“Julai 13–19. Alma 32–35: ‘Pandeni Neno Hili Mioyoni Mwenu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020.)
“Julai 13–19. Alma 32–35,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Julai 13–19
Alma 32–35
“Pandeni Neno Hili Mioyoni Mwenu”
Bila kujali ni mara ngapi umesoma Alma 32–35, soma tena wakati unapojiandaa kufundisha. Kuwa tayari kwa umaizi mpya toka kwa Roho.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki walichojifunza kutoka Alma 32–35 nyumbani, ungeweza kuwapa dakika chache kurejelea sura hii na kuandika ubaoni maudhui au mada zozote walizopata. Kama darasa, jadilini kwa nini maudhui au mada hizi ni za maana
Fundisha Mafundisho
Tunaweza kuchagua kuwa wanyenyekevu
-
Ili kuongoza majadiliano kuhusu unyenyekevu kama ilivyofundishwa katika Alma 32:1–16, ungeweza kuanza kwa kuwaalika washiriki wa darasa kutaja uzoefu ambao unaweza kumnyenyekeza mtu (Alma 32:2–5 toa mfano mmoja). Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa tayari kushiriki uzoefu wao wenyewe wa kujifunza unyenyekevu. Ni kwa namna ipi “kunyenyekezwa kwa lazima” (Alma 32:12) ni baraka? Kauli kuhusu unyenyekevu katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia kuongeza majadiliano. Ungeweza pia kusoma Mafundisho na Maagano 112:10 au kuimba wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vileKuwa Mnyenyekevu” (Nyimbo za Kanisa, namba 130), kama darasa.
Tunatumia imani katika Yesu Kristo kwa kupanda na kulisha neno Lake mioyoni mwetu.
-
Sisi wakati mwingine tunafikiri kuabudu kama kitu tu tufanyacho katika mazingira maalum kama katika majengo ya kanisa (ona Alma 32:5,9,11), lakini maelezo ya Alma ya kuabudu ni ya kina zaidi. Kwa mfano, alifundisha kwamba kukuza na kutumia imani katika Yesu Kristo ni aina muhimu ya kuabudu ambayo inachukua nafasi nje ya mazingira maalum. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa kanuni hii, ungeweza kuchora picha ya mbegu na mti ubaoni na kujadili swali kama lifuatalo: Je, mbegu huwakilisha nini? (Ona Alma 32:28; 33:22–23). Je, tunawezaje kupanda mbegu—au ushuhuda wa Yesu Kristo na Upatanisho Wake—katika mioyo yetu na kuzikuza? (ona Alma 32:36–43;33). Ni uzoefu gani tunaoweza kuushiriki ambapo juhudi zetu za kumfuata Mwokozi zilizaa matunda yenye thamani? Je, ni kwa namna gani mafundisho ya Alma yanaathiri jinsi tunavyomwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
-
“Jaribio” ambalo Alma alilielezea kuwasaidia Wazoramu kukuza imani katika Yesu Kristo linaweza pia kutusaidia kujifunza kama kanuni zingine za injili ni za kweli. Ili kulisaidia darasa kuelewa jaribio la Alma, ungeweza kuongea kuhusu jaribio ni nini Kunaweza kuweko na mtu darasani ambaye amefanya jaribio kabla na angeweza kuwasadia kufafanua hili. Je, nini dhumuni la jaribio? Je, ni kwa namna ipi jaribio ni sawa na kile Alma aliwaalika watu kufanya katika Alma 32:26—36? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki njia tofauti tofauti ambazo “wamefanyia majaribio” juu ya neno la Mungu. Ni kwa namna ipi wamekuja kujua kwamba “neno [la Mungu] ni zuri”? (Alma 32:28).
-
Je, Alma angesema nini kwa mtu ambaye anataka kupata au kuimarisha ushuhuda juu ya Yesu Kristo? Ili kuchunguza swali hili, ungeweza kuligawa darasa katika makundi mawili. Kundi moja lingeweza kusoma Alma 32:26–36 ili kugundua kile Alma angekisema kwa mtu ambaye anajaribu kupata ushuhuda, na kundi lingine lingesoma Alma 32:36–43 kugundua kile angekisema kwa mtu ambaye ushuhuda wake umefifia. Kisha mtu mmoja kutoka kila kundi angeweza kuchukua nafasi kumwakilisha Alma na kuigiza jinsi ya kumsaidia mtu kupata ushuhuda au kuimarisha ushuhuda.
Alma 31:13–23; 33:2–11; 34:17–29
Tunaweza kumwabudu Mungu katika sala, muda wowote na mahali popote.
-
Ungeweza kulisaidia darasa kutofautisha mafundisho ya Alma na Amuleki kuhusu sala na dhana za uongo za Wazoramu. Washiriki wa darasa wangeweza kurejelea Alma 31:13–23 na kuorodhesha ubaoni Wazoramu walichokiamini kuhusu sala na kuabudu. Wangeweza kutafuta kweli toka Alma 33:2–11 na 34:17–29 ambazo zinatofautiana na imani hizi. Je, mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi gani tunaweza kuboresha sala zetu na kuabudu?
-
Ungeweza kuhamasisha majadiliano kuhusu sala kwa kuandika maneno kama Nani? Nini? Lini? Wapi? Kwa nini? na jinsi gani ubaoni. Washiriki wa darasa wangeweza kupekua Alma 33:2–11 na 34:17–29 kupata majibu ya maswali haya kuhusu sala. Kwa mfano, wangeweza kujibu maswali kama haya: Wapi tunaweza kusali? Tunaweza kusali juu ya nini? Wangeweza pia kupata majibu katika maneno ya wimbo kuhusu sala kama vile “Je, Uliomba?” au “Saa Nzuri ya Sala” (Nyimbo za Kanisa, namba 140, 142). Je, tunawezaje kuboresha sala zetu?
Upatanisho wa Mwokozi ni “usiyo na Mwisho na wa milele.”
-
Amuleki alitumia maneno “usiyo na mwisho” na “wa milele” mara nyingi kuelezea dhabihu aliyoitoa Yesu Kristo kwa ajili ya dhambi zetu. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta maneno haya katika Alma 34:9–14 na kisha kuyatafuta kwenye kamusi. Ni kwa njia zipi dhabihu ya Mwokozi haina mwisho na ni ya milele? (Ona Waebrania 10:10; 2Nefi 9:21; Mosia 3:13). Kulingana na Alma 34:15–17, Je, ni lazima tufanye nini ili kupokea baraka za dhabihu ya Mwokozi? Je, humaanisha nini “kutumia imani yenu kwa toba”? (Alma 34:17).
“Usihairishe siku yako ya toba.”
-
Analojia kama ifuatayo ingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari hatari za kuhairisha toba yetu: waalike kupiga picha mawazoni mwao kwamba wamepokea mwaliko wa kushiriki katika tukio ambalo linahitaji miaka ya mafunzo na maandalizi, kama mashindano ya Olympic au muziki (chagua kitu chenye manufaa kwa darasa lako), lakini tukio hili litafanyika kesho. Jadili na darasa kwa nini wasingefaulu katika tukio hata kama wametumia siku ya leo kujiandaa. Ni kwa namna ipi mfano huu unahusiana na maonyo ya Amuleki katika Alma 34:32–35? Je, kwa nini ingekuwa hatari kuchelewesha juhudi zetu kutubu na kubadilika? Waalike washiriki wa darasa kutafakari nini wangefanya ili “kujiandaaa kwa ajili ya uzima wa milele” (mstari wa 33) na kuweka mipango kufanya hivyo bila kuchelewa.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwatia msukumo washiriki wa darasa kusoma Alma 36–38 wiki hii, ungeweza kuonyesha kwamba Alma “alihuzunishwa na uovu wa watu wake,” hivyo aliwakusanya wana wake na kuwafundisha “kuhusu vitu vinavyohisiana na haki” (Alma 35:15–16). Baadhi ya sura za kitabu cha Alma zinazofuata zinatoa maelezo ya kile Alma alipata msukumo kuwafundisha watoto wake.
Nyenzo za Ziada
Je, humaanisha nini kuwa mnyenyekevu?
Kuwa mnyenyekevu ni kutambua kwa shukrani utegemezi wako kwa Bwana—kuelewa kwamba una hitaji kila mara usaidizi toka Kwake. … Si ishara ya udhaifu, kutojiamini, au uwoga; ni kielelezo kwamba unajua wapi nguvu zako za kweli zinatoka” (Kweli Katika Imani [2004],86).
Mzee Quentin L. Cook alifafanua: “Wakati tunapotafakari kwa kina kuhusu Mungu Baba na Kristo Mwana, jinsi walivyo, na vile walivyovikamilisha kwa niaba yetu, inatujaza sisi na heshima kuu, mshangao, shukrani, na unyenyekevu. … Unyenyekevu pia hujumuisha kuwa mwenye shukrani kwa baraka nyingi na msaada mtakatifu. Unyenyekevu sio mafanikio fulani makubwa yanayotambulika au hata kushinda changamoto fulani kubwa. Ni ishara ya nguvu za kiroho. Ni kuwa na utulivu wa kujiamini kwamba siku hadi siku na saa baada ya saa tunaweza kumtegemea Bwana, kumtumikia Yeye, na kufanikisha azma zake” (“Milele ya Kila Siku,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 52, 54).