Njoo, Unifuate
Agosti 17–23. Helamani 1–6: “Mwamba wa Mwokozi Wetu”


“Agosti 17–23. Helamani 1–6 : ‘Mwamba wa Mwokozi Wetu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Agosti 17–23. Helamani1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Mawimbi yakigonga miamba

Agosti 17–23

Helamani 1–6

“Mwamba wa Mwokozi Wetu”

Je, kweli unalijua darasa lako? Jaribu kumjua vizuri mshiriki mmoja wa darasa kila wiki. Unapofanya hivyo, unaweza kuyaweka vyema zaidi mahitaji yao mawazoni wakati unapojiandaa kufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuja darasani wakiwa wamejiandaa kushiriki kitu ambacho wangeweza kutumia kufundisha kuhusu kanuni waliyojifunza katika sura hizi. Je, ni katika njia zipi zingine tunaweza kufundisha kanuni hizi kwa wengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Helamani 1–6

Kiburi hututenganisha na Roho na nguvu ya Bwana.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia huelezea “mzunguko wa kiburi” ambao ulikuwa pigo kwa Wanefi. Labda mtu fulani katika darasa angechora mchoro wa mzunguko huu ubaoni. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kutafuta mistari kwenye Helamani 1–6 ambayo wanahisi inaelezea sehemu tofauti tofauti za mzunguko huu na waziandike pembeni ya sehemu inayohusiana na mchoro. (Kama washiriki wa darasa wanahitaji usaidizi, ungeweza kupendekeza kwamba watafute toka Helamani 3:24–36; 4:11–26.) Je, wakati mwingine tunakuwaje kama Wanefi? Je, tunawezaje kuepuka tabia yao ya kiburi? Ungeweza pia kushiriki sehemu toka “Sura ya 18: Jihadhari na majivuno” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson [2014], 229–40).

    Picha
    Mzunguko wa kiburi

    “Mzunguko wa kiburi.”

  • Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Helamani 4:13 na 24–26 na kutafuta wimbo unaofundisha kuhusu utegemezi wetu kwa Mungu, kama vile “Ninakuhitaji Kila Saa” (Nyimbo za Kanisa, namba. 98). Je, ni kwa nini kiburi hututenga na Mungu? Je, tunawezaje kutambua utegemezi wetu kwa Mungu? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki ni kwa namna gani wameimarishwa na Roho wa Bwana na nguvu kwa sababu walikuwa wanyenyekevu.

  • Waumini wa Kanisa walioelezewa katika Helamani 3:33–3 waliwatesa wenzao wa Kanisa. Kwa sababu ya kiburi chao, waliwaonea masikini na kutenda kila aina ya dhambi (ona Helamani 4:11–13). Fikiria kusoma kwa pamoja Helamani 3:33–34 na 4:11–13 na waombe washiriki wa darasa kujadili njia tunazoweza kuonyesha ukarimu mkubwa na heshima kwa wengine, ikijumuisha waumini wenzetu wa Kanisa ambao wanaweza kuwa tofauti na sisi. Ungeweza kuwaaalika washiriki wa darasa kumfikiria mtu fulani wanayemjua ambaye anaweza kuwa anateseka kwa sababu ya matendo ya wengine ya kutokuwa na ukarimu na kutafakari jinsi wanavyoweza kumuimarisha na kumtia moyo mtu huyo.

Helaman 3:33–35

Usafishwaji huja kwa kutoa mioyo yetu kwa Mungu.

  • Helamani 3:33–35 ingeweza kuwatia moyo katika darasa lako wale ambao wanaweza kuwa wanapitia “shutuma … [au] mateso mengi” (mstari wa 34). Labda ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuchunguza mistari hii ili kupata ushauri ambao wangeweza kumpa mtu fulani ambaye anashutumiwa. Au labda washiriki wangeshiriki jinsi walivyopata “shangwe na faraja” katika nyakati za mateso kwa kufanya mambo yaliyoelezewa katika mstari wa 35.

  • Fikiria kulialika darasa kusoma Helamani 3:33–35 na maelezo na marejeleo kuhusu jinsi ya kuwa wasafi katika “ Nyenzo za Ziada.” Je, mistari hii na maelezo haya inafundisha nini kuhusu kutakaswa? Ni kwa namna gani kufunga na kusali kunaleta baraka zilizoelezewa katika Helamani 3:35? Je, ni kwa namna gani tunatoa mioyo yetu kwa Mungu? (Ona Helamani 3:35). Je, hii inatusaidiaje kuwa wasafi? Ungeweza pia kuandaa na kugawa vipeperushi vikiwa na moja ya maelezo au marejeleo kutoka “Nyenzo za Ziada” na waalike washiriki wa darasa bila mpangilio maalum kuchukua kimoja kujifunza. Kisha wangeweza kushiriki na kila mmoja kile walichojifunza kuhusu utakasaji.

Helaman 5:12

Kama tunamfanya Yesu Kristo msingi wetu, hatutaanguka.

  • Shetani hutuma “pepo zake kali” katika maisha yetu sote. Watu wengi katika darasa lako tayari wameshapitia hili, na dhoruba zaidi zina uwezekanao wa kuja baadae. Je, unaweza kufanya nini ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujiandaa kwa ajili ya dhoruba hizi kwa kujenga maisha yao juu ya Yesu Kristo?

    Ungeweza kuanza majadiliano kwa kuonyesha picha za mahekalu au majengo mengine na kulinganisha maisha yetu na majengo. Ni chaguzi zipi mjenzi anatakiwa kufanya? Ni chaguzi zipi tunazozifanya ambazo huathiri jinsi maisha yetu yanavyojengwa? Kisha mngeweza kusoma kwa pamoja Helamani 5:12 na mjadili kile humaanishwa kujenga maisha yetu juu ya Yesu Kristo. Je, ni kwa namna gani kuwa Naye kama msingi wetu huathiri chaguzi zingine tunazozifanya wakati tukijenga maisha yetu?

    Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi gani kuwa na Mwokozi kama msingi wetu kumewasaidia wao kukabiliana na dhoruba za maisha. Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari aina ya maisha wanayoyajenga na jinsi wanavyoweza kuhakikisha kwamba wamejengwa imara juu ya Kristo. Hadithi kuhusu Hekalu la Salt Lake katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia katika majadiloano yako.

Helaman 5:14–50

Imani yetu inaimarishwa kwa “ukuu wa ushahidi [ambao] tumeupokea.”

  • Moja ya baraka za kukusanyika katika Shule ya Jumapili ni fursa ya kuimarishana imani ya kila mmoja wetu—kama tu Walamani walivyofanya katika Helamani 5:50. Labda mngeweza kusoma Helamani 5:50 kwa pamoja na kuwaomba washiriki wa darasa kutambua “vitu ambavyo [Walamani] walivisikia na kuviona katika mstari wa 20–49. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kushrirki baadhi ya uzoefu wa kiroho ambao umewashawishi kwamba injili ni ya kweli—hata kama hawajawaona malaika au nguzo ya moto. Ni ushuhuda gani wenye ushawishi ambao wameuona wa urejesho wa injili ya Yesu Kristo?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Helamani 7–12 inaelezea jinsi Nefi alivyopata kuaminiwa na Bwana na alivyopewa nguvu kuu. Ungeweza kupendekeza kwa darasa lako kwamba kwa kusoma sura hizi, wanaweza kujifunza jinsi ya kupokea kuaminiwa zaidi na Mungu katika maisha yao.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuwa wasafi kupitia Yesu Kristo.

  • Utakaso ni “mchakato wa kuwa huru kutoka kwenye dhambi, bila mawaaa, msafi na mtakatifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo” (Mwongozo wa Maandiko, “utakaso,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

  • “Tukiisha tubu kwa kweli, Kristo atachukua mzigo wa hatia ya dhambi zetu. Tunaweza kufahamu sisi wenyewe kuwa tumesamehewa na kufanywa kuwa wasafi. Roho Mtakatifu atatuhakikishia hili; Yeye ndiye Mtakasaji. Hakuna ushuhuda mwingine wa msamaha unaoweza kuwa mkuu” (Dieter F. Uchtdorf, “Wakati Salama wa Kugeuka,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 101).

  • “Kutakaswa kupitia damu ya Yesu Kristo ni kuwa msafi, bila mawaa na mtakatifu. Kama haki huondoa adhabu kwa dhambi zilizopita, basi utakaso huondoa doa au madhara ya dhambi” (D. Todd Christofferson, “Haki na Utakaso,” Ensign, Juni 2001, 22).

  • “Wakati nia, matamanio, na hisia za mtu zinakubaliana kikamilifu na mapenzi na vigezo vya Mungu, mtu huyo ametakaswa” (Brigham Young, “Discourse,” Deseret News, Sept. 7, 1854, 1).

  • Tunatakaswa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Waebrania 13:12; Alma 13:10–12; 3 Nefi 27:19–20; Moroni 10:32–33; Mafundisho na Maagano 76:40–42).

  • Hata baada ya kuwa tumesafishwa, bado kuna uwezekno wa kuanguka kutoka kwenye neema takatifu (ona Mafundisho na Maagano 20:30–34).

Msingi imara.

Wakati wa ujenzi wa Hekalu la Salt Lake, nyufa kubwa zilipatikana katika msingi wa mawe. Ingawa ilikuwa imechukua miaka tisa mpaka kufikia hapo katika ujenzi, Rais Brigham Young alielekeza kwamba msingi wa mawe wenye nyufa uondolewe na kuwekwe mawe yenye ubora zaidi. Ilichukua miaka mingine mitano kuondoa sehemu mbovu ya msingi wa mawe na kujenga upya toka ardhini. “Nataka kuona hekalu linajengwa kwa njia ambayo litahimili hadi Milenia (“Maelezo,” Deseret News, Oct. 14, 1863, 97).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia kuhusu Yesu Kristo. Aminadabu angeweza kutohisi kama mtu anayestahili zaidi kufundisha Walamani kutubu na kuwa na imani katika Kristo (ona Helamani 5:35–41). Lakini alishiriki kile alichojua, na ushuhuda wake ulikuwa na ushawishi mkubwa. Je,, unajifunza nini kutoka katika mfano huu?

Chapisha