Njoo, Unifuate
Septemba 14–20. 3Nefi 8–11: “Nyanyukeni na Mje Kwangu”


“Septemba 14–20. 3Nefi 8–11: ‘Nyanyukeni na Mje Kwangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Septemba 14–20 . 3 Nefi 8–11 Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Kristo anawatokea Wanefi

Mimi ni Nuru ya Ulimwengu, na James Fullmer

Septemba 14–20

3 Nefi 8–11

“Nyanyukeni na Mje Kwangu”

Kwa kuangalia mawazo uliyoyaandika wakati wa kusoma kwako binafsi 3 Nefi 8–11 kunaweza kuleta msukumo wa mawazo ya nini cha kufundisha. Mapendekezo hapa chini yanaweza kukupa mawazo zaidi

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakati mwingine watu wako radhi kushiriki kama utauliza kitu maalum. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kitu fulani kutoka 3 Nefi 8–11 ambacho kimewafundisha wao kuhusu sifa ya Yesu Kristo. Ungeweza kutoa mwaliko huu siku chache kabla ili kwamba waweze kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

3 Nefi 8–10

Kama tutatubu, Mwokozi atatukusanya, kutulinda na kutuponya.

  • Sura hizi zinabeba matukio ya uharibifu na ukiwa, lakini pia yanafundisha masomo ya kiroho ambayo yanaweza kutusaidia kusonga karibu na Yesu Kristo. Labda ungeweza kuligawa darasa katika makundi matatu na ulipe kila kundi kuchunguza sura moja kutoka 3 Nefi 8–10, wakitafuta maneno au virai ambavyo vinaelezea watu walichojifunza au kupitia. Mtu mmoja toka kila kikundi kisha angeweza kushiriki na darasa kile ambacho kundi lake limekigundua. Wahimize washiriki wa darasa kujadili jinsi masomo ya kiroho yanaweza kutusaidia kusonga karibu na Mwokozi.

  • Ujumbe wa thamani katika sura hizi ni kwamba Mwokozi hutufukia katika upendo na rehema hata katika majaribu yetu magumu sana. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kumfikiria mtu fulani ambaye wanamjua ambaye anapitia nyakati zenye changamoto na kisha wapekue maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 9:12–22 na 10:1–10 ili kupata virai ambavyo vingeweza kumsaidia mtu huyo. Labda washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki uzoefu binafsi wakati walipohisi kufikiwa na Mwokozi.

3 Nefi 9:19–22

Bwana anahitaji “Moyo uliovunjika na roho iliyopondeka.”

  • Kabla ya ujio wa Mwokozi, waaminifu katika nchi ya ahadi walitii sheria ya Musa, ambayo ilijumuisha dhabihu ya wanyama. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema sheria hii ungeweza kurejelea kwa kifupi Musa 5:5–8. Kwa nini watu wa Mungu waliamriwa kutoa dhabihu ya wanyama hapo kale? Je, nia amri gani mpya ambayo Mwokozi alitoa katika 3 Nefi 9:20, na ni kwa jinsi gani inatuelekeza sisi Kwake na dhabihu Yake? Nukuu kuhusu sheria ya dhabihu katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia.

  • Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kile kinachomaanishwa kuwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka? Labda ungeanza kwa kuandika ubaoni maneno vunjika, pondeka, na dhabihu. Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kuchora picha inayowakilisha nini maneno haya humaanisha kwao au waandike maneno au virai ambavyo vinahusiana na maneno haya. Wakati washiriki wa darasa wanaposhiriki picha, maneno, au virai, wangeweza kujadiliana jinsi yanavyohusiana na kile Mwokozi alichotuamuru katika 3 Nefi 9:19–22. Nukuu kutoka kwa Mzee D.Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada” pia inaweza kusaidia.

3 Nefi 11:1–17

Yesu Kristo ni Nuru ya ulimwengu.

  • Matukio yaliyoelezewa katika 3 Nefi 11:1–17 ni baadhi ya matakatifu zaidi katika Kitabu cha Mormoni. Fikiria kuwapa washiriki wa darasa lako muda kiasi kusoma mistari hii kimya kimya. Labda ungeandika maswali machache ubaoni kutafakari wakati wakisoma, kama vile: Je, ungehisi nini kama ungekuwa miongoni mwa watu hawa? Nini kinakuvutia kuhusu Mwokozi kwenye mistari hii? Je, unajifunza nini kutokana na mfano wa Mwokozi? au Je, ni uzoefu gani ambao umekupa ushuhuda juu ya Yesu Kristo kama Mwokozi wako? Ungeweza kuwaruhusu washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya mawazo yao au misukumo.

    Yesu akionyesha makovu katika mikono Yake kwa Wanefi

    Mmoja mmoja, na Walter Rane

3 Nefi 11:10–41

Yesu Kristo alijenga mafundisho Yake na Kanisa Lake.

  • Inaweza kuwa ya manufaa kuwa makini na vitu vya kwanza Mwokozi alivyochagua kusema na kufanya wakati alipowatokea katika nchi ya Neema. Labda washiriki wa darasa wangeweka alama kwenye kweli walizozipata kutoka kwenye maneno na matendo ya Mwokozi katika 3 Nefi 11:10–41 Waalike kushiriki walichokipata. Je, tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii? Je, tunajifunza nini kuhusu Kanisa lake?

  • Ili kumaliza kutokukubaliana kulikokuweko kati ya watu juu ya ubatizo, Mwokozi alifunua kweli za muhimu kuhusu ibada hii katika 3 Nefi 11. Ili Kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua kweli hizi, ungeweza kuandika mistari ifuatayo ubaoni: 21–25, 26–27, 33–34. Waalike washiriki wa darasa kuchukua mstari au mistari miwili na kushiriki ukweli unaofundishwa kuhusu ubatizo.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Darasa lako linaweza kuvutiwa kwa kujua kwamba ugeni wa Mwokozi kwa Wanefi na Walamani uliwaathiri wao kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba watu hawa ambao awali walikuwa na mabishano waliishi miaka 200 iliyofuata kwa amani (ona 4 Nefi 1). Hii inaweza kuwatia msukumo washiriki wa darasa kusoma 3 Nefi 12–16 kujifunza nini Mwokozi alikifundisha kwa watu kwamba kilipelekea badiliko lile kubwa.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Sheria ya Dhabihu

Rais M. Russell Ballard alifafanua njia mojawapo ambayo leo tunaishi sheria ya dhabihu:

“Baada ya dhabihu ya mwisho ya Mwokozi, mabadiliko mawili yalifanywa katika utendaji wa sheria [sheria ya dhabihu]. Kwanza, ibada ya sakramenti ilichukua nafasi ya ibada ya dhabihu; na pili, badiliko hili lilisogeza fokasi ya dhabihu kutoka kwenye mnyama wa mtu hadi kwa mtu mwenyewe. Katika hali kwamba, dhabihu ilibadilika kutoka katika matoleo kwenda kwa mtoaji. …

 “… badala ya Bwana kuhitaji wanyama wetu au mazao, sasa Anatutaka sisi kuacha kila kitu ambacho si kitakatifu. …

“… Tunapoushinda ubinafsi wetu wenyewe na kumuweka Mungu mbele katika maisha yetu na kuahidi kumtumikia Yeye bila kujali gharama, hapo ndipo tunapoishi sheria ya dhabihu” (“Sheria ya Dhabihu,” Ensign, Okt. 1998, 10).

Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume kumi na Wawili alisema: “dhabihu halisi, ya kibinafsi kamwe haikuwa kuweka mnyama kwenye madhabahu. Badala yake, ni utayari wa kumuweka kwenye madhabahu mnyama aliye ndani yetu na kumuacha ateketee!” (“Jizuieni Wenyewe Yote Ambayo si Mema,” Ensign, May 1995, 68).

“Moyo uliovunjika na roho iliyopondeka”

Mzee D. Todd Christofferson alielezea nini humaanishwa kwa kuwa na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka:

“Unaweza kumtolea Bwana zawadi ya moyo wako uliyovunjika, au kutubu, na majuto yako, au roho ya utiifu. Kwa kweli, ni zawadi yako mwenyewe—vile ulivyo na vile utkavyokuwa.

“Je,, kuna kitu ndani yako au katika maisha yako ambacho ni kichafu au kisichostahiki? Unapokiondoa, hiyo ndio zawadi kwa Mwokozi. Je,, kuna tabia nzuri au ubora ambao unakosekana katika maisha yako? Unapoichukua na kuifanya kuwa sehemu ya tabia yako, unatoa zawadi kwa Bwana” (“Utakapoongoka,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 12).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fanya kazi pamoja na wana familia. “Watu ambao wana ushawishi mkubwa kwa mtu binafsi—kwa wema au ubaya—kawaida ni wale walio wa nyumbani mwake. Kwa sababu nyumbani ni mahali muhimu pa kujifunza na kuishi injili, juhudi zako za kumuimarisha mshiriki wa darasa zitakuwa za ufanisi zaidi wakati unaposhirikiana na … wanafamilia” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8).