Njoo, Unifuate
Agosti 10–16 Alma 53–63: “Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu”


“Agosti 10–16. Alma 53-63 : ‘Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 10–16. Alma 53–63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Vijana elfu mbili wapiganaji

Vijana Elfu Mbili wapiganaji na Arnold Friberg

Agosti 10–16

Alma 53–63

“Kulindwa na Nguvu Zake za Ajabu”

Wakati ukichunguza mawazo ya kufundisha katika muhtasari huu, fikiria kuhusu nini kitafanya kazi katika darasa lako, kitumie au boresha shughuli ili kukidhi mahitaji ya washiriki wa darasa.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza toka Alma 53–63, ungeweza kuwaomba kupitia sura kwa haraka na kuangalia mistari ambayo wangeweza kuishiriki na mtu fulani ambaye anakabiliana na changamoto. Waalike kushiriki mistari hii na mtu fulani nje ya darasa.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 53:17–21; 56:43–48, 55–56; 57:20–27; 58:39–40

Wakati tukitumia imani na kumuamini Mungu, Yeye atatuimarisha.

  • Unaweza kuongeza thamani katika majadiliano ya darasa lako kuhusu wapiganaji wa Helamani kwa kuchora kile ambacho washiriki wa darasa walijifunza nyumbani. Njia mojawapo ya kufanya hili ingeweza kuwa kwa kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki sifa za wapiganaji vijana ambazo zimewavutia (baadhi ya hizo zinaweza kupatikana katika Alma 53:17–21; 56:45–48; 57:20–21, 26–27; 58:40). Ni kwa namna ipi sifa hizi ziliwasaidia wapiganaji vijana wakati wa vita? Je, zinaweza kutusaidia kwa namna gani wakati wa vita vyetu vya kiroho? Washiriki wa darasa pia wangeweza kushiriki hadithi za “vijana wapiganaji” wa siku hizi.

  • Wazazi katika darasa lako labda wanatumaini kwamba watoto wao watakuza imani kama ya vijana wapigananji wa Helamani. Ili kuwasaidia wazazi na wazazi watarajiwa katika darasa lako kujifunza kutoka hadithi zao, ungeweza kutengeneza jopo la watu kadhaa ambao wanaweza kushiriki mawazo kuhusu kujenga imani kwa watoto. Waombe washiriki wa jopo hilo kusoma kabla Alma 56:47–48 na 57:20–27 na kujiandaa kushiriki umaizi kuhusu kile kilichowasaidia vijana wapiganaji kukuza imani. Wape washiriki wa darasa muda wa kushiriki umaizi wakati washiriki wa jopo wakiwasilisha mawazo. Nyenzo zingine ambazo zingeweza kukuza mjadala huu zinajumuisha maneno ya Dada Joy D. Jones katika “Nyenzo za Ziada” na ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Ombi kwa Dada Zangu” (Ensign au Liahona Nov. 2015, 95–97). Mwisho wa majadiliano, ungeweza kuwapa washiriki wa darasa dakika kadhaa kutafakari maswali kama yafuatayo: Je, akina nani wangeweza kujitegemeza katika ushuhuda wako? Unaweza kusema au kufanya nini ili kuwaimarisha?

Watoto wa Wanefi na mama yao

Mashujaa (waliofundishwa na mama zao), na Liz Lemon Swindle

Alma 58:1–12, 30–3761

Tunaweza kuchagua kufikiria vizuri kuhusu wengine na kutokasirishwa.

  • Mfano wa Helamani wakati jeshi lake lilipokuwa halipokei msaada unaweza kuwa mfano wenye nguvu kwetu wakati tunapohisi kukosewa. Ili kuhamasisha majadiliano kuhusu mfano wake, ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa kuja akiwa maejiandaa kufupisha hali ya Helamani na sababu ambazo serikali ilikuwa haitikii mahitaji yake (ona Alma 58:1–9, 30–37; 61:2–8). Ungeweza kuandika ubaoni mwitikio wa Helamani na miitikio mingine. Kisha waalike washiriki wa darasa kuchunguza Alma 58:1–12 na 30–37 na waandike chini ya kila kichwa cha habari kile Helamani alichofikiria, alichosema, na kufanya kuitikia katika hali yake na, kinyume cha kile angeweza kufikiri, kusema, au kufanya. Je, tunaweza kufanya nini kufuata mfano wa Helamani wakati tunapohisi kutendwa uovu au kutelekezwa?

  • Wakati Moroni alipomkosoa Pahorani katika Alma 60, Pahorani angeweza kuchagua kukubali kukasirika. Badala yake aliitikia kwamba “hakuwa na hasira” na “[alifurahia] katika ujasiri wa moyo wa [Moroni]”Alma 61:9). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutokana na mfano wa Pahorani, ungeweza kuwaomba wajichukulie kama wao waomeombwa kuandika taarifa kwa ajili ya gazeti la Kanisa ambayo itaonyesha mfano wa Pahorani katika Alma 61 kufundisha kuhusu jinsi ya kuepuka kuudhika kutokana na wengine. Kisha ungeweza kuwagawa washiriki wa darasa ktika makundi na waombe wasome Alma 61:3–14 na waorodheshe baadhi ya dondoo ambazo wanaweza kuzijumuisha katika taarifa yao. Ushauri wa Mzee David A. Bednar katika “Nyenzo za Ziada” unaweza pia kusaidia.

Alma 60:7–14

Tuna wajibu wa kuwainua wengine wanaotuzunguka.

  • Moroni aliandika kwamba Mungu angemwajibisha Pahorani kama kwa kujua alikuwa akiacha kutimiza mahitaji ya jeshi la Wanefi. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Alma 60:7–14 kwa pamoja, na waombe kumfikiria mtu fulani wanayemjua ambaye anaweza kuwa katika uhitaji na kuhisi kuachwa. Je, tunaweza kufanya nini ili kujua mahitaji ya wengine na kuyatimiza? Je, ni kwa namna gani mahitaji yako yametimizwa kupitia wengine, ikijumuisha dada zetu na kaka zetu wahudumu?

Alma 62:39–41, 48–51

Hatuna budi kumkumbuka Bwana nyakati za majaribu na nyakati nzuri.

  • Mwitikio wa Wanefi katika nyakati zote ngumu na nzuri (ona alma 62:39–41, 48–51) unaonyesha kwamba tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu iwe tunapitia majaribu au mazuri. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mistari na kushiriki kile kilichowavutia. Ungeweza kuwaalika kijadiliana mawazo yao katika jozi kabla ya kuwaomba wachache kushiriki na darasa zima.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuhamasisha kuvutiwa katika Helamani 1–6, ungeweza kulielezea darasa kwamba katika sura hizi Wanefi wanakuwa waovu na Walamani wanakuwa wema. Badiliko hili lina fundisho kubwa kwetu katika siku hizi hatari za mwisho.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuwafanya watoto wetu kuweza kukabiliana na dhambi.

Dada Joy D. Jones, Rais Mkuu wa darasa la Msingi, alishiriki mawazo makuu yafuatayo kukuza “kizazi kinachoweza kukabiliana na dhambi”:

“Kwa kuanza, … lazima tuwasaidie [watoto wetu] kujua bila kuwa na swali kwamba wao ni wana na mabinti wa Baba wa Mbinguni na kwamba ana matarajio matakatifu toka kwao.

“Pili, kuelewa mafundisho ya toba ni muhimu kwa ajili ya kuweza kukabiliana na dhambi. Kuweza kukabliana na dhambi hakumaanishi kutokuwa na dhambi, lakini inamaanisha kuweza kuendelea kutubu, kuwa makini na shupavu. Labda kuweza kukabiliana na dhambi huja kama baraka kutokana na mchakato wa kuepuka dhambi. …

“… kanuni ya tatu ili kuwasaidia watoto kuweza kukabiliana na dhambi ni kwa kuanza katika umri mdogo kwa upendo kuwafundisha kanuni za msingi za injili na mafundisho—toka kwenye maandiko, Makala ya Imani, kijitabu cha Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, nyimbo za darasa la msingi, nyimbo za Kanisa, na ushuhuda wetu wenyewe—ambao utawaongoza watoto kwa Mwokozi. …

“… Kuwasaidia watoto kuelewa, kufanya na kushika maagano ni kanuni nyingine. … Kuwafundisha watoto kutimiza ahadi ndogondogo wakati wakiwa wadogo kutawawezesha wao kutunza maagano matakatifu baadae katika maisha” (“Kizazi Thabiti dhidi ya Dhambi,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 88–89).

Jinsi ya kuepuka kuudhika.

Katika ujumbe wake “Na Hakuna Chochote Kitackachowaudhi” (Ensign au Liahona, Nov. 2006, 89–92), Mzee David A. Bednar alitoa ushauri ufuatao:

  • Tambua kwamba kuudhika ni chaguo. “Kuamini kwamba mtu fulani au kitu kinaweza kutufanya kuudhika, kuwa na hasira, kudhuru, au wakali hupunguza uhuru wetu wa kuchagua na kutubadili kuwa vitu ambavyo vinatumiwa. Kama mawakala, hata hivyo, wewe pamoja nami tuna nguvu kutenda na kuchagua jinsi tutakavyoitikia hali za kuudhi na za kuleta uchungu.”

  • Mtumainie Mwokozi. “Mwokozi ni mfano mkubwa wa jinsi tunavyotakiwa kuitikia matukio ya kuudhi au hali” [ona 1Nephi 19:9]

  • Kuwa muelewa katika mapungufu ya wengine. Mojawapo ya ishara kuu ya ukomavu wetu wa kiroho huonekana katika jinsi tunavyojibu udhaifu, ukosefu wa uelewa na matendo yenye kuudhi ya wengine.

  • Zungumza moja kwa moja. “Kama mtu akisema au kufanya jambo ambalo tunafikiria ni la kuudhi, jukumu letu la kwanza ni kukataa kuudhika na kisha tuzungumze naye binafsi, kwa moyo wa dhati, na moja kwa moja na huyo mtu. Njia kama hii hualika msukumo wa kiungu kutoka kwa Roho Mtakatifu na kuruhusu kutoelewana kusahihishwa na nia ya kweli kueleweka.”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia uzoefu toka nyumbani. Kwa sababu nyumbani ni kitovu cha kujifunza injili, fikiria jinsi uzoefu wa darasa lako unaweza kujengwa juu ya kianchotokea nyumbani. Kwa mfano, unaweza kuboresha shughuli nyingi katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ili kutumia katika darasa lako kuimarisha kujifunza binafsi kwa washiriki wa darasa na kama familia