Njoo, Unifuate
Juni 29–Julai 5. Alma 23–29: Kamwe “Hawakuanguka tena”


Juni 29–Julai 5. Yakobo 23-29: ‘Kamwe Hawakuanguka tena,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

Juni 29–Julai 5. Alma 23–29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Waanti-Nefi-Lehi Wakizika silaha zao

Waanti-Nefi-Lehi wakizika Silaha Zao za Kivita, na Jody Livingston

Juni 29–Julai 5

Alma 23–29

Kamwe “Hawakuanguka tena”

Wakati unaposoma Alma 23–29, kumbuka kwamba ili uweze kuwasaidia wengine kujifunza kweli zilizopo katika sura hizi, unahitaji kuwa na uzoefu wa kufaa kuhusu kweli hizo wewe mwenyewe.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuandika ubaoni mistari ambayo imewagusa wakati wa usomaji wao binafsi au kama familia. Tumia dakika chache kuwaalika baadhi ya watu kujadili kweli walizojifunza kutoka kwenye mistari waliyoiandika.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 23–25; 27

Uongofu wetu kwa Yesu Kristo na injili Yake hubalisha maisha yetu.

  • Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tunajitahidi kukuza kwa kina uongofu wetu. Labda hadithi ya Waanti-Nefi-Lehi inaweza kuwatia moyo wale unaowafundisha katika juhudi zao za kufanya hivi. Ungeweza kuanza kwa kuandika ubaoni swali kama lifuatalo: Je, kuongoka humaanisha nini? au Ni mabadiliko ya aina gani hutokea katika maisha ya watu wakati wakiongoka? Washiriki wa darasa wangeweza kauangalia majibu katika vifungu hivi: Alma 23:6–7, 17–18; 24:17–19; 25:15–16; na 27:26–30. Wangeweza kushiriki umaizi kutoka katika mistari mingine ambayo waliisoma katika Alma 23–25 na 27. Washiriki wa darasa pia wanaweza kupata majibu ya maswali haya katika ujumbe wa Mzee David A. Bednar “Kuongoka katika Bwana ” (Ensign au Liahona, Nov. 2012,106–9; ona pia “Nyenzo za ziada”). Ni mabadiliko gani waliyafanya Waanti-Nefi-Lehi kama matokeo ya uongofu wao? Ni kwa namna ipi mfano wao hututia hamasa kukuza kwa kina uongofu wetu kwa Yesu Kristo na injili Yake?

  • Ni kwa namna ipi unaweza kuwatia hamasa washiriki wa darasa kuacha desturi za uongo na kuzika silaha zao za uasi, kama Waanti-Nefi-Lehi walivyofanya? Fikiria kurejelea Alma 23:5–7 kwa pamoja. Ni baadhi ya desturi zipi nzuri ambazo injili hutusaidia kuziendeleza? Ni kipi huwakilisha “silaha za … uasi” za Walamani katika siku zetu? Ni kwa namna ipi tunaweza “kuzizika chini ardhini”? (Alma 24:17). Waalike washiriki wa darasa kutafakari desturi zipi za uongo au silaha za uasi wanahitaji kuziacha ili kwamba waweze kuishi injili kikamilifu zaidi.

Alma 24:7–16

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa tunapotubu.

  • Kama unahisi msukumo kuwa na mjadala darasani kuhusu toba, tukio la Waanti-Nefi-Lehi katika Alma 24 ni mfano mzuri wa kuigwa kuutumia. Ungeweza kumpa kazi kila mshiriki wa darasa kusoma mstari kutoka Alma 24:7–16 na waombe waandike ubaoni kitu walichojifunza kutoka kwenye mstari kuhusu toba. Kisha wangeweza kutafuta kwenye maandiko yafuatayo kwa ajili ya kupata umaizi wa ziada kuhusu toba: Isaya 53:5–6; 2 Nefi 2:6–8; and Mosia 5:2.

Alma 24:13–15; 2629

Injili huleta shangwe!

  • Katika Alma 23–29, neno “shangwe” hutokea mara 24, kuzifanya sura hizi sehemu nzuri ya kujifunza jinsi kuishi injili—na kuishiriki—huleta shangwe. Ungeweza kuwagawa washiriki wa darasa katika makundi na kuuliza kila kundi kurejelea baadhi ya mistari ifuatayo, wakitafuta sababu za kwa nini Amoni, wana wa Mosia, na Alma walipata shangwe: Alma 24:13–15; 26:12–22; na 29:1–17. Washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha ubaoni kile walichokipata. Je, tunajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu jinsi injili huleta shangwe?

  • Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Wakati fokasi ya maisha yetu ni katika mpango wa Mungu wa wokovu … na Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kujisikia furaha bila kujali nini kinatokea—au kutotokea—katika maisha yetu. Shangwe huja kutoka kwa na kwa sababu Yake. Yeye ni chanzo cha furaha yote” (“Furaha na Kuendelea Kusalia Kiroho,” Ensigh au Liahona, Nov. 2016, 82. Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao umewasaidia wao kuelewa kweli katika maneno ya Rais Nelson.

  • Alma na Amoni walipata shangwe kuu katika kushiriki injili. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta mistari katika Alma 26 na 29 ambayo ingemtia msukumo kijana kuhudumu misheni—au kumtia msukumo yoyote kushiriki injili na wengine. Fikiria kutoa dakika kadhaa kwa ajili ya washiriki wa darasa kupanga kitu ambacho wangeweza kufanya ili kushiriki injili. Waalike kutimiza mipango yao, na katika darasa lijalo unaweza kuwatia moyo kuzungumza kuhusu juhudi zao.

  • Wakati Alma alipowasaidia wengine kutubu, alikumbushwa kuhusu wema wa Mungu (ona Alma 29:10–13). Labda ungeweza kuwapa washiriki wa darasa muda kiasi kujifunza mistari hii na kuorodhesha kile ambacho Alma alikikumbuka. Je, nini hutukumbusha wema wa Mungu? Je, ni kwa namna ipi tumeuona wema wa Mungu katika maisha yetu?

Alma 26–27

Tunaweza kuwa vyombo mikononi mwa Mungu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza nini kuwa “vyombo mikononi mwa Mungu” humaanisha (Alma 26:3), ungeweza kuonyesha aina mbalimbali za vyombo au zana. Ungeweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kuleta baadhi ya zana ambazo wanatumia. Ni kwa namna ipi vyombo hivi ni vya thamani? Ni kwa namna ipi sisi ni kama vyombo mikononi mwa Mungu? Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutambua njia Amoni na wamisonari wenzake walikuwa vyombo mikononi mwa Mungu (ona, kwa mfano, Alma 26:1–5, 11–12). Ni umaizi gani tunaoupata kutoka Mafundisho na Maagano 4 juu ya kuwa vyombo mikononi mwa Mungu? Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki uzoefu wakati walipohisi shangwe ambayo huja kutokakana na kuwa chombo mikononi mwa Mungu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Mengi ya mawazo ya uongo ambayo leo hii huwapeleka watoto wa Mungu upotevuni pia yalikuwepo wakati wa Alma. Waambie washiriki wa darasa kwamba katika Alma 30–31 wataona jinsi Alma na wengine walivyofanya katika mafunzo haya ya uongo.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuongoka katika Bwana

Mzee David A. Bednar alifundisha:

“Kiini hasa cha injili ya Yesu Kristo kinajumuisha badiliko la msingi katika asili yetu lililofanikishwa kupitia Upatanisho wa Mwokozi. Uongofu wa kweli huleta badiliko katika kuamini, moyo, na maisha ya mtu kukubali na kufuata mapenzi ya Mungu (ona Matendo ya Mitume 3:19; 3 Nefi 9:20) na hujumuisha kujitolea toka moyoni kuwa mfuasi wa Kristo.”

Baada ya kunukuu Alma 23:6–8, Mzee Bednar aliendelea kwa kufafanua:

“Vitu vikuu viwili vimeelezewa katika mistari hii: (1) uelewa wa ukweli, ambao unaweza kutafsiriwa kama ushuhuda, na (2) Kuongoka katika Bwana, ambako nakuelewa kuwa ni kuongoka katika Mwokozi na injili Yake. Hivyo, muunganiko wa nguvu wa vyote ushuhuda na uongofu katika Bwana ulizalisha uimara na uthabiti na ulitoa ulinzi wa kiroho.

“Kwani walipata kuwa watu wenye haki na wakaweka chini silaha zao za uasi, kwamba hawakupingana na Mungu tena.’ Kuweka chini ‘silaha za uasi’ ambazo zilipendwa kama vile ubinafsi, majivuno, na kutotii huitaji zaidi ya kuamini tu na kujua. Msimamo, unyenyekevu, toba, na utiifu huanza kabla ya uachaji wetu wa silaha za uasi. Je, mimi na wewe tunamiliki silaha za uasi ambazo zinatuzuia kuongoka katika Bwana? Kama ndivyo, tunahitaji kutubu sasa.

“Zingatia kwamba Walamani hawakuongoka katika wamisionari waliowafundisha au katika programu nzuri za Kanisa. Hawakuongoka katika utu wa viongozi wao au katika kutunza utamaduni wa vizazi au katika desturi za babu zao. Waliongoka katika Bwana—Yeye kama Mwokozi na katika utakatifu Wake na mafundisho Yake—na kamwe hawakuanguka tena” (Kuongoka katika Bwana,” Ensign au Liahona Nov.2012, 107–9).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo toka kwa viongozi wako. Viongozi wako wa ukuhani na vikundi saidizi wanataka kukusaidia ufanikiwe. Omba ushauri wao wakati unapojitahidi kujiboresha kama mwalimu na unapotafakari mahitaji ya wale unaowafundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,5).

Chapisha