Njoo, Unifuate
Juni 8–14. Alma 8–12: Yesu Kristo Atakuja Kukomboa Watu Wake


“Juni 8–14. Alma 8–12: Yesu Kristo Atakuja Kukomboa Watu Wake,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 8–14. Alma 8–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Alma  akihubiri

Kufundisha Mafundisho ya Kweli, na Michael T. Malm

Juni 8–14

Alma 8–12

Yesu Kristo Atakuja Kukomboa Watu Wake

Anza maandalizi yako ya kufundisha kwa kujifunza Alma 8–12. Kisha rejea upya muhtasari huu kwa ajili ya mawazo ya ziada ambayo yatawatia moyo washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza katika kujifunza kwao.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache kutafakari juu ya kujifunza kwao maandiko kibinafsi au kifamilia wiki hii. Ni kwa jinsi gani kujifunza kwao kumeshawishi chaguzi walizofanya kwa kipindi chote cha wiki? Waalike washiriki wachache wa darasa kushiriki mawazo yao.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 8

Jitihada zetu za kushiriki injili zinaweza kuhitaji msimamo na subira.

  • Watu wengi wanaona ni vigumu kushiriki injili—hususani wakati wamehisi kukataliwa, kama alivyokuwa Alma. Mfano wa Alma ungeweza kuwasaidia kumtumainia Mungu na kupata ujasiri wa kuendelea kushiriki shuhuda zao pamoja na wengine. Fikiria maswali haya ya majadiliano: Tunajifunza nini kutokana na ujumbe wa malaika kwa Alma katika Alma 8:15? Vipi kuhusu jibu la Alma kwa ujumbe wa malaika, linalopatikana katika Alma 8:14–32, linatupa msukumo kuendelea kushiriki injili wakati tunapokataliwa? Ni ushauri gani tungeweza kumpa mtu aliyejaribu kushiriki injili lakini alikataliwa? Ushauri wa Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada” ungeweza kusaidia kwenye mazungumzo haya.

  • Hadithi ya Alma na Amuleki inaonesha jinsi juhudi za waumini zilivyo muhimu kwenye kazi ya umisionari. Washiriki wa darasa wanajifunza nini kutoka Alma 8:19–30 kuhusu uhusiano kati ya waumini na wamisionari wa muda wote? (Ona pia Alma 10:1–12).

    familia mbili zikikutana

    Kushiriki injili na wale tuwapendao kunaweza kuwa uzoefu wenye furaha.

Alma 9:18–30

Mungu anahukumu watoto Wake kulingana na nuru na ufahamu walio nao.

  • Kuna onyo kali katika mistari hii kwa waumini wote wa Kanisa—mara tu tunapopokea nuru na ufahamu, tunategemewa kuuthamini sana, kuurutubisha, kuuishi, na kuutumia kuwabariki wengine. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuchunguza tegemeo hili, ungeweza kuwaomba wasome mafundisho ya Alma katika Alma 9:18–30 na kushiriki jumbe wanazopata kuhusu jukumu walilonalo kwa sababu ya kile wanachojua. Kwa nini kungeweza kuwa na shutuma kubwa mno wakati tunapofanya dhambi dhidi ya nuru kuu? Toa muda kwa washiriki wa darasa kutafakari nini wanaweza kufanya kuwa wakweli zaidi kwa nuru na ufahamu waliopokea. Ungeweza kupendekeza kwamba wasome Mafundisho na Maagano 50:24 wakati wakitafakari.

Alma 11–12

Mpango wa Mungu ni mpango wa wokovu.

  • Ungeweza kuanza majadiliano ya mafundisho haya kwa kumualika mshiriki wa darasa kuchora mchoro wa mpango wa wokovu ubaoni. Kisha ungeweza kugawa sehemu za Alma 11–12 miongoni mwa washiriki wa darasa na waalike kutafuta kweli ambazo wangeongezea kwenye mchoro. Kwa mfano, mpango wa Mungu unatukomboa kutokana na nini? (ona Alma 11:38–45). Ni kwa namna gani kujua kweli hizi kuhusu mpango wa wokovu kunabariki maisha yetu?

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile Alma 11–12 inachowafundisha kuhusu mpango wa ukombozi, ungeweza kuandika vichwa vya habari vifuatavyo ubaoni: Anguko, Mkombozi, Toba, Kifo, Ufufuo, na Hukumu. Washiriki wa darasa wangeweza kuchagua moja ya mada hizi na kuchunguza Alma 11–12 kwa ajili ya kweli wanazojifunza kuhusu mada hiyo. Waalike washiriki wa darasa waandike kweli wanazozipata, pamoja na marejeleo ya maandiko, chini ya kichwa cha habari kinachohusika ubaoni. Kama darasa, jadilini ni kwa jinsi gani kujua kweli hizi kunaathiri maisha yetu na maamuzi tunayofanya.

  • Washiriki wako wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na majadiliano yenye kiini kwenye Alma 12:31–32, ambapo Alma alifundisha kwamba baada ya Anguko, Mungu aliwapa Adamu na Hawa amri—lakini baada tu ya kuwafundisha mpango Wake. Ni kwa jinsi gani kujua kuhusu mpango kunaathiri jinsi tunavyoona au kuhisi kuhusu amri? pengine ungeweza kuzungumza kuhusu baadhi ya amri mahususi; kwa mfano, ni kwa jinsi gani kujua kuhusu mpango wa Mungu kunatusaidia kufanya siku ya Sabato kuwa takatifu au kutii sheria ya usafi wa kimwili?

  • Baadhi ya washiriki wa darasa wangeweza kuwa na maswali kuhusu Alma 11:26–39, ambapo Amuleki alisema kuna Mungu mmoja tu. Maandiko yafuatayo yanafafanua jinsi washiriki wa Uungu ni “Mungu mmoja” wakati bado wakiwa viumbe waliotengana: Yohana 17:20–23; 2 Nefi 31:21; na 3 Nefi 19:29. Maelezo haya kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland yanaweza pia kusaidia: “Tunaamini Wao ni wamoja katika kila maana na kipengele cha milele kinachoweza kufikiriwa isipokuwa kuwaamini Wao kuwa watu watatu waliounganika katika kiini kimoja” (“Mungu Pekee wa Kweli na Yesu Kristo Ambaye Wewe Umemtuma,” Ensign au Liahona, Nov.2007, 40).

Alma 12:9–14

Kama hatutaifanya mioyo yetu kuwa migumu, tunaweza kupokea zaidi ya neno la Mungu.

  • Moja ya jumbe Alma na Amuleki walizofundisha mara kadhaa ulikuwa jinsi hali ya mioyo yetu inavyoshawishi kiasi gani cha ukweli tunaweza kupokea kutoka kwa Bwana. Kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ukweli wa kanuni hii, ungeweza kuwaalika wasome Alma 12:9–14 katika jozi au makundi madogo na kujadili matokeo ya kuwa na moyo mgumu. (Ungeweza pia kuwaomba wasome Alma 8:9–11; 9:5, 30–31, na 10:6 25.) Inamaanisha nini kuwa na moyo laini? (ona Yeremia 24:7; Alma 16:16; Helamani 3:35). Ni kwa jinsi gani moyo laini unatusaidia zaidi kuelewa neno la Mungu?

  • Alma alifundisha kwamba tunapofanya mioyo yetu kuwa migumu, tunapokea “sehemu ndogo” ya neno la Mungu (Alma 12:10). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu kutoka kwenye maandiko ambao unaelezea kwa mfano kanuni hii. Ni kwa jinsi gani Bwana analainisha mioyo yetu ili kwamba tuweze kuendelea kujifunza zaidi kutoka Kwake? Ni uzoefu gani binafsi tunaoweza kushiriki?

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ina maana gani kuwa na moyo laini, ungeweza kushiriki baadhi ya mifano iliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.”

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwapa msukumo washiriki wa darasa kusoma Alma 13–16 wiki hii, ungeweza kuwaambia kwamba watapata jinsi maneno ya Alma yalivyotimizwa katika maisha ya Zeezromu na watu wa Amoniha.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Chukua msimamo wa kijasiri.

Mzee Jeffrey R. Holland alitoa matumaini yafuatayo kwa wale ambao wanayanyaswa kwa kushiriki au kutetea injili:

“Kama bado, siku moja utajikuta umeitwa kutetea imani yako au pengine hata kuvumilia baadhi ya matusi ya binafsi kwa sababu tu wewe ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Nyakati kama hizo zitahitaji vyote ujasiri na ustaarabu kwa upande wako.

“… Unaweza kujiuliza kama inastahilii kuwa na msimamo wa kijasiri wa uadilifu katika shule ya sekondari au kwenda misheni na kuona tu tamaduni zako ulizozithamini mno zikitukanwa au kujitahidi sana dhidi ya jamii ambayo wakati mwingine inadhihaki maisha ya uaminifu wa dini. Ndiyo, inastahili. …

“Marafiki, hususani marafiki zangu wadogo, jipeni moyo. Upendo msafi kama wa Kristo unaotiririka kutoka kwenye uadilifu wa kweli unaweza kubadili ulimwengu. …

“Kuwa imara. Ishi injili kwa uaminifu hata kama wengine wanaokuzunguka hawaiishi kabisa. Tetea tamaduni zako kwa ustaarabu na kwa huruma, lakini zitetee” (“Gharama—na Baraka—za Ufuasi,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 6–9).

Mioyo yao ilikuwa imelainishwa.

Hotuba za mkutano mkuu zifuatazo zinatoa mifano ya watu ambao mioyo yao ililainishwa na Bwana:

  • Hadithi ya familia ya Hatfield katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Gharama ya Nguvu ya Ukuhani” (Ensign au Liahona, Mei 2016, 66–67).

  • Hadithi ya Harold Gallacher katika ujumbe wa Rais Thomas S. Monson “Mwito Mtakatifu wa Huduma” (Ensign au Liahona, Mei 2005, 55).

  • Hadithi ya David katika ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Jifunze Kutoka kwa Alma na Amuleki(Ensign au Liahona, Nov. 2016, 73–74).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tazama kupitia Macho ya Mungu. Jitahidi kuwaona washiriki wa darasa lako kama Mungu anavyowaona, na Roho atakuonyesha thamani yao tukufu na uwezekano wao. Unapofanya hivi, utaongozwa katika juhudi zako za kuwasaidia (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 6).