? Je, tunaishiriki vipi?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi Nabii Joseph Smith alivyosaidia kutimiza kazi kubwa ya na ya kushangaza ya Bwana, ungeweza kuonyesha picha ya Nabii na kulialika darasa kusoma 3 Nefi 21:9–11, wakitafuta maneno na virai ambavyo vinawakumbusha maisha na huduma ya Joseph Smith. Kwa mfano, ni kwa namna ipi Bwana “alimpatia nguvu kwamba ataleta [injili] kwa Wayunani”? (mstari wa 11). Je, kuna umuhimu gani kujua kwamba huduma ya Joseph Smith ilitabiriwa na Mwokozi? (Ona pia 2 Nefi 3).

  • Pia ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuona wao wenyewe katika kazi iliyotabiriwa katika sura hizi kwa kusoma kwa pamoja 3 Nefi 20:25–27. Kama italazimu, ungeweza kuwaonyesha kwamba tunapoweka maagano na Bwana, tunakuwa wa uzao wa Ibrahimu. Je, ni kwa namna gani sisi kama uzao wa Ibrahimu tunabariki “makabila yote ya dunia”? (Mstari wa 25). Washiriki wa darasa wangeweza kutafakari swali hili wakati wakisoma maelezo ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Zaida” na kushiriki mawazo yao.

3 Nefi 23; 26:1–12

Mwokozi anatutaka tupekue maandiko.

  • Je, uhusiano wa Mwokozi na Wanefi unaonyesha nini kuhusu Anavyohisi kuhusu maandiko? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata jibu, ungeweza kuwaomba nusu yao kusoma 3 Nefi 23 na nusu nyingine kusoma 3 Nefi 26:1–12; kisha wangeweza kushiriki na kila mmoja kile walichopata. Wangeweza pia kushiriki mawazo waliyonayo kuhusu jinsi ya kumuonyesha Bwana kwamba maandiko ni muhimu kwetu. Kwa mfano, Je, kuna tofauti gani kati ya kupekua maandiko na kuyasoma tu? (Ona 3 Nefi 23:1).

3 Nefi 24:1–6

Bwana ni kama moto wa mtakasaji.

  • Sanaa za kuonekana zinaweza kuongezea katika majadialiano yako ya 3 Nefi 24:1–6. Kwa mfano, ungeweza kuonyesha sarafu ya madini ya fedha au sabuni wakati washiriki wa darasa wakisoma mistari kutafuta jinsi vitu hivi vinahusiana na Mwokozi na kazi Yake. Pia ungeweza kushiriki pamoja na darasa ufafanuzi wa utakasaji wa madini ya fedha na sabuni ya mtakasaji katika “Nyenzo za Zaida.” Au ungeweza kuonyesha video “The Refiner’s Fire” (ChurchofJesusChrist.org). Je, ni kwa namna gani Bwana ni “kama moto wa msafishaji, na kama sabauni ya mtakasaji”? (mstari wa 2). Je, mifano hii hutufundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anvyotutakasa?

3 Nefi 24:7–18

Mungu ni mwenye rehema kwa wale wanaorudi Kwake.

  • Ungeweza kuonyesha kwamba mafundisho kuhusu zaka katika 3 Nefi 24:8–12 yanajibu swali katika mstari wa 7: “tutamrudia [Bwana] kwa namna gani?” Je, ni uhusiano gani upo kati ya “[kumrudia] [Bwana]” na kulipa zaka? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyopokea baraka zilizoorodheshwa katika mstari wa 10–12 wakati wamelipa zaka. Je, ni kwa namna ipi kweli hizi zinaweza kumsaidia mtu fulani ambaye anahangaika na ulipaji wa zaka?

  • Je, ni tabia ipi inayoelezewa katika 3 Nefi 24:13–15 mara nyingi hupatikana katika dunia ya leo? Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho wangesema kwa mtu fulani ambaye anahisi kwamba maisha ni rahisi au mazuri zaidi kwa wale ambao hawatii amri. Kulingana na 3 Nefi 24, Je, ni kwa namna gani Bwana huwabariki wale wanaomtumikia Yeye? Pia ungeweza kuwatia moyo kupata mifano katika 3 Nefi 22. (Ona pia Mosia 2:41; Alma 41:10.)

3 Nefi 25:5–6

Mioyo yetu haina budi kuwageukia mababu zetu.

  • Ili kufafanua wazo la kugeuza mioyo yetu kuwaelekea mababu zetu, ungeweza kumualika mshiriki wa darasa kugeuka nyuma na kuwaelezea washiriki wa darasa toka katika kumbukumbu (wapi wamekaa, walichovaa, na kadhalika). Kisha angegeuka kueleke darasa na kujaribu tena. Je, mfano huu unaweza kutufundisha nini kuhusu kugeuza mioyo yetu kuwaelekea mababu zetu kupitia kazi ya hekalu na historia ya familia? Baada ya kusoma 3 Nefi 25:5–6, pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi mioyo yao imewageukia mababu zao. Ungeweza pia kumualika mshauri wa kata wa historia ya familia na kazi ya hekalu kuwatambulisha katika baadhi ya nyenzo za historia ya familia. Je, ni kwa namna gani kazi hii inahusiana na ukusanyaji wa Waisraeli ulioelezewa na Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Zaida”?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Katika 3 Nefi 274 Nefi tunasoma kuhusu watu wenye “[furaha zaidi] kati ya watu wote ambao wamewahi kuumbwa kwa mkono wa Mungu” (4 Nefi 1:16). Pendekeza kwa darasa kwamba kusoma sura hizi kungeweza kutusaidia kujifunza jinsi ya kupata furaha kwa nafsi zetu wenyewe na familia zetu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Unaweza kuwa sehemu ya kitu kikuu.

Rais Russell M. Nelson alitamka:

“Hakika hizi ni siku za mwisho, na Bwana anaharakisha kazi Yake ya kuikusanya Israeli. Kukusanywa huko ni kitu muhimu sana kinachofanyika duniani hivi leo. Hakulinganishwi na chochote katika ukubwa, hakulinganishwi na chochote katika umuhimu, hakulinganishwi na chochote katika utukufu. Na kama utachagua, kama unataka, unaweza kuwa sehemu kubwa ya hilo. Unaweza kuwa sehemu kubwa ya kitu kikubwa, kitu kikuu, kitu kitukufu!

“Tunapozungumza kuhusu kukusanywa, kiurahisi tunasema kanuni hii ya kweli: Kila mmoja wa watoto wa Baba wa Mbinguni, katika pande zote za pazia, anastahili kusikia ujumbe wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. …

“… Fikiria hilo! Kati ya watu wote ambao wamewahi kuishi katika sayari ya dunia, sisi ni moja ya wale tunaopata nafasi ya kushiriki katika mwisho huu, tukio la mkusanyiko mkuu. Ni ya kupendeza kiasi gani! …

Kukusanyika huku hakuna budi kumaanisha kila kitu kwako. Hii ni kazi ambapo wewe ulitumwa kwayo duniani” (“Tumaini la Israeli” [matangazo ya ulimwenguni kote kwa ajili ya vijana, juni 3, 2018], broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).

Kusafisha na kutakasa.

Madini ya fedha hupatikana yakiwa yamechanganyika na madini mengine ya chuma. Zamani, msafishaji wa madini ya fedha angepata madini hayo kwa kuweka mchanganyiko wa chuma katika tanuru lenye joto kubwa sana. Hii ingesababisha taka (vitu visivyohusika au madini yasiyotakiwa) kupanda juu ya myeyuko wa chuma. Msafishaji angetoa taka, akiacha madini ya fedha safi, ambapo yangeweza kutambulika kwa uangavu wake wa kipekee

Mtakasaji alikuwa ni mtu ambaye alisafisha nguo na kuzifanya kuwa angavu. Nguo zingezamishwa majini zikichanganywa na “sabuni ya mtakasaji,” ambayo ilikuwa imetengenezwa kuondoa mafuta na uchafu. Wakati nguo ikiwa imelowekwa, matakasaji angeipigapiga au kuikandamiza kuondoa taka. (Ona “Moto wa Msafishaji na Sabuni ya Mtakasaji,” New Era, Juni 2016, 6–7.)

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fokasi kwa Watu, Sio Masomo. “Jinsi unavyowatendea watu ni muhimu sawa na kama vile yale unayowafundisha. Mara nyingine kushughulika kwetu zaidi na kuwasilisha somo kunaweza kutuzuia kuonyesha upendo wetu kwa wale tunaowafundisha. Ikiwa hili litakutokea, fikiria jinsi ambavyo unaweza kuzingatia katika kile kilicho muhimu zaidi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,6)

Chapisha