Njoo, Unifuate
Agosti 31–Septemba 6. Helamani 13–16: “Habari Njema ya Shangwe Kuu”


Agosti 31–Septemba 6. Helamani 13-16 : ‘Habari Njema ya Shangwe Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Agosti 31–Septemba 6. Helamani 13–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Samweli Mlamani juu ya ukuta akifundisha

Samweli Mlamani juu ya Ukuta, na Arnold Friberg

Agosti 31–Septemba 6

Helamani 13–16

“Habari Njema ya Shangwe Kuu”

Ni mafundisho gani na unabii wa Samweli Mlamani unaohisi utakuwa wa msaada sana kwa washiriki wa darasa lako? Unapojifunza Helamani 13–16, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia kupata maana katika sura hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kushiriki na mwenza kitu walichojifunza, kitu walichoelewa zaidi, au kitu walichofanya wakati wakisoma tukio la Samweli Mlamani katika Helamani 13–16 wiki hii. Kisha wape fursa baadhi yao kushiriki na darasa zima.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Helamani 13

Watumishi wa Bwana huzungumza na kutenda kulingana na mwongozo wa Mungu.

  • Bwana alimuamuru Samweli Mlamani kufanya kitu ambacho kingeonekana kigumu: kuhubiri injili kwa watu ambao awali walimfukuza nje ya mji. Kusoma Helamani 13:2–5 kungeweza kuwakumbusha washiriki wa darasa juu ya vitu vigumu Bwana aliwaamuru kuvifanya. Waalike kushiriki uzoefu wao. Ni kwa namna gani Bwana aliwasaidia? Kwa mfano, labda washiriki wa darasa wangeshiriki uzoefu wakati Bwana aliweka kitu moyoni mwao ambacho aliwataka wakiseme kwa mtu fulani (ona mstari wa 4). Ni baraka zipi ambazo washiriki wa darasa wanaziona wakati wanapofuata mwongozo wa Bwana?

    Picha
    Rais Russell M. Nelson

    Nabii huelekeza kwa Yesu Kristo.

  • Japokuwa maonyo ya Samweli Mlamani yalielekezwa kwa Wanefi wenye mioyo migumu, Helamani 13 yanabeba mafunzo kwetu sote. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana wao binafsi katika maneno yake, ungeweza kuwaalika kuchunguza Helamani 13 kwa ajili ya ujumbe ambao ni wa manufaa hivi leo. (Kama wanahitaji msaada, ungeweza kuandika mistari ifuatayo ubaoni: 8, 21–22, 26–29, 31, na 38.) Kisha wangeweza kushiriki wanachopata katika jozi, makundi madogo madogo, au darasa zima. Ni hali gani kama hiyo ambayo tunakumbana nayo kwa sasa?

Helamani 14; 16:13–23

Ishara na maajabu vinaweza kuimarisha imani ya wale ambao hawashupazi mioyo yao.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafuta ishara ambayo Bwana ametoa kwetu “kwamba [tuweze] kuamini katika jina lake” (Helamani 14:12). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichogundua wakati wakitafakari wazo hili. Hakikisha unazungumzia kwamba ishara katika maisha yetu zingeweza kuwa si za kimaigizo zaidi lakini za binafsi zaidi kuliko ishara alizotabiri Samweli Mlamani. Je, ni madhumuni gani mengine ya ishara yamependekezwa katika Helamani 14:28–30? Washiriki wa darasa pia wangeweza kushiriki vitu ambavyo Bwana amevifanya kuwasaidia wao kukuza imani juu yake.

  • Kusoma kuhusu kutimizwa kwa unabii wa Samweli Mlamani kungeweza kujenga imani ya wshiriki wa darasa katika Yesu Kristo na kazi yake. Pengine washiriki wa darasa wangetumia Helamani 14 kutengeneza chati ambayo inaorodhesha unabii wa Samweli wa kuzaliwa kwa Mwokozi na kifo chake upande mmoja na marejeleo ya maandiko ambapo utabiri huu ulitimizwa upande mwingine. Baadhi ya marejeleo yanaweza kujumuisha mistari kutoka 3 Nefi 1:15–21 na 3 Nefi 8:5–25. Je, kwa nini ni muhimu kwetu kujua kuhusu unabii huu na kutimizwa kwake?

  • Washiriki wa darasa wanaweza kujua kutoka —katika Helamani 16 na sehemu zingine za maandiko—kwamba kuona ishara na maajabu si lazima kumfanye mtu kuamini katika Kristo. Waalike kushiriki baadhi ya mifano kutoka katika maandiko juu ya watu walioona ishara lakini hawakuamini. Kulingana na Helamani 16:13–23, ni kwa nini watu wengi katika siku za Samweli Mlamani hawakuamini katika ishara na unabii? Ni kwa namna gani shetani huwashawishi watu “kutegemea nguvu zao wenyewe na … hekima” hivi leo ? (Helamani 16:15). Je, tunajifunza nini kutokana na tukio hili ambacho kinaweza kutusaidia kuepuka makosa sawa na hayo?

Helamani 15:3

Bwana Huwarudi Wale awapendao.

  • Maneno ya Samweli yanabeba maonyo mengi makali, lakini Helamani 15:3 inatoa mtazamo wa pekee juu ya kuonya kutokako kwa Bwana. Njia mojawapo ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa mtazamo huu ni kwa kusoma mstari huu kwa pamoja na kuwaalika kushiriki uthibitisho wanaouona wa upendo wa Mungu na rehema katika unabii wa Samweli na maonyo. Ni kwa namna gani maonyo toka kwa Bwana yanaweza kuwa ishara ya upendo Wake?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema ujumbe katika Helamani 15:3, ungeweza kushiriki madhumuni matatu ya maonyo matakatifu yaliyofundishwa na D. Todd Christofferson (ona “Nyenzo za Zaida”). Ligawanye darasa katika makundi matatu, na liombe kila kundi kujadili moja kati ya madhumuni haya (maandiko na video zilizopendekezwa katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kusaidia). Kisha kila kundi lingeweza kushiriki pamoja na darasa umaizi wowote kutoka katika majadiliano ambao unawasaidia wao kuelewa vyema kwamba Bwana huwarudi wale awapendao.

Helamani 16

Nabii hutuelekeza kwa Bwana.

  • Katika Helamani 16, tunajifunza nini kutoka kwa wale waliokubali mafundisho ya Samweli? Je, tunajifunza nini kutoka kwa wale waliomkataa? Ingeweza kuwa ya kuvutia kusikia washiriki wa darasa wakishiriki jinsi walivyopata ushuhuda wao wa umuhimu wa kumfuata nabii anayeishi. Wangeweza pia kushiriki jinsi wangeweza kutumia Helamani 16 au maneno ya Mzee Andersen katika “Nyenzo za Ziada” kumuelezea mtu fulani kwa nini wanachagua kumfuata nabii.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kusoma 3 Nefi 1–7 wiki ijayo, ungeweza kuwaambia kwamba wingi wa unabii wanaousoma kuhusu katika wiki hii utatimizwa katika sura hizi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Madhumuni ya uonyaji mtakatifu.

Mzee D. Todd Christofferson alishiriki madhumuni matatu ya uonyanji mtakatifu (ona “Kadiri ya Wengi Niwapendao, Ninawakemea na Kuwarudi,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 97–100):

  1. “Kutushawishi kutubu.” Ona Etheri 2:14–15; Mafundisho na Maagano 1:27; 93:41–50; 105:6.

  2. “Kutufanya bora na kututakasa.” Ona Mosia 23:21–22; Mafundisho na Maagano 101:1–5; 136:31.

  3. “Kubadilisha mwelekeo wetu katika maisha kuelekea ule Mungu aujuao kuwa ni njia bora.” Ona hadithi ya Rais Hugh B. Brown na kijisitu katika ujumbe wa Mzee Christofferson (ukurasa wa 98–99); “The will of God” (video, ChurchofJesusChrist.org).

Tunafurahi kuwa na nabii.

Mzee NeilL. Andersen alifundisha:

“Nabii hasimami kati yetu na Mwokozi. Badala yake, yeye husimama pembeni mwetu na kuonyesha njia inayoelekea kwa Mwokozi. Jukumu kubwa zaidi la nabii na zawadi ya thamani kwetu ni ushuhuda wake thabiti, uelewa wake wa kweli, kwamba Yesu ni Kristo. Kama Petro wa kale, nabii wetu anatangaza ‘[Yeye ndiye] Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai’ [Mathayo 16:16; ona pia Yohana 6:69].

“Katika siku za usoni, tukitazama nyuma kuhusu maisha yetu duniani, tutafurahia kwamba tulitembea ulimwenguni wakati wa nabii aliye hai. Siku hiyo, ninaomba kwamba tutaweza kusema:

“Sisi tulimsikiliza. Tulimwamini yeye. Tulijifunza maneno yake kwa subira na imani. Tulisali kwa ajili yake. Tulisimama pamoja naye. Tulikuwa wanyenyekevu vya kutosha kumfuata yeye. Tulimpenda” (“Nabii wa Mungu,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 27).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Pata kuwajua wale unaowafundisha. Hakuna watu wawili ambao ni sawa kikamilifu. Kila mtu unayemfundisha ana chimbuko la kipekee, mtazamo, na seti ya uwezo. Sali kujua jinsi unavyoweza kutumia tofauti hizi kusaidia washiriki wa darasa kujifunza. Unapowaelewa vizuri zaidi wale unaowafundisha, unaweza kutengeneza nyakati za thamani na za kukumbukwa za ufundishaji. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi7.)

Chapisha