Njoo, Unifuate
Juni 22–28. Alma 17–22 : “Nitawafanya Muwe Chombo”


“Juni 22–28. Alma 17–22: ‘Nitawafanya Muwe Chombo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 22–28. Alma 17–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Amoni akizungumza na Mfalme Lamoni

Amoni na Mfalme Lamoni, na Scott M. Snow

Juni 22–28

Alma 17–22

“Nitawafanya Muwe Chombo”

Kabla ya kuweza kuwasaidia wengine kugundua kweli katika maandiko, unahitaji kugundua kweli kwa ajili yako mwenyewe. Soma Alma 17–22 ukiwa na washiriki wa darasa lako akilini mwako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwapa washiriki wa darasa nafasi ya kushiriki kitu fulani walichojifunza katika kujifunza kwao binafsi au na familia, ungeweza kuwaalika wamchague mtu aliyeelezewa katika Alma 17–22 na kukamilisha sentensi kama ifuatayo: “Abishi alinifundisha ” au “Lamoni alinifundisha .”

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 17:1–4

Imani yetu inaimarishwa pale tunapotafuta kwa bidii kujua ukweli.

  • Washiriki wa darasa bila shaka wamesikia mara nyingi umuhimu wa tabia rahisi za injili. Alma 17:1–4 inaweza kuwasaidia kuona athari zenye nguvu kubwa ambazo tabia hizi zinaweza kuwa nazo kwenye maisha yetu. Ungeweza kuwaomba nusu ya darasa kuchunguza mistari hii kwa ajili ya kile wana wa Mosia walichofanya na nusu wengine kuchunguza matokeo ya kile walichofanya. Ni nini kimekuwa matokeo ya kufanya mambo haya katika maisha yetu?

  • Kwa ajili ya majadiliano ya kina juu ya baadhi ya tabia ambazo ziliwaimarisha wana wa Mosia, ungeweza kuandika ubaoni Kuchunguza Maandiko, Sala, na Kufunga. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza maandiko ambayo yanafundisha kuhusu baraka ambazo zinakuja kutokana na kujifunza maandiko, sala, na kufunga ( Mwongozo wa Mada au Mwongozo kwenye Maandiko vinaweza kusaidia). Wangeweza kuandika ubaoni kile wanachopata na kushiriki wao kwa kwao mawazo kuhusu jinsi ya kuboresha kujifunza kwao maandiko, sala, na kufunga katika njia ambayo inawavuta karibu zaidi na Mungu.

Alma 17–18

Upendo wetu unaweza kuwasaidia wengine kujiandaa kupokea injili.

  • Kuna njia nyingi za kushiriki injili, na zote ni zenye kufaa zaidi wakati upendo ukiwa motisha. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kutambua mistari katika Alma 17–18 ambayo inaonesha jinsi Amoni alivyotiwa motisha na upendo kushiriki injili. Ni kweli zipi zingine kuhusu kushiriki injili tunazojifunza kutokana na mfano huu? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu ambapo upendo wa kweli ulilainisha moyo wa mtu fulani na kumruhusu kuwa mpokeaji zaidi wa ujumbe wa injili. Maelezo kutoka kwa Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” yangeweza pia kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa kuhakikisha juhudi zetu zinapatikana kwenye upendo.

Picha
Amoni akiokoa kondoo wa Mfalme

Amoni Anaokoa Makundi ya Mifugo ya Mfalme, na Minerva K. Teichert

Alma 18–22

Kufundisha na kujifunza kweli za injili kwa ufanisi kunaweza kupelekea kwenye badiliko la moyo.

  • Pale Amoni na Haruni walipopata kuaminiwa na Mfalme Lamoni na baba yake, waliweza kuwasaidia kuelewa kweli muhimu za injili. pengine ingeweza kusaidia kama washiriki wa darasa wangetengeneza orodha ya kweli Amoni alizomfundisha Lamoni (ona Alma 18:24–39) na kuilinganisha na orodha ya kweli Haruni alizomfundisha baba wa Lamoni (ona Alma 22:1–16). Nusu ya darasa ingeweza kufanyia kazi orodha moja wakati nusu wengine wakifanyia kazi orodha nyingine. Kwa nini kuelewa kweli hizi kungepelekea Lamoni na baba yake kuamini na kutumaini katika Baba wa Mbinguni na Mwanae, Yesu Kristo?

  • Maelezo ya Haruni na Amoni wakimfundisha Mfalme Lamoni na baba yake yanatoa nafasi kubwa ya kujadili kufundisha na kujifunza injili kwa ufanisi. Ni kanuni zipi za ufundishaji washiriki wa darasa wanazigundua? (ona, kwa mfano, Alma 18:24–28 na Alma 22:7–13). Ni kanuni zipi za kujifunza wanazipata katika mifano ya Mfalme Lamoni na baba yake? (Ona kwa mfano, Alma 18:25–31; 22:17–18).

  • Kujifunza kuhusu jinsi mafundisho ya injili yanavyoweza kushawishi maisha yetu, washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza Alma 18:40–41; 20:1–15; na Alma 22:15–18, 25–27 kutafuta jinsi Mfalme Lamoni na baba yake walivyohisi na kufanya baada ya kuelewa kweli za injili na kuongoka. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinatusaidia kuja kwa Kristo? Ni nini tunaweza kufanya kujisaidia sisi wenyewe na wapendwa wetu kuelewa na kuishi kweli hizi?

Alma 19–22

Shuhuda zetu zinaweza kuwa na ushawishi wa kina sana kwa wengine.

  • Wakati wa kujifunza kwao binafsi Alma 19–22, washiriki wa darasa yaweza kuwa walitafakari matokeo makubwa ambayo ushuhuda wa mtu mmoja unaweza kuwa nayo kwa wengine. Wahimize kushiriki kile walichojifunza. Ni nini maelezo katika Alma 19–22 yanapendekeza kuhusu juhudi zetu binafsi za kushiriki injili? Hadithi ya Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kusaidia kusisitiza wazo hili.

  • Ni analojia zipi nzuri ungeweza kushiriki kuonesha kwa mfano kile kinachoweza kutokea wakati tunaposhiriki shuhuda zetu na wengine? Mifano inayowezekana ni changarawe ikitengeneza viwimbi ndani ya ziwa au hamira ikisaidia kinyunya kuvimba. Baada ya kurejea upya baadhi ya mifano ya watu wakishiriki shuhuda zao katika Alma 19–22, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyoathiriwa na shuhuda za wengine.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kama wamewahi kujiuliza jinsi ya kufanya uongofu wao thabiti na endelevu. Katika Alma 23–29, watasoma kuhusu kundi la watu ambao waliikubali injili na “hawakuanguka kamwe” (Alma 23:6).

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Shiriki injili kutokana na upendo.

Rais Dallin H. Oaks alishiriki somo lenye thamani alilojifunza kutokana na uzoefu aliokuwa nao akiwa kijana:

“Nilipangiwa kumtembelea mshiriki asiyeshiriki kikamilifu, bingwa mwenye mafanikio mwenye umri mkubwa kuliko mimi. Nikikumbuka matendo yangu, ninagundua kwamba nilikuwa na upendo kidogo kwa ajili ya mtu niliyemtemblea. Nilifanya kama jukumu tu, nikiwa na tamaa ya kuripoti asilimia 100 kwenye mafundisho yangu ya nyumbani. Jioni moja, karibu na mwisho wa mwezi, nilipiga simu kuuliza kama mwenza wangu na mimi tungeweza kwenda moja kwa moja na kumtembelea. Jibu lake la kukaripia lilinifundisha somo lisilosahaulika.

“‘Hapana, siamini kama ninawataka nyinyi kuja kwangu jioni hii,’ alisema. “Nimechoka. Tayari nimeshavaa kwenda kulala. Ninasoma, na siko tayari kabisa kusumbuliwa ili kwamba mripoti asilimia 100 kwenye mafundisho yenu ya nyumbani mwezi huu.’ Jibu lile bado linaniumiza kwa sababu nilijua alihisi motisha yangu ya kichoyo.

“Ninatumaini hakuna mtu tunayemwendea na mwaliko wa kusikiliza ujumbe wa injili ya urejesho anahisi kwamba tunafanya kutokana na sababu nyingine yoyote zaidi ya upendo halisi kwa ajili yao na hamu isiyo ya uchoyo kushiriki kitu fulani tunachokijua kuwa cha thamani” (“Kushiriki injili;” Ensign, Nov. 2001, 8).

Ushawishi wetu mara nyingi haujulikani.

Rais Gordon B. Hinckley alisimulia hadithi ambapo mmisionari alitoa taarifa kwa rais wake wa misheni mwishoni mwa huduma yake. Mmisionari alisema:

“Sikuwa nimepata matokeo yoyote kutoka kwenye kazi yangu. Nimepoteza muda wangu na fedha za baba yangu. Imekuwa ni upotevu wa muda. … Nilibatiza mtu mmoja tu wakati wote wa miaka miwili ambayo nimekuwa hapa. Na huyo alikuwa ni mvulana wa miaka kumi na miwili anayeishi nyuma ya sehemu za wazi za Tennessee.”

Rais wa misheni aliamua kumfuatilia mvulana ambaye mmsionari huyu alimbatiza. Alikua, akaoa, na akahamia Idaho. Watoto wake walikwenda misheni, na watoto wa watoto wake walikwenda misheni. Rais wa misheni alisafiri kwenda Idaho na kuwauliza watu wa familia ile kuhusu misheni zao. Baadaye alisema, “Niligundua kwamba, kama matokeo ya ubatizo wa yule mvulana mmoja mdogo katika sehemu za wazi za Tennessee uliofanywa na mmisionari aliyefikiri ameshindwa, zaidi ya watu 1,100 wamekuja Kanisani” (Mafundisho ya Gordon B. Hinckley [1997], 360–61).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tenga muda kwa wanafunzi kushiriki. “Wakati wanafunzi wanaposhiriki kile wanachojifunza, siyo tu wanahisi Roho na kuimarisha shuhuda zao, bali pia wanawahimiza washiriki wengine wa darasa kugundua kweli kwa ajili yao wenyewe. … Tenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika kila somo—katika hali fulani, unaweza kugundua kwamba majadiliano haya ndiyo somo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30).

Chapisha