Mosia 24-30: ‘Mkumbuke Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Agosti 24–30. Helamani 7–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Agosti 24–30
Helamani 7–12
“Mkumbuke Bwana”
Nefi aliwahamasisha watu wake kumkumbuka Bwana. Unaweza kufanya vivyo hivyo kwa wale unaowafundisha. Wakati unasoma Helamani 7–12, andika misukumo yako kuhusu jinsi unavyoweza kuwsaidia washiriki wa darasa kumkumbuka Bwana.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike washiriki wa darasa kuandika ubaoni baadhi ya kanuni za injili wanazozipata katika Helamani 7–12, pamoja na marejeleo ambapo kanuni hizi zinapatikana. Kisha mngeweza kuamua kama darasa zipi kati ya kanuni hizi na mistari mtajadili.
Fundisha Mafundisho
Manabii hufunua mapenzi ya Mungu kwa watu.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujifunza kutoka Helamani 7–11 kuhusu majukumu na wajibu wa manabii, mngeweza kuanza kwa kusoma kwa pamoja “Nabii” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wangeweza kutambua majukumu ya manabii yaliyosemwa na kuyaorodhesha ubaoni. Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kila mmoja kurejelea sura moja kutoka Helamani 7–11. Waombe kutafuta jinsi Nefi alivyotimiza majukumu yaliyoorodheshwa ubaoni. Ni kwa namna gani manabii wanaoishi na mitume wanatimiza majukumu haya? Je, tunawezaje kuwakubali wao katika majukumu yao?
-
Je, kwa nini manabii wakati mwingine wanatakiwa kuongea bila woga kama Nefi alivyofanya? Fikiria kuwaalika washirki wa darasa kusoma Helamani 7:11–29, wakitafuta maonyo Nefi aliyoyatoa na kwa sababu gani alitakiwa kutoogopa katika kuyatoa. Je, ni maonyo gani ya kinabii yametusukuma kutubu na kuja kwa Bwana? Katika “Nyenzo za Ziada” utakuta mfano wa ambao Mzee Neil L. Andersen aliutumia kutusaidia kuelewa hatari za kudharau maonyo ya kiunabii
Imani lazima ijengwe zaidi tu ya ishara na miujiza.
-
Njia mojawapo ya kujadiliana mistari hii ni kwa kuligawanya darasa katika makundi mawili na lialike kila kundi kusoma Helamani 9:1–20 na wajichulkulie kuwa katika sehemu ya aidha watu watano au waamuzi wakuu. Je,, watu hawa walihisi nini? Je, nini kingeweza kulishawishi kila kundi kijibu tofauti juu ya unabii ule ule wa kumiujiza? Je, tunawezaje kuhaikikisha miujiza inajenga shuhuda zetu lakini haiwi msingi wa shuhuda zetu? Je, tunaweza kuamuaje kama maneno ya nabii katika siku zetu ni ya kweli?
Bwana huwapa nguvu wale wanaotafuta mapenzi Yake na kushika amri Zake.
-
Tukio la Bwana kumbariki Nefi katika Helamani 10 linaweza kuwatia shauku washiriki wa darasa lako kuwa na bidii zaidi katika kutafuta na kufanya mapenzi ya Bwana. Washiriki wa darasa wangeweza kusoma mstari wa 1–12, wakitafuta kile Nefi alitakiwa kukipata ili kupata uaminifu wa Bwana na jinsi Bwana alivyombariki. Kisha wangeweza kushiriki mifano mingine ya watu ambao walitafuta na kufanya mapenzi ya Bwana “bila kusita” (Helamani 10:4), aidha kutoka kwenye maandiko au toka maishani mwao. Je, ni kwa vipi Mwokozi aliwabariki watu hawa kwa nguvu za “kusawazisha” (Helamani 10:9) milima katika lugha ya picha katika maisha yao? Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari njia wanazoweza zaidi kutafuta mapenzi ya Bwana na kushika amri Zake.
Bwana anatutaka sisi Tumkumbuke.
-
Wengi wa washiriki wa darasa lako wmeweka maagano kumkumbuka Yesu Kristo daima. Labda wangeshiriki na kila mmoja baadhi ya vitu ambavyo vinawasaidia “ kumkumbuka Yeye daima” (Moroni 4:3; Mafundisho na Maagano 20:77), vyote katika nyakati nzuri na ngumu. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza Helamani 12 kujua sababu za kwa nini watu wana tabia ya kumsahau Bwana. Je, tunawezaje kuaepuka tabia inayoelezewa katika sura hii? Je, ni kwa namna gani majaribu yametusaidia kumkumbuka Mungu? (Ona Helamani 11: 4–7).
-
Ili kufafanua juhudi zinazohitajika kukumbuka kitu, ungeweza kuwapa washiriki wa darasa dakika chache kupitia Helamani 12. Kisha ungeweza kuwauliza maswali kuhusu sura ili kuona kile wanachokikumbuka. Pengine wangeweza kushiriki kile ambacho hukifanya ili kukumbuka taarifa au kwa ajili ya mtihani. Je, ni kwa namna gani hii ni sawa na juhudi ambayo inahitajika “kumkumbuka Bwana”? (Helamani 12:5). Ni kwa jinsi gani hii ni tofauti? Waalike washiriki wa darasa kutafuta mstari au kirai kutoka Helamani 12 ambacho wangeweza kukiweka katika nyumba zao au kukariri ili kuwakumbusha kukumbuka ukarimu wa Mungu.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kusoma Helamani 13–16, ungeweza kuonyesha kwamba unabii wa Samweli Mlamani wa matukio yanayohusiana na kuzaliwa kwa Mwokozi na kusulubiwa yanaweza kulinganishwa na matukio katika siku yetu ambayo yatatangulia ujio wa pili wa Mwokozi.
Nyenzo za Ziada
Sikiliza maongozi ya manabii.
Mzee NeilL. Andersen alishiriki uzoefu ufuatao:
“Wale amabo huchagua kumtumikia Bwana mara zote watamsikiliza na hususan nabii. …
… Ngoja nielezee kupitia uzoefu. Familia yetu kwa miaka mingi iliishi katika jimbo la Florida. Kwa sababu Florida ina kiasi kikubwa cha mchanga, nyasi hupandwa kwa sehemu kubwa ya lundo la nyasi tuliitalo Saint Augustine. Adui mkubwa wa majani ya Florida ni mdudu wa kahawia.
“Jioni moja wakati jirani yangu pamoja nami tukiwa tumesimama kwenye ngazi, tuligundua mdudu mdogo akipita. ‘Ni vizuri upulizie dawa majani yako,’ alionya. ‘Kuna mdudu wa kahawia.’ Nilikuwa nimeyapulizia dawa majani si wiki nyingi zilizopita, na nilihisi ugumu kwamba nilikuwa na muda na pesa za kufanya hivyo tena.
“Katika mwanga wa asubuhi iliyofuata, nilichunguza majani yangu kwa ukaribu. Yalikuwa yakivutia na ya kijani. Niliangalia chini ya majani kuona kama ningeona mdudu yoyote. Sikuona chochote. Nakumbuka nikifikiria, ‘vyema yule mdudu wa kahawia alikuwa tu akipita uwanjani kwangu akielekea kwenye uwanja wa jirani yangu.’ …
“Hadithi hata hivyo ina mwisho wa kusikitisha. Nilitoka kupitia mlango wa mbele asubuhi moja siku 10 baada ya maongezi na jirani yangu. Chaa ajabu, kama vile ilikuwa imetokea usiku mmoja, Madoa ya kahawia yalikuwa yamejaa kwenye majani yangu. Nilikimbilia kwenye duka la madawa ya bustani, nikanunua dawa ya wadudu, na kupulizia mara moja, lakini nilkuwa tayari nimeshachelewa. Majani yalikuwa yameathiriwa, na kuyarudisha katika hali yake ya awali ilihitajika kupandwa upya kwa lundo la nyasi, masaa mengi ya kazi na gharama kubwa.
“Onyo la jirani yangu lilikuwa kiini cha ukuaji wa nyasi zangu. Aliona vitu ambavyo nisingeviona. Alijua kitu ambacho sikukijua. Alijua kwamba wadudu wa kahawia wanaishi chini ya udongo na wanafanya shughuli usiku, wakifanya uchunguzi wangu wa mchana kutokuwa wa manufaa. Alijua kwamba wadudu wa kahawia hawakula majani ya nyasi lakini walipata virutubisho toka mizizi yake. Alijua kwamba viumbe hawa wa inchi ndogo wangeweza kula mizizi mingi kabla sijaona matokeo yake juu ya ardhi. Nililipa bei ya majivuno yangu. …
“… Kuna wadudu wa kahawia wa kiroho ambao hujifukia chini ya kuta zetu za ulinzi na kuvamia mizizi muhimu. Wengi wa wadudu hawa wa uovu wanaonekana wadogo, wakati mwingine kama wasioonekana kabisa. …
“Hebu tusifuate mfano ambao niliuonyesha katika kushughulikia wadudu wa kahawia. Hebu kamwe tusidharau maonyo. Hebu kamwe tusiwe wenye majivuno katika uhuru wetu. Hebu kila mara tuwe wasikivu na wenye kujifunza katika unyenyekevu na imani, wenye hamu ya kutubu pale inapohitajika” (“Mnabii na Wadudu wa Kahawia wa Kiroho,” Ensign, Nov. 1999, 16–18).