Njoo, Unifuate
Septemba 28–Oktoba 11. 3 Nefi 17–19: “Tazama Shangwe Yangu ni Tele”


“Januari 28–Oktoba11. 3Nefi 17–19: ‘Tazama shangwe Yangu ni Tele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)

“Septemba 28–Oktoba 11 . 3 Nefi 17–19 Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Yesu akiwatokea Wanefi

Mwangaza wa Mwonekano Wake Uling’aa juu Yao, na Gary L. Kapp

Septemba 28–Oktoba11

3 Nefi 17–19

“Tazama Shangwe Yangu ni Tele”

Maandalizi yako ya kufundisha hayana budi kuanza kwa wewe kujifunza maandiko. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kujifunza kwako, na muhtasari huu pia unaweza kutoa mawazo kwako kukusaidia kujiandaa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Katika 3 Nefi 17:1–3, Mwokozi aliwaalika watu kurudi nyumbani na “kuandaa mawazo [yao]” kabla ya kurudi kufundishwa tena. Ungeweza kuwauliza wanafunzi jinsi walivyojiandaa kwa majadiliano ya leo na nini walikitafakari.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

3 Nefi 17; 18:24–25, 28–32

Mwokozi ndiye mfano wetu kamili wa utumishi.

  • Sote tuna fursa za kuhudumia wengine, na sote tunaweza kuwa bora katika hili. Njia mojawapo ya kujifunza kutoka kwenye mfano wa Mwokozi wa kuhudumu ni kwa kusoma 3 Nefi 17 kama darasa na kuwaalika washirikiwa darasa kutoa maoni kila wanapopata kitu ambacho kinawafundisha wao kuhusu kuhudumu. Je, tunajifunza nini kuhusu sifa ya Mwokozi ambayo ilimfanya Yeye kuwa mfano mkubwa wa uhudumu? Ni kweli zipi tunazojifunza kuhusu kuhudumu kutoka kwenye mfano wa Mwokozi? Pia ungeweza kutafuta umaizi wa ziada katika 3 Nefi 18:24–25 na 28–32. Washirikiwa darasa wangeweza kujadili vitu maalum ambavyo wanahisi msukumo kuvifanya ili kufuata mafano wa Mwokozi wa uhudumu.

    Picha
    Yesu Anawabariki Watoto wa Wanefi

    Tazama Watoto wenu na Gary L. Kapp

3 Nefi 17:13–22; 18:15–25; 19:6–9, 15–36

Mwokozi alitufundisha jinsi ya kusali.

  • Ili kuwasaidia washirikiwa darasa kujifunza kutoka katika mifano mingi ya sala na kufundisha kuhusu sala katika 3 Nefi 17–19, ungeweza kuandika ubaoni Nani? Kwa njia gani? Wakati gani? na Kwa nini? Na alika darasa kutafuta majibu ya maswali haya yakihusishwa na sala katika mistari ifuatayo: 3 Nefi 17:13–22; 18:15–25; na 19:6–9, 15–36. Je, ni umaizi gani mwingine washiriki wa darasa wanaupata wakati wakisoma mistari hii? Kauli ya Mzee Richard G. Scott katika “Nyenzo za Ziada” ingeweza kuongezea katika mjadala huu. Ungeweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki nini wanachokifanya kufanya sala zao binafsi na kama familia kuwa zenye maana zaidi 3 Nefi 18:18–21).

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza maswali ya kutafakari kuhusu sala wakati wa kusoma mistari hii Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki umaizi wowote ambao wanao kuhusu maswali haya. Au ungeweza kuwaalika baadhi ya washirikiwa darasa kuja darasani wakiwa wamejiandaa kujadili kitu walichojifunza kuhusu sala kutoka 3 Nefi 17–19. Je, walipata msukumo wa kufanya nini kuzifanya sala zao kuwa zenye maana zaidi?

  • Yesu alifundisha kwa nini hatuna budi kusali daima (ona 3 Nefi 18:15–18). Somo kwa vitendo linaweza kusaidia darasa lako kuelewa kile Alichofundisha. Kwa mfano, ungeweza kujaza chombo kwa maji kuwakilisha ushawishi wa Shetani. Jaza karatasi nyepesi (zinazotuwakilisha sisi) vizuri kwenye kitako cha kikombe (ambayo huwakilisha kusali daima). Geuza kikombe juu chini, na kisukume moja kwa moja chini kwenye chombo chenye maji. Karatasi nyepesi zitabakia kavu katika kitako cha kikombe, hata kama zimezungukwa na maji. Je, somo hili kwa vitendo na 3 Nefi 18:15–18 vinatufundisha nini kuhusu sala? ( ona pia Mafundisho na Maagano 10:5). Inamaanisha nini “kusali daima”? Je, sala inawezaje kutusaidia kujizuia na ushawishi wa Shetani? Fikiria kuwapa washirki wa darasa muda kidogo kuandika kile wanachokihisi kufanya ili kuboresha sala zao.

3 Nefi 18:1–12

Tuanaweza kujazwa kiroho wakati tunaposhiriki sakramenti

  • Kwa kuanza majadiliano kuhusu mafundisho ya Mwokozi kuhusu sakramenti katika 3 Nefi 18, ungeweza kuligawanya darasa katika makundi na kulipa kila kundi moja kati ya maandiko yafuatayo kuyasoma na kuyajadili Mathayo 26:26–28; 3 Nefi 18:1–12; na Mafundisho na Maagano 20:75–79; 27:1–4. Baada ya sehemu walizopewa, kila kundi lingeweza kufikiria swali au maswali mawili kuhusu sakramenti ambayo yanajibiwa katika mistari ambayo wamesoma na kuandika maswali yao ubaoni. Kisha sehemu ya darasa iliyobaki wangechunguza maandiko kwa ajili ya majibu ya maswali hayo. Washirikiwa darasa wangeweza kujadili jinsi wanavyoweza kuwa na uzoefu bora zaidi wa kushiriki sakramenti.

  • Je, ina maanisha nini “kujazwa” pale tunaposhiriki sakaramenti? (Ona 3 Nefi 18:4–5, 9; 20:9 Fikiria kuwaalika wshirikiwa darasa kujadili swali hili katika jozi wakati wakisoma 3 Nefi 18:1–12 kwa pamoja. Pia ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafakari mara ya mwisho walipohisi ‘kujazwa” kiroho wakati waliposhiriki sakramenti. Pengine wangeweza kujadiliana vitu ambavyo vingeweza kutuzuia kuweza “kujazwa” kupitia sakramenti na kushiriki mawazo ya jinsi ya kuvishinda vikwazo hivyo.

3 Nefi 19:9–15, 20–22

Wanafunzi wa Yesu hutafuta vipawa vya Roho Mtakatifu.

  • Fikiria kuwauliza washirikiwa darasa kufikiria juu ya kitu fulani wanachokitamani kwa dhati. Je, wako tayari kufanya nini kukipata? Hii ingeweza kupelekea majadiliano kuhusu kile wanafunzi kumi na wawili “walitamani kwa dhati,” kama ilivyoelezewa katika 3 Nefi 19: 9–15 na 20:22. Je, kwa nini hili lilikuwa la muhimu sana kwao? Kwa nini ni muhimu kwetu? Kulingana na mistari hii, ni kwa jinsi gani tunaweza kwa dhati kutafuta uwepo wa Roho Mtakatifu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Bwana alisema, “Maneno ya Isaya ni makuu” (3 Nefi 23:1). Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma 3 Nefi 20–26, ungeweza kuwaambia kwamba katika sura hizi, Yesu alifafanua baadhi ya maneno “makuu” ya Isaya. Waalike washirikiwa darasa kutafakari kwa nini maneno haya ya Isaya ni makuu. Wahimize kuja wakiwa wamejiandaa jumapili ijayo kushiriki kile wanachojifunza.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Thamani ya Sala.

Mzee RichardG. Scott alishuhudia juu ya thamani ya sala:

“Tunasali kwa Baba yetu wa Mbinguni katika jina takatifu la Mwana Wake Mpendwa, Yesu Kristo. Sala huwa na uwezo zaidi wakati tukijitahidi kuwa wasafi na watiifu, kwa madhumuni stahiki, na tukiwa tayari kile Anachotuamuru. Wanyenyekevu, kuamini katika sala huleta mwelekeo na amani.

“Usiwe na wasiwasi kuhusu hisia zako ambazo zimeelezewa bila mpangilio. Wewe zungumza tu na Baba yako mwelewa, mwenye upendo. Wewe ni mtoto Wake wa thamani ambaye Anampenda kikamilifu na Anataka kumsaidia. Wakati ukisali, tambua kwamba Baba wa Mbinguni yu karibu na Yeye anasikiliza.

“Ufunguo wa kuboresha sala ni kujifunza kuuliza maswali sahihi. Fikiria kubadilisha kuomba vitu ambavyo unataka kwenda katika kutafuta kwa dhati Yeye nachokitaka kwa ajili yako. Tena wakati ukijifunza mapenzi Yake, sali kwamba utaongozwa katika kuwa na nguvu ya kuyatimiza.

“Kama utahisi kuwa mbali na Baba yako, inaweza kuwa ni kutokana na sababu nyingi. Kwa sbabu yoyote ile, wakati ukiendelea kuomba msaada, Yeye atakuongoza kufanya kile ambacho kitarudisha ujasiri wako kwamba Yu karibu. Sali hata kama hauna hamu ya kusali. Wakati mwingine, kama mtoto, unaweza kutokuwa na tabia njema na kuhisi huwezi kumsogelea Baba yako ukiwa na tatizo. Huo ndio wakati unaohitaji sala zaidi. Kamwe usihisi kutostahili kusali.

“Ninashangaa kama tunaweza kupima uwezo wa nguvu ya sala mpaka pale tutakapo kabiliana na tatizo la kutushinda nguvu na la dharura na kutambua kwamba hatuna nguvu ya kutatua. Ndipo tutakapomgeukia Baba kwa utambuzi wa kinyenyekevu wa utegemezi wetu Kwake. Husaidia kupata sehemu maalum ambapo hisia zetu zinaweza kuelezewa kwa sauti kwa urefu na kwa kina iwezekanavyo” (“Using the Supernal Gift of Prayer,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 8).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jitahidi kupata upendo kama wa Kristo. Kama kuna mshiriki wa darasa lako ambaye anahitaji urafiki, fikiria jinsi ambavyo ungeweza kimsaidia kuhisi kuwa sehemu ya darasa. Kwa mfano, unaweza kumwalika mshiriki mwingine wa darasa kukaa na mtu huyo na kuwa na urafiki naye.

Chapisha