Njoo, Unifuate
Julai 20–26. Alma 36–38: “Mtegemee Mungu na Uishi”


“Julai 20–26. Alma 36–38 : ‘Mtegemee Mungu na Uishi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Julai 20–26. Alma 36–38,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Mtu akisali

Kielelezo na Joshua Dennis

Julai 20–26

Alma 36–38

“Mtegemee Mungu na Uishi”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanaweza kuwa na uzoefu wenye tija kuhusu Alma 36–38. Je, unaweza kufanya nini ili kujenga juu ya uzoefu huo?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia mojawapo ya kuwahamasisha washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutoka katika maandiko ni kwa kugawa darasa katika makundi matatu na lipe kila kundi sura ya kusoma kutoka Alma 36–38. Alika kila kundi kutafuta na kushiriki mstari uliowagusa kutoka sura yao waliyosoma.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 36

Tunaweza kuzaliwa Kiungu tunapokuwa wanyenyekevu na kutubu.

  • Baadhi ya washiriki wa darasa lako wanaweza kushangaa kwa nini hawajawahi kuwa na uzoefu wa uongofu wa kushangaza kama wa Alma. Ingeweza kuwasaidia wao kama ungeshiriki kile Mzee David A. Bednar alifundisha: “kwa wengi wetu, uongofu ni mchakato unaoendelea na si tukio la mara moja ambalo linatokana na uzoefu wenye nguvu au wa kustaajabisha” (“Kuongoka Katika Bwana,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 107–8). Ingawa baadhi ya vitu kuhusu uzoefu wa uongofu wa Alma si vya kawaida, uzoefu wake hufundisha kanuni ambazo sote tunahitaji kuzitumia katika oungofu wetu wenyewe unaoendelea. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuchunguza Alma 36 kupata kanuni na kuziorodhesha ubaoni. Je, nini kingine kimetusaidia kuongoka zaidi katika injili ya Yesu Kristo?

  • Alma alitumia kirai “kuzaliwa Kiungu” kuelezea uongofu wake. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa wazo hili, ungeweza kuwaalika kusoma binafsi au katika jozi mistari ifuatayo, wakitafuta kile inachomaanisha kuzaliwa Kiungu: 1 Yohana 4:7; Mosia 5:7; 27:25–26; and Alma 5:14; 22:15. Waombe washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza. Kisha wangeweza kuchunguza Alma 36, wakitafuta majibu ya swali hili: Ni kwa namna gani watu huhisi na kutenda wakati wamezaliwa Kiungu? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari jinsi walivyozaliwa Kiungu, ungeweza kushiriki kauli toka kwa Rais Ezra Taft Benson ipatikanayo katika “Nyenzo za Ziada.”

Alma 37

Maandiko yamekuwa yakitunzwa kwa kusudi la busara.”

  • Labda kwa kusoma maneno ya Alma wakati akitoa kumbukumbu takatifu kwa Helamani mwana wake kunaweza kusaidia washiriki wa darasa kushiriki jinsi gani wamehisi nguvu ya maandiko katika maisha yao. Wahamasishe kurejelea Alma 37 wakitafuta jumbe ambazo Alma alimpa Helamani kuhusu maandiko (ona hasa Mstari wa 1–19 na 43–47). Je, ni kwa namna gani tunaonyesha maandiko ni matakatifu kwetu? Je, ni kwa namna gani sisi, kama Alma, tunawafundisha wapendwa wetu “kuweka vitu vyote katika utakatifu”? (Alma 37:2). Ni kwa namna gani maandiko “huonyesha nguvu za [Mungu]” kwetu? (Alma 37:14).

  • Njia mojawapo ya kujifunza kuhusu baraka za kuwa na maandiko ni kwa kusoma kile Alma alichokisema kwenye Alma 37 huhusu kumbukumbu takatifu na vitu vingine alivyomkabidhi Helamani. Ungeweza kutengeneza orodha ubaoni ya vitu vitakatifu: bamba za Nefi na mabamba ya shaba (Alma 37:2–20), bamba ishirini na nne za Etheri na vitafsiri (Alma 37:21–37), na Liahona (Alma 37:38–47). Washiriki wa darasa wangeweza kusoma mistari hii ili kujifunza kile Alma alikifundisha kuhusu vitu hivi. Ni katika njia zipi maandiko yanaweza kupanua kumbukumbu zetu? (ona Alma 37:8). Je, tunaweza kujifunza nini kutoka maneno ya Alma kuhusu baraka za kuwa na maandiko katika maisha yetu leo?

    Picha
    Mwanamke akisoma maandiko

    Maandiko hutufundisha jinsi ya kumfuata Mungu

Alma 37:6–7, 41–42

“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.”

  • Ili kufundisha kuhusu umuhimu wa “vitu vidogo na rahisi” katika kazi ya Mungu, Alma alitoa mifano miwili: maandiko na Liahona (ona Alma 37:6–7, 41–42; ona pia 1 Nefi 17:41). Baada ya kurejelea mifano hii, pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano kutoka kwenye maisha yao wenyewe ya vitu vidogo na rahisi katika kazi ya Mungu. Ungeweza kuwasiliana na mshiriki mmoja au wawili wa darasa kabla na waombe walete kitu darasani ambacho ni kidogo na ambacho kimeleta vitu vikubwa maishani mwao. Ungeweza pia kushiriki maelezo kutoka kwa Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada.” Ili kuwasidia washiriki wa darasa kutumia kanuni hii kulingana na mahitaji yao, ungeweza kuwauliza swali kama lifuatalo: Kwa nini wakati mwingine tunashindwa kufanya vitu vidogo na rahisi? Je, tunawezaje kuzitia hamasa nafsi zetu na familia zetu kushinda hali hii?

Alma 37:38–47

Neno la Kristo linaweza kutuongoza siku hadi siku.

  • Kulinganisha neno la Mungu na Liahona kungeweza kuwatia hamasa washiriki wa darasa kuwa wenye juhudi zaidi na wasiosita kuhusu kusoma maandiko. Ili kuongoza majadiliano kuhusu hili, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Alma 37:38–47 katika jozi, wakitafuta usawa kati ya Liahona na neno la Mungu. Ungeweza kuwapa changamoto kutafuta usawa katika kila mstari. Kisha ungeweza kuandika kila mstari ubaoni na waombe washiriki wa darasa kuandika usawa walioupata mbele ya namba. Je, ulinganifu huu unapendekeza nini kuhusu jinsi usomaji wetu wa maandiko matakatifu unavyotakiwa kuwa?

Alma 38

Kushiriki ushuhuda wetu wa Yesu Kristo kunaweza kuwaimarisha wale tunaowapenda.

  • Maneno ya Alma kwa Shibloni mwanawe yanatoa mfano mzuri wa jinsi ya kuimarisha na kutia moyo wale tunaowapenda katika kuishi injili. Labda washiriki wa darasa wangeweza kusoma sura hii na kutafuta jinsi Alma alivyomuimarisha Shibloni. AIma 38 ni fupi—ungeweza hata kuchagua kuisoma kama darasa. Kisha washiriki wa darasa wangeshiriki vifungu ambavyo vimewagusa au ambavyo vimewapa mawazo kwa ajili ya kuimarisha familia zao wenyewe na marafiki.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wa dararsa wamewahi kujiuliza jinsi ya kumshauri mpendwa aliye tenda kosa kubwa sana? Elezea kwamba watapata umaizi wa kuwasaidia katika Alma 39–42.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Uongofu ni kama kuzaliwa upya.

Rais Ezra Taft Benson alifundisha: “wakati tumepitia badiliko hili kuu, ambalo pekee huletwa kupitia imani katika Yesu Kristo na kupitia ufanyaji kazi wa Roho kwetu, ni kama vile tumekuwa watu wapya. Hivyo, badiliko linafananishwa na kuzaliwa upya. Maelfu yenu mmepitia badiliko hili. Mmeacha maisha ya dhambi, wakati mwingine dhambi kubwa na za kuudhi, na kupitia kutumia damu ya Yesu Kristo katika maisha yenu, mmekuwa wasafi. Hamna nia tena ya kurudi katika njia zenu za zamani. Kiuhalisia ninyi ni watu wapya. Hii ndio humaanisha kwa badiliko la moyo” (Badiliko Kuu la Moyo,” Ensign, Okt 1989, 4).

Vitu vidogo na rahisi

Rais DallinH. Oaks alifundisha:

“Nilikumbushwa juu ya nguvu ya vitu vidogo na rahisi baada ya muda kwa kitu nilichoona katika matembezi ya asubuhi. … Njia ya miguu ya saruji nene na imara [ilikuwa] ikipata ufa. Je,, hii ni matokeo ya baadhi ya msukumo mkubwa na wenye nguvu kutoka chini? Hapana, ufa huu unasababishwa na ukuaji mdogo wa taratibu, wa mojawapo ya mizizi ukipenyeza nje kutoka kwenye mti uliopakana. …

“Ndivyo ilivyo athari yenye nguvu baada ya muda ya vitu vidogo na rahisi tunavyofundishwa katika maandiko na manabii wanaoishi. Fikiria kujifunza maandiko ambako tumekuwa tukifundishwa kushirikisha katika maisha yetu ya kila siku. Au fikiria sala za binafsi na sala za kupiga magoti za familia ambazo ni utaratibu wa kila siku kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu. … Japo kila moja ya taratibu hizi zinaweza kuonekana kuwa ndogo na rahisi, baada ya muda zinapelekea kwenye kuinuka na kukua kwa nguvu kiroho. Hii hutokea kwa sababu kila moja ya hivi vitu vidogo na rahisi hualika wenza wa Roho Mtakatifu, Mshuhudiaji ambaye hutuelimisha na kutuongoza kwenye ukweli” (Vitu Vidogo na Rahisi,” Ensign au Liahona, Mei 2018, 90).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waalike wanafunzi kufundishana. Wakati washiriki wa darasa wanatoa shuhuda au kushiriki umaizi, wanaweza kuwafikia au kuwatia hamasa washiriki wengine wa darasa katika njia ambayo usingeweza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,30.)

Chapisha