Njoo, Unifuate
Juni 1–7. Alma 5–7 : “Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?”


“Juni 1–7. Alma 5–7 : ‘Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Juni 1–7. Alma 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Yesu amemshikilia mwana kondoo

Hamjasahauliwa, na John McNaughton

Juni 1–7

Alma 5–7

“Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?”

Unaposoma Alma 5–7, fikiria kuhusu washiriki wa darasa lako ambao ni mfano wa mafundisho katika sura hizi. Fikiria njia unazoweza kusaidia kuwahusisha katika majadiliano yako ya Jumapili.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Toa dakika chache kwa washiriki wa darasa kukumbuka kile walichosoma katika Alma 5–7 na kutafuta ukweli ambao wangependa kushiriki darasani. Kisha waombe kuushiriki na mtu aliyekaa karibu nao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Alma 5:14–33

Lazima tupate uzoefu—na kuendelea kuhisi—mabadiliko makuu ya moyo.

  • Washiriki wa darasa walitakiwa kutafakari maswali katika Alma 5:14–33 kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Ungeweza kuanza majadiliano juu ya mistari hii kwa kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki maswali gani kutoka katika mistari hii yalikuwa ya maana kwao. Kisha ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kufanya kazi katika makundi kurejea upya Alma 5:14–33 na kugundua kile inachomaanisha kupata uzoefu wa mabadiliko ya moyo kupitia Mwokozi na Upatanisho Wake. Wangeweza pia kutafuta baraka ambazo zinakuja kutokana na moyo uliobadilika. Sitiari zipi zingine zimetumika kuelezea mabadiliko aliyoyaeleza Alma? (Kwa mfano, ona Yohana 3:1–7; 2 Wakorintho 5:17; Dale G. Renlund, “Kuhifadhi Mabadiliko Makuu ya Moyo,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 97–99.) Tunawezaje kudumisha mabadiliko ya moyo katika maisha yetu yote? (ona Alma 5:26).

    Picha
    Msichana akisali kando ya kitanda

    Tunapomgeukia Mungu, tunaweza kupata uzoefu wa “mabadiliko ya moyo.”

Alma 5:44–51

Tunaweza kupata ushahidi wetu wenyewe wa Mwokozi na injili Yake kupitia Roho Mtakatifu.

  • Kama Alma, washiriki wa darasa lako wamepata ushuhuda wao wenyewe wa Mwokozi na injili Yake. Kuwasaidia kujifunza nini Alma alifanya kupokea ushahidi wake kupitia Roho, ungeweza kupitisha vipande vya karatasi vyenye neno Ushuhuda lililoandikwa juu ya karatasi. Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi katika jozi kurejea Alma 5:44–51 na kutumia kile wanachojifunza katika mistari hii kuandika “maelezo ya upishi” kwa ajili ya ushuhuda. Kwa mfano, “viungo” vya upishi vingeweza kuwa kweli ambazo zinaunda ushuhuda wetu. “Maelekezo” kwa ajili ya mapishi yangeweza kuwa vitu tunavyohitaji kufanya ili kupata ushuhuda. (Ona ujumbe kutoka kwa Mzee Dieter F. Utchdorf katika “Nyenzo za Ziada” kwa ajili ya mawazo kadhaa.) Ni “viungo” gani na “maelekezo” yapi wangeweza kuongeza kwenye maelezo yao ya upishi kutoka kwenye uzoefu wao wenyewe au uzoefu mwingine katika maandiko? Zialike jozi kushiriki kile walichojifunza na kile wanachofanya ili kumwalika Roho Mtakatifu kushuhudia ukweli kwao.

Alma 6

Tunakusanyika kama Watakatifu kusikiliza neno la Mungu na kufanya kazi Yake.

  • Kuwakumbusha washiriki wa darasa kuhusu umuhimu wa kukusanyika pamoja kama jamii ya Watakatifu, ungeweza kuwaalika kufikiria kwamba mtu fulani wanayemjua anahisi kwamba kuwa kanisani si muhimu. Ni nini wangeshiriki kutoka Alma 6 kumfundisha mtu huyu kuhusu baadhi ya baraka za kuwa kanisani? Tunawezaje kukamilisha vyema lengo la kukusanyika ambalo Alma alilielezea?

Alma 7:7–16

Mwokozi alijichukulia juu Yake dhambi zetu, maumivu, na mateso.

  • Kunaweza kuwa na watu ndani ya darasa lako wanaohitaji kwa haraka kujua nini Alma 7:7–16 inafundisha—kwamba Mwokozi alijichukulia juu Yake sio tu dhambi zetu bali pia maumivu yetu, mateso, magonjwa, na udhaifu wetu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kugundua hili? Pengine ungeweza kutengeneza chati ubaoni yenye vichwa vya habari Kile mwokozi alichoteseka na Kwa nini aliteseka. Darasa lingeweza kukamilisha chati baada ya kusoma Alma 7:7–16. Inaweza pia kusaidia kufikiria mambo mengine ambayo Mwokozi alivyoateseka wakati wa maisha Yake (ona mifano katika “Nyenzo za Ziada”).

  • Baada ya kujadili kile Alma alichofundisha katika Alma 7:7–16, pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati Mwokozi alipowasaidia, ambayo inamaanisha kwamba aliwasaidia (ona “Nyenzo za Ziada” kwa mifano ya jinsi Yesu anavyotusaidia sisi). Ungeweza pia kushiriki nukuu ifuatayo kutoka kwa Rais Dallin H. Oaks: “Mwokozi wetu amefunua kwamba Yeye ‘alishuka chini ya vitu vyote’ (M&M 88:6). … Tunaweza pia hata kusema kwamba kwa kujishusha chini ya vitu vyote, Yeye aliwekwa mkamilifu ili kutuinua na kutupa nguvu tunazohitaji kuvumilia mateso yetu. Tunahitaji tu kuomba” (“Kuimarishwa na Upatanisho wa Yesu Kristo.,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 64).

  • Alma alitangaza kwamba kuja kwa Mkombozi “ni muhimu sana kuliko” kitu kingine chochote. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kujifikiria kwamba wako kwenye darasa la historia wakijadili matukio muhimu sana ya kihistoria. Ni mistari gani kutoka Alma 7 ambayo wangeweza kushiriki ili kuunga mkono dai la Alma katika mstari wa 7? Ni ushauri gani Alma aliwapa watu wake ambao unaweza kutusaidia kujiandaa kwa ujio wa Mwokozi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwatia moyo washiriki wa darasa kusoma Alma 8–12, ungeweza kushiriki pamoja nao kwamba sura hizi zinasimulia hadithi za wanaume wawili. Mmoja alikuwa asiyejali kuhusu Kanisa na mmoja alikuwa mtesaji mwenye ari, lakini wote wakawa watetezi mashujaa wa imani.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kupata ushuhuda wetu wenyewe.

Mzee Dieter F. Uchtdorf alitoa mpangilio ufuatao wa maandiko kwa ajili ya “kupokea ushuhuda binafsi wenye chanzo katika ushahidi wa Roho Mtakatifu”:

Kwanza: Hamu ya kuamini. Kitabu cha Mormoni kinatutia moyo: ‘[ikiwa] mtaamka na kuziwasha akili zenu, hata kwenye kujaribu juu ya maneno yangu, na kutumia sehemu ya imani, … hata ikiwa [nyinyi] hamwezi ila kutamani kuamini’ (Alma 32:27). … Mungu anatuahidi msaada mtakatifu hata kama tuna hamu tu ya kuamini, lakini inatakiwa iwe ya kweli na si hamu ya kusingizia.

Pili: Chunguza maandiko. Kuwa na maswali; yachunguze, pekua katika maandiko kwa ajili ya majibu. Tena, Kitabu cha Mormoni kina ushauri mzuri kwa ajili yetu: ‘Ikiwa mtatoa nafasi, ili mbegu ipandwe ndani ya mioyo yenu’ kupitia kujifunza kwa bidii neno la Mungu, mbegu nzuri ‘itaanza kuvimba ndani ya vifua vyenu’ kama hamtakataa kwa kutoamini. Mbegu hii nzuri ‘itaanza kukua ndani ya nafsi [yenu]’ na ‘kuangaza kuelewa [kwenu]’ (Alma 32:28).

Tatu: Fanya mapenzi ya Mungu; tii amri. … Tunahitaji kuja kwa Kristo na kufuata mafundisho Yake. Mwokozi alifundisha: ‘Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo’ [Yohana 7:16–17; italiki zimeongezwa]. …

Nne: Tafakari, funga, na sali. Kupokea ufahamu kutoka kwa Roho Mtakatifu, lazima tumwombe Baba wa Mbinguni kwa ajili ya ufahamu huo [ona Alma 5:45–46; Moroni 10:3–4]” (“Nguvu ya Ushuhuda Binafsi,” Ensign au Liahona, Nov,2006, 38–39).

Yesu Kristo aliteseka nini?

Ni mateso gani mengine ambayo Mwokozi aliyapitia?

Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo anatusaidia sisi?

Ni katika njia zipi zingine Yesu alitusaidia?

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiboreshe kuwa mwalimu aliye kama Kristo. Kama mwalimu, ni muhimu kutafakari njia unazoweza kuwasaidia wanafunzi kujenga imani kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Fikiria kutumia maswali ya kujitathimini kibinafsi kwenye ukurasa wa 37 wa Kufundisha katika Njia ya Mwokozi ili kukuhamasisha.

Chapisha