“Agosti 3–9. Alma 43–52: ‘Simama Imara Katika Imani juu ya Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)
“Agosti 3–9. Alma 43–52,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Agosti 3–9
Alma 43–52
“Simama Imara Katika Imani juu ya Kristo”
Tofauti na kurejelea shuguli zilizopendekezwa hapa, tafuta mwongozo wako mwenyewe wakati kwa sala ukisoma Alma 43–52 na kutafakari kuhusu jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua mafundisho yanayofundishwa.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutoka Alma 43–52, ungeweza kuwauliza jinsi wangemjibu mtu ambaye husema “Sioni jinsi gani vita vilivyoelezewa kwenye Kitabu cha Mormoni vina umuhumu katika maisha”
Fundisha Mafundisho
Vita katika Kitabu cha Mormoni hutufundisha kuhusu vita vyetu dhidi ya uovu.
-
Katika kujifunza kwao binafsi na kama familia wiki hii, washiriki wa darasa wanaweza kuwa wametafakari au kuandika mawazo yao kuhusu kufanikiwa kwa Wanefi kujilinda dhidi ya Walamani na jinsi Walamani walivyowavamia Wanefi. Kama washiriki wa darasa walifanya hivi nyumbani, waalike kushiriki kile walichokipata. Au ungeweza kuwapa washiriki wa darasa muda wa kupata umaizi huu wakati wa darasa kwa kutumia maandiko kama yale yanayopatikana kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Wakati washiriki wa darasa wanashiriki kile walichokipata, wahimize kijadiliana kuhusu jinsi tunavyoweza kufuata mfano wa Wanefi katika kujilinda sisi wenyewe dhidi ya mwovu na jinsi tunvyiweza kutambua mashambulizi ya kiroho ya Shetani kwetu.
Kama tuna ushujaa katika kutetea imani yetu, tunaweza kuwavutia wengine kuwa waaminifu.
-
Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kufuata mfano wa Moroni kwa ushujaa kutetea imani yao katika injili ya urejesho ya Yesu Kristo? Washiriki wa darasa wangeweza kusoma Alma 46:11–22 na kutambua kile Moroni alikifanya na kile alichofundisha ambacho kiliwavutia watu wake kuwa waaminifu zaidi. Ungeweza kuandika vitu hivi uaboni chini ya kichwa cha habari Mfano wa Moroni. Kisha ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kutafakari matendo ya Moroni na kupendekeza nini tunaweza kufanya leo kutetea imani zetu. Ungeweza kuandika umaizi wao chini ya kichwa cha habari Kiushujaa kutetea Injili Leo. Ni kweli zipi na maadili ambayo manabii wetu wametufundisha hivi karibuni ambayo tunatakiwa kufundisha na kutetea?
-
Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia kile Moroni alichofanya na bendera ya uhuru katika maisha yao? Waalike kusoma Alma 46:11–22 na watafute kweli ambazo Moroni alifundisha na kuwaomba watu kuzikubali. Ni kweli zipi na maadili ambayo viongozi wa Kanisa wanasisitiza katika siku zetu? Ungeweza kurejelea baadhi ya hayo kwenye Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” au ujumbe wa mkutano wa hivi karibuni.) Je, ni changamoto zipi ambazo tunazo katika kutetea imani yetu katika ulimwengu leo? Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Moroni? Wape washiriki wa darasa fursa ya kutengeneza bendera zao wenyewe za uhuru ambazo zinaweza kuwakumbusha kwa ujasiri kuishi na kutetea imani zao.
Shetani hutujaribu na kutudanganya kidogo kidogo.
-
Washiriki wa darasa lako wanaweza kunufaika kwa kusoma Alma 47, ambayo huonyesha jinsi usaliti wa Amalikia unafanana na Shetani anachokifanya kutudanganya. Ungeweza kuanza kwa kumuuliza mfu fulani kufupisha tukio lipatiakanalo katika Alma 47. Ili kuongeza mvuto, ungeweza kuwaomba washiriki wawili wa darasa kuvuta taswira kwamba wao ni Amalikia na Lehonti na waisimulie hiyo hadithi. Je, Amalikia alifanya nini ambacho hutukumbusha vitu ambavyo Shetani hufanya kutujaribu na kutudanganya? Wahamasishe washiriki wa darasa kurejelea kwenye mistari maalum wakati wakijadiliana swali hili. Nukuu katika “Nyenzo za Zaida” inabeba mfano mwingine mzuri wa jinsi shetani anavyotudanganya. Ni ushauri gani tunaoshauriana kila mmoja wetu kutusaidia kuwa makini na jinsi shetani anavyotujaribu hivi leo? Tunaweza kufanya nini ili kujilinda?
Wakati tukijaribu kuwa waaminifu kama Moroni, tutakuwa zaidi kama Mwokozi.
-
Mjadala kuhusu sifa za Moroni ungeweza kuwavutia washiriki wa darasa kujitahidi kufuata mfano wake. Ungeweza kuanza kwa kuonyesha picha ya Moroni, kama mojawapo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Kisha waalike washiriki wa darasa kujifunza Alma 44:3–4 na 48:7–13 na waandike ubaoni maneno na virai vinavyomuelezea Moroni. Kisha mngeweza kusoma kwa pamoja Alma 48:17 na kujadili jinsi tabia ya Moroni, kama zile zilizoorodheshwa ubaoni, zilimuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuwa kama Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa zaidi kama Moroni?
Tunaweza kujiimarisha nafsi na familia zetu dhidi ya majaribu.
-
Washiriki wa darasa lako wangeweza kunufaika kwa kusikia kutoka kwa kila mmoja akizungumza jinsi wanavyoweza kujikinga wao na familia zao dhidi ya udanganyifu na majaribu ya Shetani. Ili kutia hamasa mjadala wa aina hiyo, mngeweza kusoma kwa pamoja Alma 48:7–9; 49:1–9; and 50:1–6. Wakati tunapofikiri kuhusu mahitaji yetu kwa ajili ya ulinzi wa kiroho dhidi ya dhambi, tunaweza kujifunza kutoka kwa juhudi za Wanefi kujilinda. Je, ni kwa jinsi gani tunajenga ulinzi wa kiroho kuzilinda nafsi zetu na familia dhidi ya dhambi na ushawishi wa maovu? Wahamasishe washiriki wa darasa kushiriki mawazo ambayo yamefanya kazi kwao. Je, kwa nini ni muhimu “kutoacha kufanya maandalizi”? (Alma 50:1).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Njia mojawapo ya kuwahamaisha washiriki wa darasa kusoma Alma 53–63 ingeweza kuwa kwa kuwaambia kwamba matukio katika sura hizi yangeweza kuwavutia wao na familia zao kuwa watiifu zaidi na kukuza imani dhabiti zaidi.
Nyenzo za Ziada
Madhara ya kukata tamaa katika majaribu madogo.
Ili kufundisha kwamba “dhambi kubwa huingia katika maisha yetu wakati kwanza tunapokubali majaribu madogo,” Rais Spencer W. Kimball alishiriki hadithi hii:
“Ngamia na mmiliki wake… walikuwa wakisafiri kuvuka matuta ya mchanga jangwani wakati upepo ulipoanza. Haraka msafiri alipiga hema na kuingia ndani, akifunga vizibao kujikinga na vipande vidogo vya mchanga kutokana na tufani kali. Ngamia bila shaka aliachwa nje, na wakati upepo mkali ulipopeperusha mchanga kwenye mwili wake na katika macho yake na pua aliona si ya kuvumilika na mwishowe aliomba kuingia kwenye hema.
“‘Kuna sehemu ya kunitosha mimi tu,’ alijibu msafiri.
“‘Lakini naweza kuweka tu pua yangu ndani ili niweze kupumua hewa isiyo na mchanga?’ ngamia aliomba
“‘Vyema, labda ungeweza kufanya hivyo,’ alijibu msafiri, na akafungua kizibao sehemu ndogo sana na pua ndefu ya ngamia ikaingia ndani. Je, ni kwa jinsi gani ngamia alikuwa yuko sawa! Lakini punde ngamia alichoshwa na mchanga uliopeperushwa machoni na masikioni mwake … :
“‘Mchanga urushwao na upepo ni kama kikwaruzio katika kichwa changu. Je, ninaweza kuweka tu kichwa changu ndani?
Kwa mara nyingine msafiri alikubali kwamba kukubali ombi bila kufikiria kwa kina kusingemharibia chochote, kwa kuwa kichwa cha ngamia kingeweza kuchukua nafasi sehemu ya juu ya hema ambapo yeye mwenyewe alikuwa hatumii. Hivyo ngamia aliweka kichwa chake ndani na akaridhika tena—lakini kwa muda mfupi tu.
“‘robo ya mwili tu,’ aliomba, kwa mara nyingine msafiri alikubali na punde mabega ya mbele ya ngamia na miguu ilikuwa ndani ya hema. Hatimaye, kwa mchakato huo huo wa kuomba na kukubaliwa, sehemu ya kati ya ngamia, robo ya sehemu ya nyuma na vyote vilikuwa ndani Lakini sasa palikuwa pamebanana sana kwa ajili ya wawili, na ngamia akamfukuza nje msafiri kwenye upepo na dhoruba”(Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Spencer W. Kimball [2006], 106–7).