“Septemba 21–27. 3 Nefi 12–16: ‘Mimi ndimi Sheria na Nuru,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)
“Septemba 21–27 . 3 Nefi 12–16 Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Septemba 21–27
3 Nefi 12–16
“Mimi ndimi Sheria na Nuru”
Kila mtu katika darasa lako ana uwezekano wa kupata kitu fulani maalum chenye maana kwao katika mafundisho mengi ya Mwokozi yenye nguvu kutoka 3 Nefi 12–16. Waache washiriki wa darasa washiriki kanuni ambazo ziliwavutia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kumpa fursa kila mtu kushiriki kile walichojifunza katika 3 Nefi 12–16, ungeweza kuandika namba kuanzia 12 hadi 16 ubaoni. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kutafuta mstari katika sura hizi ambao umekuwa wa manufaa kwao kisha waandike namba ya huo mstari chini ya sura inayo endana nao ubaoni. Chagua mistari michache ya kusoma kwa pamoja, na jadilini kwa nini ina maana.
Fundisha Mafundisho
Mafundisho ya Mwokozi hutuonyesha jinsi ya kuwa wanafunzi wa kweli.
-
Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia hupendekeza kufupisha mistari katika 3 Nefi 12–14 ili kumalizia kirai “wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo …” ungeweza kuwaomba washiriki wowote wa darasa ambao walifanya shughuli hii kama wangekuwa tayari kushiriki walichojifunza. Ungeweza kuandika virai ambavyo havijakamilika ubaoni, pamoja na marejeleo kama haya: 3 Nefi 12:3–16, 38–44; 13:1–8, 19–24; na 14:21–27 (au vifungu vingine ulivyopata kajika kujifunza kwako binafsi). Washiriki wa darasa wangeweza kuchagua sura ya kusoma, binafsi au katika makundi, na kupendekeza njia ya kukamilisha kirai kilicho ubaoni kulingana na kile mistari hiyo inafundisha. Wahamasishe washiriki wa darasa kutafakari na pengine kuandika kile watakachofanya kumfuata Yesu Kristo kwa uaminifu zaidi kwa sababu ya kile walichojifunza kutoka mistari hii.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 12:48, ungeweza kuwaalika mmoja au zaidi kujifunza ujumbe wa Mzee Jeffrey R. HollandHivyo Hatimaye—Kuweni Wakamilifu” (Ensign au Liahona, Nov. 2017, 40–42) kabla ya darasa na kushiriki umaizi ambao unawasaidia wao kuelewa mstari huu.
Mawazo yetu hupelekea vitendo.
-
Majadiliano ya 3 Nefi 12:21–30 yangeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi kudhibiti mawazo yetu kunaweza kutusaidia kudhibiti matendo yetu. Kwa kuanza majadiliano, ungeweza kutengeneza chati ubaoni ikiwa na vichwa vya habari kama Matendo Tunayotaka kuyaepuka na Mawazo na Hisia ambazo Hupelekea Matendo hayo Kisha ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kupekua 3 Nefi 12:21–22 na 27–30 na kuanza kujaza chati. Je, ni matendo na mawazo gani mengine washiriki wa darasa wangeweza kuongezea kwenye orodha? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza “kutokubali vitu hivi kuingia mioyoni” mwetu? (3 Nefi 12:29). Je, tunawezaje kuvitoa nje wakati vinapoingia? Baada ya kusoma ushauri wa Rais Ezra Taft Benson katika “Nyenzo za Zaida,” ungeweza kutengeneza chati yenye vichwa vya habari Matendo kama ya Kristo tunayotaka kutenda na Mawazo yanayopelekea matendo hayo na muijaze kama darasa.
Huduma yetu na kuabudu lazima kufanywe kwa sababu sahihi.
-
Kujifunza 3 Nefi 13 huwasilisha fursa kwa ajili ya washiriki wa darasa kuchunguza kwa nini wanafanya mambo mazuri. Ili kuanza majadiliano, mngeweza kusoma kwa pamoja mstari wa 1–2 na 16 na kushiriki maana hii ya wanafiki: “Wanafiki; neno la Kigiriki [lililotumika katika Agano Jipya] kumaanisha ‘mtu ambaye haonyeshi uhalisia’ au mtu ambaye huongeza sehemu ya yasiyo ya kweli’” (Mathayo 6:2, tanbihi a). Pengine mshiriki mmoja au wawili wa darasa wangefurahia kujifanya au kuigiza kama wanasaidia masikini au wanafunga. Je, kwa nini kujifanya au kuigiza ni mfano mzuri wa unafiki? Je, tunawezaje kuhakikisha huduma zetu, sala, na kufunga ni vya dhati na si vya kinafiki?
-
Baada ya kupata matendo mazuri yaliyosemwa kwenye 3 Nefi 13:1–8 na 16–18, washiriki wa darasa wangeweza kujadili ni nia zipi ambazo zingeweza kumpelekea mtu kufanya vitu hivi au vitu vingine Mungu ametuamuru tufanye. Je, tunaweza kusema nini kwa mtu fulani ambaye anatuuliza kwa nini tunatenda matendo mazuri? Wahimize washiriki wa darasa kutafakari nia zao binafsi kwa kufanya matendo mazuri kama haya. Je, tunawezaje kutakasa nia zetu?
Kama tunatafuta “vitu vizuri” kutoka kwa Baba wa Mbinguni, tutapokea.
-
Ili kuelewa mwaliko wa Bwana wa kuomba, kutafuta, na kubisha, ingeweza kusaidia kwa kuchunguza nini maneno haya humaanisha. Je, kila neno humaanisha nini kuhusu kile Bwana anatualika kufanya? Je, tunaomba, kutafuta, na kubisha kwa namna ipi? Je, ni kwa namna gani ahadi katika 3 Nefi 14:7–8 zimetimizwa katika maisha yetu? Washiriki wa darasa wangeweza kurejelea ushauri wa Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za ziada,” wakitafuta maswali anayouliza na mialiko anayoitoa. Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari na kuandika majibu yao ya maswali yake na mipango yao kutimiza mialiko aliyoitoa.
-
Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza wasiwe na uhakika kuhusu nini Mwokozi alikimaanisha Aliposema, “Kwani kila mmoja ambaye huuliza, hupata”(3 Nefi 14:8). Je, ni kwa nini baadhi ya sala huonekana kama hazijibiwi, na je kwa nini sisi wakati mwingine tunapata majibu ambayo hatuyataki? Kurejelea baadhi ya maandiko yafuatayo kama darasa kungeweza kusaidia kujibu maswali haya: Isaya 55:8–9; Helamani 10:4–5; 3 Nefi 18:20; na Mafundisho na Maagano 9:7–9; 88:64. Wahimize washiriki wa darasa kushiriki kile wanachokipata. Je, ni kwa namna gani umaizi huu unaathiri jinsi tunavyosali?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwatia msukumo washiriki wa darasa kusoma 3 Nefi 17-19 , nyumbani, ungeweza kuwaalika kufikiria ingekuwaje kama wangesikia Mwokozi akisali kwa ajili yao na familia zao. Katika sura hizi watasoma kuhusu watu ambao walikuwa na uzoefu huu mtakatifu.
Nyenzo za Ziada
Tunaweza kudhibiti mawazo yetu.
Rais Ezra Taft Benson alifundisha:
“Akili imefananishwa na jukwaa ambapo muigizaji mmoja tu huwepo kwa wakati huo akifanya kazi yake. Kutoka mrengo mmoja Bwana, ambaye hukupenda, anajaribu kuweka katika jukwaa la akili yako kile ambacho kitakubariki. Kutoka katika mrengo mwingine mwovu, ambaye hukuchukia, anajaribu kuweka katika jukwaa la akili yako kile ambacho kitakulaani.
“Wewe ni meneja wa jukwaa—ni wewe ambaye huchagua ni wazo gani litachukua nafasi katika jukwaa. … Utakuwa kile ambacho unakifikiria—kile ambacho mara zote unakiruhusu kuchukua nafasi katika jukwaa la akili yako. …
Kama mawazo hututengeneza kuwa tulivyo, na tnatakiwa kuwa kama Kristo, lazima tufikiri mawazo yanayoendana na Kristo” (“Fikiria kuhusu Kristo,” Ensign, Apr. 1984, 10–11).
Mungu hutaka kuzungumza nawe.
Rais Russell M. Nelson alisema:
“Je, utafutaji wako utafungua nini kwako? Ni hekima gani unayopungukiwa? Je,, unaona hitaji gani muhimu kwako kujua au kuelewa? Fuata mfano wa Nabii Joseph. Tafuta sehemu ya ukimya ambako utakwenda mara kwa mara. Jinyenyekeze mbele ya Mungu. Mimina moyo wako kwa Baba yako wa Mbinguni. Mgeukie Yeye kwa ajili ya Majibu na faraja.
“Omba katika jina la Yesu Kristo kuhusu matatizo yako, hofu zako, udhaifu wako—ndio, mahitaji ya moyo wako. Na kisha sikiliza! Andika mawazo ambayo yanakuja kwenye akili yako. Andika hisia zako na zifuatilie kwa vitendo ambavyo unashawishiwa kufanya. …
“Je,, ni kweli Mungu anataka kuongea na wewe? Ndiyo! … Ninawahimiza kuwa na uwezo zaidi wa kiroho kuliko sasa kupokea ufunuo binafsi. …
“Oh, Kuna mengi zaidi Baba yako wa Mbinguni anataka wewe uyajue” (“Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 95).