“Julai 6–12. Alma 30–31: ‘Uwezo wa Neno la Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Julai 6–12. Alma 30–31,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Julai 6–12
Alma 30–31
“Uwezo wa Neno la Mungu”
Baada ya kusoma Alma 30–31 na kutafuta msukumo wa kiungu kwa ajili ya maisha yako mwenyewe, sikiliza misukumo kuhusu jumbe zipi zitawabariki washiriki wa darasa lako
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kama unahisi kwamba washiriki wa darasa wanasita kushiriki, ungeweza kuwapa dakika chache kurejelea Alma 30–31 au notisi walizoandika katika kusoma kwao nyumbani wiki hii. Kisha wangeweza kushiriki na mwenzi au darasa ujumbe wenye nguvu walioupata.
Fundisha Mafundisho
Adui anajaribu kutudanganya kwa mafundisho ya uongo.
-
Wakati ukifikiria mahitaji ya darasa lako, Je, ingesaidia wao kuelewa tofauti kati ya kweli za injili na udanganyifu wa Shetani kama ungetumia somo kwa vitendo? Kama ndivyo, ungeweza kuwaonyesha baadhi ya vitu bandia, kama hela au mwanasesere aliye kama chakula, pamoja na hela halisi na chakula halisi. Je, tunawezaje kujua kwamba vitu bandia si vitu halisi? Kisha darasa lingetambua mafundisho ya uongo ya Korihori katika Alma 30:6–31. Je, nini kinaweza kuwa cha kuvutia katika mafundisho haya? Je, ni nini kweli za injili hutoa ambacho mafundisho ya udanganyifu ya Shetani hayawezi? Waalike washiriki wa darasa kushiriki kilichomsaidia Alma kutambua kati ya mafundisho ya kweli na mafundisho ya uongo (ona Alma 30:32–54). Ni njia zipi saidizi zingine ambazo washiriki wa darasa wamezipata?
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza jinsi ya kujikinga wao wenyewe kutokana na mafundisho ya uongo, ungeweza kurejelea maelezo kuhusu mpinga-Kristo katika Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Ni mistari ipi katika Alma 30:6–31 inaonyesha kwamba Korihori anafaa katika maelezo haya? Ni mafundisho gani toka kwake ni sawa na mafundisho ya uongo katika siku zetu? (Ona Alma 30:12–18, 23–28). Je, tunawezaje kuepuka kudanganywa na mafundisho haya?
Mambo Yote Yanamshuhudia Mungu.
-
Kwa sababu tunaishi kwenye ulimwengu sawa na wa Alma, ambapo baadhi ya watu wanafundisha kwamba hakuna Mungu, ushuhuda wa Alma katika Alma 30:39–44 ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako. Ungeweza kuwaalika kusoma mistari hii na kuorodhesha ubaoni juu ya kweli na ushahidi anaoutoa Alma ambao unashuhudia kuna Mungu. Ni shuhuda zipi zingine ambazo tunazo kwamba Mungu Anaishi? Kama sehemu ya mjadala, fikiria kushiriki maelezo toka kwa rais M. Russell Ballard katika “Nyenzo za Ziada.” Ungeweza pia kumwalika mtu kuja akiwa amejiandaa kuimba wimbo kuhusu wema wa Mungu, kama vile “Jinsi Ulivyo Mkuu” (Nyimbo za Kanisa, na. 86), au mngeweza kuimba kwa pamoja.
-
Wakati Alma akiongea na Korihori, aliona kwamba Korihori alikuwa “amemweka mbali Roho wa Mungu kwamba hangekuwa na nafasi ndani [yake]” (Alma 30:42). Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kupekua Alma 30:39–46, wakitafuta marejeleo mengine kuhusu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hufanya jukumu lipi katika kushuhudia kwetu kuhusu uhalisia wa Mungu na Yesu Kristo? Je, tunaweza kuwasaidiaje wale ambao wana mashaka au maswali kutafuta ukweli kupitia Roho Mtakatifu?
Neno la Mungu lina nguvu ya kuongoza watu katika haki.
-
Je, kuna washiriki wa darasa lako ambao wangeshiriki uzoefu wakati “uwezo wa neno la Mungu” (Alma 31:5) uliwasaidia wao au mtu mwingine wanayemjua kufanya mabadiliko katika maisha yao? Ungeweza kuwasiliana kabla na washiriki wa darasa ili kwamba waweze kujiandaa kushiriki uzoefu wao. Watie moyo kushiriki mistari kutoka Alma 31 ambayo inatumika katika uzoefu wao. Washiriki wengine wa darasa wangeweza pia kushiriki njia ambazo kwazo neno la Mungu lilikuwa na “matokeo ya nguvu zaidi katika akili [zao]” (Alma 31:5). Washiriki wanaweza kunufaika katika kusoma kutoka maandiko mengine ambayo yanashuhudia kuhusu nguvu za neno la Mungu (ona “Nyenzo za Ziada” kwa ajili ya mifano michache).
-
Wakati washiriki wa darasa lako wakijifunza Alma 31 wiki hii, wanaweza kuwa wamevutiwa na mfano wa Alma wa kusali kwa ajili ya Wazoramu. Fikiria kuwauliza walichojifunza kutoka sura hii kuhusu kuwafikia wanafamilia au marafiki ambao wameiacha njia ya injili au wanahangaika na imani yao. Ungeweza kuwaomba pia kupekua Alma 31 kwa pamoja na kuorodhesha ubaoni vitu walivyoviona kuhusu Alma ambavyo vilimsaidia kuwaokoa Wazoramu. Ni kwa nama ipi tunatumia neno la Mungu zaidi katika juhudi zetu za kuwaokoa wengine? (Kwa umaizi wa ziada, ungeweza kushiriki nukuu toka kwa Mzee Jeffery R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”)
-
Je, ni kipi washiriki wa darasa wanakipata katika Alma 31:30–38 ambacho kinaweza kuwasaidia wale wenye huzuni kwa ajili ya dhambi za wengine kama Alma alivyokuwa?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waulize washiriki wa darasa ni fundisho gani au kanuni zipi za injili ambazo wangeweza kuzifundisha kuondoa uongo Alma aliougundua kati ya Wazoramu. Waambie kwamba wakati wakisoma Alma 32–35 watagundua jinsi Alma alivyotumia neno la Mungu kuwasaidia Wazoramu kuona umuhimu wa kubadilika.
Nyenzo za Ziada
Maandiko kuhusu nguvu za neno la Mungu.
Vitu vyote vinaonyesha kwamba kuna Mungu.
Rais Rais M. Russell Ballard alifundisha kwamba “ushahidi wa milele” Alma alioutoa wa kuwepo Mungu “unaendelea kushuhudia kwetu hata leo” (ona Alma 30:44):
Wana anga wanaoiangalia dunia kutoka angani wamesema jinsi ilivyo nzuri inavyoonekana kuwa hai kutoka angani. Seneta wa Marekani Jake Garm aliandika kuhusu uzoefu wake katika anga: “ni vigumu kwangu kuuelezea uzuri wa dunia. Ina uhai, inashangaza, uzoefu wa kiroho wa kuiangalia dunia toka angani wakati wa kusafiri mara ishirini na tano kwa spidi ya sauti. Pia ningeweza kuangalia katika giza la ombwe ya anga na kuona mabilioni ya nyota na mamilioni ya sayari mbali-miaka mingi. Ulimwengu ni mpana sana kwamba haiwezekani kuuelewa. Lakini niliweza kuuelewa mkono wa Mungu katika vitu vyote. Nilihisi uwepo wake kupitia siku zangu saba katika anga. Najua kwamba Mungu aliumba dunia hii na ulimwengu. … Ninajua kwamba Mungu anaishi na ni Muumba wetu sote’ (barua kwa M. Russell Ballard, 3 Machi 1988)” (“Upendo wa Mungu kwa watoto Wake,” Ensign, Mei 1988, 58).
Waimarishe wengine kwa neno la Mungu.
Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:
“Je, sisi kweli tunawakuza vijana na waumini wapya katika njia ambayo itawasaidia wao wakati wa msongo wa mawazo wa maisha? Au tunawapa aina ya elimu ya dini—isiyoleta nguvu za kiroho? … Wakati wa majira ya baridi kali miaka kadhaa iliyopita, Rais Boyd K. Packer aliona kwamba idadi kubwa ya kulungu ilikuwa imekufa kwa njaa wakati matumbo yao yalikuwa yamejaa nyasi Katika juhudi za dhati za kusaidia, mashirika yaligawa kilichokuwepo wakati kilicho cha msingi ndicho kilikuwa kikihitajika. Kwa majuto walikuwa wamewalisha kulungu lakini hawakuwa wamewatunza . …
Shetani kwa hakika ana hila kwenye mafundisho yake; Je, kwa nini nasi tuwe? Iwe tunawaelekeza watoto wetu nyumbani au kusimama mbele ya umma kanisani, kamwe tusifanye imani yetu kuwa ngumu kutambulika. … Toa hotuba za kiroho. Fundisha fundisho liliofunuliwa” (“Mwalimu toka kwa Mungu,” Ensign, Mei 1998, 26–27).