“Julai 27–Agosti 2. Alma 39–42: ‘Mpango Mkuu wa Furaha,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Julai 27–Agosti 2. Alma 39-42,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Julai 27–Agosti2
Alma 39–42
“Mpango Mkuu wa Furaha”
Mafundisho ya Alma katika Alma 39–42 yana wingi wa mafundisho na yanafafanua ukweli. Wakati unapojifunza sura hizi, tafakari ni kweli zipi zinaweza kuwa na maana sana katika darasa lako na nini unaweza kufanya ili kuwasaidia wao kugundua kweli hizi.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwapa fursa washiriki wa darasa kushiriki mawazo yao na umaizi kuhusu Alma 39–42, ungeweza kuwaalika kwa ufupi kurejelea sura hizi na kutafuta kitu ambacho Alma alikisema au alichokifanya kilichowavutia.
Fundisha Mafundisho
Dhambi ya uasherati ni chukizo mbele za Bwana.
-
Je, tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye tukio la uzoefu wa Koriantoni kuhusu dhambi na toba? Labda washiriki wa darasa wangesoma Alma 39:1–14, baadhi yao wakitafuta kile Koriantoni alikosea, wengine wakitafuta kile kilichompelekea kutenda dhambi, na wengine wakitafuta ushauri Alma aliompa. Wakati wakishiriki vile walivyovipata, wangeweza kujadili jinsi gani tunaweza kuepuka kufanya makosa sawa na hayo.
-
Watu wanapotenda dhambi ya uasherati, mara nyingi wanakuwa na hisia za kukata tamaa na wanaweza kuhisi hawana thamani sana. Ni kanuni ipi katika Alma 39–42 inawashawishi washiriki wa darasa kuhisi tumaini ambalo linapelekea toba? Kushiriki maelezo toka kwa Dada Joy D. Jones katika “Nyenzo za Ziada” kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa tofauti kati ya ustahiki na thamani yetu katika uwepo wa Mungu. (Ona pia Lynn G. Robbins, “Hata Saba Mara Sabini,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 21–23.)
-
Kama sehemu ya majadiliano, ingeweza kusaidia kwa washiriki wa darasa kujadili viwango vya Bwana kuhusu ubikira. Mjadala wako unaweza kusaidia zaidi kama utajikita katika kanuni na si katika orodha ya nini cha kufanya au kutofanya. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutambua kanuni ambazo Alma alimfundisha Koriantoni katika Alma 39. Kama nyongeza, wangeweza kurejelea “usafi wa kimwili” katika Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana wakiwa na maswali mawazoni kama: “kama ningetaka kufupisha ushauri wote huu kwa kanuni moja , Je, ningesema nini?” au ni kanuni zipi ambazo unazipata hapa ambazo zinakusaidia kuishi sheria ya ubikira?” Washiriki wa darasa pia wangeweza kurejelea sehemu hii katika Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, wakitafuta baraka za kuishi sheria ya ubikira na madhara ya kutoitii sheria hii. Je, ni kwa namna gani kanuni hizi ni tofauti na dunia inachokifundisha? Ni kwa namna gani kanuni hizi huathiri jinsi tunavyofikiri kuhusu sheria ya ubikira? Darasa lako linaweza kunufaika kwa kusoma kauli toka kwa Dada Wendy Nelson katika “Nyenzo za Ziada” wakati wanapojibu maswali haya.
-
Wakati mwingine ni rahisi kuamini kwamba chaguzi zetu haziwaathiri wengine—kwamba dhambi zetu ni binafsi. Je, Alma alimfundisha nini Koriantoni katika Alma 39:11–12 kuhusu matokeo ya chaguzi zake? Waalike washiriki wa darasa kutafakari mtu ambaye anaweza kuathiriwa na chaguzi wanazozifanya, zote nzuri na mbaya. Wangeweza pia kushiriki ni kwa namna gani matendo na mifano ya wengine imewasaidia wao kuchagua yaliyo ya haki.
Upatanisho wa Yesu Kristo hufanya mpango wa wokovu uwezekane.
-
Alma alimfundisha Koriantoni kweli ambazo sote tunahitaji kuzielewa, ikijumuisha kweli kuhusu dhumuni la maisha, ulimwengu wa kiroho, ufufuko na hukumu. Fikiria kuchukua moja ya mafundisho ya Alma na wape washiriki wa darasa dakika mbili kupekua Alma 40–42 (kila mmoja au katika jozi) na waandike kadiri wawezavyo kweli kuhusu mada hiyo ambazo wamezipata. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kushiriki na kila mmoja au na darasa kile walichokipata. Ungeweza kurudia mchakato huu kwa kila mada kadiri muda unavyoruhusu. Kwa nini kweli hizi zilikuwa muhimu kwa Koriantoni mtoto wa Alma kuzielewa?
-
Maelezo ya Alma ya hali ya nafsi baada ya maisha haya inaweza kuvutia mawazo ya washiriki wa darasa juu ya umuhimu wa kuja kwa Kristo na kutubu dhambi katika maisha haya. Ungeweza kuandika utakatifu (atubuye) na uovu (asiyetubu) ubaoni na waalike washiriki wa darasa kupekua Alma 40:11–26 na kuorodhesha ubaoni maneno au virai ambavyo Alma alitumia kuelezea hali ya kila moja ya makundi haya ya watu baada ya kufa. Je, mafundisho haya yanawezaje kutuhamasisha kutubu? Kwa zaidi kuhusu nini hutokea katika ulimwengu wa Roho ona 1 Petro 3:18–20; 4:6 na Mafundisho na Maagano 138:29–37.
-
Je, nini kinakuja mawazoni mwa washiriki wa darasa lako wakati wakisikia maneno “rejeshwa” au “urejesho” Waalike kupekua Alma 41 kujua jinsi Alma alivyotumia maneno haya. Alimaanisha nini? Je, nini kitarejeshwa kwetu? Je, kwa nini kinaweza kusaidia kuuona mpango wa Baba wa Mbinguni kama “mpango wa urejesho”? (mstari wa 2
-
Baadhi ya washiriki wa darasa lako wanaweza kushirirki swali lililoonekana kuwepo mawazoni mwa Koriantoni—Je, ni haki au sawa kwamba Mungu atupendaye angewaadhibu watoto Wake? (Ona Alma 42:1). Labda ungewauliza washiriki wa darasa kutafakari jinsi wangeweza kujibu swali hili na kutafuta majibu katika Alma 42:7–26.
-
Kama unahisi ingekuwa sawa, washiriki wa darasa lako wangenufaika kwa kutafuta mstari toka Alma 42 ambao wangeuelezea kwa kutumia mchoro au alama ambayo inafafanua kwa nini tunahitaji Upatanisho wa Mwokozi. Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki walichokichora, na washiriki waliobaki wangejaribu kutafuta sura inayowakilisha mchoro. Kisha wangeweza kujadiliana kile walichojifunza kuhusu umuhimu wa dhabihu ya Mwokozi.
Nyenzo za Ziada
Thamani ya nafsi ni kuu.
Dada Joy D. Jones alifundisha:
“Acha nionyeshe haja ya kutofautisha maneno mawili muhimu: thamani na ustahiki. Hayalingani. Thamani ya kiroho ina maana kujithamini sisi binafsi jinsi Baba wa Mbinguni anavyotuthamini, sio jinsi dunia inavyotuthamini. Thamani yetu iliamuliwa kabla ya kuzaliwa kwetu hapa duniani. ‘Upendo wa Mungu hauna mwisho na utadumu milele.’
“Kwa upande mwingine, ustahiki unapatikana kupitia utiifu. Tunapotenda dhambi, tunakuwa si wastahiki kamili, lakini kamwe hatukosi thamani! Tunaendelea kutubu na kujitahidi kuwa kama Yesu, thamani yetu ikiwa ingali kamili. Kama Rais Brigham Young alivyofundisha: “Roho mdogo zaidi, aliye duni sana humu duniani … ana thamani kupindukia.’ Bila kujali chochote, daima tunayo thamani mbele ya macho ya Baba wa Mbinguni” (“Thamani Isiyo Kipimo,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 14).
Mtazamo wa kidunia kuhusu upendo huu hauko sawa na mtazamo wa Mungu.
Dada Wendy Nelson alitofautisha jinsi dunia inavyotazama mahusiano ya kimapenzi—na kile alichokiita “ Mapenzi katika ndoa yaliyotawazwa na Mungu”:
“Mahusiano ya kimapenzi ya kidunia chochote hukubalika. Mapenzi katika ndoa, utunzaji makini huwepo ili kuepusha chochote na kila kitu—kuanzia lugha mpaka muziki na filamu—ambazo humhuzunisha Roho, roho yako, au ya mwenzi wako.
“Wakati mahusiano ya kimapenzi ya kidunia ni ya matamanio, mapenzi katika ndoa huleta upendo zaidi.
“Mahusiano ya kimapenzi ya kidunia huwadhalilisha wanaume na wanawake na miili yao, wakati mapenzi katika ndoa huheshimu wanaume na wanawake na hufurahia mwili kama moja ya zawadi kuu ya maisha.
“Katika mahusiano ya kimapenzi ya kidunia, mtu huhisi kutumiwa, kuonewa, na hatimaye upweke zaidi. Mapenzi katika ndoa, wanandoa huhisi muunganiko na kupendwa zaidi, kukuzwa zaidi na kueleweka.
Mahusiano ya kimapenzi ya kidunia huleta madhara na hatimaye huaribu mahusiano. Mapenzi katika ndoa huimarisha ndoa. Husaidia, huponya, na huheshimu maisha ya wanandoa na ndoa yao. …
Mahusiano ya kimapenzi ya kidunia huleta wasiwasi kwa sababu kamwe hayatimizi ahadi zake. Mapenzi katika ndoa yaliyotawazwa na Mungu ni matukufu na yataendelea milele kwa waume na wake washikao maagano” (“Upendo na Ndoa” [mkutano wa ibada ulimwenguni kote, Jan. 8, 2017], broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).